Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda MUNGU siku hizi anawasikiliza WACHINA zaidi!:-(

>> Wednesday, September 08, 2010

[Tahadhari: HUU ni mtazamo wa KIBINADAMU tu Zee la Jazba:-(!]


Kama ni maswala ya kukua kwa UCHUMI na mafanikio mengine mbalimbali YA NCHI NA WATU wa nchi fulanifulani siku hizi,...
.... labda kuna ambaye atadai anauhakika MUNGU anawasikiliza zaidi WAHINDI na WACHINA ambao wengi wao hawafuati MUNGU Kikristo wala KIISLAMU.:-(


Swali
  • AU?
  • Lakini si MUNGU wako wakati unaibiwa inasemekana ni MUNGU wa akuibiaye pia kwa hiyo mafanikio ya akuibiaye labda yamewezekana kwa msaada wa Mungu?



Lakini LABDA,...
......YA MUNGU,...
.... ayajuaye ni MUNGU MWENYEWE,...
..... na juhudi za BINADAMU ZA kutaka KUYAJUA SANA ya MUNGU ni kupoteza MUDA hasa ukizingatia hata YA KIBINADAMU yale ya JIRANI YAKO, rafikiyo au hata NDUGUYO ,...


....hata yale madogo madogo ya alichofanya BAFUNI KISIRI LEO ambacho kibusara za kibinadamu HUFANYWA KWA SIRI ni SHUGHULI NZITO KUYAJUA  au hata KUYAHISI  hasa KAMA tu mtu aka   JIRANI YAKO, rafikiyo au hata NDUGUYO  hudhaniwa anaaibu halafu ni KIBONGE YA MHESHIMIWA kwa hivyo KISIRI  halambi kamasi au tu hawezi  kujisikilizisha furaha  ndogo ndogo ZA SIRI mwenyewe kisiri.:-(


NI wazo tu hili MHESHIMIWA na kuna uwezekano LIMEPINDA!:-(

Bila kusahau: Kwa watakao kututumua makalio; MCHINA OYEEE!!!!


Hebu George Carlin anyambulishe ya -God BLESS America



 2PAC adinye-God BLESS the DEAD



Amkeni Choir washushe ngoma nzito iitwayo-Mimi Yesu




Au tu Sonu Nigam, Shreya Ghosal na Salim Merchant walete ndude-Shukran ALLAH

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 10:53 am  

limungu la kichina na kihindi ni dili kweli sasa

Yasinta Ngonyani 1:05 pm  

Kaaazi kweli kweli...mmmhh nadhani hapa sisemi kitu...

Simon Kitururu 4:59 pm  

@Komandoo Kamala + Da Yasinta: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP