Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Heri ya Mwaka mpya wa Kalenda ya Kirumi!

>> Sunday, December 31, 2006Katika siku hii heshima yangu kwa wanawake wote!Mama yangu Zilpah Asante kwa yote! Namuachia Shaggy aelezee kwenye wimbo Strength of a woman....


Kwa wengine nawaaga mwaka huu kwa wimbo huu wa Capleton...

Read more...

Dini au Utaifa kwanza?

>> Saturday, December 30, 2006


Hivi wewe ni Muislamu au Mkristo kwanza halafu ndio Mtanzania au ni Mtanzania kwanza halafu ndio mpagani?
Nauliza tu, usitishike!

Read more...

Chakula cha Mawazo-Biblia !


Katika vitabu ninavyovipenda kimoja wapo ni biblia. Leo naendelea kusoma historia ya kitabu hiki kama nilivyosema kwenye video hapo juu.Nitaandika zaidi siku nyingine lakini kwa kifupi historia ya kitabu hiki huwa inanizingua sana .Najaribu kukisoma na kuendelea kujifunza kutoka kwa watu wengine wengi . Na kila mara nakutana na watu wengi wenye maelezo tofautitofauti wakiwamo hawa hapa chini...

na mwingine huyu hapa..


Pia ningeomba mtu mwenye data nzuri za kuaminika kuhusu historia ya Kuran zaidi ya hii hapa anisaidie dondoo za vitabu au sehemu nayoweza kujenga picha zaidi ya jinsi kilivyoandikwa na kutunzwa mpaka sasa.Ningependa zaidi kujua histori ya jinsi maandishi yalivyokuwa yanaandikwa au kukaririwa katika kipindi Quran ilipoandikwa.
Nakuacha na Injili ya Yuda hapo chini, wakati nikiendelea kutafakari kasoro na upungufu wa kiubinadamu unaotukabili sisi wanadamu.

Read more...

Wakati tukondani ya KWANZAA na tukisubiri Mwaka mpya wa Kalenda ya Kirumi...

>> Thursday, December 28, 2006


Kabla sijasema sana ningependa kuachia The Last Poets wamwage shairi....


Watu weusi bado tumegawanyika sana.Moja ya mgawanyiko ni ule wa Weusi wa Afrika na weusi wenye asili ya Afrika ambao kuwako kwao mbali na Afrika ni matunda ya utumwa, na wengine ambao walihama wenyewe. Waafrika ndani ya Afrika bado tumegawanyika sana pia, kimakabila , kidini,kiutajiri au umaskini na mambo mengine kemukemu ikiwa mpaka rangi.Unakumbuka katika kundi la watu weusi bado tunabaguana kwa rangi , nani mweupe na nani mweusi? Watu weusi waishio mabara mengine nao wamegawanyika kwa hali ya mali,elimu na hata jinsi ya toni za mwonekano wa rangi ya weusi wao . Marekani na sehemu nyingi bado ile hali iliofanya watumwa weupeweupe kupewa kazi za ndani na wale weusi kabisa kazi za nje bado upo.Hivyo bado wale weupe weupe mara nyingi huonekana wazuri kuliko weusi kabisa. Hiki kitu ndio kile kile kinachofanya akina dada kujichubua Afrika katika kutafuta kuwa weupe weupe kwa imani ya kuwa ndio uzuri. Hivi uzuri ndio nini?Haya mambo ambayo binadamu anajitengenezea akilini na kutengeneza mazingira ya kuhalalisha mtazamo yanazingua sana.

Binadamu ni kiumbe wa ajabu sana! Kila wakati na kila siku yuko shuleni. Anajifunza ladha na anajifunza kuishi katika mazingira yake. Ndio maana kila siku utasikia, alah! Hiyo fasheni imepitwa na wakati! Halafu ghafla atakuambia nilipoonja bia kwa mara ya kwanza sikupenda ladha yake.Wakati yeye ndiye ajulikanaye kwa unywaji wa bia. Binadamu huyo huyo katika kutafuta kujiridhisha huwa anapenda kujifananisha na wenzake na kujipima kupitia wenzake. Hii pamoja na kujipatia furaha pia huleta mikwaruzo ndani ya jamii.Mikwazuzo hii hutugawa lakini pia kutujenga.Tatizo letu watu weusi bado tumeshindwa kuunganisha nguvu zetu na mikwaruzo yetu inatubomoa zaidi yakutuletea changa moto zakutujenga.


Tukirudi kwenye KWANZAA, mimi naona ni moja ya jambo ambalo pamoja na mengine linajaribu kuunganisha watu weusi. Na nafikiri jambo lolote liunganishalo watu weusi wenye asili ya Afrika ni jambo muhimu kwa sababu umoja tuna uhitaji sana sisi kama watu weusi.Vizazi vijavyo vya watu weusi vitashindwa kutuelewa ni namna gani Afrika pamoja na mali zetu bado tumefanikiwa kuwa masikini na wanyonge hivi.Kizazi chetu hiki tu bado tuna maswali ilikuwaje wakoloni wachache waliweza kututawala .Unakumbuka tulikuwa tunawabeba kuwasafirisha maporini? Unakumbuka mara nyingi ilikuwa waafrika wanne wanambeba mzungu mmoja na anatoa amri hata huko msituni, huku watu wakitii?Sasa fikiria baada ya miaka kadhaa sisi ndio tutakuwa somo.Vizazi vijavyo watajiuliza, hivi hawajamaa vipi? Kila siku kugombana tu huku wakijua maugomvi yao yananufaisha wengine.

Sasa hivi kuna Wamarekani weusi watambuao umuhimu wa Afrika katika maisha yao lakini wapo wengi wachukiao Afrika na waafrika.Wao kwa wao hawana umoja , wamegawanyika hadi kwenye maadili.Waangalie wengine hawa hapa wakijielezea....


Nasi Afrika hatujakuwa mfano mzuri wakujivunia. Na katika hili na kubaliana na wale wanaoenzi nguzo saba za kwanzaa ambao wanatafuta maadili kutoka Afrika ilikujisikia kamili.Kwani hata kwa hili kuna kaumoja kanajengeka. Kumbukeni kama watu weusi ni miaka mingi imepita bila kula raha na kufurahia uweusi wetu.Ngoja Mighty Diamond wakukumbushe hapa chini...Sasa mimi na wewe tunafanyanini katika kuleta mikwaruzo yetu na tofauti zetu kama watu weusi iwe inatujenga zaidi ya kutubomoa?

Samahani nilisahau kuwa bado tuko katika shamra shamra za KWANZAA, kusubiri mwaka mpya na kadhalika nyingi!Haya basi tuendelee kufurahi. Nakuacha na Lagbaja hapa chini.


Heri ya KWANZAA!

Read more...

Bado Mawazoni!

>> Tuesday, December 26, 2006
Leo nasikiliza sana Zouk, kama za Kassav hawa hapa chini.....lakini pia mdundiko na nyimbo mbalimbali nazipitia pia ingawa wimbo huu hapa chini uitwao Kiuno Viuno unanifikirisha kidogo!Hii sio kutiana majaribuni?

Read more...

Nafikiria nini kuhusu Krismasi na Mwaka Mpya!

>> Monday, December 25, 2006


Nafikiri binadamu mara nyingi hutafuta sababu ya kusherehekea.Hii ni kawaida.Tanzania katika mila zetu utakuta sherehe hizi nyingi tu. Kuhusu Krismas kama siku ya kusherehekea kuzaliwa kwa yesu ni tarehe iliyo buniwa tu. Tafiti nyingi zinadai kuwa kwa kufuata kalenda tuitumiayo na mambo mengi yaliotokea kipindi cha kuzaliwa kwa yesu inawezekana kabisa ikawa Aprili ndio kipindi.Hata hivyo hakuna uhakika asilimia mia wa siku hiyo.Na nukuu nyingi hizi zilizoko kwenye biblia ziliandikwa miaka mingi baada ya kufariki kwa yesu.

Kuhusu mwaka mpya ndio hivyo tena ukifuatilia historia ya kalenda na ukajiuliza kwanini watu wengi walikuwa na kalenda tofautitofauti, na bado wana kalenda tofautitofauti utapata jibu.

Kuhusu Santa Klaus au Saint Nicholaus- askofu wa mji wa Myra,Uturuki na kuibiwa na Waitaliano waliomhamishia mji wa Bari na kuingia dili na kanisa ilikukuza utalii kwa kumtangaza. NAfikiri unajua nafikiria nini. Lakini Cocacola Kampani ilimtafutia vazi zuri ilikupendeza akitangaza Coca cola.

Tukiachana na hilo, nadhani asilimia kubwa yetu tunapenda sherehe na tunapenda zawadi.Nafikiri hakuna haja ya kufuatilia sana mambo haya maana utaondoa utamu wa sherehe yako. Heri ya Krismas na Mwaka Mpya, lakini kumbuka siku ya krismas na mwaka mpya zaweza kuwa ni siku yoyote ile uamkapo, na hizi siku tusheherekeazo ni binadamu kama mimi na wewe waliozitunga.

Read more...

Wakati bado Soul na Funk ikiniburudisha- Hello Brother Curtis Mayfield!

Brother Curtis Mayfield Semanaye basi!

Superfly!
Move on Up!

Read more...

James Brown afariki!


Mzee James Brown ndio kaanza hivyo. Mimi kama mpenzi wa Soul , Funk amekuwa akiniburudisha muda mzefu tu. Uwezi pia kusahau mchango wake kwenye Hiphop na miziki mingine.Mzee kafariki akiwa na umri wa miaka 73 baada ya kupata nimonia.Pumzika Mzee!

Hapa Chini mwaka 1966 akikupa zile nyimbo zake. Baba ana mkoba mpya na pia ule wimbo najisikia vizuri


Hapa chini katika mwaka 1966 vilevile akinipa nyimbo kadhaa ukiwamo ule utukumbushao kuwa leo inawezekana ikawa ni siku yetu ya mwisho kuwasiliana ,kusalimiana, kushikana mikono na kadhalika. Duh unajua hii leo inawezakuwa siku ya mwisho kwetu wote?Samahani nilio wakosea na nimewasamehe mlionikosea.Kama hatukutani tena bye bye!

Read more...

Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya!


Read more...

Leo Mawazoni-Tanzania hali ni mbaya haikubaliki

>> Wednesday, December 20, 2006


Sitaki hata kuongelea hili swala kwasababu Mwandani kaliongelea vyema na yeyote ambaye hajamsoma Eldridge Cleaver namshauri amsome.Lakini ukitaka kufaidi anayosema usiishie kusoma historia yake Eldridge tu.

Read more...

Sanaa Babu kubwa!

>> Tuesday, December 19, 2006

Ijumaa iliyopita nilipata kushuhudia bomba ya kazi ya sanaa iliyofanikishwa na Wasanii wa kitanzania Arnord Chiwalala, Menard Mponda na Aliko Mwakanjuki. Hii kazi ya kimataifa ilihusisha Tanzania na Umataifa kwa namna ambayo ukitaka kuelewa kongoli hapa. Nitaipandisha kwenye blogu baadaye.Kutokana na matatizo ya kitekinolojia ndio maana haijapanda bado.Halafu kongoli watch the recorded broadcast in Real Player

Read more...

Cola za Kiislam VS Coca Cola.

>> Tuesday, December 12, 2006

Inanizingua sana mara nyingine ninavyostukia jinsi gani mazingira ya vita yanavyoweza kuzua aidia za biashara.Leo nimeamua kuangalia jinsi mazingira ya vita yanavyo neemesha biashara za cola.

Miaka ya themani mpaka tisini kulikuwa na vita ya Cola (Cola War) ambayo ilihusisha Coca Cola na Pepsi. Hii ilisababisha Cola hizi mbili kutangazwa kupita kiasi, hivyo kuuzwa sana.

Sasa hivi kuna vita ya Cola ambayo inaibuka ihusishazo Cola ziuzwazo kwa malengo ya kupiga vita utawala wa vinywaji vya Cola kutoka Marekani na pia maadili yake. Vinywaji kama Qibla Cola , Mecca Cola na Zam Zam Cola ambavyo vimeanzishwa na kuwalenga zaidi waislamu ni miongoni tu mwa vinywaji hivi.Nawasifu wabunifu wa miradi hii ambayo inakusudia kutumia asilimia kadhaa ya faida itokanayo na mauzo ya vinywaji hivi kusaidia Jamii zao.

Coca Cola katika tangazo mwaka 1917


Ukifuatilia kinywaji cha Coca Cola utagundua jinsi asilimia kubwa ya ukuaji na utawanyikaji wa kinywaji hiki ulivyo saidiwa na vita. Kinywaji hiki ambacho mwanzo wake kilitumia malighafi kadhaa ikiwamo cocaine hapo kitambo , ndio kinywaji cha kola maarufu kupita vyote mpaka sasa. Vita kuu ya pili ya dunia ilisaidia kukitawanya kinywaji hiki baada ya mwenye kiwanda kukubaliana na serikali ya marekani ku peleka kinywaji hiki kwa wanajeshi wakimarekani popote walipo duniani na kwa kufanya hivyo kiwanda hakitahusishwa katika mgao maalumu wa sukari ambao ulikuwepo Marekani kutokana na upungufu wa sukari.


Vita vilisababisha uanzishaji wa viwanda sehemu mbalimbali duniani ilikukidhi mahitaji ya kinywaji hiki kwa wanajeshi.Na pale vita vilivyozua kasheshe nchini Ujerumani hivyo Kiwanda cha Coca Cola kikaanzisha Fanta pale Ujerumani. Hivyo utaona kuwa kutokana na vita Fanta ikazaliwa.


Mecca Cola na muanzilishi wake Mr Tawfik Mathlouthi
Sasa leo hii tuko katika vita vyingine ambavyo vinaleta msuguano kati ya nchi za magharibi na za Kiislam.Na hii vita inaonyesha kuzalisha wanunuzi wapya wa vinywaji vipya na kwa asilimia kubwa si kwa sababu ya utamu wa vinywaji hivi, bali maadili yahusishwayo na vinywaji hivi.
Qibla Cola

Vinywaji hivi kama Mecca Cola, Qibla Cola , Zam Zam Cola nk, vinafanikiwa sana katika jamii wazilengazo. Inasemekana watengenezaji wa Mecca Cola walishawahi kulalamika kuwa katika soko la Uingereza wanapata tabu kutokana na kuwepo kwa Wapakistani wengi ambao hupendelea Qibla Cola ambayo hutengenezwa na Wapakistani.

Zam Zam Cola


Nachojiuliza tu ni kwamba je hii staili ya kuvitangaza kwa kuvihusisha na dini itafaa katika muda mrefu?Nashangaa kwanini kampuni zitengenezavyo vinywaji hivi haviungani ilikuwa na nguvu zaidi ya kupambana na Coca cola?Au ndio ushindani wa kibiashara utakaoleta ubora katika kampuni hizi?Kama ndio hivyo hii si ndio ileile filosofia ya kimagharibi ambayo Coca Cola inaindeleza?


Je, na Afrika tunahitaji kinywaji chetu cha Cola ambacho kwa kukinywa tutakuwa tunajua kuwa pasenti fulani inaenda kusaidia Afrika?

Read more...

Kutoka mdomoni mwa Spika wa Bunge la Tanzania

>> Tuesday, December 05, 2006

Wiki kadhaa zilizopita nilipata kusikia hoja moja kwa moja kutoka mdomoni mwa Spika wa Bunge, Mzee Samwel Sitta. Kuna mengi aliongelea. Ingawa pia kuna mengi hakuweza kuyaongelea kutokana na muda mdogo uliokuwepo na maswala na maswali kuwa mengi.

Aliongelea umeme. Akasema kuwa sasa hivi ndani ya Tanzania kuna mpango wakutumia nyanja tatu za uzalishaji wa umeme. Kuna Wachina ambao wataanza kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe katika sehemu mbili tofauti Tanzania.Pia kuna mpango wa kuongeza sehemu moja ya uzalishaji wa umeme kwa maji.Umeme wa gesi unafanyiwa mpango kuingizwa katika mfumo pia. Kwa kifupi kuhusu mashine mpya za dharura ziletazo majadiliano mengi mtandaoni amesema zinahitajika na pia kuwa bila mashine hizi za muda sehemu kama za Mwanza zingekuwa zinakosa umeme masaa ishirini na nne.

Kuhusu matatizo ya Zanzibar alisema tatizo kubwa liko katika uhasama uliojengeka kabla na baada ya mapinduzi. Asilimia kubwa ya wenye asili ya kiarabu au kipeshia ndio waliokimbia visiwa baada ya mapinduzi. Na wengi wao ,takribani laki tatu wako Uarabuni. Hawa na ndugu zao ndio wenye pesa na elimu. Maana hawa ndio walioweza kuwasomesha ndugu zao visiwani na hata nje. Lakini hawa ndio ambao wanachuki juu ya yaliyotendeka baada ya mapinduzi. Baadhi yao walilazimika kuolewa na wasiowapenda hata kuzalishwa na wasiowapenda. Sasa hivi wengi wao ndio wako katika upinzani visiwani.Kwa mtazamo wa Spika hawa jamaa hatakama wanaona ukweli wa mambo hawawezi kuukubali kwani bado yale machungu yayaliowatokea bado yapo ndani ya jamii yao. Hivyo ni vigumu kudili nao kwani mara nyingi ni machungu ya kihistoria ya wapandishayo mori na sio hali halisi ya mambo.

Kuhusu Umoja wa Afrika Mashariki , yeye anaona hakuna haja ya Watanzania kuuogopa muungano. Alisema kunanjia nyingi za kisheria ambazo zitawalinda Watanzania katika mambo mengi. Anasema kuwa kwa mfano ndani ya muungano kutakuwa na sheria kama za kuzuia asiyekuwa Mtanzannia kumiliki ardhi Tanzania nk.Alisisitizia kuwa tunahitaji kuungana ililikukuza soko la Afrika Mashariki kwani tukijitenga ni vigumu kuvutia wawekezaji wenye kuvutiwa na soko na pia itasaidia kujengea wanaafrika mashariki soko kubwa zaidi la bidhaa zao.

Aligusia pia maswala ya Watanzania waishio ughaibuni na maswala ya usalama wao. Anasemakuwa serekali inajua matatizo ya Watanzania Ughaibuni na inayafanyia kazi. Anasema baadhi ya misiba iliyotokea Ughaibuni ilipewa hadhi iliyokaribia ya msiba wa kitaifa Tanzania. Alisisitiza watu kujisajili kwenye mabalozi yao ilikuwezesha baadhi ya mambo yawe rahisi kwa balozi kushughulikia.Alisema serikali inafuatilia vifo na matatizo ya Watanzania ughaibuni.

Kuhusu wawekezaji wa Kiafrika kusini alidai kuwa si kweli kuwa wao ni wabaya. Alidai matatizo mengi ya kibiashara na dhuluma za kibiashara hufanywa na wahindi.Alisema kuwa kwanza mfumo uingizwawo na waafrika kusini unasaidia kurekebisha biashara. Kwa mara ya kwanza unaweza kupata uhakika wa bei za vitu na pia wameleta utumiaji wa viwango vya ubora wa bidhaa ndani ya biashara Tanzania. Anasema si kweli kuwa Waafrika kusini hawanunui bidhaa za Tanzania. Anasema wao hutoa viwango vya ubora wa bidhaa watakazo kuzinunua. Katika mazao hutoa mpaka aina za mbegu za vyakula watakavyo kuviuza. Na watanzania wote wafikiao viwango vitakiwavyo ,bidhaa zao huingizwa dukani.Alisema kuna tatizo sana kwa wahindi kufanya biashara chini ya meza na kupeleka pesa nchi za nje.

Haya ni baadhi tu ya aliyo yasema muheshimiwa.Maswali mengi hakujibu kutokana na muda.Nikikumbuka mengine aliyoongelea nitayaandika hapa.

Read more...

Baada ya mafanikio ya Asia je, ni Afrika iatakayofuata?


Hakuna ujanja, baada ya Asia itakuwa ni zamu ya Afrika.Huu ndio mtazamo wangu.Kwa jinsi uchumi wa Asia unavyokua ni rahisi kujua kuwa na gharama za uzalishaji wa bidhaa zifanyazo makampuni mengi yaende Asia kuongezeka. Na kama kawaida ya mfumo wa biashara ulioshamiri duniani lifuatalo ni wawekezaji kukimbilia katika sehemu ambazo wanaweza kuzalisha bidhaa zao kwa bei ya chini. Sehemu ambayo haijatumiwa kisawasawa katika uzalishaji mali ni Afrika. Asia ilipata umaarufu kama sehemu ya kuzalisha mali kwa sababu kubwa mbili,unafuu wa gharama za uzalishaji na pili, uwepo wa wafanyakazi wenye taaluma za kazi.Ingawa pia huwezi kupuuzia nguvu ya idadi ya watu waishio Asia ivutiayo wawekezaji kwa sababu ya soko kubwa.

Tatizo kubwa la Afrika ni ukosekanaji wa wafanyakazi wenye taaluma za kazi.Ukosefu wa mfumo uelewekao uwezeshao mambo kufanyika. Hapa na maanisha udhaifu wa institutions na mifumo iwezeshayo mambo kufanyika. Tatizo la nishati za umeme ziwezeshazo uendeshaji wa viwanda.Ukosefu wa nguvu za ununuzi kutokana na umasikini wa watu.Haya ni baadhi tu ya mambo yatatizayo. Lakini, bado kila kukicha utakutakuwa inakaribia siku ambayo dunia haitakuwa naujanja wa kukwepa Afrika kwani ,Afrika inazidi kuwa ndio sehemu itakayo kuwa inatoa faida zaidi katika mitaji ya wawekezaji.

Inashangaza jinsi viongozi wetu Afrika wanavyoweka umuhimu wa mambo gani yatendeke ili kuboresha nchi zao. Unakuta kiongozi anazunguka dunia kutafuta wawekezaji katika viwanda wakati anajua wawekezaji hao hawawezi kufanya lolote bila ya nishati ya umeme. Mifano ipo mingi tu ambayo hata haileweki kuwa hawa viongozi wetu wanafikiria nini.

Si ajabu sasa hivi kuona Wachina wakihamia Tanzania ingawa kwao Uchina ndio wawekezaji wengi wa kimataifa bado wanakimbilia. Hii ni moja tu ya kidokezo kuwa tabaka la wenye navyo Uchina linazidi kuongezeka hivyo wengine inabidi wakimbilie sehemu ambazo wanaweza kujishamirisha bila kuwa na mtaji mkubwa.Pamoja na sera za serikali kusababisha hili kuwezekana sasa, lakini ukweli kwamba hili ni jambo ambalo imefikia kipindi chake kutokea hasa ukiangalia mwelekeo wa uchumi dunia nzima.Ukiangalia hata mwelekeo wa nguvu za nchi ziendeshazo mifumo iliyojengeka duniani zinavyobadilika utapata dondoo nyingine.

Sitaki kuusifu huu mfumo wa kibepari ambao umetunyonya kwa mamia ya miaka, lakini najua mfumo huu unakasumba moja, nayo ni kwamba hufikia wakati mewnye nguvu anakuwa hana uwezo tena wa kutawala mwelekeo wa mfumo. Kwa mfano kuna savei nyingi zioneshazo kuwa asilimia mpaka 60% za Waulaya na Wamarekani wanatishika na ukuaji wa uchumi wa nchi kama Uchina, lakini hakuna ujanja wawezao kuufanya kujitoa katika mahusiano na na nchi hizi sasa hivi. Kwani Wachina wameweza kuwazidi kete katika mchezo wao wenyewe.

Mifumo iundwayo na binadamu mimi naamini huweza kuchezewa kete na binadamu. Ukiangalia maswala ya demokrasia, imedhihirika mara kibao kuwa ilikuwa sio nia ya waihubiriyo baada ya walengwa kuitumia kwa kuchaga kidemokrasia maswala ambayo wahubiri hawakuya dhamiria.Mfano kidemokrasia , Wapalestina wakachagua Hamas jambo ambalo ilikuwa si nia ya Marekani kuhubiri demokrasia itakayo chagua maadui zao. Hili limetokea Venezuela pia baada ya Chavez kushinda tena. Naamini sio demokrasi tu zinaweza kutoa jawabu kinyume bali hata maswala mengine. HAPA NA MAANISHA INGAWA WANAOTULENGA AFRIKA WANATULENGA ILIKUTUNYONYA TWAWEZA KUWAGEUZIA KIBAO WAKAJAKUJIKUTA KUWA SISI NDIO TUMEWAZIDI TUKITUMIA AKILI.Itafurahisha siku tukifikia sehemu China waliyofikia ambapo hakuna ujanja nchi nyingine zawezakuwaletea bali kudili nao tu, hata ikiwa kwa shingo upande.

Afrika na pamoja na umasikini wa serekali zetu hatuwezi kujitoa kirahisi katika mfumo.Bado asilimia kubwa za pesa ziendeshayo shughuli Afrika ni tupewazo na wamagharibi. Mpaka uendeshaji wa Afrika Union unashindikana kutokana na ukosefu wa pesa na kila ukifanikiwa ni kwasababu kunamfadhili katoa pesa.Sasa tuna taratibu gani au strateji gani zitakazo tupa nguvu ya kuja kuzishika nyenzo za kiuchumi za nchi zetu?Je , mipango hii tuwekayo inatazama mbele? Au ndio kama maswala ya umeme?Kwa maana maswala yaumeme hayakupewa mstari wa mbele kama maswala ya rada na ndege ya Raisi. Je, Viongozi wetu wanaona mbele?

Read more...

Vyakula vipo duniani, mbona twafa njaa?-----Na .1Konokono huyu kanona!

Konokono huliwa sehemu nyingi lakini ni maarufu zaidi Ufaransa , Uspain ,Italy na Ureno. Afrika kusini kwa sasa ndio inaongoza katika nchi za Afrika katika biashara ya kimataifa ya konokono. Ushawasikia wakinamama hawa wa Western Cape township walivyojiajiri katika maswala ya kukusanya konokono?Kwa habari zaidi kuhusu kama unadhurika (allergy) kivyovyote kuhusu msosi huu soma hapa

Chura aliye nona kabla ya kuingizwa jikoni.


Kwa habari zaidi kuhusu msosi wa chura na kama unazurika naye (allergy) soma hapa


Chura hawa washaiva , karibuni mezani.

Panzi ni msosi babu kubwaNyoka ni msosi mahali pengi.King Cobra pichani ni miongoni mwa nyoka ambao katika mitaa ya nchi kama Thailand, damu yake pia ni kinywaji kiaminiwacho kuongeza nguvu za tendo la mapenzi na pia dawa kwa magonjwa


Bado najiuliza, nini kinasababisha tufe njaa Tanzania ?Kwa maana sidhani hata inahitaji kuangaika sana kutafuta mnyama, mdudu, ndege nk ambaye analika.

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP