Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STORI za MAKANDE hunoga zaidi kama UMSIMULIAYE machachari ya MAKANDE anajua MAKANDE ni nini.:-(

>> Thursday, September 16, 2010

Ni vigumu  KUMCHEKESHA MTU kwa stori ya matatizo ya  kutafuta kitu cha kuchambia katika choo cha STENDI,...

.... kama  umpaye stori ya KUCHEKESHA YA  jinsi  MTU ajistukiavyo ana ubunifu  katika kutatua tatizo la makokoneo katika choo cha stendi hajui  NI NINI CHOO , achilia mbali hiyo STENDI.:-(

Swali:
  • UMESHAWAHI kuongelea utamu wa  PIZZA MBAYA kwa asiye jua PIZZA  ni nini ukaeleweka?

  • Na umeshawahi kuleta utani wa USHUZI uliotokana na tumizi MADHUBUTI la MLO WENYE MAHARAGE na ukashindwa kueleweka na ambaye amewahi kula MAHARAGE na kujua juhudi zake MAHARAGE katika kutengeneza gesi fulani ambazo ajuaye MAHARAGE kwa kuwa amewahi kula maharage anajua  NI NINI KICHEKESHACHO na  kama hacheki ni staili yako tu ya kumwaga kichekesho ndio HAICHEKESHI?

Ndio,...
....nahisi ni kweli kuwa KIKUCHEKESHACHO kinahitaji ujuzi,...
... na kama  kuna kikuchekeshacho basi labda jua kwa uhakika katika HICHO kunakitu vizuri tu UNAKIJUA.:-(
Ndio,...
... stori za MAKANDE  zinaeleweka vizuri kama tu STORI za MATOKE na kukaanga KUMBIKUMBI zielewekavyo kwa ajuaye KUMBIKUMBI ni nini.:-(


Swali:
  • Hivi unakumbuka KUMBIKUMBI ni MCHWA?
NI wazo tu hili KUMBUKA MHESHIMIWA hata kama sasa hivi umevaa bonge la BICHIKOMA na wala sio BUGALUU!:-(Ngojea SAMMY DAVIS Jr arudie -Mr BojanglesMr SAMMY DAVIS Jr aendelee
Au tu Michael JACKSON apeirispekti kuwa SAMMY DAVIS Jr katika WASANII WEUSI  tokea enzi yeye  alikuwa  MKALI kitu nikubalianacho naye katika  ndude -YOU were THERE

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

emu-three 2:10 pm  

Nimekumbuka ule usemi wa akunyimaye kunde kakupunguzia mashuzi...
Atakayezungumzia jambo,huenda analijua kama sio mbeya, ni kama aisifuye mvua huwa imemnyea, kwani hutasifia kitu kama hujakionja utamu wake.
Ni kweli kama hali halisi huijui sidhani utafungua mdomo kama sio mpayukaji, mdomo kama vuvuzela...nakuunga mkono mkuu Simon!

Masangu Matondo Nzuzullima 8:33 pm  

Ndiyo maana huwa nagomba mtu anapojenga hoja ambayo imeegemea katika falsafa au kanuni ambayo sisi wasomaji wengine twaweza tusiielewe. Halafu tukipuyanga anaanza kutugombesha. Tazama maoni yangu kuhusu suala hili hapa:

http://koeromkundi.blogspot.com/2010/07/markus-hayati-mwalimu-nyerere.html

Baba Mtakatifu - endelea kutusomesha.

By the way - makande ndiyo Masangu kwa Kisukuma!!!

Markus Mpangala 3:04 pm  

wajuzi kama wazua methali, ni kama watwanga pilipili ni kama watunga mashairi.... JE WOTE WANGELIKUWA WAJUZI INGELIKUWAJE? si unajua pamoja na ukosefu wa ujuzi kile kisimuliwacho unakielewa kuwa hakikuchekeshi lakini umeelewa kuwa kilikuwa kinakusudia kuwa kichekesho????

Kwani mbinu za kuwa bonge la bingwa wa kudeku upenyo wa bafu la mama sarafina lina ufundi wa matege ya jicho ama mguu? Si wajuzi nao wanakuwa na simulizi ambazo hutoa harufu mdomoni? na wangelikuwa wajuzi kuna kitu kingeitwa MAHIRI? au labda GWIJI au labda mwanazuoni aliyekomaa kama solo thang??
kwanza siyo kila ujuzi unachekesha hata kama kuna umahiri wa kusimulia wa shaban robert au wole soyinka. kama tu ujuzi wa shigongo usionichekesha wala kunishtua hata kama anajulikana ni mjuzi....

si unajua wana hip hop ni wengi lakini waimbaji chiriku si wanasifiwa kwa zao sauti hata kama wana mashavu na koromeo la kugida ugimbi na mshikaji wa mjusi? Kumbe kila simulizi inakuwa na uhaba wa lugha anuai kujenga matumizi ya kubana pua ukiona simulizi za wazua methali....

NAIGA NAACHA TU MKUU

SIMON KITURURU 9:25 am  

@emu -three:Cha kusikitisha kuna wakati hasa katika kuwasikiliza wanasiasa wetu huwa napatahisia wengi tu wanafungua midomo kupayuka bila hali halisi kuijua.:-(

@Mwl Masangu Matondo Nzuzullima:Sikujua kuwa Makande ndiyo Masangu.:-)

@Markus: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP