Tukiangalia UTU kwa kuangalia MAANDALIZI ya MSICHANA siku ajuayo KWA MARA YA KWANZA anakwenda kumvulia MTU ampendaye NGUO!:-(
>> Thursday, September 23, 2010
[Tahadhari: Taralila inawazo dhaifu na ukilichungulia labda limekaa vibaya.:-(]
Maandalizi yoyote, yanayo na kwasababu
Siku ya kutoa yote, ukurutu si adabu
Kwa kuwa si kivyovyote, mtu huenda kwa babu
Andalizi la kuvua, ni silika tu ya utu.
Andao la msichana, kama funzo la silika
Na silika za msichana, UBINADAMU hakika
Za uchafu kuukana, hata usio hakika
Za BINADAMU za UTU , jifunze kwa MSICHANA.
Ya uvulana ya UTU , si kama ya kisichana
Yale yenye utukutu, mbele za watu mchana
Ya kukojolea vitu,mbele hata ya Anna
Hata soni haioni,na hilo si ni bayana?
Utajifunza tu KITU, kwa kufikiria UTU
Na uchi katika MTU, wengi ni KIPIMA utu.
Ya msichana ni UTU, hata yafichavyo KITU
Pasipo ya MSICHANA, ya MVULANA si kitu.
Swali:
- Unafikiri kila kitu kingekuwa KINAFANYWA kwa maandalizi kama ya siku ya kwanza wajua labda NANIHII inaweza KUNANILIWA -Tanzania kimaandalizi ya kutawala DUNIA unadhani tungekuwa wapi?
- Unauhakika andalizi la kukutana na mpenzi wako mara ya kwanza kwa nia ya kufanya dhambi ya asili aka UASHERATI hayana mchecheto kiasi kwamba kwa kujiandaa sana kuvaa ambavyo utamvulia mtu ukasahau KUSAFISHA nyumba, kula au kuwa uendacho kufanya ni DHAMBI Kikristo au KIISLAMU ingawa labda sio dhambi kibaolojia?
Ainisho la taralila:
Ndio,....
...UKIFIKIRIA unaweza kugundua shughuli za MAANDALIZI ni tofauti siku unuiapo na kujua kesho,....
..... utakwenda KUMSUTA Khadija au tu utafanya wa muhimu MTIHANI .
Na kujua ya kesho kibinadamu ni kawaida kwa kuwa labda leo umeshajua kuwa utasikia njaa tena kesho ,....
.... kwa hiyo labda MAANDALI ya kama kesho utakula tena ni maandalizi tofauti kidogo na umeyazoea tokea uzaliwe na kwa hayo HUJIHAMI.
Ila,...
... kumbuka tu KATIKA SWALA HILOHILO LA MSOSI kama itakuwa ni kweli kwako KWA MARA YA kwanza utakula KONOKONO wa kuchemshwa KESHO,...
.. na kwenu konokono hamjawahikusikia ni chakula ,waweza kujikuta unajiandaa vizuri katika zoezi zima la kukabiliana na HILO BONGE la msosi kwa wastaarabu WAFARANSA hasa kama lengo ni kujifanya sio mshamba kwa wastaarabu WAFARANSA katika yako ya KUJIHAMI.:-(
Swali:
- AU?
Ndio,...
... nakubali HII HOJA ya maandalizi ya MSICHANA siku ya kwanza aliyoamua kuwa leo atamvulia mtu/MVULANA mpaka kificha eneo ANUAI angeiandika tu vizuri zaidi MSICHANA ambaye kashapitia hilo ndani ya safari ndefu za mpaka NATAKA -SITAKI, Baba MKALI, unajua hii ni dhambi ila nakupenda,....nk..... ila baada ya kusimuliwa na MOJA ya hawahawa FLOWERS aka MSICHANAZ jinsi maandalizi ya siku hiyo muhimu yaliyonuwiwa kwa hiari yawezavyo kuwa na shughuli tofauti kabisa KIMAANDALIZI na zenye umakini wa hali ya juu,....
....nikapata MOTISHA wa leo kujiaanda sana katika shughuli zangu kwa kuwa ghafla nikajistukia labda KILA SIKU ikiandaliwa kwa umakini ina nafasi kubwa ya mafanikio zaidi hata ikiwa fanikio lenyewe kwa KIKISTO ni dhambi ,...
....na Kwa KI BUDHA si dhambi ila BUDHA anafanya lifikiriwe zaidi bila VITISHO.:-(
....na Kwa KI BUDHA si dhambi ila BUDHA anafanya lifikiriwe zaidi bila VITISHO.:-(
Swali:
- Si unakumbuka lakini inasemekana wasichana wengi hata baada ya kujiandaa sana kwa shughuli nzima ya uasherati wa mara ya kwanza , BAADA YA shughuli huwa hawawi na uhakika kama maandalizi yalilipa kwa kuwa bado hubakia na hisia labda SHUGHULI haikufanywa kwa maringo yenye UFANISI wenye kiwango cha kutosha?
- Hivi MHESHIMIWA, hivi LILE halikufanyi ufikirie na HILI?
Ni moja tu ya WAZO MHESHIMIWA na wala usijihangaishe sana kulielewa kama HUKULIELEWA!:-(
Moja kwa moja katika kubadili mkao hapa kijiweni Trombone SHORTY aachie-Somethin' Beautiful
Bilal arudie-Soul SISTA
Au tu Method Man na D'angelo wamalizie tu kwa-Break ups 2 make ups
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
nanukuu "Tukiangalia UTU kwa kuangalia MAANDALIZI ya MSICHANA siku ajuayo KWA MARA YA KWANZA anakwenda kumvulia MTU ampendaye NGUO!:-(" Duh! mtakatifu Simon hapa kazi ipo!!
Maandalizi ni sifa ya utukufu, hata `kamvulana kanavyohangaika siku akikubaliwa kuwa kamsichana kana kuja, anahaha kiasi kwamba hata kuku akidonoa mlangoni kwa bahati mbaya atasema
'karibu mpenzi'
Swali: Hivi msichana akimvulia nguo mvulana wake kwa mara ya kwanza, huyo mvulana atakuwa kavaa, na huyoo mvulana itakuwa mara yake ya kwanza kuchungulia nyeti za wasichana?
Emu-Three! Mmmh!
Ila mkuu hii imekaa viabaya ile mbaya...lol!
Mtakatifu ya leo kubwa kuliko tena taralila imesindikizwa na mashairi.
mkuu hivi leo umewaza nini? nashindwa kufahamu niseme nini.
@Da Yasinta: Mmmh!:-(
@emu-three: Swali gumu hilo.:-(
@Kadinali Chacha: :-)
@Askofu Fadhy: :-)
Post a Comment