Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Mtoto wa MJINI anaweza kudhania UMEMTUKANA ukimuita ``MKULIMA´´ .:-(

>> Wednesday, September 22, 2010

Kuna uwezekano JEMBE linauwezo wakumtupa MKULIMA,...

... kama mambo yote  kimuonekano MWENYE trekta ndio mjanja kuliko mtumia jembe.:-(

Na kwa kuwa wajanja wanatumia PENI na KOMPUTA hata katika kuiba HATA ya WAKULIMA,...
.... yaweza kueleweka ukikuta VIJANA KIJIWENI  huku wakikuona UNACHEMSHA katika jitihada zako za kuwaambia wakashike jembe  huku wanashuhudia waheshimiwao katika TAIFA  wako mbali na JEMBE.:-(

Swali:
 • Kwani unabisha MKULIMA WA JEMBE  na FISADI MTUMIA PENI  wakishindana katika utamaduni wetu mpya wa UMISS aka FASHENI SHOO labda kiulaini tu ni  FISADI ndio atashinda hata angalau kwa kufikiriwa ndiye mwenye paja laini?


Hata bila kuchunguza sana utastukia kuna shughuli zinadharaulika TANZANIA !:-(

Swali
 • Unabisha?

Na tokea watajirikao haraka haraka KWA NJIA ZISIZO HALALI  kuonekana WAJANJA,...
.... karibu shughuli zote hata AMBAZO ZILIKUWA ZINAHESHIMIKA ambazo HUWEZI KULIA vizuri OFISINI ukatajirika  KIRAHISI zimepungua heshima zikiwemo:
 • Ualimu
 • Unesi
 • ...nk ,
 • Ukulima

Ndio kuna waoanishao  bado UKULIMA  na vitu NISHAI,....
.....na labda kumbuka hilo ukiwa unatafakari waongeleao sera za KILIMO KWANZA huwa wanamlenga nani na wanageuzaje swala zima la MVUTO wa UKULIMA ambao TANZANIA ndio inaudai ni UTI  WA MGONGO.

Ndio UKULIMA ni mgumu na JAMII inaabudu wapendao ulaini wa shughuli na lolote gumu kama HALINA pesa kuonekana NISHAI,...
...na kwa bahati mbaya JAMII haifunzi watu kufikiria  MAMBO kiundani  kwa hizyo ni MWENYE BUSARA KUDHARAULIWA  kirahisi kisa hawezi kununua BIA na kutuliza mawazo yeye anakunywa GONGO.:-(.


Swali
 • AU?
 • Si ukiwa MWIZI na bonge la BENZI unaweza kusikilizwa kuliko ukiwa MKUU wa SHULE ya KIJIJI mwenye busara  na baiskeli yako tu ya zamani ya aina ya SWALA?Ukitaka kujua TANZANIA tuko matatani,.....
... angalia hata hizi PROFESHENI muhimu tu zitazamwavyo:

 • Walimu ambao ndio tegemeo la TAIFA katika kuondoa ujinga, wanadharauliwa hasa kisa hata mishahara yao tu haiwawezeshi kuishi vizuri.

 • Mapolisi walindao amani , hawana amani WAO WENYEWE  kwa kuwa hawawezikutegemea kazi wakaishi vizuri.
 • Manesi wahudumiao WAGONJWA  ndio kabisaa  hata sijui wanapata wapi nguvu za kuhangaika na wagonjwa NA MATAPISHI YAO bila kusahau UHARISHO siku nyingine, DAMUDAMU KWA SANA, ....wakati  wanadharaulika na mishahara yao ndio hivyo tena .:-(


 • Wakulima ndio hivyo tena - MJINI unaweza hata kukosa mchumba kwa kujulikana we MKULIMA kitu ambacho ni cha ajabu kwa kuwa bila WAKULIMA maakuli hakuna.:-(

Angalau sikuhizi WACHUNGAJI katika ujasiliamali wakujianzishia MAKANISA unaweza kujikuta  WANAOFANIKIWA KUWATISHA  vizuri WAUMINI WAO  kuhusu JEHANAMU wanaweza wakajikuta WANAPATA  sadaka nyingi kwa hiyo VIPRADO na angalau tu  MVINYO wa nyumbani ambao hukatwa katika bajeti ya MVINYO wa KANISANI  unaweza kukuta haukosekani nyumbani kwa MCHUNGAJI.:-(

NAWAZA TU KWA SAUTI  MHESHIMIWA usikonde!

Hebu  Jermiah arudie -Wizi Mtupu
Bonta aendelee katika ndude - Nauza Kura Yangu


Au tu Ras Lion na Joni Woka wabadili mkao kwa-HII KITU

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 1:46 am  

Mtoto wa mjini kumuita mkulima!!!, ha ha haaaaa. Umenikumbusha visa vya shuleni enzi hizo..
Hata na redio ya mkulima maarufu kama dudu proof

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! 7:46 am  

..ni sawa na kumwambia mporipori...lol!

asichojua mtu ni kuwa mkulima yaweza kuwa chochote kama mmoja wa viongozi kujiita mtoto wa mkulima kisha ukastukia dili kuwa ni bonge la fisadi :-(

Markus Mpangala 2:01 pm  

Duh!!!!! mwanafalsafani

SIMON KITURURU 4:13 pm  

@CHIB: :-)
@Kadinali CHACHA o'WAMBURA:Ndio hapooo sasa!:-(
@Mkuu Markus: Mmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP