Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA KUJISIKIA KUFAKUFA.

>> Tuesday, March 11, 2008

Kuna wajanja wanatumia kila njia kukwepa kufa.
Au inawezekana ikawa ni ujanja kukwepa kufa pale iwezekanapo.

Lakiniiiii.......

......Kufa , kwa mwingine ni kitendo cha kuogopa, wakati kwa mwingine ni kipunguzio cha shida za kuwa hai.

Swali:

  • Kwa wale wanaojiua na wenzao kwa kisingizio cha dini , ukiwakamata kabla hawajalipua bomu, uwape adhabu gani?
DUH!

Maisha matamu , maisha machungu kama unaishi.
Mara nyingi ujanja wa kufikiria na kufanikisha uwe hai ndio ukufanyao ukumbuke kuwa kuna kifo.

MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA PEPONI WALE WOTE WALIOTUTANGULIA!

Swali:
  • Hivi kwanini kwa kiswahili watu tunawaombea waliotutangulia walale huko mahali pema peponi hata kama tunajua baadhi yao wangependa peponi yao iwe baa na sio sehemu ya kulazwa?
DUH!

Siku njema!

Tuliza siku na Koffi akiwa na Papa


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP