Yuko wapi Mwalimu wa kiafrika aliye wafunza mababu zetu?
>> Wednesday, September 13, 2006
Ni rahisi kuwa na maswali kuhusu matatizo ya Tanzania bila kuwa na majibu. Na kuna uwezekano wa kuwa na majibu ya maneno bila ya kuwa na ya vitendo. Na mara nyingi sana utasikia jibu kwamba elimu ndio suluhisho la matatizo mengi ya Tanzania. Kwa vitendo swala hili linafanyiwa kazi kwa kuongeza shule na walimu. Cha kusikitisha ni kwamba bado wakati tunasisitiza uongezwaji wa shule na walimu kuna sehemu tunaziacha wazi katika kuujenga uwezo wa kufikiri na wakutatua matatizo wa Mtanzania.
Kuna maswali haya ambayo inabidi yaangaliwe.
1.Je, watu wafundishwe wafikirie nini?
2.Je, wafundishwe jinsi ya kufikiria?
3.Je, waachiwe wajigundue wenyewe kwa ubunifu wao wenyewe?
Elimu ya asili ya Kitanzania ilikuwa inatolewa ilikuwezesha mtu kuweza kukabili maisha yake. Katika maswala ya Jando wanaume walifundishwa jinsi ya kuishi na kuyakabili maisha kama wanaume. Unyago ulimfunza mwanamke kuyakabili maisha kama mwanamke. Hii ni mifano tu ya karibu . Lakini elimu hii yetu ambayo tuliletewa, mwanzoni haikuandaliwa kutuwezesha kuyakabili maisha ambayo yalibadilishwa kwa uwepo kwa ukoloni. Cha zaidi yalikuwa yanalenga kutuwezesha kuwa watumishi wazuri ambao bado watakuwa wanatekeleza amri ya Watawala ambao hawakuwa Watanzania. Elimu ilikuwa ni ufunguo wa maisha ya kutumika na kujibu ndio mzee, na siyo yakufundisha kufikiria jinsi ya kutatua matatizo yetu wenyewe. Na hii si Tanzania tu.Afrika kusini walifikia kuhakikisha kuna kuwa na ufa mkubwa kati ya wazungu na waafrika ili kuhakikisha kuwa Mzungu atatawala, na mwafrika atatawaliwa.
Je, elimu ya Tanzania imebadilika tokea enzi za mkoloni?
Je, Mtanzania na elimu yake anauwezo gani wakuchangia katika maendeleo ya nchi?
Je, Watanzania hawaelimishwi sasa hivi ili kuchangia mafanikio ya uchumi wa nchi za nje na sio Tanzania yenyewe?
Inawezekana elimu yetu haina kasoro kubwa.
Sasa kwanini Mtanzania hata ambaye amemaliza chuo kikuu ni vigumu sana kuyakabili maisha ya Kitanzania?
Kama elimu ya zamani za mababu iliwawezesha kuyakabili maisha ya jamii katika kipindi hicho , basi elimu ya leo inatakiwa itufunze kuyakabili mazingira ya jamii hii ya leo.
Ni kweli ni vigumu kujitoa katika mfumo wa uchumi wa dunia. Hatuwezi kuikwepa elimu hii ya nje kirahisi. Ukiwaangalia wachina, tofautiyao ni kwamba wanajaribu kumjenga mwananchi kielimu ambayo itamfanya aajirike. Hawakazanii sana aende chuo kikuuu wala nini. Pia huakikisha wanajifunza kutoka katika wapevu na kuunyonya utaaluma wao pale wapatapo nafasi. Hii inasababisha wana lalamikiwa kuwa ni wezi wa taaluma. Lakini je si ndio maswala hayo hayo yanasababisha viwanda vingi viamishiwe kwao?Ka maana wapelekao viwanda wanakuta kuna watu ambao wanauwezo na taaluma ya kufanyakazi.Labda mtu atasema ni kwasababu ya wingi wao ndio maana kila mtu anakimbilia kufanya nao biashara. Lakini lazima ikubalike kuwa wanawaandaa wananchi wao sio kama Waingereza, wamarekani au Wajerumani wawaandavyo wananchi wao. Wanawaanda wakijua kuwa hawa ni wachina na katika mfumo unaowawezesha kujitatulia matatizo yao ndani ya nchi yao.
Basi ningependa elimu yetu itufunze jinsi ya kufikiri.Ningependa hata ituonyeshe ninini vya muhimu vya kulenga katika kufikiri. Ituwezeshe kufikia uwezo wakutatua matatizo yetu.Matatizo yetu iwe njaa, magonjwa au umasikini uliokithiri hivi sasa.
Nchi kama Tanzania haifai kukumbwa na njaa. Elimu za zama zilizopita ziliwawezesha mababu zetu enzi hizo kujua jinsi ya kusindika mazao. Ukaushaji wa mazao yetu , nyama, viazi, mihogo nk ilikuwa ni kawaida. Elimu yetu basi ituletee hekima za kuendeleza walipoishia mababu zetu. Ikibidi tujifunze kula hata nyoka kama wafanyavyo Wachina.Tujifunze kula hata mbwa kama wafanyavyo Wathailand.Lakini je hii ni lazima?.Kwanini tusijifunze kuwazalisha baadhi ya wanyama pori wasio adimika sana kama swala nk, kwa zumuni la kuwageuza wawe kitoweo cha kawaida cha Mtanzania? kwani nilazima nyama zisizokuwepo katika mataifa yalioendelea lazima zibakiwe na jina nyama pori?Kwa nini tusisikie NGO's zkishughulikia miradi mipya ya mambo mapiya ambayo ni uniq kwa Tanzania? Tunahitaji kufikiri kama walimu waliofundisha mababu zetu jinsi ya kuyakabili maisha.Inabidi tusiyatupe yote yetu mazuri ya kiafrika kwa kisingizio cha kwamba yamepitwa na wakati.Inabidi elimu yetu ya sasa itusaidie kubainisha yale ya zamani yatufaayo ilituyachanganye na ya sasa ili kujiokoa kama Watanzania.
Fela Kuti anakuambia Teachers don't teach me nonsense
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Usinifunze kabisa upuuzi, ewe mwalimu!
Post a Comment