LABDA ni rahisi kugeuza MANENO yageuke VITENDO kama hatuangalii KAMA hicho NI KITENDO sahihi wakati una PAKA a.k.a nyau MALAYA na utakacho mpaka katika TENDO ni watoto wa MBWA WAKO malaya!:-(
>> Monday, September 27, 2010
[Tahadhari: Wazo limepinda!:-(]
Wakati tunaangalia UWEZEKANO wa KILA MTU aongeaye kuwa anaweza KUTENDA,...
.... ni rahisi kugundua KUWA kwa kuwa hata kuanguka ni KITENDO,...
... LABDA kila mtu tukiomba aanguke sakafuni ,....
... kila mtu LABDA anaweza KUANGUKA SAKAFUNI kama hatujaongezea masharti AANGUKEJE kwa maringo na aangukie nini,...
Katika hatua ya kwanza ya kulainisha taralila na tukiwarudi PAKA na MBWA malaya wakati lengo ni kulenga tu swala hilo hilo la MANENO na VITENDO,...
Kuwa na PAKA JIKE malaya,...
.... wakati unania ya kuzalisha MBWA,....
.... kunauwezekano bado unasilaha ya mafanikio ya kupata ZE TOTOZ ZA MBWA kama unajua kutumia ulichonacho ambacho katika mfano huu ni PAKA JIKE MALAYA kwa kuwa upo uwezekano kuwa kuna mwenye MBWA JIKE MALAYA ambaye naye shida yake ni PAKA JIKE malaya na katika kutatua TATIZO mkibadilishana tu mlivyonavyo- tatizo SOLVED ,....
Swali:
- Si unakuwa suluhisho la tatizo lako inaweza kuwa ndio tatizo la MWENZIO?
- Si unakumbuka hata mababu katika kutatua matatizo yao walitumia mpaka BARTER TRADE kama suluhisho kwa kuwa mwenye magimbi asiye na MWIDU au MLENDA aliweza kubadilishana na mwenye MWIDU au MLENDA ikiwa ni katika kutatua uhaba wa ASICHONACHO ingawa pia twajua wenye ALMASI enzi za MKOLONI waliopewa PIPI katika kubadilisha BIDHAA kutokana na MAHITAJI?
- Au?
Tatizo tu linaweza kujitokeza iwapo WEWE kwa kuwa unajua una PAKA malaya,...
... ukafikiri basi unaweza kumlazimisha AJIFUNGUE watoto wa MBWA .:-(Swali:
- Unafikiri unaweza KULAZIMISHA mfumo wa NCHI MBOVU uzalishe MAENDELEO hasa kama MAENDELEO huhitaji MFUMO MZURI ufanyao kazi mpaka kwa mjumbe wa nyumba kumikumi hata kama RAIS MBOVU?
Kwahiyo labda,...
.... ILI maneno yageuke KITENDO sahihi KIHITAJIWACHO,...
.... twahitaji zaidi ya MSEMAJI,....
.... ingawa bado labda MSEMAJI ni muhimu vilevile katika uwezekano wa TENDO kufanyika KISAHIHI likiwa ni tendo SAHIHI kwa kuwa ,....
... mara nyingi ingawa tendo la kubinya JIPU ni tendo ,....
... waweza kukuta bado UKWELI NI KWAMBA tendo sahihi ni kutolibinya JIPU na kungojea liive vizuri ili lipasuliwe.:-(.Na kuhusu lile swala la kuwa una PAKA na wahitaji MBWA,....
... huwezi kujua ,...
... LAKINI labda ungeweza kusubiri PAKA azae watoto wa paka na baadaye uwauze paka na kununua MBWA malaya atakaye kutotoleshea watoto wa mbwa BAADAYE.:-(
Swali :
- Umenielewa?
- Kwani ni kwanini unafikiri WAKATI UNAHARAKA unafikiri unahitaji uwe na haraka sana hata katika kuelewa au tu katika ......nyingine?
Tuendelee na Curtis Mayfield katika mdinyo-Freddy is DEAD
Curtis Mayfield arudie kudinya-Superfly
Na hatuwezi kuacha kipele bila kukunwa na hii kucha-Pusherman
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mkuu nichotaka kusikia ni mabadiliko Tanzania. Miaka 49 ya ukoloni wa mtanzania kwa mtanzania imetosha.
Mimi siyo mshabiki wa Chama chochote cha siasa lakini namwangalia mtu mwenye vision na uchungu na nchi yake. Hakika ningukuwa Tanzania kura yangu ingeenda kwa Dr. Slaa.
Ahadi ni kawaida kwa mwanasiasa yeyote yule, lakini hata Obama ameshaanza kurudisha vikosi vyake toka Iraq. Hivyo kila kitu kinawezekana mkuu. Roma haikujengwa siku moja.
@ Mkuu Malkiory Matya: Nakubaliana nawe 100%. Nachodokonyoa ni kukumbusha kuwa sio rahisi na ndio maana kuna wafuasi wa OBAMA wanafikiri kashindwa kazi wakati kuna mengi aliyoahidi katimiza. Nachojaribu kusema ni kwamba hii kitu tukizungumzia NCHI yoyote kuna watakao katishwa tamaa hasa ukizingatia hata Wanasiasa wafikiriwao ndio wema bado wao ni binadamu na sio MALAIKA.
Na Mkuu yote hii ni katika kuwaza tu hasa kutokana na wadau niliowapa sikio hivi karibuni waniwekavyo mkao wa kuwaza.:-(
Tuko Pamoja MKUU!
...ati haraka? si katika vitu vyote kwa kuwa wawezakuta mlevi anaogopa kuwa na haraka ya kulewa....ili tu agide zaidi wake ulabu...lol!
Ndiyo...na labda ndo zake sababu mlala-puu kushadadia mafisadi ili tu apate kanga nk bila kuwa na haraka ya maendeleo :-(
ni mpaka hapo utakapostukia dili kuwa alileweshwa maneno ya kipuuzi akawa na haraka ya 'rambaramba' akiuza maendeleo ya ukweli :-(
Post a Comment