Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

DUNIA imejaa MAKELELE ya WENGINE na usipoangalia WEWE MWENYEWE unaweza USIJISIKIE hata UKIJAMBA!.:-(

>> Friday, September 10, 2010Sitanii,...
... DUNIA imejaa MAKELELE YA WENGINE kitu kifanyacho:--

  • Ukienda SOKONI  kununua NYANYA waweza kujikuta umerudi na NYAMA ambazo umenunua kutokana na vishawishi vya mtu mwingine.:-(
  • Ukienda KAZINI waweza kujikuta HUJISIKILIZI kwa kuwa hapo umsikilizaye ni BOSI WAKO na labda hata pia wafanyakazi tu wengine.:-(
  • Ukiwa SHULENI katika mkao wa kuhakikisha UNAFAULU waweza kujikuta hujisikilizi kwa kuwa hapo umsikilizaye ni MWALIMU ambaye naye anakufundisha yasiyo yake kwa kutumia vitabu vya WENGINE.:-(
  • Ukitembea mtaani  wawezajikuta HUJISIKILIZI kwa kuwa MDADA badala ya KUJISIKILIZA uko bize unakwepa magari huku ukihakikisha mwendo wako katika kutingisha ile kitu SINGIDA -DODOMA huharibu mwendo wa maringo kwa kuwa umestukia UNATUMBULIWA macho na watokwa udenda hata wale WAUME wa vimwana wengine.:-(
  • Ukienda KANISANI/MSIKITINI waweza kujikuta hujisikilizi kwa kuwa hapo ni kawaida kumsikiliza PADRE/SHEKHE mjuzi wa kukutishia hata JEHANAMU  kwa kutumia  mifano ya TISHA -TOTO ya yaliyowakuta watu WENGINE.:-(
  • Nyumbani unaweza kujikuta hujisikilizi kwa kuwa asikilizwaye zaidi kwenu  ni BABA  na wala sio wewe au vidubwana vingine.:-(
Swali:
  • Mheshimiwa umejisikiliza leo ANGALAU ili kutambua ndani yako ni nini ile KITU roho inapenda?
  • Si MHESHIMIWA kunauwezekano UKIJISIKILIZA VYEMA  SASA HIVI unaweza hata kujistukia kuwa unanyege kitu ambacho labda  kutokana na MAKELELE ya wengine umechelewa kukistukia kitu ambacho sasa hivi kinazalisha TATIZO jingine?


Ndio,....
...kwa bahati mbaya UKIJISIKILIZA VIZURI unaweza pia kustukia kuwa NI KWELI UNAUMWA kitu ambacho sio KIBAYA ,....

.....na UJISIKIAVYO  wala sio uchovu tu wa kawaida ambao ungependa kuuoanisha na uliyofanya jana usiku bila nguo , ulichofanya shambani katika miondoko ya KILIMO KWANZA au tu visingizio tu VINGINE.:-(NI WAZO tu hili MKUBWA!

Basi tupitie tu tena NIGERIA tukaonywe madhara ya shule na NKEM OWOH katika pambio-School NA goodthing.
IJUMAA NJEMA MHESHIMIWA!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP