Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

LABDA pigisha lugha yako PUNYETO , mie we' SIKUELEWI!:-(

>> Friday, September 10, 2010

Pigisha lugha punyeto, saidia icheue
Hata kwa wale wazito, ipenye iwafikie
Ujumbe ule MZITO, na gizani uchipue

Na zogo si kusikia , kwetu wenye masikio


Elezea tuelewe, kama weye wayajua
YA werevu kama wewe, yale tusiyoyajua
Maisha ni kama jiwe, kwa ugumu  we wajua
Elezea wayajue, wale wenye masikio.


Tupo wenye masikio, na shida si kusikia
Akili si  mtindio, ukisema twasikia
Hata bila  zile mbio, taratibu twajongea
Tatizo ni hiyo  lugha, hatwelewi wacholonga

Kusikia twasikia, na kusoma tunasoma
MASIHA twamsikia, ZERO anachokisema
Kile tunachosikia, neno BATA   kama MAMA
Makali ya lugha yake,  hayajadindisha ncha



Aongea MAULANA, ustadh nakwambia
YA leo kama tu jana, yasimama nakimbia
Ujumbe ule mwanana, matusi ninadhania
Pigisha lugha punyeto,na  makali yake noa

Uprofesa  wa lugha, sio wake mwenye lugha
Kama lugha ni kilugha, kwa iliyo yake lugha
Kama TUZO lake lugha, hatwelewi kisa lugha.
Sema nasi tuelewe, pigisha lughako nyeto


Chakusema ka´unacho, sema  nasi tuelewe
Tafadhali  ulonacho, usikigide mwenyewe
Hata kama ni kichocho,utwambie tukwelewe
Umewahi kuchunguza , kama weye twakwelewa?


Swali:
  • Unaielewa yangu LUGHA?
  • Unadhani mie nakuelewa hata kama najua yako lugha?
  • Unadhania UNAUHAKIKA hakuna faida za kutoelewa yasemwayo katika  LUGHA uielewayo?
  • Unafikiri  ujumbe ni muhimu sana hata katika NDOMBOLO YA SOLO ya KIFARANSA kwa wanakijiji cha MKULANGA ambao KIFARANSA hakipandi wapendao NDOMBOLO?

NIMEACHA  wazo  MKURUGENZI  na kama hujastukia niandikacho hapa ni KISWAHILI na ni ruksa KUTOELEWA madhumuni ya BARUA HII Mkuu KAMA  unahisi lugha yangu yahitaji PUNYETO!:-(

Mie naenda zangu chooni  kufanikisha ,...
.....  IJUMAA NJEMA na WIkienDI NJema MHESHIMIWA !!




Hebu moja kwa moja TAYLOR MALI anyuke shairi-The The Impotence of Proofreading




Saul WILLIAMS amwage-Coded Language


Au tu DJ Krust na Saul Williams warudie - Coded Language

10 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:17 pm  

Mt. Duh!:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 4:11 pm  

Hitimisho: Hakuna aelewaye kila tu, si lazima kuelewa kila kitu na hakuna sababu wala faida ya kuelewa kila kitu.

Kwingineko: wakati mwingine tunaweza kupenda tunavyovielewa lakini mara nyingi hata hivyo tunapenda tusivyovielewa. Hali kadhalika japo tunaweza kuelewa tusivyovipenda mara nyingi pia hatupendi tuvielewavyo - mpapurano wa mambo aiii!!!

Godwin Habib Meghji 9:17 pm  

Prof Masangu umenisaidia kwa commeny yako. maana nilikuwa naumiza kichwa kuelewa. "hakuna aelewaye kila kitu" Si lazima kuelewa kila kitu, Ila ni vizuri kujaribu kuelewa kila kitu...

Masangu Matondo Nzuzullima 1:23 pm  

Godwin, hata mimi sijui kama nimeelewa.

Napenda niongezee hapo kwenye comment yako kwamba kujaribu kuelewa kila kitu ni kupoteza muda kwa sababu haiwezekani. Isitoshe, tunajuaje kwamba sasa tunaelewa tukielewacho?

malkiory 2:05 pm  

Unajua ukisoma kwa jujuu posti za Kitururu mara moja mtu anaweza kufikiria jamaa ni mpenda matusi! mfano maneno kama vile PUNYETO, MALAYA, n.k ambayo mwandishi hupendelea kuyatumia katika kuwa puzzle wasomaji wake.

Nilichojifunza katika posti za mtakatifu Simon ni kwamba zimejaa mantiki ya hali ya juu. Shida moja ni kwamba mtu kama mimi ambaye nimezoe kukotoa zaidi kuliko fasihi, huwa inanichukua muda kidogo kungamua tafsiri halisi.

emu-three 9:59 am  

Kwa kweli lugha nipana, yajaza hata dunia.Ni kama uonavyo upeo wa macho yako, sivyo mwisho wa dunia. Ajuayo Simon, yaweza yakawa usiku wa giza kwangu mimi au kwako,
lakini ukitaka cha mvunguni sharti uiname!

chib 5:21 pm  

Mimi naona sikuelewa

Anonymous 8:09 pm  

Nimpenda hii, nimpenda, nimpenda... nimelewa, nimkubali... yote bila kupiga lugha punyeto...hehehe

Anonymous 8:10 pm  

sijalewa ila nimeelewa!!!

Simon Kitururu 8:32 am  

@Wote: Mmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP