Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UTAMU wa ASALI usifuatilie NYUKI ASIYEJUA KUOSHA MIKONO na utamu wa NYAMA YA KUKU WA KIENYEJI usifuatilie KUKU katika matembezi yake alikula NINI!:-(

>> Saturday, September 18, 2010

Na  UTAMU wa sehemu za siri za MTU,...
... labda zahitaji kufumbia macho kumbukumbu kuwa SEHEMU ZA SIRI shughuli zake chafu nyingine ni NINI.:-(


Swali:
  •  SI unajua ukifuatilia ya JIKO CHAFU ambayo chakula chake umeshakigida unaweza kuharisha bure hata kama chakula kilikuwa salama?
  • Si MHESHIMIWA unatambua hili ni wazo tu ?

Ndio,...
...ukiufuatilia sana UTAMU ,...
... unaweza kustukia mpaka utamu ULIVYOVALISHWA ulimbwende mpaka na chembechembe za haja kubwa,....


... na kung'amua kuwa labda siri ya UTAMU si UTAMU,....
....na UCHUNGU labda  ni moja ya siri za MSELEBUKO  WAKATI UNAUKATIKIA SINDIMBA UTAMU  kwa kuwa labda kitengenezacho ile kitu TAMU kimetengenezwa kwa machungu au tu vile uvichukiavyo kwa kunuka na  VILE wala usivyovioanisha  na ujisikiavyo  wakati NANIHII tamu.:-(

Ni wazo tu hili lenye KIBIONGO Mheshimiwa!
Na nakutakia WIKIENDI mwanana MKUU!

Moja kwa moja ngojea NAS na DAMIAN MARLEY wadinye -LAND of PROMISE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 1:37 pm  

ukijitia kufatilia sana unaweza kujikuta unakuwa mtu wa njaa siku zote

Markus Mpangala 2:24 pm  

katika kujua kuwa ukikaa baharini kuna upepo mwanana wakati unasahau kuwa hewa ni kiburudisho ukitafutacho na ukikosa unawasha na kiyoyozi au lie ndude hilohilo la pangaboi.labda gizani, ukiwa unachungulia tundu la hewa itolewayo yenye harufu ya kunukia na pafyumu itengenezwayo na madikodiko ya maharagwe ya mbeya ni sawa na hewa ya kufuatilia ile ya midambwada ya kondeni kuwa si muhimu.

AU
wakati naaiga kuandika kama mtakatifu nikifutalia utakatifu kumbe miye siyo mtakatifu na wazo la neno ndani ya kitoweo cha utakatifu ni muwali lazima nifuatilie.

SASA Mtani wangu Fadhy shemeji, katika kujua tunafuatilia na katika kuona harufu ya manukato apakayo binadamu ni kwakuwa tu yananukia kwa ampendaye basi huku wengine tunahisi ukoko mkavu. au katika kujua damu ya mbu ni kuambukizwa malaria. je tutafuatilia panadol au?

Ni wazo la kiheshimiwa tu hili lenye bonge la kimbaumbau?

SIMON KITURURU 7:27 am  

Mmmmmmh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP