Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Stereotaipu!

>> Monday, September 18, 2006




Posta la Minstrel shoo limuonyeshalo mtu mweusi kwa jicho la kizungu enzi hizo





Ukiwa unaangalia haya maswala ya steretaipu kama mtu mweusi, ni rahisi kusahau kuwa watu wengine nao wanalalamika mambo kibao. Nimegongana na atiko moja ambayo imenizingua sana.Hii ni ya maswala ya dunia iwaonavyo waislamu hasa katika maswala ya kuandamana mara wakisikia dini au Mtume kakashifiwa. Nafikiri hata hakuna haja ya kuelezea sana nini vyombo vya habari vya magharibi vinavyotaka tuamini kuhusu waislamu. Mambo kibao yalisemwa kitu ambacho kikanikumbusha ni jinsi gani wana dunia tunavyoweza kujitengenezea picha za watu wengine akilini.

Pia nilikutana na habari iliyoandikwa na kikundi kinachotetea muonekano wa Waitali. Hiki kikundi kinapinga mambo ya kufanya waitalia waonekane kama mamafia. Waitaliano ukiwa unawajua kwa kupitia sinema za holiwudi , basi utadhani wote ni Mamafia. Watu weusi huwa mara nyingi huwekwa katika kundi la wazembe. Wanaume weusi husifika kuwa wamebarikiwa ujazo kwenye sehemu za siri pia. Wanawake weusi ni mambo kibao, ukiachilia kuwa wamebarikiwa kimaumbile hasa sehemu za nyuma. Vile vile huwezi kusahau maswala yaliyoletwa na minstrel shows tokea enzi hizo za utumwa Marekani, wamishenari na wakoloni wengine Afrika.

Nikapitia tena habari nyingine za Waasia ambao wanaishi Marekani.Wao wanalalamika kwanini hata holiwudi hupenda kuwapa roli za udaktari au roli ambazo si babu kubwa.Wanalalamika kuwa mbona watu weusi siku hizi wanacheza roli zote mpaka za uraisi wa Marekani kwenye sinema, lakini hata Jackie Chan hapati roli ambazo anaweza kumpiga busu mwanamke wakizungu. Mimi binafsi kabla sijakutana na playboy wakichina hata sikumoja haikunijia akilini kuwa kuna mchina playboy.

Ukipitia katika tovuti za watu weupe kama hii hapa,, ambao wanachukia watu wa rangi nyingine, utakuta nao wanalalamika kuwa eti watu wote wengine wanaruhusiwa kuwa wabaguzi isipokuwa wao weupe tu ndio wanaonekana wabaya wakibagua au kustereotaipu.

Ukiachana na haya yote, utakuta sura za mtoto wa kiafrika afaye na njaa, maswala ya muafrika vitani na maswala ya waislamu yanatawala katika kipindi hiki.Ukiwa unaamini vyombo kama Televisheni huwezi kushangaa ukawa huamini kabisa kuwa Waislamu wanaweza wakawa watu wa amani.Lakini watu wanajua hata katika ukristo kuna kasheshe kibao ila ni vigumu kufananisha na jinsi waislamu wanavyoonyweshwa kwenye luninga.
Cha kujiuliza, ni nani afaidikaye na stereotaipu hizi?






Mwanamke mweusi ana stereotaipu ya kuwa ni kiboko kwa kunengua pia




Si ukweli kuwa stereotaipu hizi huwaumiza watu wote. Kuna akina Bert Wiliams ambao waliwahi kutengeneza karia na kulipwa sana kwakucheza roli wazungu walizopenda kumuhusisha mtu mweusi nazo. Ingawa pia inaaminika alisaidi kuchangia kuingia kwa watu weusi katika biashara ya burudani, swali ni, Je mtu mweusi amejikomboa katika hizi roli akina Bert Williams walizo anzisha?



Bert Williams , mtu mweusi ambaye alicheza utu weusi kama ulivyopendelewa na watu weupe







Je, mambo haya ya kustereotaipu watu yatasaidia kuiweka dunia kwenye amani?

Katika kipindi hiki ambacho naona vita imeondoka kutoka kuwalenga Warusi kuja kwa waislamu wenye imani kali, ningefurahi kuwa watu wakumbuke kuwa mara nyingi muonekano utolewao kwenye vyombo vya habari sio ukweli mzima.

Chakusikitisha ni kwamba bado muonekano wa watu weusi unahitaji ukarabati zaidi take tusitake.Ingawa akina Kofi Annan, kama alivyofanya Bert Williams wanacheza roli zao. Tunahitaji akina Mandela , akina Nyerere, na akina mimi na wewe kusaidia kufuta stereo type ya mtu mweusi kama ijulikanavyo sasa au kuigeuza iwe ni ile tunayoweza kujivunia.

Angalia mambo haya kwenye video hapo chini .Ingawa aliyeingiza muziki anafanya utani je wewe unahisi ujumbe wa video hii ni nini?


2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Jeff Msangi 9:04 pm  

Simon,
Lazima leo nikusifu kwa jinsi ambavyo hapa kwenye uwanja wako huwa hapaishi mijadala mizito.Kila nikikutembelea huwa najifunza mengi ambayo kama watu wangekuwa wanajali,basi tungefika mahala pazuri sana.

Umenikumbusha kitu kimoja ambacho siku za hivi karibuni hapa Canada kinazidi kushamiri.Kinaitwa reverse racism.Sisi weusi tunaambiwa kwamba siku hizi tunazidi kujichimbia huko kwenye ubaguzi kwa kubagua wenzetu.

Binafsi naamini kwamba kuna ukweli katika hiyo reverse racism.Sisi pia ni wabaguzi.Pengine sisi sio wabaguzi sana dhidi ya wazungu lakini ukiangalia kwa makini tunavyowaongelea wahindi,wachina,wajapan na wengineo utauona ukweli.

Cha msingi ni kama ulivyosema.Tuelimishane.

Simon Kitururu 12:05 am  

Nakubaliana kabisa nawewe Jeff. Ni rahisi kwetu kulaumu wengine , lakini tunacho hiki kitu.Stereotaipu zamakabila ndio usiseme! Kwa mfano kwetu enzi hizo Baba yangu anampeleka mama kumtambulisha kwa ndugu, wako ndugu waliokuwa wanataka kumtenga, kwanza kwa sababu yeye ni kabila jingine, pili kwasababu ni mweusi zaidi ukilinganisha na complexion za ndugu za baba. Sasa fikiria hii inatokea hata kwa weusi kwa weusi. Usianze sasa kuchokoza zile za mchaga mwizi na mpare bahiri ndio utachoka.Nakumbuka kuna kipindi kile Malecela alikuwa waziri mkuu, kuna washikaji walikuwa wanakataa kumsikiliza wakidai, huyo mgogo atatuambia nini!Haya mambo watu huwa hawayaongelei, ingawa yana athari zake katika utaifa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP