Ni rahisi kuongelea uwezekano wa kuwa RAIS NYERERE hakuwa na VIMADA wengi kama RAIS JACOB ZUMA,...
>> Friday, September 10, 2010
.... kuliko kuongelea ni jinsi gani RAIS Mikail SERGEYEVICH Gorbachev alikosea KUENDESHA NCHI ya URUSI kama tu RAIS Kambarage NYERERE alivyokosea kuiendesha TANZANIA
kwa kinagaunaga kama siri za uendeshaji nchi huzijui ,HUNA UZOEFU, na pia vyanzo vyako vya data za nini kiutekelezaji VINATAKIWA VIFANYIKE na KWA STAILI ya MKAO GANI hutoka tu kwa ambao KAMA Mheshimiwa AJUZA hawajawahi kutekeleza kitu.
kwa kinagaunaga kama siri za uendeshaji nchi huzijui ,HUNA UZOEFU, na pia vyanzo vyako vya data za nini kiutekelezaji VINATAKIWA VIFANYIKE na KWA STAILI ya MKAO GANI hutoka tu kwa ambao KAMA Mheshimiwa AJUZA hawajawahi kutekeleza kitu.
:-(
Swali:
- Kwani ni kweli kuna la kushangaza ikiwa WATU wanajadili kirahisi tetesi za labda Dr Slaa ana demu kama Rais KIKWETE ukizingatia ugumu wa kuongelea TEKNIKALITIZI za KISIASA na mikakati yake ya jinsi gani ya kutekeleza kikweli na KITEKELEZEKE na kufanya HIGHWAYS za Dar-es SALAAM zisiwe na msongamano wa magari kama zile za TUKUYU?
- Ushachunguza elimu za WALALAMIKIAO udaku halafu ukaoanisha na kwanini kama wewe ni mfanya biashara mwenye nia ya kuuza biashara yenye wateja wengi sharti uuze UDAKU?
Ndio,...
... maswala ya kuongelea jinsi NYERERE alivyokosea ni magumu kwa mtu wa kawaida ambaye hajawahi kuwa RAIS au hata angalau AMIRI JESHI MKUU wa JESHI LA MGAMBO,...
...na ni rahisi kumuongelea Rais MKAPA kama mtu wa kawaida MWANAUME na si o kama RAIS mwenye URAIS USIOUFAHAMU kwa kuwa KIRAHISI ukimuongelea kama BINADAMU wakawaida ambaye akila sana ANAWEZA KUVIMBIWA,...
....unaweza kuunganisha KIRAHISI kuwa kwakuwa RAIS MKAPA ni MWANAUME kama wanaume wengine wowote basi;...
Kabla sijaendelea:
- SI MHESHIMIWA unakumbuka kucheza kwa tahadhari na wazo langu katika TARALILA hii na STAILI yake YAKUSHUSHWA ili kunielewa naongelea nini ingawa SI LAZIMA unielewe?
Au niulize tu kinamna:
- Unafikiri kuanza kwa mbeya apendaye udaku KUONGELEA MAMBO BINAFSI ya WATU na MKAKATI wa PASHKUNA aliye choshwa na udaku kuacha kuongelea mambo ya watu NANI ana kazi ngumu?
PIA,...
...labda ni BUSARA za KIBINADAMU PIA , kuchagua kuongelea mambo RAHISI ya watu,....
.... ukizingatia MAISHA YENYEWE MAGUMU tayari KITU KIFANYACHO labda ni matumizi mabaya ya muda baada ya kukomaliwa na maumivu ya MAISHA NDANI YA SIKU halafu tena uendelee tena na kujiumiza kichwa kwa kujadili mambo usiyoyajua kama ya ni jinsi gani KAWAWA alifanikisha VIJIJI vya UJAMAA KIUTEKELEZAJI viwepo wakati MADIWANI mpaka WAKUU WA WILAYA na ----,----,-----wanashindwa kufanikisha mtaani KWAO watu wafyeke majani au angalau wazibue mitaro ya kupitisha maji machafu hata kwa KIPOROJO tu.:-(NIMEACHA WAZO HILI MHESHIMIWA kwa KULIKATIZA na usikonde kama HUNIELEWI ukizingatia kutoelewa ni moja ya sifa BOMBA ya ubinadamu wa BIN-adamu!:-(
Hebu twende Zimbabwe mwaka 1978 ili - Thomas Mapfumo na The Blacks Unlimited walete ndude-KUYAURA
Tubakie Zimbabwe Thomas Mapfumo amwage mdinyo-Moyo WANGU
Au tu baki tu na Oliver Mtukudzi na Ringo Madlingozi wakite TENA kitu mwanana -Into Yami
Basi bwana Oliver Mtukudzi ngojea tu atubakize hapa hapa Zimbabwe kwa shughuli nzito iitwayo-Todii
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kuyaura... unipeleka mpaka ungonini nilikuwa na bibi yake baba alikuwa anaitwa kuyaura ikiwa na maana kuachama au kupika mwaya.. ahsante
Post a Comment