Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STAILI ya KUJISHEBEDUA ya MTU mbele ya MPENZI ikihitaji kudhalilisha watu WENGINE!

>> Wednesday, September 08, 2010

Kuna ambao katika kujitahidi waone kane wao BOMBA mbele ya MTU ,....
.... wanafikiri wanahitaji kudhalilisha watu wengine.:-(

Swali:
  • Kwani huja stukia amdhalilishaye MTU kwa kutaka sifa tu mbele ya watu wengine kuwa yeye MJANJA?


UDHAIFU ni kitu cha ajabu,...
... kwa kuwa kinaweza kumfanya MNYONGE AJITUTUMUE kupita kiasi yote ikiwa ni katika tu kuficha UDHAIFU.

Na katika KUNDI LA WATU kwa bahati mbaya  kitu ambacho sio kitu cha ajabu,....
.....wala haihitaji uchunguzi sana utastukia  kunawahitajio waonekane zaidi ya wengine  wadhaniwao ni MASHUJAA  kama hustukii kuwa labda uudhanio ni USHUJAA wa mtu labda ndio siri ya  wake UDHAIFU.:-(


Swali:
  • AU?

Kwa hiyo labda MBELE za WATU,...
.... apayukaye KWA NGUVU ili wote TUSIKIE labda ni ambaye hana hoja na mwenye lakusema  lenyesuluhisho  kakaa kimya na kwa wasio wajanja ndiye aonekanaye ZOBA.

Kwa hiyo labda MBELE za watu,....
......fikiri a pia uwezekano wa APAYUKAYE kwa SAUTI ili wote tusikie inaweza ikawa ni staili yake yakutaka TUSIKILIZE na tusiangalie kwa kuwa udhaifu wake upo wazi zaidi UKIMWANGALI  kwa kuwa waweza kustukia ni mtoa jicho na wapenda kupewa JICHO wanastukia kiutoa jicho ni ZOBA.:-(


Swali
  • Si kunauwezekano mkao wa wazo hili umekaa sawa?

Ndio,...
..... kumbuka tu ingawa KIPAYUKWACHO ili kumchekesha KIPENZI MLENGWA ambaye inafikiriwa akichekelea KINENWACHO anapunguza makali ya kukataa IKIFIKIA muda MAZINGIRA YAKIKAA SAWA ya kuombwa SEHEMU ZAKE ANUAI cha weza kuwa ni MATUSI kwa wengine,....
.... UPAYUKAJI pia  ambao unadhalilisha wengine kwa ajili ya kumchekesha MLENGWA bado ni UDHAIFU kwa APAYUKAYE.:-(



Ndio,...
.... STAILI ya KUJISHEBEDUA mbele ya UJIPENDEKEZAYE KWAKE ili kuonekana SPESHO  kwa umlengaye huku ukidhalilisha wengine,...
....labda ndicho kihakikishiacho UMATI udhaifu  wa ajitutumuaye.:-(


Swali:
  • Sasa nini kwani HUNIELEWI? Lione vile!:-(

Ni wazo tu hili MKURUGENZI ingawa ruksa kununa!

Hebu Busta Rhymes abadili kwa  ndude-Touch it



Busta Rhymes na Pharell wadunge-Lyte ya ass on fire



Busta Rhymes na Janet Jackson warudishe-What's it gonna be



Au tu Nerd warudishe -Lap Dance

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:43 am  

Mtakatifu ujumbe huu wa leo ni mkali na pia unaonekana una mlengwa...:-(

Mija Shija Sayi 8:58 am  

Yasinta umenena!! Ila kukaa kimya nako kama una suluhisho si vyema. Inasemekana hapa duniani ujanja kuwahi!!!!

Ni wazo tu.........

Simon Kitururu 5:00 pm  

@Da Yasinta: Wala ujumbe huu hauna mlengwa maalumu mwaya!
@Da MIJA:Wala sibishi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP