Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wasichana wa Kiafrika!

>> Tuesday, September 12, 2006

Kuna watu wasemao kuwa mpaka nguvu ya wanaume ya utawala wa maswala ya jamii itakapotoweka na wanawake kushika hatamu, basi wanawake watatumiwa kama visafisha macho. Hivyo kutokana na ukweli kuwa wanawake ni viumbe vilivyobarikiwa uzuri na mvuto wa penzi basi basi wanaume watapenda kuwaona nusu uchi ilikukidhi haja zao. Hivyo itatafutwa kila sababu ya kuwezesha akinadada wakae nusu uchi kama uwaonavyo katika picha za hapo chini.















































Alek Wek mwanadada mrembo atokaye Sudan
















Vicky atokaye Cape Town Afrika kusini















Mwanadada mrembo Cynthia Masasi awakilishaye Tanzania katika fani.











Ila wengine wanasema ni wanaume ambao husababisha wanawake wavae kujifunika kila sehemu.

Kwa mtazammo wangu siamini kuwa kuna jambo linaloweza kuwa na jibu moja. naamini mtazamo wa jamii haujagundishwa na wala hauwezi kudumazwa. Hubadilika kutokana na mambo mengine yaiathiriyo jamii kijamii. Naamini kuwa hata maswala yakigeuka na ikawa ni wanawake waiendeshayo dunia, haitatokea kuwa ni wanawake wote watajifunika kama waonekanavyo madada wa kiislamu. Kwasababu si ukweli kuwa ni wote ambao wanapenda fasheni za nusu uchi sasa hivi wanalazimishwa kuvaa hivyo.Pia naamini binadamu hupenda kuvunja miiko. Ukimng'ang'aniza awe kitu fulani, mar nyingi ndio unampa nguvu ya kukipiga vita kitu hicho. Kuna wakati huwa nafikiria nguo zinapewa umuhimu kupita umuhimu wake hasa kwenye nchi za joto.
Siwezi kuachia bila kusema, JAMANI WANAWAKE NI WAZURI !






Wanawake wa kisomali katika nguo za nguvu.Kama unataka kuona figa basi ulie tu

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

mwandani 3:23 pm  

Kuna wakati niliwahi kumuuliza dada mmoja kwa nini alivaa nguo ilishonwa kwa kutumia kitambaa kidogo wakati uwezo wa kununua kitambaa kikubwa anao na washonaji pia wako wengi, akaniambia kuvaa nguo ndogo ni maamuzi siyo uchache wa pesa.

Miye nikamuuliza kuwa haoni vibaya kuwapa watu misuko suko mtaani, akadai ati kuwa yeye nguo fupi anavaa kwa ajili yake mwenyewe wala si kwa ajili ya kutesa watu mitaani. Wanaokodoa macho wana matatizo. Hata kama hakungekuwa na mwanamume duniani angejipendeza vile vile.

Maisha 6:02 pm  

halafu wanamsema cynthia...wakati utamaduni wenyewe ndio huuhuu wa kuvaa uchi....

Maisha 3:17 pm  

mwandani,huwa hiyo ndiyo excuse wanawake tunatumia.kuna poem moja mtoto mmoja aliisoma wakati tunafanya vagina monologues pale little theatre.pasrts of it go like this:

"y short skirt is not an invitation
a provocation or an indication
that i want or i give it or that i hook"

as much as i was for the vagina monologues i was against this poem.mitazamo kama hiyo ndiyo inaleta swali "nani alaumiwe?" pale mwanamke anapobakwa kwa sababu mwanaume alishindwa kujizuia kutokana na nguo dada aliyovaa.

huku ni kufumbia macho the obvious.while i agree there are maniacs out there who do not need a woman to be half dressed for them to rape them bado nadhani mtakubaliana nami kama wanaume kuwa mavazi yetu kina dada yanachangia kutamanisha wanaume.

huwa sipendi kuingiza mambo ya imani na dini lakini hapa ndio huwa nawaambia wakrosto wenzangu hata biblia inasema amwangaliae mke wa mwenzie na kumtamani amezini nae.je wewe mke wa mtu ukivaa kiguo chako cha kuaibisha halafu mume wa mtu akakutamani in the eyes of the almighty nani atahukumiwa?hapo ndipo tunapokumbuka kuwa hata edeni Mungu alimwambia Eva naitoa tamaa yako naiweka kwa mumeo na atakutawala.mwanaume ni kiumbe cha tamaa.mbona tunataka kufumbia macho hiyo fact?

inauzi kwa kweli...

Simon Kitururu 6:10 pm  

Huwa sipenndi kuongelea mambo ambayo sina uhakika kwa mfano mambo ya hisia za mwanamke. Ila nilikuwa na cheki mjadala wa wasenge kwenye TV .Wakaulizwa kwanini wasenge ni rahisi kufanya mapenzi na watu wasio wajua kirahisi kuliko watu straight? Msenge mmoja akajibu ni kwa sababu wanawake ni wagumu kutoa penzi kutokana na tamaa hafifu ya ngono ukilinganisha na wanaume. Lakini hiki kitu sina uhakika nacho sana kwa maana nawajua wasichana ambao unaweza kutishika kwa jinsi wanavyotoa ngono. Halafu sizungumzii ngono ya kulipia hapo!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP