Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Cola za Kiislam VS Coca Cola.

>> Tuesday, December 12, 2006

Inanizingua sana mara nyingine ninavyostukia jinsi gani mazingira ya vita yanavyoweza kuzua aidia za biashara.Leo nimeamua kuangalia jinsi mazingira ya vita yanavyo neemesha biashara za cola.

Miaka ya themani mpaka tisini kulikuwa na vita ya Cola (Cola War) ambayo ilihusisha Coca Cola na Pepsi. Hii ilisababisha Cola hizi mbili kutangazwa kupita kiasi, hivyo kuuzwa sana.

Sasa hivi kuna vita ya Cola ambayo inaibuka ihusishazo Cola ziuzwazo kwa malengo ya kupiga vita utawala wa vinywaji vya Cola kutoka Marekani na pia maadili yake. Vinywaji kama Qibla Cola , Mecca Cola na Zam Zam Cola ambavyo vimeanzishwa na kuwalenga zaidi waislamu ni miongoni tu mwa vinywaji hivi.Nawasifu wabunifu wa miradi hii ambayo inakusudia kutumia asilimia kadhaa ya faida itokanayo na mauzo ya vinywaji hivi kusaidia Jamii zao.

Coca Cola katika tangazo mwaka 1917






Ukifuatilia kinywaji cha Coca Cola utagundua jinsi asilimia kubwa ya ukuaji na utawanyikaji wa kinywaji hiki ulivyo saidiwa na vita. Kinywaji hiki ambacho mwanzo wake kilitumia malighafi kadhaa ikiwamo cocaine hapo kitambo , ndio kinywaji cha kola maarufu kupita vyote mpaka sasa. Vita kuu ya pili ya dunia ilisaidia kukitawanya kinywaji hiki baada ya mwenye kiwanda kukubaliana na serikali ya marekani ku peleka kinywaji hiki kwa wanajeshi wakimarekani popote walipo duniani na kwa kufanya hivyo kiwanda hakitahusishwa katika mgao maalumu wa sukari ambao ulikuwepo Marekani kutokana na upungufu wa sukari.


Vita vilisababisha uanzishaji wa viwanda sehemu mbalimbali duniani ilikukidhi mahitaji ya kinywaji hiki kwa wanajeshi.Na pale vita vilivyozua kasheshe nchini Ujerumani hivyo Kiwanda cha Coca Cola kikaanzisha Fanta pale Ujerumani. Hivyo utaona kuwa kutokana na vita Fanta ikazaliwa.


Mecca Cola na muanzilishi wake Mr Tawfik Mathlouthi












Sasa leo hii tuko katika vita vyingine ambavyo vinaleta msuguano kati ya nchi za magharibi na za Kiislam.Na hii vita inaonyesha kuzalisha wanunuzi wapya wa vinywaji vipya na kwa asilimia kubwa si kwa sababu ya utamu wa vinywaji hivi, bali maadili yahusishwayo na vinywaji hivi.
Qibla Cola

















Vinywaji hivi kama Mecca Cola, Qibla Cola , Zam Zam Cola nk, vinafanikiwa sana katika jamii wazilengazo. Inasemekana watengenezaji wa Mecca Cola walishawahi kulalamika kuwa katika soko la Uingereza wanapata tabu kutokana na kuwepo kwa Wapakistani wengi ambao hupendelea Qibla Cola ambayo hutengenezwa na Wapakistani.

Zam Zam Cola














Nachojiuliza tu ni kwamba je hii staili ya kuvitangaza kwa kuvihusisha na dini itafaa katika muda mrefu?Nashangaa kwanini kampuni zitengenezavyo vinywaji hivi haviungani ilikuwa na nguvu zaidi ya kupambana na Coca cola?Au ndio ushindani wa kibiashara utakaoleta ubora katika kampuni hizi?Kama ndio hivyo hii si ndio ileile filosofia ya kimagharibi ambayo Coca Cola inaindeleza?


Je, na Afrika tunahitaji kinywaji chetu cha Cola ambacho kwa kukinywa tutakuwa tunajua kuwa pasenti fulani inaenda kusaidia Afrika?

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mjengwa 11:03 pm  

Simon,
Nafurahia kusoma hoja zako nzito. Keep it up!
/maggid

Egidio Ndabagoye 8:09 pm  

Hapo Kwenye Coca cola kuna maswali mengi Saimon.
Nitarudi tena baadae

Anonymous 11:31 am  

Ubepari una namna ya kutafuta kila njia ya kuingia makucha yake kwenye mifuko ya watu. Nchini India nimekuta wauza vyakula vya papo kwa hapo kama McDonalds wanauza hadi "McDonalds" za mapishi ya kihindi!

Sasa kuna huyu mwanadada mwanablogu toka Morocco, nimekuta ameandika juu ya Santa (baba krisimasi) wa Kiislamu! Utaona nia ya kuwa na Santa huyu wa Kiislamu ina msukumo wa kibiashara. Tazama hapa:
http://tinyurl.com/uvfuq

Simon Kitururu 11:44 am  

Duh Santa mpaka wa Kiislamu !

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP