Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Leo katika shukrani: AHKSANTE MJUSI!

>> Friday, September 24, 2010

ASANTE MJUSI,..
.... kwa kupunguza mbu na mende TANZANIA!

Asante sana na kwa binamu zako  MABUIBUI unaoshirikiananao  EWE  jemedari MJUSI ,...
... kwa kupunguza hata INZI  kwa  uwezo wenu udhaniwao NI MDOGO kwa kuwa  hamna nguvu za ubongo kama wa BINADAMU ambao na miakili yao,...
....INZI na MBU wawatoa jasho hapa  TANZANIA!:-(


Swali:
  • Huwa unakumbuka kuwa kuna vitu uvidharauvyo kama tu PANYA ambavyo vina mchango tu mkubwa wa muhimu kwako  hata katika tu kufanya kuwe na uwiano katika mazingira ili kuwe na neema kwako?

  • SI unakumbuka kuna WATU uwadharauo  pia ambao ndio WAKUSAIDIAO  kwa mengi AMBAYO NI MUHIMU KWAKO , hata YALE YAFANYAYO ujisikie vizuri chooni kwa kuwa walilima chakula kikusaidiacho uende chooni , WALIKIJENGA CHOO ili usijisaidie majanini, na LABDA wakakisafisha pia choo ili ujisaidie kwa uroda na kufaidika na harufu utengenezazo mwenyewe tu kwa kuwa choo ni kisafi?
  • Unauhakika INZI na MBU hawahitajiki DUNIANI  kwa kuwa weye lengo lako ni KUWAUA?


Tukiachana na HILO,.....
....pamoja na yale mengine kama  ya MINYOO, makonokono na MAJONGOO yadharauliwayo,...
....ingawa ni muhimu katika udongo wa MAZAO YAPENDWAYO NA MTUZ  kurutubika;.....

ASANTENI WOTE enyi  NDUGU, marafiki, NYIE NISIOWAJUA ,wale NISIOWAFAHAMU na pia ENYI MAADUI kwa yote  WAPENDWA!

Nawatakieni IJUMAA na WIKIENDI Mwanana!

Na moja kwa moja hebu RENEGADES warudie wimbo wa Lionel Ritchie katika Steel Pans ULE ujulikanao kama-ALL night longAu tu na  MBARAKA Mwinshehe atulize TU  mshawasha kwa kuongelea nifikiriacho sasa hivi ambacho ni -SHIDA

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDNA 8:55 pm  

Ijumaa njema kwako pia Mtakatifu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP