Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

David Mwanaka -Mzimbabwe Mweusi' alimaye mahindi Uingereza!

>> Friday, July 14, 2006

Je umemsikia David Mwanaka ?Mkulima huyu ananizingua sana.Manayake anafanyakinyume cha wale Wazungu wa Zimbabwe Uingereza. Msome hapa

Read more...

AlQaiDa/Talibani mbaya lakini......

>> Friday, July 07, 2006

Kwa wale wasafiri wa anga za magaribi miaka mingi watakubaliana na mimi. Enzi hizo Mtu mweusi alikuwa ndio mtu mbaya mipakani. Madawa na kila uhalifu walikuwa wanaoanisha na rangi nyeusi mipakani mwa nchi za viwanja vya juu. Siku hizi angalau Waarabu na Waislamu weupe wenye madevu marefu wanasaidi watu weusi tupite kirahisi kidogo.Hata Rasta kama mimi Mara kibao au karibu zote nakatiza tu siku hizi.

Read more...

Biblia imetafsiriwa Kiafrika!

Nimecheki BBC wananiambia Biblia imetafsiriwa kiafrika na imevunjwa bikira hapo kenya .Kongoli hapa basi usome habari hiyo.Ila Kama umeshaisoma Biblia hiyo tupashe basi. Bwaya Upo?
Sasa hivi ina semekana katika Afrika ni Pentekoste na makanisa ya kiavenjeliko ndio yanayoongoza kukua Afrika.Kongoli hapa kushuhudia. mimi nachojiuliza nikwamba kwanini makanisa na wainjili kutoka Ulaya wanakazania kwenda Afrika wakati huku kwao ulaya siwaoni wakihubiri kwa hawa Waulaya ambao wengi wao hata Mungu hawaamini tena. Mwandani niambie huko Australia Ukristo Unaanguvu?

Read more...

Shikamoo Mwalimu!

Nilivyokuwa mtoto niliamini Watu wazima wanajua kila kitu. Niliamini hata hawaanguki. Watu wazima kama wazazi niliamini ndio kila kitu duniani wanajua.Ni mambo mengi wanatufundisha lakini tukifikia kuamini kila kitu wanajua basi tumepotea. Sasa baada ya kukua na kuingia duniani kisawasawa nashangaa kukutana na watu bado wanaamini mtu akiitwa profesa anajua kila kitu. Watu wanasahau kuwa kila binadamu ana mipaka yake. Au una fikiri Profesa Lipumba anaweza kutibu mifupa kama profesa Sarungi?

Read more...

Hivi Baiskeli Weusi hatuwezi Kuendesha?

Nilikuwa naangalia Tour de France! Sioni hata mweusi mmoja.Hakuna katika timu ya Marekani wala sehemu yoyote ya dunia hii mtu mweusi akiendesha baiskeli hata kwa kuwakilisha tu. Je, ni kweli hatuwezi kuendesha Baiskeli? Nimemkumbuka Madenge alikuwa anaendesha baiskeli mpaka za miti.nimekumbuka kuwa ni mwaka huu tu Nascar kumepatikana dereva wa kwanza mweusi. Monfils na akina Wiliams sisters wanawakilisha weusi katika Tenis.Sasa jamani baiskeli vipi?

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP