Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!

>> Sunday, March 30, 2008

Habari yako ndugu...
Ifuatayo ni taarifa kwa vyombo vya habari. Tunategemea ushirikiano wako.
Asante!


Fomu za tuzo za Vinara zatolewa!

Fomu za ushiriki katika kinyang'anyiro cha kuwania Tuzo za Vinara wa
filamu Tanzania 2007/8 zimeanza rasmi kutolewa jana katika vituo
mbalimbali nchini ikiwa ni hatua ya kwanza kabla ya kutolewa kwa tuzo
hizo.
Tuzo hizo zitakazotolewa kwa mara ya kwanza nchini, zimeandaliwa na
kampuni ya One Game Promotions na kudhaminiwa na Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya dovu Power Malt.
Mratibu tuzo hizo, Khadija Khalili, amesema kuwa, kutokana na sababu
zilizo nje ya uwezo wao, fomu hizo zilichelewa kutoka kwa tarehe ya
awali hivyo kusababisha kuongezwa kwa muda wa kurejeshwa fomu na
kupokea filamu zitakazoshiriki katika tuzo hizo hadi Aprili 18 badala
ya Machi 31 kama ilivyotangazwa awali.
Alisema watengenezaji wa filamu nchini wanakaribishwa kutuma nakala za
filamu zilizotengenezwa kati ya Januari 2007 hadi Machi 31, 2008, kwa
ajili ya kuwania tuzo hizo.
Khalili alisema kuwa, jopo la majaji litakutana baada ya Aprili 18
kuchagua watakaowania tuzo za Vinara wa Filamu Tanzania 2008.
Alisema fomu za kushiriki kuwania tuzo hizo zinapatikana katika vituo
vilivyotangazwa awali ambavyo ni ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) kwa Omari Mayanga, pia zinapatikana kwa wasambazaji wa filamu
ambao ni Wananchi Wote, GMC, Kapico na Game First Quality.
"Fomu zilizojazwa na nakala ya filamu iliyopo kwenye mfumo wa VCD na
DVD zitumwe kwenye ofisi za BASATA zilizopo Ilala Bungoni jijini Dar
es Salaam au ofisi ya One Game Promotion," alisema.
Vipengele vitavyoangaliwa na majaji katika filamu hizo kuwa ni Filamu
Bora ya Mwaka, Muigizaji Bora wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji Bora wa
Mwaka wa Kike, Muigizaji Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kiume, Muigizaji
Bora Chipukizi wa Mwaka wa Kike, Mwongozaji Sinema Bora wa Mwaka,
Mchekeshaji Bora wa Mwaka, Mwandishi Bora wa Filamu, Mtunzi Bora wa
Filamu, Filamu Bora ya kutisha, Muigizaji Mwandamizii Bora wa kike
(supporting actor), Muigizaji Bora Mwandamizi wa Kike, Adui Bora
kwenye Filamu, Wimbo Bora wa Mwaka (Sound Track), Mhariri Bora wa
Filamu ambao wote watapata tuzo na zawadi. Pia itatolewa tuzo ya
heshima kwa wale waliotoa machango wao kukuza sanaa nchini.

DUH!
Tulia na Mighty Sparrow... baada ya kupata ujumbve hapo juu....

Endelea na COCOA TEA akizidi kukumbusha kuhusu .....BARACK OBAMA

Read more...

ILE KITU NATAKA!

Binadamu tajiri......!
Hapungukiwi ILE KITU NATAKA

Umasikini humfanya mtu awe na busara katika
uchaguzi wa ILE KITU NATAKA

Matajiri wenye uhakika na dengu, malazi na...,
utacheka uchaguzi wao wa ILE KITU NATAKA

Ferarri kwao ni ILE KITU NATAKA,
wakati Corolla ni aina ileile ya ILE KITU NATAKA

Kabla ya kufa binadamu...,
hupungukiwi ILE KITU NATAKA

Kwa sababu......
Ukweli ni kwamba unataka ILE KITU NATAKA.

JUMAPILI NJEMA!
Twende Kameruni kumalizia na msanii MANU DIBANGO

Akikupa CADANCE


Au endelea na MANU DIBANGO katika staili hiii, akiwa na LES LITTLES...

Read more...

ZILE NYIMBO ZIIMBWAZO KATIKA LUGHA TUSIZOELEWA!Duh!

Starehe za miziki, mara nyingi ni jinsi ikusuuzavyo roho.

Hebu mpate huyu dada akiimba wimbo kama asikiavyo....

(Kama unaujua wimbo wa Mariah Carey, unajua naongelea nini!:-))


Katika enzi zangu za kutembelea vilabu, gongo , mbege, konyagi, dodoma waini, na... nilistukia kuwa nyimbo za injili zinapigwa baa, chobisi na... hata kupita pale nyumbani kwa walokole au nyumbani kwa mchungaji.

Maswala ya ndombolo ya solo, sukusu, kibinda nkoi au kibinda nanihii......nk., yalinigundulisha kuwa, naweza kucheza miziki nisiyoelewa inasema nini ,na demu wa nyumba ya jirani aniringiaye, nikampata kama bonasi.

Lakini...
.......kisa cha kumpata hausigeli wa nyumba ya jirani kilikuwa na utata!
Katika kumpata Zubeda wa jirani, ilihitaji kuonyesha ujuzi wa kuondoka Ngwasuma dingiridingiri mpaka chini, nilikatika kisawasa, nilicheza sana, wengine waweza wakasema nilidansi sana, halafu mpaka yule wahusika wamuaminio kuwa ni muhimu ndani ya maeneo, akaja mezani kwangu, halafu akaonyesha kuzimia staili yangu .(Samahani kwa msio na .... au hata msio na uumee ,...au wale wasio na uke , njugu , peremende na....nahisi mnastori zenu za yule hausiboi, baba mkwe,mchaga wa kioski cha jirani, mpare fundi viatu au....yule aliyeng'ang'ania nanihiii na....)

DUH!
Lakini yule Mkongo, Mbongo, na.. aimbaye kwa lugha ya lingala,kikerewe na... au.... na.... atakuwa ni miongoni mwa watu ambao hata kabla sijafa nakumbuka kawimbo fulani ambako sikuelewa anasema nini. Lakini kalikuwa kawimbo kazuri.

Yule bingwa maeneo , si lazima aelewe msanii katika fani anasema nini ndani ya utundu au hata maisha.
KITU KIKUHUSUCHO , UTAELEWA KICHINA, kigagagigikoko kama embe dodo limekuchekea!

DUH!

Swali:

  • Ushawahi kuelewa mbwa anazungumza lugha gani wakati kakukenulia meno tayari kukuondolea ile siri uifichayo kuwa wewe muoga?

Hebu msikilize kidogo PAPA SAN akilia, kabla sijaendelea kunong'ona.


Nyimbo ni lugha!
Wewe, mimi na yeye, tunajaribu mara nyingine kusikiliza MUHUBIRI , SHEKHE, BABA, HAUSI GELI , MLONDA, na... anasema nini.

AU?

Tupo wengi tutamaindi ukikosea tundu la choo cha shimo na kunya pembeni.

AU?

SAMAHANI!

Nilitaka kusema tuko wengi tutachukia ukikosea sentensi au neno ndani ya lugha.

Nisemavyo si usikiavyo!
Naweza nikakuimbia mpaka juzi yake....
Naweza kukutongoza mpaka nikalia.....

Atanikililia nanihii!
Unajua tabasamu naweza nisipate?

USIKIACHO NDICHO ULICHOSIKIA.

AU?

Swali:
  • Hapa naandika maandishi, huhisi kama unasikia sauti yangu kuwa nasema nanihii kwa kutumia sauti?
  • AU?
Naacha!
Mpate Vanessa Paradis


Swali:

  • Hivi wewe unaongea lugha gani?
  • Unaijua hiyo lugha eeh?
DUH!

Read more...

UKIMUOMBEA MTU KWA MWENYEZI MUNGU , UNAMUOMBEA NINI?

Samahani ! Sijaenda Kanisani!
Samahani! Sijaenda msikitini!
Samahani!Sijaenda kwenye sinagogi wala pale... na pale....

DUH!

Najua lakini maswala ya ijumaa , jumapili , juma kuminatatu, asubuhi ,jioni na...kama mtu wa imani, inaweza kumaanisha kitu fulani.

AU?

Duh!

N
ashukuru wewe umeenda msikitini, kanisani , kule wa Hindu , na...... , halafu ukakumbuka kuniombea.

AU?

Nami sijaenda na sikuenda maeneo ya kumuomba MWENYEZI MUWEZESHA YOTE, lakini nimekuombea na nakuombea.
Nahisi katika vitabu fulani , ukisoma haraka haraka , unaweza kuamini mimi ni miongoni mwa wale watoto wapotevu.

Swali:

  • Katika vitabu fulani ,si ni ukweli mwana mpotevu anastukia akipata kibano ,baaada ya muda fulani uitwao baadaye na kutubu?
  • Lakini wewe ambaye hujapotea, UJAPOATE?
  • Ushatubu dhambi zako?
  • Hivi ni dini gani zile zikuwezeshazo kutubu ukizidisha nanihino?
  • Au hauna dhambi?

Nashukuru wewe umeenda maeneo ya kukutana au kukuruhusu kupiga magoti , kuinama na........................ katika kunyenyekea na kumtii Mwenyezi Mungu kiheshima, katika hali ya kusawazisha matatizo , dhambi zako na pia kutuombea sisi wenye dhambi.
Swali:
  • Unauhakika ukipiga magoti , kuinama , kurukaruka, MWENYEZI MUNGU hatastukia kuwa kisiri, unatamani nanihiii......ngono na asiye wako, kilaji , kudokoa mboga jikoni , au kuiba mahindi ya kuchoma shamba la jirani?

AU?

Swali:
  • Weye ambaye una uhakika wa ...Unaweza kunipiga jiwe kwa sababu nimepotea?
  • Una uhakika?
Staili ya kupotea, kwa jina jingine inaitwa UBINADAMU.
Naamini kabisa, bila ya nguvu za Mwenyezi Mungu, Allah, Yahweh , Murungu na...., unaweza kutamani kakitu kaliko katazwa kinamna.

Swali:
  • Ushawahi kutamani nanihino ambayo imekatazwa na baba?(Samahani!Nilimaanisha iliyokatazwa na DINI fulani uifuatayo iongeayo ukweli mtupu?)
Staili ya kupotea, ni ubinadamu.

Naacha!

Swali:
  • Kwanini unahisi kwa imani yako wewe au yule , una.. au anaweza kuamini nimepotea kwa sababu nimesema nimepotea?
  • Umepotea?
  • Kwanini imaniyako inakuponza ulazimike kuamini kuwa ni ukweli?

SAMAHANI ! NAJIULIZA TU!Usinitukane ukiwa chooni au pale sehemu ulipo.

AU?

Msikilize MUNISHI....



Duh!
Namsikiliza Marvin Gaye lakini vile vile!Msikilize basi.

AU?

BAADAYE BASI!

Read more...

Nani Hapendi kuwa BWANA MKUBWA kama Robert Mugabe?

>> Friday, March 28, 2008

Sikatai ukweli kuwa wapo binadamu ambao hawapendi kuwa mabwana mkubwa kinamna!

Lakini...
...ukifuatilia vitu fulani, utastukia kuwa asilimia kubwa ya binadamu wote wakiwa katika ulaji , ni vigumu kuwatoa mezani.

Ubwana mkubwa una ulaji wake.
Ubwana mkubwa hauko tu katika vitu au taito za ofisi zilizo waziwazi.

Mtu anaweza akakutawala kisaikolojia , ukatawalika bila hata kujua ukurupuke vipi.
Mabwana mkubwa wako kisaikolojia pia hawataki kuachia kiti hicho.

Swali:

  • Ushawahi kusikia Mwalimu wako , hata baada ya wewe kumzidi madarasa akakataa kiti cha ukweli kwamba ni mwalimu wako?

  • Ushawahi kumstukia aliyekufundisha ukafaulu , awezavyo kutumia kisa hicho kutengeneza ubwana mkubwa sehemu nyingine ? Namaana ,hujawahi kusikia jamaa akisema kitu kama ;`` nilimfundisha Nyerere mimi! ´´, kwa sababu Nyerere baabu kubwa?


UKIFIKIRIA SANA, HAKUNA ALIYEWAHI KUWA KATIKA ULAJI AKAUACHIA KIRAHISI .

Katika Ubwana Mkubwa naamini :
  • Mwalimu Nyerere alifikia kiwango ambacho hakuhitaji awe ofisini ili awe Bwana Mkubwa,bado alikuwa Bwana Mkubwa. Angenyanyua simu wewe kama Rais ungejibu na kusema; ndio Mzee!
  • Bill Clinton bado anauhusudu ubwana mkubwa na ndio moja ya motisha yake ya kufanya kila njia Mrs Clinton awe ofisini.
  • Putin wa Russia , kuachia Uraisi na kuchukua Uwaziri Mkuu ni dalili hizo hizo za kutotaka kuondoka jikoni.
  • Fidel Castro , kumuachia mdogo wake Urais na kuwa mshauri Mkuu wa serikali, ni dalili za kutotaka kucheza mbali.

  • Wanasiasa Tanzania ambao tokea tuzaliwe mpaka leo hii ni waheshimiwa wabunge, ambao wameacha kulala bungeni kutokana na televisheni............ni katika swala hilohilo la ugumu wa kuachia kakitu ulikozoea.

Naweza kuendelea milele........


Lakini watu wanasahau kuwa...........
....Ubwana mkubwa unakuweka katika sehemu ambayo mahitaji yako husikilizwa kirahisi.

Kisaikolojia, ubwana mkubwa unaleta utiifu kwa walengwa iwe kwa nguvu za mabavu au vinginevyo.
  • Mtoto anaweza akasababisha utii amri zake za kununuliwa pipi kwa kuililia hadharani na wewe ukatii amri.
  • Kama unapenda michezo ya ubaba na mama chumbani, unaweza ukajikuta unatii amri ya kununua ile zawadi ambayo ulikuwa unafikiria ni kupoteza fedha , ili usinuniwe chumbani.

Nachojaribu kusema ni:

Robert Mugabe na miaka yake themanini na ushe, hataki kuachia Urais na baadhi ya watu wanashangaa sana, lakini si kitu cha kushangaza.Wengi wangependa kufanya kama yeye kama mazingira yange ruhusu.

Jamaa kanogewa!

Lakini pia....
....
tusisahau kuwa kuna watu kama hawa akina Robert Mugabe ambao wanaonekana wabovu, wakiachia maeneo, yanakuwa kama Iraki. (Siumecheki jinsi hata upinzani ulivyogawanyika Zimbabwe?)

Unakumbuka mambo yakumtoa Saddam Hussein katika uongozi Iraki kwasababu alikuwa mtu mbaya anaye ua watu wengi, yamesababisha watu wazuri walioingia kurekebisha nchi, kutengeneza mazingira ambayo yanaua watu wengi kwa siku kuliko hata mtu mbaya Saddam Hussein . (Lakini nafikiri unajua kisa cha kumtoa Saddam hakikua kwasababu muuaji.)

Sasa nachojaribu tena kusema ni;

Asilimia kubwa ya watu wakiustukia Ubwana Mkubwa katika anga yoyote ya maisha ,ni vigumu kuiachia.

  • Mtoto akijua akilialia anapewa atakacho, hawezi kuacha kulialia.
  • Mwanadada akigundua akikunyima nanihii inakusababisha usikilize matakwa yake ya kumuachia akacheze mdundiko, atakunyima nanihii.
  • Dume zima likistukia likinuna lifikapo nyumbani haliulizwi kwanini limechelewa kurudi nyumbani, litanuna halafu na maji ya kuoga litachemshiwa.

Wakati unangalia wikiendi hii Robert Mugabe anavyogombania ubwana Mkubwa, kumbuka kuwa inawezekana hata mimi na wewe kila siku tunagombania kubakia na ubwana mkubwa kinamna , ubwana mkubwa ambao kama unatimiza angalau kupata nanihii, hatutaki kuuachia kirahisi.

Swali:
  • Ushawahi kuona mzee anakubali kirahisi kuwa kaishiwa nguvu na anahitaji msaada wako kumpeleka chooni na kumchamba?
WIKIENDI NJEMA!
Hebu twende SENEGAL kidogo kuwasikiliza hawa jamaa DAARA J wakikupa kibao ALLAH

Au endeleza tena na DAARA J live

Baadaye!

Read more...

Bikira Wawili Usiku wa Ndoa.

Usiku huu wa ndoa.....,
wote tuko butu.

Tufurahi kuanza ndoa.

Maswali ni mengi .
Nashindwa kukohoa.


Matarajio ya umati....
Kuna kitu tutaondoa.


Sijui tuzime taa , kabla hatuja chojoa?

Kama kipofu...,
.....amwongozaye kipofu,
dunia msitu.

Nani atatuokoa?


Tunajua tuna kucha zihitajizo kunoa.

Nani wakumuuliza jinsi ya kunoa?

Na...
....tusipojiuliza nani twa mkomoa?

--------------------------------------
Najaribu kuongelea jinsi dunia inavyobadilika haraka sasa hivi, na ukweli kwamba hakuna ajuaye kwa uhakika jinsi ya kukabili mambo kibao, kisiasa(wengine wanasema siasa ya China bado ni mbaya wakati inakuza uchumi) na , kiuchumi(angalia Marekani kila mtu anavyo ongelea ni njia gani ya kujikwamua), kimaisha, kidini(wengine watakuambia Uislamu bomba na bado wengine watakuambia mambo yote ni Usayantoloji),nk.

Kila mtu anavutia kwake,kwa sababu na uwezo wake wa ubongo wa kibinadamu.

AU?

DUH!
Tulia na Aaron Neville akikuambia TELL IT LIKE IT IS.

Pilipili ni kali, je tuzidi kuinunua?
Baadaye Basi!

Read more...

KIJIWENI NA ADUI AKUCHEKEAYE!

>> Thursday, March 27, 2008

Naweza kusema adui mzuri ni yule akuonyeshaye kuwa anakuchukia.

Kujua bomba la kitu!

Binadamu ni mjanja halafu hana uhakika, jambo ambalo hufanya wanadamu wengine wakuchekee ingawa moyoni mwao wanakujambia kinywani.

Lakini.....
...binadamu anaweza akawa anauhakika na nini anataka akufanyie cha kukudhuru lakini akakuchekea kwanza kabla haujakaa golini akulenge.

Swali:

  • Sasa akikuonyesha chuki halafu akajikuta anahitaji msaada wako hapo baadaye afanyeje?
  • Sasa akikuonyesha makucha yake ya uadui, akiwa na kiu utampa maji?
Lakini.....
.... matatizo ya adui akuchekeaye kama huna machale fulani, ndiye awezaye kukuumiza zaidi kunako. Akuchekeaye waweza ukajikuta ndiye awezaye kufikia ile sehemu yako ya siri ya maumivu.

Mapenzi yako alinacha na adui akuchekeaye utastukia machungu yake pale anapokuweka konani baada yakustukia umenasa.
Chuki itakayojitokeza baada ya wewe kunasa kutoka kwa adui akuchekeye, inaweza kusababisha ukumbuke sura ya mnuno wa adui uliyejua anakuchukia siku zote kama ilikuwa inakitabasamu fulani vile.

Swali:
  • Ushamchekea adui leo?

Maadui ndio wafanyao tuwathamini marafiki.
``Maadui ni muhimu sana´´; inaweza ikawa ni sentensi iletayo maana katika anga fulani.

DUH!

Unawakumbuka baadhi ya maadui hawa ambao inasadikika kuwa wanatudhuru Africa, Amerika, Ulaya , Asia na pote duniani?
Nina maanisha ya maadui hawa hapa:
  • Ujinga
  • Magonjwa
  • nk
Ngoja Niachie hapa kukuzingua Mkuu!

Lakini......
.... Chekewa na Mchekee!
.....Jifanye hujui au Jifanye umesahau!
Kumbuka tu kuwa katika lolote ufanyalo;
KUJUA UNAFANYA NINI NI BOMBA LA KITU, hata kama ujuacho ni busara ya kuwa hujui.

Ngoja YingYang Twins wakunong'oneze(samahani kwa lugha na wadada nusu uchi katika kideo) .

Read more...

NANI KAKUAMBIA KILA MTU ANAKWENDA BAA KWA FURAHA?

Asili ya uelewaji wako kitu, unaweza kujengwa na uzoefu ua ukosefu wa uzoefu wako katika jambo .
Tatizo liwakumbalo binadamu wawili tofauti katika uelewaji wa jambo moja, ni jinsi binadamu hawa wawili wanavyoweza kuwa wamejengeka tofauti kutokana na makuzi tofauti , mazingira tofauti au kutokana na ukweli kuwa hawa binadamu wawili ni tofauti.

Swali:

  • Ushawahi kuelewa ni kwanini binadamu wengine wengi(hasa wazungu), wanaongea na mbwa au paka wao kama wanaongea na mtu?
  • Unakumbuka wenye majonzi na wenye furaha unaweza kuwakuta msikitini au kanisani wakipata na kuwakilisha mahitaji yao ya kidini tofauti kwa pamoja mbele ya Mwenyezi Mungu?
Katika mwendo wa kuishi na kunyosheana vidole, imefikia wakati watu hujisahau na kudhani wanajua yote kuhusu watu wengine.
Maeneo, utawasikia watu kibao ambao wamejipa UTAALAMU WA KWANINI.
Taaluma hii ya kujipa ndio huamua mambo kibao kuhusu kwanini watu wengine wanaonekana au wanafanya hiki na kile.

  • Ni rahisi kufikiri kila uonacho kuhusu mtu fulani ni lazima ukielewe.
  • Ni rahisi kufikiri kuwa umekielewa uonacho.

Ngojea ni kupe kastori:

---------Hadithi! Hadithi!-----------

Hapo zamani za kale , wakati bado niko mdogo, mitaa ya Songea, nilikuwa nakatazwa kucheza mpira na unifomu za shule kutokana na udongo mwekundu wa Songea na sababu nyingine kadhaa. Nilikuwa nakatazwa kupitiliza saa kumi na mbili jioni michezoni hasa kutokana na wazazi kutaka kuhakikisha najisomea na kumalizia zile Home Work.

Niliyekuwa namuogopa sana kushikwa naye nikivunja sheria alikuwa ni Baba yangu. Kwa bahati mbaya ilikuwa inatokea mara kwa mara anayenidaka nacheza mpira au nimepitiliza muda ambao natakiwa kuwa nyumbani alikuwa Baba.

Mdingi alichokuwa anafanya kilikuwa kinawashangaza marafiki zangu! Alikuwa anaweza kuja kujiunga katika kushangilia au analeta stori na marafiki zangu na hata pipi anaweza akatununulia.

Kitu ambacho marafiki zangu walikuwa hawajui ni jinsi mimi jasho linavyonitoka, kwa maana pamoja na Mdingi kucheka nasi, ninlikuwa najua ni kibano gani nitapata pale tu nitakapofika nyumbani. Kwa sababu ilikuwa napata kibano cha kuotea mbali.

Lakini....
...Kesho yake nikikutana na marafiki zangu , hawakawii kusifia jinsi gani nilivyokuwa na Baba poa, kutokana na wao kutojua jinsi gani nilipata kibano pale nilipofika nyumbani baada ya kuachana nao.

-------Mwisho wa Hadithi-------

Dhumuni ya hadithi hii ni kutaka kumkumbusha jamaa huyu na yule kuwa , unaweza ukawaunaona kisehemu tu cha sura nzima ya kitu kama utakuwa unajenga hoja kutokana na kumuona mwanadada yule kavaa kimini na yuko uchochoroni. Anaweza akawa kakimbia kibano ndani kwao na hayuko uchochoroni kuuza nanihiii.

Swali:
  • Unafikiri mtu akiwa na ze bia au ze gongo mbele yake , maana yake anafurahia maisha?
  • Ushawahi kujisikia vizuri baada ya kulia?
  • Ushawahi kulia kwa furaha?
DUH!

Kuna watu wanafuraha nyumbani.
Lakini kuna watu wako mbali na furaha za nyumbani.
Kuna watu nyumbani ni sehemu ya kujilaza tayari kwa maumivu ya kesho.

SIKU NJEMA!
Pumzika na..Basement Jaxx wakikuambia DO YOUR THING


Read more...

USHAWAHI KUIANGALIA MAITI YA MBU?

>> Tuesday, March 25, 2008

Mbu hulalamikiwa wote!
Lakini si mbu wote wahitajio damu yako.


Staili za kumuua mbu ziko kibao.
Unaweza ukambinya.
AU?
Mbu aliyeuawa , maiti yake haiangaliwi sana.
Mara kwa mara baada ya kumuuambu, unasahau kuwa umeua, labda mpaka upate malaria ndio unajaribu kukumbuka baadhi ya maiti fulani za matunda.
SWALI:

  • Unanielewa?
DUH!
Usitishike!
ENDELEZA LIBENEKE!
Mpate lakini NASIBU MWANUKUZI aka RAS NAS akiwa na Ali Jabang na Aliou Cissokho wakiwa na MANDINGO TRIO

Read more...

Ngojea Niseme!DUH!

>> Monday, March 24, 2008


Ngojea nikupe dondoo za yaliyonikuta..
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket

Photobucket
DUH!

Kuna watu wananigombania kuhusu post zangu hapa katika blogu yangu kama vile nimewalazimisha wajekunichungulia hapa kinamna!:-(
Wanadai hawaelewi nasema nini.


DUH!
Malizia kidogo Pasaka na Manu DIBANGO akikupa kitu WOA!

Read more...

UTAMU WA WALI na KUKU ULIOKULA JANA!

>> Sunday, March 23, 2008

Leo ni leo!

Ubwabwa uliokula jana hausaidii sana kukidhi mahitaji ya leo ya mlo kama una njaa ya hata kiporo cha mlenda.
Sikukatalii kuwa jana ule wali uliokula ulikuwa mtamu kweli kama huo wali uliula.

Lakini....
... kama leo tumbo halipati kitu unafikiri nikikusimulia utamu wa wali jana unamsaada sana katika kutatua swala la leo?

Swali:

  • Umestukia hadithi za UTAMU wa pilau jana inavyonoga, kama wakati unasimuliwa leo bado umeshiba na unauhakika wa mlo?
  • Ushastukia hadithi zako za utamu wa wali uliokula jana inaweza zikawa ni adhabu masikioni mwangu kama na njaa na sina pakula leo?

DUH!

Nisikutishe!
  • Napenda stori za jana.
  • Nafurahia unapomsifia Nyerere , Kenyatta hata Iddi Amini kwa waliyofanya jana.
  • Napenda hata ukumbushiavyo jinsi hali ya hewa ilivyokuwa nzuri jana.
  • Napenda hadithi za wanadada na wanakaka walivyokuwa waaminifu katika mahusiano ya walioishi jana.
  • Usiseme kwa jinsi navyopenda hasa ugusiapo jinsi miziki ya jana ilivyo kuwa bomba.

  • Napenda mpaka zile nakadhalika kadhaa, zilizokuwa bomba jana.

Sasaaaaaaaaaa........!

Swali:
  • Mimi wa leo , utamu wa wali uliokula jana unanihusu nini?

DUH!

Utamu wa jana unaweza kuwa motisha ya kuongezea kautamu juu ya utamu leo.
Utamu wa wali jana unaweza ukageuka kuwa utamu wa wali leo na kachumbari na glasi ya gongo au mbege juu yake leo.

Lakini hadithi za utamu wa wali uliokula jana waweza ukawa ni ukatili dhidi ya masikio yangu leo mwenye njaa.

NASIKILIZA LAKINI!
ENDELEA KUNIPA HADITHI ZA UTAMU WA UGALI WA MUHOGO ULIOKULA JANA.


Endeleza siku kwa kusikiliza ushahiri wa Rafael Casal

akitukumbusha utamu wa mapenzi ya jana.


Au turudi tu katika ZOUK na kuendelea na Jocelyne Beroad wa Kassav

Read more...

Maswala ya Kujinyea!

Nirahisi kunyoshea mtu mwingine au kitu kingine kidole kwa swala ulilojifanyia mwenyewe.

Lakini pia, mjanja ni lazima ajue kuwa hata kama unamnyoshea mtu au kitu kingine kidole kwa jambo lizaliwalo kutokana na kalkulesheni zako za kudaka kutolipa, ni lazima ukiri icho kitu hata kimoyo moyo kama unataka kujifunza au kutatua.

Lakini.....!

Maswala mengi yatutiayo matatizoni ni maswala ambayo yanaweza kumtokea binadamu yeyote.
Tatizo ni kwamba sisi binadamu tumekuwa watumwa wa mitazamo ya jamii ifanyayo tuwe waoga kufanya chochote ambacho katika jicho la jamii kinatufanya tuonekane hatuna mpango.

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba, tukishaanguka katika mtazamo wa jicho la jamii , wengi wetu tunaamua kuzoea mazingira ya pale tulipoangukia.Jambo hili linatufanya tusiweze kujinasua katika makucha ya pale tulipoangukia.Hukawii kujikuta unaamua kuendelea tu kunywa gongo kama ushazoea na unajua jamii inakuita mlevi wa gongo, hata kama mbege ndio kinywaji ulichopenda kunywa hapo enzi za kale.



Kuhusu maswala ya kujinyea......

DUH!
Kwenda haja kubwa kuna starehe zake!(Samahani , nilikuwa namaaninsha kujinyea.)
Kuna watu husahau kuwa moja ya jambo ulifanyalo mapema baada ya kuzaliwa ni kujinyea.

Lakini....

... hili ni jambo ambalo jamii itaendelea kukufunza tokea uanze kuelewa mambo mpaka utakapo zeeka kuwa, ni noma kujinyea.

Kwa bahati mbaya ni kwamba, jamii haiachi mpaka ufe kukukumbusha kuwa kujinyea ni jambo la kukutia aibu na ni jambo la kuwanyea wale wakuhusuo.

Swali:

  • Hivi unakumbuka ma astronauti waondokapo kwenda anga za juu na waingiapo tena duniani huvaa nepi ili kuwaruhusu wajinyee kistaarabu?

Nadhani unamkumbuka huyu Lisa Novak na alivyodakwa akiwa na nepi yake katika harakati za kumfukuzia mpenzi wa mpenzi wake?


DUH!

Hili swala la kunyewa pia......!

Mara nyingi watu hawataki ujinyee ili kuogopa wao wenyewe kunyewa kiaina na myo wako.

Mambo ufanyayo yanaweza kumdhuru mtu mwingine akuhusuyo bila wewe kunuia kufanya hivyo.

Kwa mfano ; kama wewe unafuatilia uchaguzi wa Uraisi Marekani , utakuwa umeshuhudia jinsi gani akina Obama, Clinton na.... inabidi wajitete sana kutunza uhalali wao katika uchaguzi kwa makosa ya watu wengine wawahusuo.

Unaweza ukajikuta unadanganya kuwa wewe ni nani kutokana tu na kukwepa kuunganishwa na mnyo wa mtu , vitu , hata...... ambavyo jamii inafikiri vimejinyea.



Sasaaa!

Unajua tena mimi na wewe si malaika na tuko katika jamii hii ambayo haiachi kutukumbusha tusijinyee.

SWALI:
  • Unakumbuka mimi na wewe ndio jamii?
  • Wewe ni mnyosheaji vidole eeh?

Basi ngojea na mimi nijaribu kukumbusha kitu ambacho najua kwa njia moja au nyingine ni ngumu kufanikiwa;
USIJINYEE!

Jumapili Njema!

Nakuacha na Sheryl Crow

akikupa kibao LOVE is FREE

Read more...

You are filling up kenyaunlimited with useless posts.DUH!Nimeshajitoa katika Agrigeta Hiyo kinamna!

>> Friday, March 21, 2008

DUH!
I tried to get U guys to delete me from that webring.
I am in the mood to do and write... Well, the same useless things.

DUH!

Nilijaribu lakini kutowasumbua!
Ngojea nimuache Culture


Kenyaunlimited watu, kama hamkunielewa its ok. Lakini kusema kuwa nilikuwa na fill up kenyaunlimited with useless posts, NAAMINI HAMUELEWI NASEMA NINI katika post zangu. Naamini naweza nikawa nawalipisha kitu fulani lakini , HAMUWEZI KUSEMA POST ZANGU USELESS!
Naendeleza kujaza hapa nachoandika kama kawaida na naweka picha za wadau wangu niliowadaka kinamna kama kawa .... Na sibadili staili hii NG'OO , Just incase mnaolalamika mnaelewa naongelea nini katika post zangu, kitu ambacho sina uhakika kama mnanielewa.
BASI MBELE KWA MBELE!

AU?

DUH!
Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket


DUH!
Pumzika na FELA KUTI




Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket
Photobucket

Photobucket

Photobucket


Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket



Kwa wanaonielewa , endelea na Buju Banton



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket



Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket

Photobucket


TULIA na GOKH-BI SYSTEM

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP