Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Simulizi za aina tofauti tofauti za MNATO!

>> Thursday, September 09, 2010

[Tahadhari: Kunauwezekano taralila hii ni ya KIJINGA.:-(]




MNATO!

Kwa kawaida MNATO ni KING'ANG'ANIZI,....
....na ndio maana HATA kwenye mfereji wa tako wa aliyevaa GWAGURO na asiyestukia wawezakuta MNATO umeng'ang'ania na wala sio KWA KUJIBANZA hata kama sio kwa juhudi ZILE  za KIDONDA NDUGU kinukacho na INZI.:-(

Mnato ni kama MBALAMWEZI,....
.... na kwenye tundu lenye kipenyo,  MNATO waweza kujipenyeza hata kwa WIZI.:-(

Swali. 
  • AU?

MNATO ni KUNATA,....
.... na katika KUNASIA  silazima kuwe na vitu viwili ili kitu kiweze KUNATA.:-(



Swali::
  • AU?
MNATO ni zaidi ya HISIA,...
.....na ingawa KARATASI MOJA ikikunjwa yaweza kutosha katika kutimiza mahitaji ya KUNATISHA MNATO ingawa labda wahitaji mchango wa angalau MBWA DUME na JIKE kama nia ni kushuhudia mnato wenye HISIA.:-(



MNATO!

Swali:
  • Hivi MHESHIMIWA weye huwa huna tabia za kuchokozwa FIKIRA na mambo madogo dogo YA KIJINGA kama vile ya kushuhudia MHESHIMIWA umheshimuye suruali imeingia mnato na ukashindwa KUMSTUA kitu ambacho kikakufanya ujiulize NI MAMBO MANGAPI MUHIMU ambayo umeyastukia na unashindwa MUHUSIKA kumstua?

  • SI unajua kushindwa kumstua mtu kwa jambo dogo kama lile la kuwa ANA PUA CHAFU a.ka KAMASI KAVU linachungulia katika pua ya mheshimiwa kutokana na mheshimiwa kukosea mahesabu ya kuchamba pua baada ya bonge la MPENGO laweza kusababisha mazoea ya kutostua mtu angalau akumbuke kutumia KONDOMU wakati anaenda kujifariji na MKE wa mtu ujuaye kwa kuwa wewe ni daktari wake kuwa ana UKIMWI au kaswende haijapona vizuri?



Twende zaidi kidogo ya simulizi la MNATO!:-(

Mambo madogo madogo na labda ya KIJINGA yanaweza kuamsha fikira tofauti na zenye JAMBO MUHIMU tu na la BUSARA kama unamchezo wakuangalia jambo dogo kama MPIRA na kufikiria kujenga STEDIAMU yenye  ukumbi wa mikutano , CHUMBA cha kumbukumbu na historia  za MICHEZO Tanzania, mradi wa choo cha kulipia karibu na hilo LIUANJA, hoteli isaidiayo watu kula ili waweze kufanikiwa kunya ,....

.... ikiwa vyote wala havina uhusiano wa moja kwa moja na huo MPIRA au wafanyakazi wa ADIDAS watengenezao huo mpira ambao wala hawauchezi mpira.:-(

Swali:
  • Si unajua unaweza kuona choo na badala ya kufikiria kunya AU wala kukojoa, ukapata fikira za biashara ya RANGI za nyumba kisa ukuta wa choo mchafu hasa kutokana na baadhi ya wabunifu kuchambia UKUTA?

NI wazo tu hili MHESHIMIWA usikonde!:-(

Hebu George Carlin aongelee-Stuff



George Carlin aendelee na -Our similarities



Au hebu tu House of PAIN watulize mshawasha kwa-Jump around




Asanteni sana WADAU wote,...
...mkiwemo hawa waliomo katika baadhi ya picha nilizo zidaka juzi ya janayake.:-(

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP