Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Diplomasia hata kwa Papa......

>> Thursday, September 28, 2006

Sayansi ya diplomasia ni ngumu. Ni rahisi kunyoshea mtu vidole, lakini katika maswala ya diplomasia na siasa lazima kuna mtu huwa anashinda. Hivi karibuni hakuna hata lakusita, Papa jasho limemtoka kujitetea kuhusu Uislamu.Mcheki hapa anavyoomba msamaha. Lakini nahisi kumfukuza Askofu Milingo kutoka Ukatoliki kutokana na msimamo wake wa kuoa haikumtoka jasho hata kidogo. Kwa hisia zangu ni mchezo wa diplomasia tu na kwamba Waislamu wamegundua ka kitu. Zamani ilikuwa inachukua zaidi ya miaka mamia kabla kanisa halijaomba msamaa.Zamani liliua watu kwa wao kusimamia ukweli lakini likuwa mwiko kukiri.Check Galileo controversy na nyinginezo. Je ni hii janja ya Alqaida ya kufa kufa ambao inafanya viongozi wa dini nyingine wasikilize? .Ofukozi ndiooo ukweli wenyewe.Papa akiwa katika gia ya upoleAskofu milingo akiwa na mwanamke wake ampozaye roho.

Papa akijaribu kujieleza kidiplomasia kwa mmoja wa viongozi wa wajanja waliogundua.

Read more...

Nina Ndoto

>> Saturday, September 23, 2006

Nina ndoto siku moja WaTanzania tutakuja kupendana.Kwamaana sasa hivi hata katika mablogu maoni mengi ni ya matusi na kujaribu kukatishana tamaa.
Nina ndoto siku moja tutagundua kuwa umiliki wa mali si muhimu sana katika maisha.
Nina ndoto kwamba Tanzania haitakuwa ina wasiwasi itakumbwa na njaa.
nina ndoto kuwa ndugu na jamaa katika dunia yetu watagundua kuwa kweli sisi ni ndugu na jamaa.

Nina ndoto kuwa Tanzania itafikia kuwa elimu ni jambo ambalo Mtanzania akiamua kulipata, hulipata bila ya kipato cha familia au chake kuwa kama ndio kithibitisho cha upataji wake wa elimu.
Nina ndoto kuwa Tanzania na Watanzania watadhihirika kuwa ni kielelezo cha jinsi uungwana na waungwana watakavyo kuwa.
Nina ndoto..................
Alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhh!
Sasa Desmond Tutu ananitisha !Anasema kwa mtazamo wake Waafrika Kusini wamepoteza dira! Halafu nasikitika kwasababu namuunga mkono. Maadili ya mwanzo ya kupigania uhuru,usawa na umoja hayaendani na ya sasa ambayo ndugu kwa ndugu wauana, wabakana,nk.Anashangaa hata inavyo fikia hata Mzee Zuma anaachiwa tu,na labda atakuja kuwa Raisi wa South Afrika.

Msome hapa akilalamika.

Alaaaaaaaaaaah!
Sasa kwanini watu tunaamuatu kutukanana bila sababu? Je tumekosa pakupelekea matatizo yetu?. Wakatoliki walikuwa wakienda kutubu kwa Padre.Waislamu kwa mashehe kupata mawaidha.Sisi wengine tulikuwa tuna enda kwa wazee wetu. Wote tulikuwa na ndugu na jamaa ambao tuliweza kusawazisha mabo yetu. Sasa ni kweli tumekosa pa kwenda kupeleka mambo ya zinguayo mioyo yetu mpaka twatukanana wenyewe kwa wenyewe?Mpaka twafikia kuumizana na maranyingi bila sababu? Mpaka twauana wenyewe kwa wenyewe?Je ni umasikini tu huu? Wamagharibi wana Matherapi, wana masaikolojisti sasa kwanini sisi tuue tamaduni zetu ambazo zilikuwa zimejengeka , zikiunganisha haya mambo yote kama kweli hili ndio pungufu sasa?


Nina ndoto siku moja Waafrika tutaamka nakugungua kuwa bado hatujachelewa na tuna weza kuokoa baadhi ya mambo yetu ambayo ndio msingi wakusimama kwetu kama waafrika.

Hivi ile ndoto ya Martin Luther King iliendaje vile? Hivi inatuhusu sisi Waafrika ?


Ndoto yako ni ipi?

Read more...

LEO, KAMA NI SIKU YA MWISHO!

>> Tuesday, September 19, 2006Malaika mweupe , Shetani Mweusi au?

Binadamu, binadamu, binadamu! Kwa nini unajifanya kusahau kuwa hujui kama sekunde ijayo inaweza kuwa ya mwisho katika maisha yako?

Kama kuna mbinguni na hii ni sekunde ya mwisho, basi mimi nitakwenda motoni:-(
Je, naogopa? Jibu ni, naogopa kwa herufi kubwa.

WEWE JE?

Kisirisiri naamini baaada ya kufa haitakuwa kama watu waaminivyo sasa.
Itakuwaje ubongo wa kibinadamu ambao unapungufu zinazofanya tusielewe ya Mungu na ya shetani leo, uwe umepatia kuelewa au kutabiri maisha baada ya kifo?

Lakini lolote litokealo naamini wafanyao maovu hawatafaidi kama watendao mema.

Iweje ubongo huu ambao unafanya tuogope hata kujiuliza au kukosoa maswala ya vitabu vya dini ambavyo maandishi yake yalinukuliwa na binadamu mpungufu, utuwezeshe kuelewa kuwa ni ukweli safari yetu ya mwisho ni motoni au mbinguni?

Labda unajiuliza kama nina imani kuwa kuna Mungu!
Labda unaamini mie nimepotea!
Unaweza kuwa umepatia katika yote mawili.
Hivi malaika ni weupe?

Basi usisahau kuniombea!Namsikiliza Aswad akiniimbia swala la upendo.


Read more...

MTOTO WA TANZANIA NA RAFIKIYE.


Naomba urafiki! Nitakupa pipi!
Anhaa! Unaninyima kitumbua chako ee! Basi tupingulie urafiki!


Ni matumaini yangu rushwa haianzii huku.

Read more...

MTOTO WA KIAFRIKA NA WAKUBWA ZAKE.Weeee! Kaa kimya , wakubwa wanaongea!Nenda kacheze nje!
Ntakupiga makonzi wewe ohooo!We jifanye husikii tu!
Aswad wakikupa kibao African Children

Read more...

ORGAZIMU, KUPIGA BAO AU.......!

Je, si ni safari ya ghafula ya damu kutoka katika viungo vya sehemu za siri tu?
Je, si ni mchezo uchezekao ubongoni ukipata misaada kupitia mishipa ya fahahu, kupitia mishipa ya damu na ukisaidiwa na kuhani homoni tu?
Sasa kwanini mtu ahitaji kiumbe mwingine kutosheleza ahueni hii?
Sasa kwa nini huyu kiumbe aitwaye mwanamke ni muhimu sana kwangu katika kuleta ahueni hii?
Labda kwako si muhimu!Usijali!
Najiuliza tu!

Read more...

MAMBO YA KIUCHIUCHI, SHEPU ZA MATAKO NA MATAMANIO


Nice ass

Huwa na shangaa sana jinsi binadamu anavyojenga sababu na anavyo halalisha matamanio.
Katika nchi za magharibi nilizowahi kuishi, utakuta wanawake kwa wanaume walio wengi wana ladha tofauti katika swala la vikalio, na uwezo wake wakufariji matamanio.Hii hasa ni katika kukidhi mvutanio wa jinsia ukifananishwa na wa watu weusi wenye asili ya Afrika. Kinacho nishangaza ni kwamba asilimia kubwa ya watu weusi watakuambia shepu kubwa za vikalio ni muhimu katika matamanio yao. Weupe watasema vikalio vilivyopigika pasi ndio vina mvuto mkubwa.

Cha kujiuliza, ni nini hasa kinatofautisha mvuto wa ngono katika ujazo wa tako?


Sauna ya Kifini ijumuishayo wanaume na wanawake.Ukiingia katika maswala ya kukaa uchiuchi, naamini katika nchi za magharibi hakuna mabingwa kama waskandinavia. Ukisikia utamaduni wa sauna ,kwenye nchi kama Finland basi ni kasheshe.Huko kukuta dada, kaka,mama,baba,binamu na marafiki wako uchi ndani ya sauna, ni jambo la kawaida.Halafu utamanudi huu wa sauna huendana na pombe . Kwa kifupi ratiba ya sauna iko hivi; unavua nguo, unajimwagia maji au kuoga kidogo, unaingia sauna ambako unapigwa na joto kali na kutowa majasho vibabab vya kutosha, unatoka kwenda kuogelea au kujimwagia maji baridi, halafu unaketi kupata bia moja.Ukimaliza hapo unarudi sauna tena halafu mchezo unajirudia. Cha ajabu ni kwamba mara nyingi watu hawa hawaunganishi watu kukaa uchi na maswala ya ngono!

Ukirudi Afrika utakuta pia kuna tamadunni kibao ambazo kuona matiti ya mwanamke ni kawaida tu.


Nice ass!
Nachojiuliza ni kwa nini kwa wengine hapa duniani kukaa uchi ni jambo la ajabu, wengine wanapandisha ashki na wengine ni jambo la kutia aibu? Na bila kuwasahau wale wajivunialo hili jambo ambao kwako ungefunga machoi kuwaona uchi!

Je, haya mambo si vitu tu ambavyo ubongo unafanya kila mtu avitafsiri kivyake?
Je, ni vitu vya maana vya watu kupigania au kuvichukulia umuhimu?
Je, ushawahi kujiuliza ukipendacho hakina matamanio kwa kila mtu?
Je, kwanini wengine wanaringa?

Najiuliza tu , katika hii treni ya mawazo!

Read more...

Anonymous Nr.1

>> Monday, September 18, 2006

Leo nilijikuta namsikiliza yule anonymous anifurahishaye. Si mwingine basi ni yule mpiga miziki wa Nigeria ambaye hapendi kuonekana sura, Lagbaja. Ananizingua sana katika upangaji wake wa muziki na pia jinsi atumiavyo sauti yake ambayo haifichi hata kiduchu Uafrika. Pata vibao vyake viwili hiviHapa anakupa Skentele Skontolo


Hapa anakuambia Never Far Away

Read more...

Najisikia vibaya kwa kuwa najisikia vizuri!

Kuna mambo mengine mengi katika maisha ambayo hukatisha tamaa. Moja wapo linalonisumbua leo ni ukweli kuwa miongoni mwa viongozi wa Ivory Coast alihalalisha kumwagwa uchafu wa sumu kutoka magharibi nchi mwake.Sasa raia kibao wanaumwa kutoka na na uchafu huo wa sumu ulioletwa na meli nchini humo.Hili pamoja na mengi tu yamekuwa yana nizingua.

Kwa bahati nzuri nimefanikiwa kula chipsi dume na kachumbari leo .Kitu ambacho sijawahi kukifanya kwa muda mrefu kutokana naukosefu wa mihogo katika anga niliyopo.Ghafula nikaanza kujisikia vizuri. Na nikamalizia na wimbo wa James Brown I feel good kama uonekanavyo hapa chini.Lakini naanza kujisikia vibaya kwa kujisikia vizuri kutokana na kitu kidogo kama hiki.


Read more...

Stereotaipu!
Posta la Minstrel shoo limuonyeshalo mtu mweusi kwa jicho la kizungu enzi hizo

Ukiwa unaangalia haya maswala ya steretaipu kama mtu mweusi, ni rahisi kusahau kuwa watu wengine nao wanalalamika mambo kibao. Nimegongana na atiko moja ambayo imenizingua sana.Hii ni ya maswala ya dunia iwaonavyo waislamu hasa katika maswala ya kuandamana mara wakisikia dini au Mtume kakashifiwa. Nafikiri hata hakuna haja ya kuelezea sana nini vyombo vya habari vya magharibi vinavyotaka tuamini kuhusu waislamu. Mambo kibao yalisemwa kitu ambacho kikanikumbusha ni jinsi gani wana dunia tunavyoweza kujitengenezea picha za watu wengine akilini.

Pia nilikutana na habari iliyoandikwa na kikundi kinachotetea muonekano wa Waitali. Hiki kikundi kinapinga mambo ya kufanya waitalia waonekane kama mamafia. Waitaliano ukiwa unawajua kwa kupitia sinema za holiwudi , basi utadhani wote ni Mamafia. Watu weusi huwa mara nyingi huwekwa katika kundi la wazembe. Wanaume weusi husifika kuwa wamebarikiwa ujazo kwenye sehemu za siri pia. Wanawake weusi ni mambo kibao, ukiachilia kuwa wamebarikiwa kimaumbile hasa sehemu za nyuma. Vile vile huwezi kusahau maswala yaliyoletwa na minstrel shows tokea enzi hizo za utumwa Marekani, wamishenari na wakoloni wengine Afrika.

Nikapitia tena habari nyingine za Waasia ambao wanaishi Marekani.Wao wanalalamika kwanini hata holiwudi hupenda kuwapa roli za udaktari au roli ambazo si babu kubwa.Wanalalamika kuwa mbona watu weusi siku hizi wanacheza roli zote mpaka za uraisi wa Marekani kwenye sinema, lakini hata Jackie Chan hapati roli ambazo anaweza kumpiga busu mwanamke wakizungu. Mimi binafsi kabla sijakutana na playboy wakichina hata sikumoja haikunijia akilini kuwa kuna mchina playboy.

Ukipitia katika tovuti za watu weupe kama hii hapa,, ambao wanachukia watu wa rangi nyingine, utakuta nao wanalalamika kuwa eti watu wote wengine wanaruhusiwa kuwa wabaguzi isipokuwa wao weupe tu ndio wanaonekana wabaya wakibagua au kustereotaipu.

Ukiachana na haya yote, utakuta sura za mtoto wa kiafrika afaye na njaa, maswala ya muafrika vitani na maswala ya waislamu yanatawala katika kipindi hiki.Ukiwa unaamini vyombo kama Televisheni huwezi kushangaa ukawa huamini kabisa kuwa Waislamu wanaweza wakawa watu wa amani.Lakini watu wanajua hata katika ukristo kuna kasheshe kibao ila ni vigumu kufananisha na jinsi waislamu wanavyoonyweshwa kwenye luninga.
Cha kujiuliza, ni nani afaidikaye na stereotaipu hizi?


Mwanamke mweusi ana stereotaipu ya kuwa ni kiboko kwa kunengua pia
Si ukweli kuwa stereotaipu hizi huwaumiza watu wote. Kuna akina Bert Wiliams ambao waliwahi kutengeneza karia na kulipwa sana kwakucheza roli wazungu walizopenda kumuhusisha mtu mweusi nazo. Ingawa pia inaaminika alisaidi kuchangia kuingia kwa watu weusi katika biashara ya burudani, swali ni, Je mtu mweusi amejikomboa katika hizi roli akina Bert Williams walizo anzisha?Bert Williams , mtu mweusi ambaye alicheza utu weusi kama ulivyopendelewa na watu weupeJe, mambo haya ya kustereotaipu watu yatasaidia kuiweka dunia kwenye amani?

Katika kipindi hiki ambacho naona vita imeondoka kutoka kuwalenga Warusi kuja kwa waislamu wenye imani kali, ningefurahi kuwa watu wakumbuke kuwa mara nyingi muonekano utolewao kwenye vyombo vya habari sio ukweli mzima.

Chakusikitisha ni kwamba bado muonekano wa watu weusi unahitaji ukarabati zaidi take tusitake.Ingawa akina Kofi Annan, kama alivyofanya Bert Williams wanacheza roli zao. Tunahitaji akina Mandela , akina Nyerere, na akina mimi na wewe kusaidia kufuta stereo type ya mtu mweusi kama ijulikanavyo sasa au kuigeuza iwe ni ile tunayoweza kujivunia.

Angalia mambo haya kwenye video hapo chini .Ingawa aliyeingiza muziki anafanya utani je wewe unahisi ujumbe wa video hii ni nini?


Read more...

Yuko wapi Mwalimu wa kiafrika aliye wafunza mababu zetu?

>> Wednesday, September 13, 2006

Ni rahisi kuwa na maswali kuhusu matatizo ya Tanzania bila kuwa na majibu. Na kuna uwezekano wa kuwa na majibu ya maneno bila ya kuwa na ya vitendo. Na mara nyingi sana utasikia jibu kwamba elimu ndio suluhisho la matatizo mengi ya Tanzania. Kwa vitendo swala hili linafanyiwa kazi kwa kuongeza shule na walimu. Cha kusikitisha ni kwamba bado wakati tunasisitiza uongezwaji wa shule na walimu kuna sehemu tunaziacha wazi katika kuujenga uwezo wa kufikiri na wakutatua matatizo wa Mtanzania.

Kuna maswali haya ambayo inabidi yaangaliwe.
1.Je, watu wafundishwe wafikirie nini?
2.Je, wafundishwe jinsi ya kufikiria?
3.Je, waachiwe wajigundue wenyewe kwa ubunifu wao wenyewe?

Elimu ya asili ya Kitanzania ilikuwa inatolewa ilikuwezesha mtu kuweza kukabili maisha yake. Katika maswala ya Jando wanaume walifundishwa jinsi ya kuishi na kuyakabili maisha kama wanaume. Unyago ulimfunza mwanamke kuyakabili maisha kama mwanamke. Hii ni mifano tu ya karibu . Lakini elimu hii yetu ambayo tuliletewa, mwanzoni haikuandaliwa kutuwezesha kuyakabili maisha ambayo yalibadilishwa kwa uwepo kwa ukoloni. Cha zaidi yalikuwa yanalenga kutuwezesha kuwa watumishi wazuri ambao bado watakuwa wanatekeleza amri ya Watawala ambao hawakuwa Watanzania. Elimu ilikuwa ni ufunguo wa maisha ya kutumika na kujibu ndio mzee, na siyo yakufundisha kufikiria jinsi ya kutatua matatizo yetu wenyewe. Na hii si Tanzania tu.Afrika kusini walifikia kuhakikisha kuna kuwa na ufa mkubwa kati ya wazungu na waafrika ili kuhakikisha kuwa Mzungu atatawala, na mwafrika atatawaliwa.

Je, elimu ya Tanzania imebadilika tokea enzi za mkoloni?
Je, Mtanzania na elimu yake anauwezo gani wakuchangia katika maendeleo ya nchi?
Je, Watanzania hawaelimishwi sasa hivi ili kuchangia mafanikio ya uchumi wa nchi za nje na sio Tanzania yenyewe?

Inawezekana elimu yetu haina kasoro kubwa.

Sasa kwanini Mtanzania hata ambaye amemaliza chuo kikuu ni vigumu sana kuyakabili maisha ya Kitanzania?

Kama elimu ya zamani za mababu iliwawezesha kuyakabili maisha ya jamii katika kipindi hicho , basi elimu ya leo inatakiwa itufunze kuyakabili mazingira ya jamii hii ya leo.

Ni kweli ni vigumu kujitoa katika mfumo wa uchumi wa dunia. Hatuwezi kuikwepa elimu hii ya nje kirahisi. Ukiwaangalia wachina, tofautiyao ni kwamba wanajaribu kumjenga mwananchi kielimu ambayo itamfanya aajirike. Hawakazanii sana aende chuo kikuuu wala nini. Pia huakikisha wanajifunza kutoka katika wapevu na kuunyonya utaaluma wao pale wapatapo nafasi. Hii inasababisha wana lalamikiwa kuwa ni wezi wa taaluma. Lakini je si ndio maswala hayo hayo yanasababisha viwanda vingi viamishiwe kwao?Ka maana wapelekao viwanda wanakuta kuna watu ambao wanauwezo na taaluma ya kufanyakazi.Labda mtu atasema ni kwasababu ya wingi wao ndio maana kila mtu anakimbilia kufanya nao biashara. Lakini lazima ikubalike kuwa wanawaandaa wananchi wao sio kama Waingereza, wamarekani au Wajerumani wawaandavyo wananchi wao. Wanawaanda wakijua kuwa hawa ni wachina na katika mfumo unaowawezesha kujitatulia matatizo yao ndani ya nchi yao.

Basi ningependa elimu yetu itufunze jinsi ya kufikiri.Ningependa hata ituonyeshe ninini vya muhimu vya kulenga katika kufikiri. Ituwezeshe kufikia uwezo wakutatua matatizo yetu.Matatizo yetu iwe njaa, magonjwa au umasikini uliokithiri hivi sasa.

Nchi kama Tanzania haifai kukumbwa na njaa. Elimu za zama zilizopita ziliwawezesha mababu zetu enzi hizo kujua jinsi ya kusindika mazao. Ukaushaji wa mazao yetu , nyama, viazi, mihogo nk ilikuwa ni kawaida. Elimu yetu basi ituletee hekima za kuendeleza walipoishia mababu zetu. Ikibidi tujifunze kula hata nyoka kama wafanyavyo Wachina.Tujifunze kula hata mbwa kama wafanyavyo Wathailand.Lakini je hii ni lazima?.Kwanini tusijifunze kuwazalisha baadhi ya wanyama pori wasio adimika sana kama swala nk, kwa zumuni la kuwageuza wawe kitoweo cha kawaida cha Mtanzania? kwani nilazima nyama zisizokuwepo katika mataifa yalioendelea lazima zibakiwe na jina nyama pori?Kwa nini tusisikie NGO's zkishughulikia miradi mipya ya mambo mapiya ambayo ni uniq kwa Tanzania? Tunahitaji kufikiri kama walimu waliofundisha mababu zetu jinsi ya kuyakabili maisha.Inabidi tusiyatupe yote yetu mazuri ya kiafrika kwa kisingizio cha kwamba yamepitwa na wakati.Inabidi elimu yetu ya sasa itusaidie kubainisha yale ya zamani yatufaayo ilituyachanganye na ya sasa ili kujiokoa kama Watanzania.


Fela Kuti anakuambia Teachers don't teach me nonsense

Read more...

Martin Luther King Jr , Alqaida na Peter Tosh mawazoni

>> Tuesday, September 12, 2006

Martin Luther King Jr alisema kama mtu hajagundua kitu ambacho anaweza kukifia basi hana sababu ya kuishi. Cheki aliyosema hapa


Miaka mitano baada ya 9/11 nimejikuta namkumbuka Peter Tosh katika wimbo uitwao Equal Rights , akisema kuwa kila mtu anataka kwenda mbinguni, lakini hakuna atakaye kufa.

Kutokana na maswala ya haki aliyoimba, nilijaribu kufikiria bongo za wanadini wenye siasa kali wanavyoweza kujiosha ubongo mpaka wakaamini kuwa wanatafuta haki katika umwagaji damu za watu wasio na hatia.


Martin Luther King Jr aliwahikusema kama mtu hajagundua kitu ambacho anaweza kukifia, basi hastaili kuishi. Najiuliza tu !Je hawa watu wanaojiua hivi hakuna kauwezekano kuwa kaugunduzi kao ka kakitu ka kujiua, kalikuwa potofu?


Mzee Osama anashauri ujiue lakini naona yeye binafsi hajisikii kufakufa bado

Wafuasi wa Alqaida naona wamepata kitu cha kukifia kwa hiyo wameamua kujifia.Kinacho nisikitisha wameamua kujiua ilikuua na raia ambao hawajaamua kufa.
Kinachonizingua ni jinsi viongozi wa Alqaida wanavyoshindwa kufikia maamuzi ya kujiua kama wawashaurivyo wafuasi wao. Kila siku utasikia tu kuwa wamejichimbia sehemu au wamekimbia .Sasa kwanini hawataki kuwa mfano katika kujiua?Nashindwa kuelewa wana roho ya namna gani kuhalalisha mauaji ya raia wasio na hatia kwa kisingizio cha dini.

Nikiwa bado nafikiria jambo hili maswali hayaishi kunijia. Je Peter Tosh anaweza kuwa si sahihi? Je mimi na wewe leo hii tuko tayari kufia kitu?

Pia wakati maswala haya ya 9/11 yanaendelea hapa duniani, nashindwa kujizuia kukiri kuwa Waarabu wametusaidia sana watu weusi katika kutuondoa katika kitambulisho cha watu hatari.Angalau sio watu pekee tuangaliwao kwa kijicho kibaya fulani tukikatiza katika nchi za watu.

Lakini bado narudi katika swala la usawa ambalo linanukuliwa sana kama ni jambo linalo sababisha matatizo ya kujisikia kufakufa na watu wasio na hatia katika dhamira ya kufikisha ujumbe.Usawa ambao wote, Martin, Peter na Osama wanadai ni muhimu katika kuwepo amani. Nasikitika kuwa huu usawa sioni kabisa ukiota mizizi. Sasa, Je? Iko siku Waafrika tutafikia kufakufa na watu wasio na hatia katika hali ya kutaka kufikisha ujumbe wa amani?Kwanini hatujilipua kipindi hiki? Au tatizo ni dini zetu hazitu ahidi manono mara baada ya kujiua ndio maana bado hatujisikii kufa kufa ?
Peter Tosh alisema kila mtu anataka kwenda mbinguni lakini hakuna atakaye kufa

Ninamsifu Martin Luther King Jr kwa kufia alichokiamini. Natatizo na hawa wanaojiua ilikuua watu wengine wasio na hatia! Bado naendelea kufikiria nakukuna kichwa kuhusu swala hili! Bado namsikiliza Peter Tosh hapa katika huu wimbo wake mwingine akiwa na Mick Jagger akiniambia Walk dont look back.
Bado najiuliza........

Read more...

Wasichana wa Kiafrika!

Kuna watu wasemao kuwa mpaka nguvu ya wanaume ya utawala wa maswala ya jamii itakapotoweka na wanawake kushika hatamu, basi wanawake watatumiwa kama visafisha macho. Hivyo kutokana na ukweli kuwa wanawake ni viumbe vilivyobarikiwa uzuri na mvuto wa penzi basi basi wanaume watapenda kuwaona nusu uchi ilikukidhi haja zao. Hivyo itatafutwa kila sababu ya kuwezesha akinadada wakae nusu uchi kama uwaonavyo katika picha za hapo chini.Alek Wek mwanadada mrembo atokaye Sudan
Vicky atokaye Cape Town Afrika kusiniMwanadada mrembo Cynthia Masasi awakilishaye Tanzania katika fani.Ila wengine wanasema ni wanaume ambao husababisha wanawake wavae kujifunika kila sehemu.

Kwa mtazammo wangu siamini kuwa kuna jambo linaloweza kuwa na jibu moja. naamini mtazamo wa jamii haujagundishwa na wala hauwezi kudumazwa. Hubadilika kutokana na mambo mengine yaiathiriyo jamii kijamii. Naamini kuwa hata maswala yakigeuka na ikawa ni wanawake waiendeshayo dunia, haitatokea kuwa ni wanawake wote watajifunika kama waonekanavyo madada wa kiislamu. Kwasababu si ukweli kuwa ni wote ambao wanapenda fasheni za nusu uchi sasa hivi wanalazimishwa kuvaa hivyo.Pia naamini binadamu hupenda kuvunja miiko. Ukimng'ang'aniza awe kitu fulani, mar nyingi ndio unampa nguvu ya kukipiga vita kitu hicho. Kuna wakati huwa nafikiria nguo zinapewa umuhimu kupita umuhimu wake hasa kwenye nchi za joto.
Siwezi kuachia bila kusema, JAMANI WANAWAKE NI WAZURI !


Wanawake wa kisomali katika nguo za nguvu.Kama unataka kuona figa basi ulie tu

Read more...

Kesi nyingine tena kwa O.J Simpson

>> Wednesday, September 06, 2006
O.J Simpson's Mug Shot

Kwa mwendo huu naona huyu O.J Simpson ataendelea kushitakiwa mpaka atakapo kuwa marehemu. Kesi yake ile aliyoshtakiwa kumuua mke wake, iligawanya sana maoni ya watu kutokana na rangi za ngozi zao. Watu wengi weusi walimtetea O.J na weupe waliamini kuwa ni kweli alimuua mke wake ambaye alikuwa ni mweupe. Aliposhinda ile kesi weupe walidai kuwa hakushinda kihalali.Weusi walidai kuwa watu weupe wanadai hivyo kwasababu tu ni mtu mweusi kashinda safari hii. Kesi hii ilizua sana mijadala kuhusu kama ni kweli mahusiano ya watu wasiofanana kwa rangi ni busara. Katika ukurasa mpya ile familia ya marehemu wa mke wake wamefungua kesi mpya ya kutaka kumiliki jina lake , kupendeka kwake na persona(sijiu hili neno ni nini kwa kiswahili .Kwa ujumla wanataka kummiliki O.J Simpson. Kongoli hapa kwa habari hii au angalia hapa. Kinachonizingua ni jinsi wanasheria wanavyoweza kuwa wabunifu ili tu kutengeza kesi. Kwa mtazamo huu siku moja usije shangaa umemilikiwa na mtu mwingine ukiwa unajazajaza ma form bila kuyasoma.

Read more...

Anonymous!

>> Tuesday, September 05, 2006
Lagbaja Akiwa ndani ya mask kama kawaida yake.
Kama kawaida katika mablog nayopitia huwa nakuta Ma anonymous kibao. Wengi wao wanaongea mambo mengi ya busara, lakini wako wachache ambao huusudu sana kutukana. Inanikumbusha kuwa Tanzania zamani tulikuwa tunaogopa mashushushu.Hivyo labda bado watu huogopa kujulikana.

Lakini kuna wale ambao hawapendi tu kujulikana sura kama huyu mwanamziki wa Kinaijeria aitwaye Lagbaja .Yeye hapendi tu kujulikana sura. Lakini yeye sababu yake kubwa kujificha sura ni kwamba anaamini kuwa yeye kama vile pia jamii ya Kiafrika haina sura wala sauti. Huyu ni miongoni mwa wale wanamuziki wa Kinaijeria nao wapenda ambao wameathiriwa na akina Fela Kuti ,Sunny Ade nk.Unaweza kumsikiliza katika DUDU REDIO . www.duduradio.com . Kuna baazi ya nyimbo zake pale.Lagbaja is a Yoruba word that means somebody, nobody, anybody or everybody. It perfectly depicts the anonymity of the so called “common man”. The mask and the name symbolize the faceless, the voiceless in the society, particularly in Africa.

Read more...

BWANA ASIFIWE!

Bwana Asifiwe!Bwana Asifiwe! Amina!

Najiuliza tu hivi ni kweli Bwana anapenda asifiwe au kuna upungufu katika lugha?

Read more...

PUTIN SAFARINI AFRIKA-WADAI NI NEW SCRAMBLE FOR AFRICA
Putin akiwa na Waziri wa mambo ya nje wa Afrika kusini Nkosazana Dlamini-Zuma


Raisi wa China ameonekana barani Afrika hivi karibuni na sasa imefikia zamu ya Putin wa Rashia.Hizi ziara zimekuwa ziki ongelewa na kuchambuliwa katika Televisheni za ulaya. Lugha itumiwayo inanifanya nishangae na kujiuliza kuwa hivi hawa jamaa wanasahau kirahisi au wanataka kutuzingua tu!Hasa wanavyozungumzia mashwala ya utoaji malighafi Afrika kama vile ni jambo jipya au jambo ambalo lilikuwa limesitishwa .


Hu Jintao akiwa na Mugabe katika mchezo wake wa chesi ya kuendeleza matakwa yake Afrika

Ukiwa unafuatilia maswala ya bara la Afrika ,utagundua tokea enzi za ukoloni mpaka leo hali haijabadilika sana.Hapa nazungumzia maswala ya bara hili kutumiwa kama chanzo cha malighafi. Chakushangaza ukiwa una tazama habari katika Televisheni kama BBC siku hizi wameanza kudai kuwa eti hii ni new scramble for African Raw material.Ninajiuliza tu!Hivi ni lini mataifa ya nje yalisitisha kuchukua malighafi za Africa mpaka sasa hivi isemekane ni mambo yanaanza upya?

Natamani itakapofikia wakati Afrika itaweza kumiliki malighafi zake au kuwa kama Venezuela ambayo imeweza kumiliki malighafi zake chini ya Hugo Chavez. Cha muhimu inabidi kuzifanyia kazi malighafi zetu barani Afrika na kuuza mali zilizo kamilika.Hugo Chavez yeye hakubaliani na kuuza malighafi za nchi kiholela bila raia kufaidika.

Read more...

I HAVE BEEN TO TANZANIA. U HAVE BEAUTIFUL ANIMALS THERE!

>> Monday, September 04, 2006Tanzania is a beautiful country I have seen beautiful animals there. Is that all there is to see?
Halo!Kumbe wewe Mtanzania!Nimetembelea mara nne nchi yenu.Mna wanyama na mbuga nzuri sana nchini kwenu!Hii ni baadhi tu ya maoni ya baadhi ya Wazungu baada ya kugundua natokea Tanzania. Sikatai, Tanzania tuna wanyama pori wazuri. Na mbuga zetu zinavutia. Kinachonisikitisha ni ile baadhi ya watu kuona kuwa zaidi ya mbuga za wanyama basi Tanzania hakuna kitu kingine kifaacho kuitembelea.

Picha kama hizi ndio zilizomo vichwani mwa watu wengi kuhusu Afrika.Sio Wazungu tu bali watu wa mabara mbalimbali mpaka hata Wapakistani hawakawii kuhisi wao wameuchinja kuliko Waafrika.

Halafu hukawii kupitia sehemu nyingine ukakutana na mwingine naye akaanza yake. Mimi nimefika Tanzania mara nyingi sana katika miradi ya kusaidia wananchi.Unajua nchi yenu ina magonjwa sana. Ukimwi na umasikini umekithiri. Nawapenda sana Watanzania ndio maana kila siku najaribu kuja Tanzania kujaribu kusaidia. Mimi sikatai tunahitaji misaada. Magonjwa na umasikini vipo sana. Lakini kuna baadhi ya hawa watu wengi ambao hupenda kutuhubiria jinsi gani wanatusaidia bila kukiri kuwa wanajisaidia pia . Utakuta kwanza ni wao wanafaidika. Wengi wao hata katika jamii zao hawana kitu cha kujivunia. Kwa kuja katika jamii masikini Afrika inawasababisha wajisikie vizuri kwa kujiona kuwa pamoja na yote, bado maisha yao si mabaya.Wengine ni kazi tu .Na hata wengine wameanza kushikwa siku hizi kwa tabia zao mbaya mpaka za unajisi wa watoto wadogo nk.Tabia ambazo wanajua kuwa nirahisi kuziendeleza Afrika bila kushikwa.Rev. Bonnke akiokoa Waafrika


Nivigumu kuwasahau hawa wengine wanaokuja kutuhubiria dini. Utashangaa mikutano mikubwa ya wahubiri kutoka nje wakiubiri wakiwa na wakalimani wao huku kwetu. Unawezaukashangaa ukiona kuwa hawa watu ni mara chache sana waka hubiri katika nchi zao.Na wanafurahia wingi wa umati unaotoke kuja kuwashuhudi Afrika, kitu ambacho hakitoke kwao. Sasa je ni ukweli wanatupenda sisi zaidi kuliko watu wa nchi zao mpaka waje kutuhutubia sisi na sio watu wa nchi zao?
Baadhi ya watu wa maboti waliobahatika kufika hai Ulaya.


Cha kusikitisha ni kwamba kila siku katika Talevisheni zao siku hizi.Hasa katika mitaa ya ulaya imeongezeka sura moja. Hii ni ya watu kwenye ngalawa na viboti vya ajabu ajabu wakijaribu kukatiza bahari kwenda Spain kutoka Afrika magharibi.Kila siku utasikia wengine wamezama baharini,wengine wameenda kumwagwa jangwani na kadhalika.Hua mara nyingine hujiuliza hivi moyo kama wakufunga safari hizi za kufa nakupona ukiwekwa katika kitu kingine si tungekua mbali Afrika? Cha ajabu siku hizi bongo unakuta Wachina wakiuza mpaka machungwa wakati sisi tukijaribu sana kukimbia. Nikiangalia wasenegali wanavyozamia siachi kujiuliza maswali mengi tu. Hivi Watanzania karibu tutarudi katika maswala ya kuzamia meli kwenda Ulaya?

Read more...

Wamarekani weusi na Afrika!

>> Saturday, September 02, 2006

I aint going back to Africa!
Watu weusi bado tunahitaji watu wamfano. Watu wakujivunia. Bara la Afrika ni bara lenye mengi ya kujivunia.Ni kweli ukifuatilia habari nyingi duniani watu weusi ambao hupewa muda na nafasi ni wale ambao wana sifa mbaya. Bara la Afrika ni mara nyingi huambatanishwa na magonjwa, umasikini na sifa nyingine mbaya.Sasa hivi imefikia kuwa sisi weusi wenyewe kuliponda bara letu wenyewe.Katika mizunguko yangu nimekutana na wamarekani weusi wengi ambao hawakawii kuponda Waafrika na Afrika kwa ujumla. Hawakawii kulaumu kuwa tuliwauza enzi za utumwa.

Mimi naamini kuwa Waafrika wa Afrika tunatakiwa tuwemfano wa kueneza sifa nzuri za Afrika.Kama kuna Muafrika ambaye anatangaza Afrika vizuri kuliko wote basi anaweza kuwa ni Mandela. Lakini naamini kila mmoja anaweza kuchangia katika kuendeleza sifa za bara letu. Hawa wamarekani weusi wapondao Afrika huweza kuathiri sana Waafrika ambao wanawaheshimu na kuwachukulia wao kama mfana. Je ni kweli bara la Afrika linastahili tu kuwa chanzo cha matani na mapungufu tuu?Angalia jinsi ya mitazamo ya baadhi ya Wamarekani weusi hawa katika matani:


Eddy Muphy

Eddy Griffin

Jamie FoxxNingependa siku moja listi ya Greatmen kutoka Afrika iwe haihesabiki kutokana na wingi wa watu ambao wamefanya mambo makubwa Afrika.
Mwangalie Burning Spear akikuimbia wimbo Greatmen hapa

Read more...

KWA MPENZI HAUSIGELI!

Hivi ni kweli umempindua binamu kuwa nyama ya hamu?Nasikia siku hizi unapendeza tokea siku ya kwanza. Nasikia hautumii chupi za kitenge tena. Lakini je ni ukweli baba mwenye nyumba huku lazimisha utoe uroda mara mama mwenye nyumba aendapo kazini?Mpenzi hausigeli!Bado nasikia unaongoza katika kuwafunza watoto wa kiume wa mwenye nyumba maswala ya ngono.Nasikitika hawakupi shahada ya ukufunzi katika hilo. Je ni kweli wewe ni mwoga wa kushitaki polisi mambo ambayo hutendewa hapo majumbani? Je ni kweli haki zako hazifuatiliwi hapo majumbani?Je ni kweli kazi yako haitambuliki kitaifa? Mpenzi Hausigeli!Kama wewe ni kweli nyama ya hamu kwanini haujulikani kwa hilo!Mpenzi Hausigeli, sikuhizi kuna ukimwi hivyo nakuomba uripoti polisi kama unadhalilishwa. Mpenzi hausigeli ,kumbuka usipate mimba kwa maana mara nyingi penzi hufa mara upatapo mimba!Lakini Mpenzi , kama yote nayosikia ni kweli , naamini bado binamu ndio nyama ya hamu halisi. Nahisi wewe unalazimishwa tu kukizi hamu za watu. Kwa leo naishia hapa mpenzi.Usiwasalimie wenye nyumba. Kwa maana unakumbuka penzi letu ni la siri.
Wako,
Paskari

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP