Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NI silika ya kawaida ya KIBINADAMU PIA kwa mtu kutaka kukuchungulia UKIKAA uchi!:-(

>> Saturday, September 18, 2010

[Tahadhari: Jihadhari na vijineno kama `` uchi´´, .....,..... katika TARALILA HII  kwa kuwa labda havina maana uifikiriayo!:-(]





Ya KIBINADAMU yanaviitwavyo TABIA,...
... lakini ikumbukwe tu kuwa TABIA NZURI na TABIA MBAYA ni vitu tu alivyojitungia BINADAMU  kama tu alivyojitungia kuosha mpaka ndizi zenye MAGANDA kutokana na aliyojifunza ya USAFI yale  ya DUNIA.:-(



Kama tu binadamu ajifunzavyo kunywa BIA,...
.... ndivyo ajifunzavyo TABIA ya kuvaa chupi  hasa baada ya kustukia  BINADAMU WAKUBWA waanzapo  kukaripia au hata KUMUANGALIA KWA KIJICHOPAPO,...


.....  hasa kwa VISA MTOTO ASIVYOVIJUA vya haohao wenyewe WAKUBWA  kuhisi MWANADAMU  huyo MTOTO maungo yake ya chini yameanza kuchora RAMANI zenye ratiba zianzazokushamiri katika kuashiria ukubwa UWATIAO VISHAWISHI WAKUBWA   au kuchonga ya wakumbushayo wakubwa zisizo MWANANA ZILE NDUDE ZILIZOWAKUTA  waliposhambuliwa  KATIKA yao  YA KIKUBWA   ambazo zinaanza kufananafanana NA ZA MTOTO  sehemu za siri ZISIZO hata na matumizi ya kikubwa   YA ZAIDI YA  kikubwa yale YA MSALANI  katika makubwa ya DUNIA.:-(




Swali:
  • AU?



Kaa vizuri basi wewe BINADAMU,...
... kwa kuwa ingawa tukikuchungulia utalalamika kama uliyojifunza ya KIUSTAARABU WA KIBINADAMU YALIVYOKUFUNZA,...


...lakini kumbuka na akuchunguliaye afanyacho ni  TABIA SAHIHI yenye haki na sifa zote za KIBINADAMU.:-(

Kwa hiyo labda usitutie MAJARIBU  kwa ujuayo tutayachungulia hata yale ya UFISADI wako utakayo kuyaficha kama vile KWA HAYO haumwagi kinamna damu,...
.... hata kama wajua  kile KIMEREMETACHO ambacho kikawaida twajua si rahisi kuwa uchi hivyo wakiweka wazi na kutaka  tusikipige chabo labda hata KUKICHOKONOA kwa kulalamika  kama vile uchi wenye damu.:-(

Swali:
  • Kiheshima  ukimuona MHESHIMIWA kakaa uchi na kutotaka kumchungulia vizuri uone zaidi eneo ANUAI ,... unafikiri inamaana hamu ya kuchungulia HUNA WAKATI HUO  kwa kuwa kitabia weye MSTAARABU ambaye umefudhu katika kufundwa yaliyo uchi yafumbiwe macho?


NI ANGALIZO tu katika WAZO HILI  na usikonde kama hunielewi  MHESHIMIWA ! 
Si unajua tena lugha kicheche, ndio maana KATIKA  matumizi ya lugha yanaweza kurahisisha KUTOELEWEKA pia!.:-(


Tubadili kwa kuwapata tena Amadou na Mariam wadinye - Je pense a toi



Au tu tuwapate Soul Brothers waendelee na-Umshado


Au tu na Sipho MABUSE arudie ndude-Jive Soweto

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:48 pm  

Mmmmmhhh:-(

MARKUS MPANGALA 2:15 pm  

Katika kufikirisha yatendekayo chini ya zuria tu eti hata lile jekundu kwakuwa lina rangi.... basi kila kionekanacho kimeshika chupa ya BIA kinalewa na kujikojolea. Sasa maajabu ni kuvaa pekozi ambalo kiuhalisi ni bonge la mtindo wa kujifananisha na kijana wa zamani wakati mvi zinauzwa ili ujue kuwa weye ni limzeee au likijana la zamani. Au katika fikra za kitakatifu ni utakatifu... au ni ANGALIZO....
katika blogu ya kusoma hata ukashindwa kutoa maoni kwakuwa inakushindwa labda mfumo wa umeng'enywaji wa fikra hukondeshwa kwakuwa anuai wazo linashindwa kushibishibwa na kiandikio kikikosea mcharazo wa herufi na kuleta kisu badala ya busu.

Kweli watu waonekanao kuwa wanaonekana kwakuwa huonwa ni wale wale wachukiao kunenwa ati wanaonekana kama wanakula kitimua moto la kitimoto na kuungia na viungo vya binzari na nyongeza ya kitoweo cha senene.

Heeeee kumbe TABIA.... na waonekanao kuwa wana tabia ni wanatabia kwakuwa tu wanajua ni tabia yao kuwanogesha na kuwatemea mate wale waliojipaka kinyesi ili kumkimbia mgaombo wa jiji....

EDNA 4:06 pm  

Haaaa,yaani nimchungulie mheshimiwa nanilii....? hahahaa Mie thimo kabithaa.

o'Wambura Ng'wanambiti! 5:44 pm  

tatizo si kuchungulia bali nia ya chungulio hilo :-(

Simon Kitururu 7:28 am  

@Wote:Mmmmmhh!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP