Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tekenya mawazo na VIJANA FM.

>> Tuesday, September 28, 2010

Au ngojea  Rugarabamu aongelee KIUMADHUBUTI  ishu ifuatavyo:





Tumejenga chombo cha habari ambacho kitakuwa ni jukwaa la vijana kushiriki, kubadilishana na kujenga mawazo kwa ajili ya maendeleo endelevu Tanzania.





Changia mawazo yako hapa:


Nawasilisha tu miye Mtakatifu Simon Kitururu KATIKA HILI na sihusiki na hiyo ndude HAPO JUU ambayo nauhakika ni  bomba sana  MWAYEGO.:-(

Hebu katika kuendeleza nanihii yenye hali ya hewa tofauti hapa kijiweni  NGUZA VIKING na Papi Kocha warudie mkuno -SEA



Au tu MANU DIBANGO alainishe zaidi kwa ndude -WOA



TUKO PAMOJA MHESHIMIWA!:-(

Read more...

LABDA ni rahisi kugeuza MANENO yageuke VITENDO kama hatuangalii KAMA hicho NI KITENDO sahihi wakati una PAKA a.k.a nyau MALAYA na utakacho mpaka katika TENDO ni watoto wa MBWA WAKO malaya!:-(

>> Monday, September 27, 2010

[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]


Wakati tunaangalia UWEZEKANO wa KILA MTU aongeaye kuwa anaweza KUTENDA,...


.... ni rahisi kugundua KUWA  kwa kuwa hata kuanguka ni KITENDO,...
... LABDA kila mtu  tukiomba aanguke sakafuni ,....
... kila mtu LABDA anaweza KUANGUKA  SAKAFUNI kama hatujaongezea  masharti AANGUKEJE kwa  maringo  na aangukie nini,...


....vitu viwezavyo kufanya KITENDO CHA KUANGUKA kiaminiwacho huwezwa na KILA MTU kiwe  na  watakaokosea kuanguka  kwa kuwa KATIKA kuanguka kwao MAJAJI watadai  KUNA USIO usahihi katika KUANGUKA hasa kama KATIKA KUANGUKA AANGUKAYE  hakuonyesha maringo yahitajiwayo KUTOKANA NA MASHART yakama WAGOMBEA U-Miss MBAGALA au tu katika kuanguka MUANGUKAJI aliangukia mavi ya kuku kitu ambacho kilitakiwa kukwepwa katika usahihi wa MUANGUKO.:-(



Katika hatua ya kwanza ya kulainisha  taralila na tukiwarudi PAKA na MBWA malaya wakati lengo ni kulenga tu swala hilo hilo la MANENO na VITENDO,...

Kuwa na PAKA JIKE malaya,...
.... wakati unania ya kuzalisha MBWA,....
....  kunauwezekano bado unasilaha ya mafanikio ya kupata ZE TOTOZ ZA MBWA kama unajua kutumia ulichonacho ambacho katika mfano huu  ni PAKA JIKE MALAYA kwa kuwa upo uwezekano kuwa kuna mwenye MBWA JIKE MALAYA ambaye naye shida yake ni PAKA JIKE malaya na katika kutatua TATIZO mkibadilishana tu  mlivyonavyo-  tatizo SOLVED ,....

...aka tatizo laweza tatuliwa kirahisi zaidi  kwako kisa tu una PAKA  kuliko kwa ambaye hana PAKA na anahitaji MBWA  katika ujazo wa matatizo yenu wahusika.:-(

Swali:
  •  Si unakuwa suluhisho la tatizo lako inaweza kuwa ndio tatizo la MWENZIO?
  • Si unakumbuka hata mababu katika kutatua matatizo yao walitumia mpaka BARTER TRADE kama suluhisho  kwa kuwa mwenye magimbi  asiye na MWIDU au MLENDA aliweza kubadilishana na mwenye MWIDU au MLENDA  ikiwa ni katika  kutatua uhaba wa ASICHONACHO  ingawa pia twajua  wenye ALMASI  enzi za MKOLONI waliopewa PIPI katika kubadilisha BIDHAA  kutokana na MAHITAJI?
  • Au?




Tatizo tu linaweza kujitokeza iwapo WEWE kwa kuwa unajua una PAKA malaya,...
... ukafikiri  basi unaweza kumlazimisha AJIFUNGUE watoto wa MBWA .:-(


Katika kuendelea kurahisisha taralila,.....
Swali:
  • Unafikiri unaweza KULAZIMISHA mfumo wa NCHI MBOVU uzalishe MAENDELEO hasa kama MAENDELEO huhitaji MFUMO MZURI  ufanyao kazi mpaka kwa mjumbe wa nyumba kumikumi hata kama RAIS MBOVU?

Kwahiyo labda,...
.... ILI maneno yageuke KITENDO sahihi  KIHITAJIWACHO,...
.... twahitaji zaidi ya MSEMAJI,....
.... ingawa bado labda MSEMAJI ni muhimu  vilevile katika uwezekano wa TENDO kufanyika KISAHIHI likiwa ni tendo SAHIHI kwa kuwa  ,....


... mara nyingi  ingawa tendo la kubinya JIPU ni tendo ,....
... waweza kukuta  bado UKWELI NI KWAMBA tendo sahihi  ni kutolibinya JIPU na kungojea liive vizuri ili lipasuliwe.:-(.


Na kuhusu lile swala la kuwa una PAKA na wahitaji MBWA,....
... huwezi kujua ,...

... LAKINI labda  ungeweza kusubiri PAKA azae watoto wa paka na baadaye uwauze paka na kununua MBWA malaya atakaye kutotoleshea watoto wa mbwa BAADAYE.:-(


Swali :
  •  Umenielewa?
  • Kwani  ni kwanini unafikiri WAKATI UNAHARAKA unafikiri unahitaji uwe na haraka sana hata katika kuelewa au tu katika ......nyingine?
NAWAZA TU MKUU na usikonde!

Tuendelee na Curtis Mayfield katika mdinyo-Freddy is DEAD





Curtis Mayfield arudie kudinya-Superfly





Na hatuwezi kuacha kipele bila kukunwa na hii kucha-Pusherman

Read more...

SOMO- kama unafuatilia YANAYOMKUTA Mtukufu Rais BARRACK OBAMA baada ya ahadi nyingi!

Kusema ni rahisi  zaidi kuliko KUTENDA ndivyo  isemekanavyo,....
.... hata kama kuna wabishao kwa kudai kuwa   KUTONGOZA KWA MSENGE  MPYA ambako ni KUONGEA  ahadi za unajisi aka KUSEMA kitu kwa limtu asilolijua vizuri  KUWA kitundu cha tako kinahitajiwa  ,....
....ni kugumu zaidi  kuliko kwa msenge KULAWITI mtu ASIYEMJUA ambacho ni kitendo hata kama ni CHA KISENGE  katika kuhitimishwa KITENDO   kimyakimya.:-(




Swali:
  • Si unajua Rais OBAMA sio maarufu sana kama alivyokuwa katika KAMPENI au tu mwanzoni mwa URAIS wake MAREKANI?

  • Si unajua aliyokuwa akiahidi Rais OBAMA katika KAMPENI  yangekuwa yanatendeka kirahisi MAREKANI ingekuwa bomba sana tu au angalau ingekuwa inawashinda WACHINA katika ukuaji kiuchumi?
  • Si unajua GEREZA la GUANTANAMO bado lipo?


Ndio,...
...kuahidi ni RAHISI kwa kuwa uhitajicho ni kujua tu KUSEMA,....
.... ingawa ili maswala yaote mimba labda baada ya kuongea VITENDO huhitajika.:-(




Swali:
  • AU?
Ndio,...
.... labda MAZINGIRA ya utekelezaji kwa OBAMA,...
... ni tofauti na yale yaliyomkabili  RAIS MWINYI katika kufanikisha utekelezaji,....
....ingawa LABDA twaweza kujifunza KITU siye kama WATANZANIA ambao tunakaribia UCHAGUZI kuwa,......
.... WAKATI tuko katika HOBI  ya kuichukia CCM kwa kuwa KWA kivitendo vyake WEWE na MIMI bado ni MASIKINI au bado tunakunywa soda  au angalau kula kuku  pale tukitembelewa na MGENI tu,....

... tukumbuke tu UPO UWEZEKANO kuwa HATA WAKIINGIA WAPINZANI KUENDESHA SERIKALI ambao mpaka sasa hivi tunawajua tu  zaidi katika FANI YA KUONGEA na SIO KUTENDA,...
... labda nao KIVITENDO bado watafanya UWANJA wa FISI ubakie kuwa UWANJA wa FISI ,...
.... na hilo ni kama kwa bahati nzuri haujageuzwa kuwa UWANJA WA MINYOO kwa kuwa na FISI nao WAMEKUFA.:-(


Swali :
  • SI unakumbuka hili ni  MOJA YA WAZO TU wakati huu tunaelekea katika UCHAGUZI ZE BONGO?



NIMEACHA hili wazo MHESHIMIWA!:-(


MIYE  naelekea kwa JOHN KITIME kuendelea kusoma HISTORIA ya MUZIKI TANZANIA
....na nikitoka hapo ntapitia SWAHILI STREET kabla ya kuondoka mtandaoni kwa muda:-(

Tukiachana na hilo:
Hebu Trombone SHORTY  apulize tena Trombone katika -Where Y'AT




Trombone SHORTY aimbe tu tena-Somethin' Beautiful




Au tu Curtis Mayfield adunge tu-Move on UP


JUMATATU NJEMA KIKORE!

Read more...

Aongeaye KIPARE kwa sauti ya KISUKUMA anaweza kustukiwa na WAPARE kuwa anaongea KIPARE kwa sauti ya KISUKUMA.:-(

>> Sunday, September 26, 2010


Lakini  ni KWELI pia,...
.... MPARE anaweza tu kuwa na SAUTI YA KISUKUMA katika kuongea  pia.:-(



Swali:
  • Kwani unadhani MLOKOLE hawezi kuongea KIHUNI?
  • Na siunakumbuka  kuwa AONGEAYE KISWAHILI kwa sauti ya KICHAGA bado aongeacho ni KISWAHILI?

NDIO,...
..HILI NI WAZO TU MKUU wa KITONGOJI!:-(

Hebu tumsikilize NDALA KASHEBA , King KIKII na wengine....wanaongea nini katika ndude-NI KWELI




Ndala KASHEBA alete-Yellow CARD



Au tu tudake Mpenzi Luta kutoka kwa Mutombo Audax na Maquis Original Zembwela


Read more...

Ukichunguza GWAGURO CHAFU unaweza kugundua kuna maeneo ni CHAFU zaidi!:-(

Katika  mtawanyiko wa UCHAFU,....
....hata ukimuangalia MTU msafi,....
.....unaweza kugundua katika UCHUNGUZI kuwa  MTU adaiye ni msafi si kila maeneo ni msafi sana.:-(

Swali:
  • SI unajua hata wakati MTU anaoga kuna maeneo anayaosha zaidi?

Ndio,...
.... ukizingatia maswala ya KIKWAPA au tu UKURUTU shingoni ,...
.... waweza kugundua hata katika KUCHAFUA shati, ....
.... kama tu chupi kuna maeneo unayachafua zaidi.:-(


Ndio,...
...hata MTU umdhaniaye ni MCHAFU,...
.....kuna uwezekano sio mchafu kila KITU kinamna.:-(


Swali:
  • SI unajua hata MWIZI aliyekuibia labda anaweza kuwa MOJA YA SIFA ZAKE ni  ya kuwa ni BOMBA la baba mzuri  kwa watoto wake  AU MME MZURI na kila akiiba  anaiba ili awe MTU MZURI kwa MKE wake kwa kumletea alivyo kuibia?
NI moja ya WAZO tu hili katika mahubiri ya jumapili MHESHIMIWA!

JUMAPILI NJEMA MKUU!


Hebu Superblue warudie - Joy in My Soul


Lost BOYS waje na -Peace, LOVE and NAPINESS


Au tu ONYX warudie -Slam HARDER

Read more...

Tangazo: CHEKA UPASUKE!

>> Saturday, September 25, 2010






SASA UNAWEZA TAZAMA FILAMU,SERIES NA VICHEKESHO KUPITIA CHEKA UPASUKE...

NAPENDA KUWAPA TAARIFA WADAU WOTE WA CHEKA UPASUKE KUA, PAMOJA NA KUCHEKA PAKA KUPASUKA SASA WATAWEZA ANGALIA FILAMU BILA CHENGA FILAMU MPYA TOKA NJE NA ZENGINE KIBAO KILA SIKU, MTAPATA VINJALI NA KUTAZAMA MKIWA HAPA CHEKA UPASUKE. FILAMU ZOTE NI SALAMA  HIVYO BASI KATIKA KUZIDI KUENDELEZA BURUDANI  ZAIDI KWA WADAU WA CHEKA UPASUKE NAWASIHI TENA KUENDELEA KUWEPO ENEO HILI MAANA MAMBO ZAIDI PAMBA MOTO BILA KUSAHAU VICHEKESHO BADO VIPO KILA SIKU KAMA KAWAIDA PIA KATUNI . NAPENDA KUTOA SHUKURANI ZANGU ZA PEKEE KWAKO SIMON KWA KUENDELEZA GURUDUMU LA BURUDANI.PIA KUWASHUKURU WANANCHI WOTE KUENDELEA KUA PAMOJA KATIKA KUSOGEZA GURUDUMU. ASANTENI SANA.




JINA LA BLOG: CHEKA UPASUKE



KWA PAMOJA TUNAENDELEZA!


Nimewakilisha ujumbe WAKUU na MIYE Simon KITURURU ni mjumbe tu kwa HILI ,...
...kazi kwenu KATIKA kufanyia kazi   KIWANZABANGA!:-(




Na wakati kunavyakuchekesha,...
... hebu cheki hii ndude niliyotumiwa na mdau Samson Simon :....:-(

Read more...

Katika siasa za TANZANIA ZA UCHAGUZI mtu akisema-``FUCK Wapinzani´´!:-(


....ukisema WAPINZANI ni SHENZI,...
.... labda HUJAGUNDUA  kila upande  aliopo  MTU kama  kuna zaidi ya PANDE moja,...
... basi HUO   ni  upande wa UPINZANI.:-(


Swali  
  • Tukitumia mfano wa  mlango wa choo na shughuli ikiwa ni mlango ubaki wazi - SI UNAJUA Auvutae HUKU na ausukumae KULE   hata kama wahusika misuli yao haifanani  wote  wanapingana NA NI WAPINZANI  katika msukumo , na ukiwauliza malaya zao watathibitisha kuwa  wao ni WAPINZANI kisa mmoja anataka afunge MLANGO wa CHOO na mwingine anataka afungue mlango wa MSALANI?




Ndio ,...
...kwa kawaida kuna kitu cha tatu kama ANGALAU  KUNA hata wawili waongeleao UPINZANI,..

... ingawa WAWILI huwa wanatosha katika kupingana kitu kisababishazho kuzaliwa  au kusababisha kuwe na kitu UPINZANI.:-(

SWALI:
  • AU?
LABDA   kila upande ni upande wa upinzani,...
.... na  inategemea tu na tafsiri ya wahusika katika MHUSIKA kujisikia NI MPINZANI .:-(

Na ingawa kuna  wadaio  MPINZANI ni atakaye kunyoa kitu AU KUNG'OA KITU,...
... lakini ukichunguza na kufikiria VIZURI unaweza kukubaliana hata KWA WASIWASI NA MIMI  kuwa   afikiriaye anang'oa kitu hata akifanikiwa kung'oa labda naye tutakuwa TU tuna ushahidi ninini kang'olewa eneo anuai wakati anafikiria KANG'OA.:-(

Ni moja ya MTAZAMO TU MHESHIMIWA ,  na samahani kwa neno NA WAZO  la kilokole lenye neno  ``FUCK´´ katika KICHWA CHA HABARI YA taralila yangu hii  isiyokaa mkao wa KITAALAMU kwa WASTAARABU ambao neno na tendo ``FUCK´´ wamejifunza kuamini AU KUAMINISHWA  ni MATUSI.:-(




Moja kwa moja PETER TOSH aunganishe-Johnny BE GOOD


Peter TOSH na MICK JAGGER walete-Walk AND dont look BACK





DENNIS BROWN adunge-Revolution


DENNIS BROWN adinye-Land of PROMISE





ASWAD wakite kitu orijino ambacho mpaka akina DENNIS BROWN  walikopi BITI katika -DUB FIRE


AU tu ALICIA KEYS ajaribu na DAMIAN MARLEY katika- WELCOME TO JAM ROCK



Au tu BOB MARLEY amalizie na kitu bomba kiitwacho-LIVELY UP URSELF

Read more...

Leo katika shukrani: AHKSANTE MJUSI!

>> Friday, September 24, 2010

ASANTE MJUSI,..
.... kwa kupunguza mbu na mende TANZANIA!

Asante sana na kwa binamu zako  MABUIBUI unaoshirikiananao  EWE  jemedari MJUSI ,...
... kwa kupunguza hata INZI  kwa  uwezo wenu udhaniwao NI MDOGO kwa kuwa  hamna nguvu za ubongo kama wa BINADAMU ambao na miakili yao,...
....INZI na MBU wawatoa jasho hapa  TANZANIA!:-(


Swali:
  • Huwa unakumbuka kuwa kuna vitu uvidharauvyo kama tu PANYA ambavyo vina mchango tu mkubwa wa muhimu kwako  hata katika tu kufanya kuwe na uwiano katika mazingira ili kuwe na neema kwako?

  • SI unakumbuka kuna WATU uwadharauo  pia ambao ndio WAKUSAIDIAO  kwa mengi AMBAYO NI MUHIMU KWAKO , hata YALE YAFANYAYO ujisikie vizuri chooni kwa kuwa walilima chakula kikusaidiacho uende chooni , WALIKIJENGA CHOO ili usijisaidie majanini, na LABDA wakakisafisha pia choo ili ujisaidie kwa uroda na kufaidika na harufu utengenezazo mwenyewe tu kwa kuwa choo ni kisafi?
  • Unauhakika INZI na MBU hawahitajiki DUNIANI  kwa kuwa weye lengo lako ni KUWAUA?


Tukiachana na HILO,.....
....pamoja na yale mengine kama  ya MINYOO, makonokono na MAJONGOO yadharauliwayo,...
....ingawa ni muhimu katika udongo wa MAZAO YAPENDWAYO NA MTUZ  kurutubika;.....

ASANTENI WOTE enyi  NDUGU, marafiki, NYIE NISIOWAJUA ,wale NISIOWAFAHAMU na pia ENYI MAADUI kwa yote  WAPENDWA!

Nawatakieni IJUMAA na WIKIENDI Mwanana!

Na moja kwa moja hebu RENEGADES warudie wimbo wa Lionel Ritchie katika Steel Pans ULE ujulikanao kama-ALL night long



Au tu na  MBARAKA Mwinshehe atulize TU  mshawasha kwa kuongelea nifikiriacho sasa hivi ambacho ni -SHIDA

Read more...

Tukiangalia UTU kwa kuangalia MAANDALIZI ya MSICHANA siku ajuayo KWA MARA YA KWANZA anakwenda kumvulia MTU ampendaye NGUO!:-(

>> Thursday, September 23, 2010

[Tahadhari: Taralila inawazo dhaifu na ukilichungulia labda limekaa vibaya.:-(]

Maandalizi yoyote, yanayo na  kwasababu
Siku ya kutoa yote, ukurutu si adabu
Kwa kuwa si kivyovyote, mtu huenda kwa babu
Andalizi la kuvua, ni silika tu ya utu.


Andao la msichana, kama funzo la silika
Na silika za msichana, UBINADAMU hakika
Za uchafu kuukana, hata usio hakika
Za BINADAMU za UTU , jifunze kwa MSICHANA.


Ya uvulana ya UTU , si kama ya kisichana
Yale yenye utukutu, mbele za watu mchana
Ya kukojolea vitu,mbele hata ya Anna
Hata soni haioni,na hilo si ni bayana?


Utajifunza tu KITU, kwa kufikiria UTU
Na uchi katika MTU, wengi ni KIPIMA utu.
Ya msichana ni UTU, hata yafichavyo KITU
Pasipo ya MSICHANA, ya MVULANA si kitu.






Swali:
  • Unafikiri kila kitu kingekuwa KINAFANYWA kwa maandalizi kama ya siku ya kwanza wajua labda NANIHII inaweza KUNANILIWA -Tanzania kimaandalizi ya kutawala DUNIA unadhani tungekuwa wapi?

  • Unauhakika andalizi la kukutana na mpenzi wako mara ya kwanza kwa nia ya kufanya dhambi ya asili aka UASHERATI hayana mchecheto kiasi kwamba kwa kujiandaa sana kuvaa ambavyo utamvulia mtu ukasahau KUSAFISHA nyumba, kula au kuwa uendacho kufanya ni DHAMBI Kikristo au  KIISLAMU ingawa labda sio dhambi kibaolojia?











Ainisho la taralila:

Ndio,....
...UKIFIKIRIA unaweza kugundua  shughuli za MAANDALIZI  ni tofauti  siku  unuiapo na kujua kesho,....
..... utakwenda KUMSUTA Khadija au tu utafanya wa muhimu  MTIHANI .

Na kujua ya kesho kibinadamu ni kawaida kwa kuwa labda leo umeshajua kuwa utasikia njaa tena kesho ,....
.... kwa hiyo labda MAANDALI ya kama  kesho utakula tena ni maandalizi tofauti kidogo na umeyazoea tokea uzaliwe  na kwa hayo  HUJIHAMI.


Ila,...
... kumbuka tu  KATIKA SWALA HILOHILO LA MSOSI kama itakuwa ni kweli kwako KWA MARA YA kwanza  utakula KONOKONO wa kuchemshwa KESHO,...
.. na kwenu konokono hamjawahikusikia ni chakula ,waweza kujikuta unajiandaa vizuri katika zoezi zima la kukabiliana na HILO BONGE la msosi kwa wastaarabu WAFARANSA  hasa kama lengo ni kujifanya sio mshamba kwa wastaarabu WAFARANSA katika yako ya KUJIHAMI.:-(

Swali:
  • AU?

Ndio,...
... nakubali HII HOJA  ya maandalizi ya MSICHANA siku ya kwanza aliyoamua kuwa leo atamvulia mtu/MVULANA   mpaka kificha eneo ANUAI angeiandika tu vizuri zaidi MSICHANA ambaye kashapitia hilo ndani ya safari ndefu za mpaka NATAKA -SITAKI, Baba MKALI, unajua hii ni dhambi ila nakupenda,....nk.

.... ila baada ya kusimuliwa na MOJA ya hawahawa FLOWERS aka MSICHANAZ jinsi maandalizi ya siku hiyo muhimu yaliyonuwiwa kwa hiari yawezavyo kuwa na shughuli tofauti kabisa KIMAANDALIZI na zenye umakini wa hali ya juu,....
....nikapata MOTISHA wa leo kujiaanda sana katika shughuli zangu kwa kuwa ghafla nikajistukia labda KILA SIKU ikiandaliwa kwa umakini ina nafasi kubwa ya mafanikio zaidi hata ikiwa fanikio lenyewe  kwa KIKISTO ni dhambi ,...
....na Kwa KI BUDHA si dhambi ila BUDHA anafanya lifikiriwe zaidi bila VITISHO.:-(


Swali:
  • Si unakumbuka lakini inasemekana wasichana wengi hata baada ya kujiandaa sana kwa shughuli nzima ya uasherati wa mara ya kwanza , BAADA YA shughuli huwa hawawi na uhakika kama maandalizi yalilipa kwa  kuwa bado hubakia na hisia labda SHUGHULI haikufanywa kwa maringo yenye UFANISI wenye kiwango cha kutosha?
  • Hivi MHESHIMIWA,  hivi LILE halikufanyi ufikirie na HILI?


Ni moja tu ya WAZO MHESHIMIWA na wala usijihangaishe sana kulielewa kama HUKULIELEWA!:-(

Moja kwa moja katika kubadili mkao hapa kijiweni  Trombone SHORTY aachie-Somethin' Beautiful




Bilal arudie-Soul SISTA


Au tu Method Man na D'angelo wamalizie tu kwa-Break ups 2 make ups

Read more...

VYAKULA vinazidi kuwa BANDIA kama sura za WAIGIZA SINEMA wa HOLLYWOOD!:-(



Tunakokwenda LABDA badala ya watu kulima MPUNGA,...
....wanasayansi watagundua jinsi ya kulima UBWABWA ULIOIVA tayari ,...

...au tu  hata kuotesha PILAU ILIYOIVA na YA MOTO kama ILE ikufanyayo upende kuhudhuria MISIBA YA WATU USIOWAJUA kwenye sahani yako.:-(

Hebu tufuatilie mjadala wa GENETICALLY  modified food ....









OKEI,...
...najaribu tu KUKUMBUSHIA kuwa kuna vitu watu walavyo siku hizi ambavyo viko kwenye majaribio tu na madhara yake hakuna ayajuaye.

Na kwa sisi tuishio nchi masikini ,...
....kirahisi tu tunafanyiwa majaribio hata bila kujua kwa sababu kwanza ni MASIKINI tudhaniao kila UITWAO  msaada ni MSAADA ,...
....na pia hatukawii kushindwa kujilisha wenyewe.:-(


Cha ajabu ni kwamba,....
... vyakula ambavyo sasa hivi kuna watu katika nchi kama BONGO  wanaviona ni vya KIMASIKINI hasa kwa staili vilimwavyo,...
.... hivyo ndivyo vyazidi kuthaminiwa na MATAJIRI nchi zilizoendelea hasa kutokana na kutoathiriwa na madawa au tu kuchezewa na wataalamu wa kisayansi.:-(



Swali pembeni kidogo ya chupi ya hoja:
  • SI unajua asilimia kubwa ya sura za WACHEZA SINEMA wa siku hizi wa HOLLYWOOD uwaonao katika sinema za KIMAREKANI ukiachilia mbali NYONYOZ BANDIA ni kweli pia hata SURA zao sio halisia?

BASI BWANA MKUU nimeacha WAZO !

Na moja kwa moja ngojea FELA KUTI arudie kitu-Coffin for HEAD of STATE




Au tu FELA arudie kudunga-Mr Grammarticologylisationalism is the Boss

Read more...

Kitu chanya kiduchu katika RIPOTI kuhusu TANZANIA kwenye HABARI ZA DUNIA !

>> Wednesday, September 22, 2010

MKUU nashea tu ripoti ya Global Campaign for Education;

'Back to School?' - the worst places to be a school child.

20 September 2010 The Global Campaign for Education today launched their report 'Back to School?' of the worst places to be a school child in 2010.......


Kigusacho TANZANIA ambacho kinauchanya ni  :
Progress is being made as in Tanzania three million extra children are now able to go to school.


AU  kwa lugha ya kitaalamu:

Ripoti inadai kuna ongezeko la watoto milioni tatu  wenyeuwezo wa kwenda  SHULE Tanzania. 


Na hicho MIMI BINAFSI naamini ni kitu kizuri .:-(



 Ukitaka kujua zaidi nenda kwenye ripoti kwa kubofya HAPA


KUMBUKA najaribu kuegemea kwenye UCHANYA kwa kuwa halihalisi si nzuri bado  .:-(

Read more...

Mtoto wa MJINI anaweza kudhania UMEMTUKANA ukimuita ``MKULIMA´´ .:-(

Kuna uwezekano JEMBE linauwezo wakumtupa MKULIMA,...

... kama mambo yote  kimuonekano MWENYE trekta ndio mjanja kuliko mtumia jembe.:-(

Na kwa kuwa wajanja wanatumia PENI na KOMPUTA hata katika kuiba HATA ya WAKULIMA,...
.... yaweza kueleweka ukikuta VIJANA KIJIWENI  huku wakikuona UNACHEMSHA katika jitihada zako za kuwaambia wakashike jembe  huku wanashuhudia waheshimiwao katika TAIFA  wako mbali na JEMBE.:-(

Swali:
  • Kwani unabisha MKULIMA WA JEMBE  na FISADI MTUMIA PENI  wakishindana katika utamaduni wetu mpya wa UMISS aka FASHENI SHOO labda kiulaini tu ni  FISADI ndio atashinda hata angalau kwa kufikiriwa ndiye mwenye paja laini?


Hata bila kuchunguza sana utastukia kuna shughuli zinadharaulika TANZANIA !:-(

Swali
  • Unabisha?

Na tokea watajirikao haraka haraka KWA NJIA ZISIZO HALALI  kuonekana WAJANJA,...
.... karibu shughuli zote hata AMBAZO ZILIKUWA ZINAHESHIMIKA ambazo HUWEZI KULIA vizuri OFISINI ukatajirika  KIRAHISI zimepungua heshima zikiwemo:
  • Ualimu
  • Unesi
  • ...nk ,
  • Ukulima

Ndio kuna waoanishao  bado UKULIMA  na vitu NISHAI,....
.....na labda kumbuka hilo ukiwa unatafakari waongeleao sera za KILIMO KWANZA huwa wanamlenga nani na wanageuzaje swala zima la MVUTO wa UKULIMA ambao TANZANIA ndio inaudai ni UTI  WA MGONGO.

Ndio UKULIMA ni mgumu na JAMII inaabudu wapendao ulaini wa shughuli na lolote gumu kama HALINA pesa kuonekana NISHAI,...
...na kwa bahati mbaya JAMII haifunzi watu kufikiria  MAMBO kiundani  kwa hizyo ni MWENYE BUSARA KUDHARAULIWA  kirahisi kisa hawezi kununua BIA na kutuliza mawazo yeye anakunywa GONGO.:-(.


Swali
  • AU?
  • Si ukiwa MWIZI na bonge la BENZI unaweza kusikilizwa kuliko ukiwa MKUU wa SHULE ya KIJIJI mwenye busara  na baiskeli yako tu ya zamani ya aina ya SWALA?



Ukitaka kujua TANZANIA tuko matatani,.....
... angalia hata hizi PROFESHENI muhimu tu zitazamwavyo:

  • Walimu ambao ndio tegemeo la TAIFA katika kuondoa ujinga, wanadharauliwa hasa kisa hata mishahara yao tu haiwawezeshi kuishi vizuri.

  • Mapolisi walindao amani , hawana amani WAO WENYEWE  kwa kuwa hawawezikutegemea kazi wakaishi vizuri.
  • Manesi wahudumiao WAGONJWA  ndio kabisaa  hata sijui wanapata wapi nguvu za kuhangaika na wagonjwa NA MATAPISHI YAO bila kusahau UHARISHO siku nyingine, DAMUDAMU KWA SANA, ....wakati  wanadharaulika na mishahara yao ndio hivyo tena .:-(


  • Wakulima ndio hivyo tena - MJINI unaweza hata kukosa mchumba kwa kujulikana we MKULIMA kitu ambacho ni cha ajabu kwa kuwa bila WAKULIMA maakuli hakuna.:-(

Angalau sikuhizi WACHUNGAJI katika ujasiliamali wakujianzishia MAKANISA unaweza kujikuta  WANAOFANIKIWA KUWATISHA  vizuri WAUMINI WAO  kuhusu JEHANAMU wanaweza wakajikuta WANAPATA  sadaka nyingi kwa hiyo VIPRADO na angalau tu  MVINYO wa nyumbani ambao hukatwa katika bajeti ya MVINYO wa KANISANI  unaweza kukuta haukosekani nyumbani kwa MCHUNGAJI.:-(

NAWAZA TU KWA SAUTI  MHESHIMIWA usikonde!

Hebu  Jermiah arudie -Wizi Mtupu




Bonta aendelee katika ndude - Nauza Kura Yangu


Au tu Ras Lion na Joni Woka wabadili mkao kwa-HII KITU

Read more...

Katika kutetea haki ya watu KUJISAIDIA HADHARANI!:-(

>> Tuesday, September 21, 2010

 [Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]


Kuna MAMBO huhitaji uwe na kidhaniwacho ni TABIA MBAYA hadharani,...
..... laasivyo unaweza KUJINYEA BURE HADHARANI  wakati ni kweli ulipo hakuna vyoo hadharani na labda katika kibano hicho BUSARA ni kunya HADHARANI!:-(

Swali:
  • Unadhani kati ya KUJIKOJOLEA au kwenda msalani pembeni ya gari la MBUNGE hadharani  kama umebanwa ni nini  busara?
  • Unauhakika ni rahisi hivyo kujisaidia HADHARANI wakati unalaumu wajisaidiao HADHARANI wakati vyoo vya uma haviko hapo HADHARANI?


Na wakati niko katika HOJA nawezakusema  pia  UDHAIFU wa wenye tabia nzuri HADHARANI,....

... ni moja ya kichangiacho TABIA MBAYA HADHARANI!

Swali:
  • Kwani unafikiri kwa kuwa unaTABIA NZURI zikufanyazo umekaa kimya HADHARANI wakati adhaniwaye KIBAKA  anabwengwa  bila uhakika kama kweli KAIBA, wananafunzi wananyanyaswa kwenye DALADALAZ mbele yako, watoto wanatukanana ,........ hakuna uwezekano TABIA YAKO NZURI YA KUKAA KIMYA hadharani  inachangia TABIA MBAYA uzichukiazo HADHARANI?


Ndio,...
.... kuna hata MABLOGA wajulikanao kwa tabia nzuri MTANDAONI,...
....INGAWA wanatabia NZURI wakijulikana majina tu ,...
...na ukiwastukia kumbe ni haohao  wenye tabia mbaya chumbani/WAKIWA ANONYMOUS unaweza  hata kuanza KUHISI  kuwa mmoja wa waliowahi kukutukana mtandaoni ni  yule MCHUNGAJI / SHEKHE wako  ambaye anatabia nzuri sana na unadhani hana matusi ya nguoni  kwa jinsi umjuavyo HADHARANI kisa umestukia KITU kwa KUSTUKIA kumbe Simon KITURURU umdhaniaye hana adabu HADHARANI ni yule mwenye tabia nzuri kweli  chobisi asikoonekana.:-(

Ni wazo tu hili MKUU na nakutakia KAMANYOLA bila JASHO Mkuu!
Au ngojea nikuage kwa ung'eng' e -BADAYEZ!


Kwa kubadili hali ya hewa hapa KIJIWENI  tumrudie Lil VICIOUS wakati bado kinda ingawa msiniulize BUSARA za kumuachia mtoto aongee aongeayo  LIL VICIOUS ni nini tukianza na -FREAKS


Au tu Lil VICIOUS arudie- NIKA



Lil VIcious amalizie  na-The GLOCK


Au tu tubadili kwa kumuachia mtoto wa Will Smith kwa jina Willow alainishe kwa-Whip my HAIR

Read more...

Nawasiwasi na UNDANI wa sifa MTU apewazo kama zile za ``JAMAA linapenda SANA WANAWAKE!``:-(

Kunasifa zinazopotosha ukweli wa JAMBO,....
..... ndio maana kuna KIDUME  apendaye sana matumizi ya uke wa MWANAMKE,....

.....awezaye kupata sifa kuwa anapenda sana WANAWAKE,...

...kitu ambacho SI KWELI kwa kuwa  ukimchunguza HUYO KIDUME kwa UNDANI ,...

....labda kipendwacho  ni kidude tu na sio LIMWANAMKE ZIMA  na HILO DUME  likipata UKIMWI kwa furaha tu litausambaza vyakutosha kwa wakutosha WANAWAKE liwachukiao ingawa wakati yuko katika KITENDO CHA KUWAGAWIA MDUDU VIMWANA  jamii inampasifa ``ANAPENDA SANA WANAWAKE´´.:-(


Swali:

  • Si inajulikana kuwa kunatofauti ya mwanaume KUPENDA NGONO na MWANAUME kupenda MWANAMKE?

Ndio,....
.... hata ubishe  bado kuna uwezekano hata wadaio WANAPENDA mpira wa MIGUU SANA labda wapendacho ni zile tu hisia mchezo huo uwapandishazo  ,...

... na kama hisia hizo wandelizipata kwa kushangilia mashindano ya MBIO za mbuzi  wangekuwa washabiki sana tu wa MBUZI na ungesikia wanasifa wanapenda sana MBUZI na zio hisia mbuzi wazipandishazo jazba.:-(

Ni moja ya wazo tu hili DUNIANI na unaruhusiwa kuendelea KUNUNA kama bado umenuna!:-(

Moja kwa moja turudi Trinidad  kukutana na Machel Montano wakati bado kinda akishuka-Too YOUNG to SOCA



Au tu tumdake tena Machel Montano wakati bado kinda katika ndude nyingine-School Days



Tukutane na Machel Montano wakati mkubwa afundishe -What is SOCA music



Au tu Machel Montano, HD na Collie buddz wadunge-FLY AWAY

Read more...

Ukichunguza ni wapi BINADAMU hutolea hasira zao waweza hisi tabia za BINADAMU wakiwa na hasira ni za KIMALAYA!:-(

Kulengesha hasira kwa kikutiacho hasira tu ni bonge la SANAA,...
....na si watu wengi wanapatia kulengesha hasira kwa aliyewatia HASIRA,...
.....na hasira zao huzigawa ovyoovyo kama tu MALAYA WAGAWAVYO,...
... ndio maana kuna WAKOROFISHWAO na LIMKE  na kuanza kupiga WATOTO wasiohusika na yao ya WAZAZI.:-(

Swali:
  • Unabisha?


Wengi wenye hasira,....
...... chochote kilichombele yao wanaweza kukitolea hasira,....
.... ndio maana hata mtandaoni unaweza kukuta LIMTU limechukizwa na LIMPENZI lake huko  na  kuja mtandaoni kutoa hasira  kwa kutukana  WATU WENGINE ovyo.:-(



Swali:
  • Unabisha?
  • Unafikiri wewe unajua kukwepa kulengesha HASIRA ZAKO kwa yahasira yako yasiyo WAHUSU?


Ndio kuna waudhiwao na KUKU,...
.... na kwa kuwa tu wamuonaye mbele yao NI BATA basi wanafikiri  kwa hasira za KUKU ni sahihi kumpiga BATA bonge la teke.:-(

Swali:
  • Unabisha?

Na ni  ndio,....
...pamoja na yote ni vizuri kumbuka KUNAWAKUCHEKEAO kutokana na kwamba walikotoka WAMESHACHEKESHWA na mambo mengine ,...
... na nikweli wala llabda siku hiyo wewe HUCHEKESHI.:-(

Swali:
  • Si unajua  kuna WAUME wa watu  ambao huchekewa na kufurahishwa zaidi kwa kuwa tu mama watoto wakati KIDUME yuko kazini alichekeshwa na kufurahishwa vizuri tu na HOUSEBOY aka kwa lugha ya kitaalamu -´´Mtumishi wa nyumbani wa KIUME``?
  • Si unakumbuka si kweli furaha zako haziwafurahishi hata adui zako hasa ukizingati kuwa wewe ukitabasamu unakuwa mzuri kweli  kwa kila mtu na sio tu kwa mpenzi wako wa siri PADRE kwa kuwa hata SHEKHE  anapata ile kitu roho -samahani -MWILI  YA MTU inatamani ?

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na ruksa kulibishia!:-(












Hebu Heavy D arudie tena ndude- Mr BIG STUFF



HEAVY arudie na -Nuttin' but LOVE



Au tu Heavy D and The BOYS warudie pia na ndude-Now tha we have found LOVE








Ndio niliwadaka Jacaranda wakifanya vitu vyao







Read more...

Hebu tumsikilize tena NYERERE....

>> Monday, September 20, 2010



Au hebu tuwasikilize wengine wanazungumza nini......








Au tu tuendelee na wengine....

NI HILO tu KIJEBA!

Read more...

Labda ni KWELI hakuna KUKU WAWILI WAKIENYEJI wafananao UTAMU!:-(

>> Sunday, September 19, 2010



Ndio,...
...na LABDA hakuna WATU wawili ULIOWAONJA tabia zao au angalau sehemu zao za siri WENYE KUFANANA utamu.:-(

Swali:
  • Unafikiri upendayo ya BIBI  ya kupika uyoga yanafanana na ya MAMA au dada yako katika kupika uyoga uleule?
  • Unafikiri MAHARAGE ya mbeya ni maji mara moja kwa kila MTU?


  • Unafikiri kama KUMA ingekuwa ni ile ile kwanini BABA WATOTO angetaka kuonja na ya MKE wa jirani?



Ndio,..
...ni KWELI hakuna KUKU wa KIENYEJI au tu  WA KISASA MUUZA SURA YA KIKUKU ambaye anafanana utamu na mwingine,..

...kwa kuwa UKIFANANISHA waweza kuanza kuamini kama MIMI kuwa ,...



....kwa kuwa hata WEYE ujitulizavyo ili UPATE UTAMU kwa mke wako NA UJITULIZAPO KWA KUIBIA  zile za chapuchapu migombani,....


....labda ni tofauti kwa kuwa KUNAUWEZEKANO MKUBWA TU kuwa migomba yenyewe hutegemea mbolea KATIKA KUFANYA NDIZI za MATOMBO ni tamu zaidi ya NDIZI HIZOHIZO ZA MOROGORO MJINI na ndio maana labda  MAHINDI  ya SONGEA yaliozoea MBOLEA ZA CHUMVICHUMVI ni tofauti  KIUTAMU na yale yaliyozoea mbolea za mavi ya KUKU kwa UTAMU.:-(.:-(

Swali:
  • Unauhakika kuku wa jana ni kweli ni mtamu vilevile kama kuku wa leo?

SAMAHANI MUHESHIMIWA  hili ni wazo tu na SAMAHANI NYINGINE iliyodinda kwa kuwa katika TARALILA HII kunaneno KUMA.:-(

Moja kwa moja ngojea FELA KUTI aingilie ukutiukuti GHAFLA kwa ndude-WHO no KNOW  go KNOW



Roy AYERS na FELA Ransome KUTI wapulizie muendeleo katika ndude-AFRICA



Fela Kuti alete -Wakawaka



Fela arudie mdinyo-FOGOFOGO




Au tu FELA KUTI na GINGER BAKER waanzishe UPYA kudunga kwa - Let's Start





Ndio,...
....nipo na wadau kama ionekanavyo katika michoro niliyochora juzi ya jana:-(

Read more...

NI silika ya kawaida ya KIBINADAMU PIA kwa mtu kutaka kukuchungulia UKIKAA uchi!:-(

>> Saturday, September 18, 2010

[Tahadhari: Jihadhari na vijineno kama `` uchi´´, .....,..... katika TARALILA HII  kwa kuwa labda havina maana uifikiriayo!:-(]





Ya KIBINADAMU yanaviitwavyo TABIA,...
... lakini ikumbukwe tu kuwa TABIA NZURI na TABIA MBAYA ni vitu tu alivyojitungia BINADAMU  kama tu alivyojitungia kuosha mpaka ndizi zenye MAGANDA kutokana na aliyojifunza ya USAFI yale  ya DUNIA.:-(



Kama tu binadamu ajifunzavyo kunywa BIA,...
.... ndivyo ajifunzavyo TABIA ya kuvaa chupi  hasa baada ya kustukia  BINADAMU WAKUBWA waanzapo  kukaripia au hata KUMUANGALIA KWA KIJICHOPAPO,...


.....  hasa kwa VISA MTOTO ASIVYOVIJUA vya haohao wenyewe WAKUBWA  kuhisi MWANADAMU  huyo MTOTO maungo yake ya chini yameanza kuchora RAMANI zenye ratiba zianzazokushamiri katika kuashiria ukubwa UWATIAO VISHAWISHI WAKUBWA   au kuchonga ya wakumbushayo wakubwa zisizo MWANANA ZILE NDUDE ZILIZOWAKUTA  waliposhambuliwa  KATIKA yao  YA KIKUBWA   ambazo zinaanza kufananafanana NA ZA MTOTO  sehemu za siri ZISIZO hata na matumizi ya kikubwa   YA ZAIDI YA  kikubwa yale YA MSALANI  katika makubwa ya DUNIA.:-(




Swali:
  • AU?



Kaa vizuri basi wewe BINADAMU,...
... kwa kuwa ingawa tukikuchungulia utalalamika kama uliyojifunza ya KIUSTAARABU WA KIBINADAMU YALIVYOKUFUNZA,...


...lakini kumbuka na akuchunguliaye afanyacho ni  TABIA SAHIHI yenye haki na sifa zote za KIBINADAMU.:-(

Kwa hiyo labda usitutie MAJARIBU  kwa ujuayo tutayachungulia hata yale ya UFISADI wako utakayo kuyaficha kama vile KWA HAYO haumwagi kinamna damu,...
.... hata kama wajua  kile KIMEREMETACHO ambacho kikawaida twajua si rahisi kuwa uchi hivyo wakiweka wazi na kutaka  tusikipige chabo labda hata KUKICHOKONOA kwa kulalamika  kama vile uchi wenye damu.:-(

Swali:
  • Kiheshima  ukimuona MHESHIMIWA kakaa uchi na kutotaka kumchungulia vizuri uone zaidi eneo ANUAI ,... unafikiri inamaana hamu ya kuchungulia HUNA WAKATI HUO  kwa kuwa kitabia weye MSTAARABU ambaye umefudhu katika kufundwa yaliyo uchi yafumbiwe macho?


NI ANGALIZO tu katika WAZO HILI  na usikonde kama hunielewi  MHESHIMIWA ! 
Si unajua tena lugha kicheche, ndio maana KATIKA  matumizi ya lugha yanaweza kurahisisha KUTOELEWEKA pia!.:-(


Tubadili kwa kuwapata tena Amadou na Mariam wadinye - Je pense a toi



Au tu tuwapate Soul Brothers waendelee na-Umshado


Au tu na Sipho MABUSE arudie ndude-Jive Soweto

Read more...

UTAMU wa ASALI usifuatilie NYUKI ASIYEJUA KUOSHA MIKONO na utamu wa NYAMA YA KUKU WA KIENYEJI usifuatilie KUKU katika matembezi yake alikula NINI!:-(

Na  UTAMU wa sehemu za siri za MTU,...
... labda zahitaji kufumbia macho kumbukumbu kuwa SEHEMU ZA SIRI shughuli zake chafu nyingine ni NINI.:-(






Swali:
  •  SI unajua ukifuatilia ya JIKO CHAFU ambayo chakula chake umeshakigida unaweza kuharisha bure hata kama chakula kilikuwa salama?
  • Si MHESHIMIWA unatambua hili ni wazo tu ?

Ndio,...
...ukiufuatilia sana UTAMU ,...
... unaweza kustukia mpaka utamu ULIVYOVALISHWA ulimbwende mpaka na chembechembe za haja kubwa,....


... na kung'amua kuwa labda siri ya UTAMU si UTAMU,....
....na UCHUNGU labda  ni moja ya siri za MSELEBUKO  WAKATI UNAUKATIKIA SINDIMBA UTAMU  kwa kuwa labda kitengenezacho ile kitu TAMU kimetengenezwa kwa machungu au tu vile uvichukiavyo kwa kunuka na  VILE wala usivyovioanisha  na ujisikiavyo  wakati NANIHII tamu.:-(

Ni wazo tu hili lenye KIBIONGO Mheshimiwa!
Na nakutakia WIKIENDI mwanana MKUU!

Moja kwa moja ngojea NAS na DAMIAN MARLEY wadinye -LAND of PROMISE

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP