Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

VYAKULA vinazidi kuwa BANDIA kama sura za WAIGIZA SINEMA wa HOLLYWOOD!:-(

>> Thursday, September 23, 2010



Tunakokwenda LABDA badala ya watu kulima MPUNGA,...
....wanasayansi watagundua jinsi ya kulima UBWABWA ULIOIVA tayari ,...

...au tu  hata kuotesha PILAU ILIYOIVA na YA MOTO kama ILE ikufanyayo upende kuhudhuria MISIBA YA WATU USIOWAJUA kwenye sahani yako.:-(

Hebu tufuatilie mjadala wa GENETICALLY  modified food ....









OKEI,...
...najaribu tu KUKUMBUSHIA kuwa kuna vitu watu walavyo siku hizi ambavyo viko kwenye majaribio tu na madhara yake hakuna ayajuaye.

Na kwa sisi tuishio nchi masikini ,...
....kirahisi tu tunafanyiwa majaribio hata bila kujua kwa sababu kwanza ni MASIKINI tudhaniao kila UITWAO  msaada ni MSAADA ,...
....na pia hatukawii kushindwa kujilisha wenyewe.:-(


Cha ajabu ni kwamba,....
... vyakula ambavyo sasa hivi kuna watu katika nchi kama BONGO  wanaviona ni vya KIMASIKINI hasa kwa staili vilimwavyo,...
.... hivyo ndivyo vyazidi kuthaminiwa na MATAJIRI nchi zilizoendelea hasa kutokana na kutoathiriwa na madawa au tu kuchezewa na wataalamu wa kisayansi.:-(



Swali pembeni kidogo ya chupi ya hoja:
  • SI unajua asilimia kubwa ya sura za WACHEZA SINEMA wa siku hizi wa HOLLYWOOD uwaonao katika sinema za KIMAREKANI ukiachilia mbali NYONYOZ BANDIA ni kweli pia hata SURA zao sio halisia?

BASI BWANA MKUU nimeacha WAZO !

Na moja kwa moja ngojea FELA KUTI arudie kitu-Coffin for HEAD of STATE




Au tu FELA arudie kudunga-Mr Grammarticologylisationalism is the Boss

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

chib 10:03 am  

Ni kweli, wenye nazo wanatafuta kwa nguvu vyakula asilia, wakinunua vyakula kutoka kwetu, wanataka maelezo kamili wapi kimelimwa, mbegu gani zilitumika na aina ya mbolea
hata Michele Obama ana bustani ya mboga hapo white house anayolima kwa njia asilia.
Sie tunalishwa vyakula bandia, wanasubiri baada ya miaka 20 tutakuwaje. :-((

Yasinta Ngonyani 11:13 am  

Hakika sasa naweza kuamini ni mwisho wa dunia maana kila kitu ni bandia:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP