Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Dini au Utaifa kwanza?

>> Saturday, December 30, 2006


Hivi wewe ni Muislamu au Mkristo kwanza halafu ndio Mtanzania au ni Mtanzania kwanza halafu ndio mpagani?
Nauliza tu, usitishike!

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 7:22 am  

Mzee Simon,swali nzuri sana,Dini au Utaifa sawa,nami naomba unijibu,MILA AU UTAIFA?

Kwanza tunanzungumzia dini gani?pili dini zote zililetwa na wakoloni,tatu tukisema dini kwanza tunawatanguliza wakoloni kwanza,mimi naona utaifa kwanza.

Dini bila imani na matendo mema ni kazi bure,Dini bila kuambiana yakweli ni kazi bure.

Ningependelea uulize Mila na Desturi kwanzaa au utaifa?Imani yako na matendo yako ndio yatakayo kufikisha mbali.

Nikisema dini kwanza wakati mimi ni mchafu,mchafu katika ufisadi,ulevi,ngono,ubinafsi na k.n itakuwa ni sawa?

Tuangalie upande wapili WAJANE NA YATIMA,utatanguliza dini kwanza au utaifa?Matendo yako Mzee Simon,Dini ni nini wakati matendo yetu ni machafu?

Rastafarian ndio Imani na kizazi kilichobakia duniani,natanguliza UTAIFA KWANZA,najivunia kuwa mimi ni mweusi kizazi cha YAKOBO,na pia vivevile mwafrika(Mtanzania).

Naomba tuchunguze dini ya mtu mweusi kabla ya wakoloni,naomba tujiulize maswali hii dini ya wakoloni waliotuletea inamanufaa gani katika maisha yetu ya leo?

Jah live.

Anonymous 1:33 pm  

Swali zuri Simon, limenifikirisha. Halafu changamoto za Luihamu nimezipenda pia. Kabla hatujaendelea, dini ni nini? Na je, kuwa na dini maana yake kutokuwa mchafu kama Luihamu anavyohoji?

Nimependa vitu vikali hapa kwako Simon. Hongera sana ingawa huwa napita mara nyingi bila taarifa (kuacha maoni). Naona shughuli imepamba moto.

Anonymous 2:43 pm  

Utanzania. Uafrika. Sio Uafrika/Utanzania kwanza na dini baadaye bali Uafrika mwanzo na mwisho. Maana katika uafrika wangu kuna utamaduni, mila, historia, n.k. Dhana za kidini/kiimani zimebebwa ndani ya utamaduni wangu huo hivyo hakuna mgawanyiko au tofauti kati ya imani yangu na utamaduni/utaifa wangu. Kwahiyo nikisema utaifa kwanza ina maana kuwa utaifa huo unajumuisha dhana ambayo huwa tunaiita "dini." Dhana hii ni moja ya tawi katika mti ambao ndio utaifa/utamaduni/uafrika/utanzania wangu.

Anonymous 7:09 pm  

Nakubaliana na mawazo yote yaliyotolewa...

Cha kukumbuka ni kwamba udini kwa sasa unazidi kujenga/kuota mizizi katika nchi yetu.

Wengi wetu kuanzia walio nchini na wale ambao wapo nje ya nchi, wamekuwa na mitazamo ya kidini zaidi kuliko utaifa. Hii imetokana na uhuru wa dini kutumiwa vibaya ndani ya nchi yetu. Kazi kubwa itakuwepo huko mbeleni iwapo tutaendelea kunyosha vidole ili kujua yule ni mtu wa dini gani?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP