Kitu chanya kiduchu katika RIPOTI kuhusu TANZANIA kwenye HABARI ZA DUNIA !
>> Wednesday, September 22, 2010
MKUU nashea tu ripoti ya Global Campaign for Education;
20 September 2010 The Global Campaign for Education today launched their report 'Back to School?' of the worst places to be a school child in 2010.......
Kigusacho TANZANIA ambacho kinauchanya ni :
AU kwa lugha ya kitaalamu:
Na hicho MIMI BINAFSI naamini ni kitu kizuri .:-(
'Back to School?' - the worst places to be a school child.
20 September 2010 The Global Campaign for Education today launched their report 'Back to School?' of the worst places to be a school child in 2010.......
Kigusacho TANZANIA ambacho kinauchanya ni :
Progress is being made as in Tanzania three million extra children are now able to go to school.
AU kwa lugha ya kitaalamu:
Ripoti inadai kuna ongezeko la watoto milioni tatu wenyeuwezo wa kwenda SHULE Tanzania.
Na hicho MIMI BINAFSI naamini ni kitu kizuri .:-(
Ukitaka kujua zaidi nenda kwenye ripoti kwa kubofya HAPA
KUMBUKA najaribu kuegemea kwenye UCHANYA kwa kuwa halihalisi si nzuri bado .:-(
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kitururu, haya mafanikio japo mimi bado nitayaita ni mafanikio ya kisiasa zaidi ya kitaalamu au kielimu.
Unajua hata wazo la Nyerere la elimu kwa wote lilikuwa chanya sana. Lakini hili la kukimbilia kiasi/quantity kuliko ubora/quality itatufanya vilema wa zao la mfumo wetu wa elimu.
Kama utakumbuka programu ya UPE (Universal Primary Education). Nyerere kama mwanasiasa alikuwa sahihi kutangaza sera ya elimu kwa wote, lakini je maandalizi yalikuwepo? jibu ni hapana.
Je walimu walikuwepo wa kutoa elimu hiyo kwa kila mtu? jibu ni hapana. Hapo sasa ni pale ambapo hata waliofeli darasa la saba walilazimika kuwa walimu. Tusichanganye siasa na elimu.
@Mkuu Malkiory Matiya: Usemalo ni kweli kabisa.
Kazi ipo!
Ila katika ulimwengu wa habari ambao kila siku kisikikacho ni NEGATIVE nilijisikia ahueni angalau kwa kitu fulani ingawa undani wa kitu icho yaweza kuwa uozo.:-8
TAWIRE mwalimu Matiya.
Pengine tujisifie kwa kujenga shule ambazo hadhi yake ni Day Care Centres. ni sehemu ya watoto kucheza mbali na nyumbani. kati ya hizo wanafunzi huingia gabbage in na wahitimu wake ni gabbage out. Gazeti la Mwananchi la jana lilitoa picha ya ubao wa mwalimu wa kingereza. sentensi zilizokuwepo moja ilisomeka "where are do you come from?"
Chakujiuliza ni :
Je tusubiri tupate shule na walimu wa uhakika au tujikongoje na yale tuliyonayo ambayo ni uozo?
Kazi ipo!:-(
Yah, uzuri hutangazwa kwa mbwembwe, nasi hatuna budi kujipongeza!
Lakini baada ya kujipongeza, sasa twatakiwa kujiuliza `kwenda shule tu inatosha, ...mmmh, unafika shule unakuta majengo, mnacheza mwisho, mnaingia darasana, mnakaa chini sakafuni, vumbini nk,...mwalimu yuko wapi, hakuna ...mnacheza weee, mmmh, mwisho wa miaka saba, umemaliza shule...what is your name? mmmmh hivi mwalimu alitufundisha hilo kweli...mmmh, kwanza hatukuwa na mwalimu wa `maneno kama hayo' ....
Wenzenu watoto wa wakubwa wamepelekwa ulaya, au wapi sijui, wakirudi, mzungu kasingiziwa, `yes yes sana', na unajua tena makampuni mengi ni ya `wakuja' kama hujuii yes, bwana kalagabahwe, `hujasoma'!
Ni hayo tu mkuu!
Post a Comment