Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NAOGOPA KUONJA NANIHII!Ikiwa CHUNGU je?

>> Friday, March 07, 2008

Kuonja kitu fulani , hukufunza utamu au uchungu wa nanihii!
Ukionja kama ni tamu , kuna utamu wake.
Ukionja ukaungua, kunafundisho lake ingawa uchungu utauona .

Swali:

  • Hivi ni lazima uonje ili kuwa na uhakika wa utamu wa dagaa wa kigoma?

Duh!

Utamu wa ushabiki wa kitu fulani , hata kama ni mpira wa miguuu, unazidi pale mnaposhinda.Mkishindwa au ladha isipolenga utamu , kasheshe.

Kwa rafiki zangu wamshabikiao Mzee Obama , wiki hii , Hillary Clinton aliposhinda, hata taarifa za habari walikuwa wanakwepa ladha yake.

Kuhusu matokeo ya uchaguzi wa kidemokrasia hapo Kenya, kuna ambao walianza hata kuhisi kuwa labda kweli Afrika tumelaaniwa baada ya kuonja ladha yake fulani ya matokeo fulani.

DUH!
Msikilize kidogo Peter Gabriel akiwa na akina Papa Wemba, na....wakikupa..IN YOUR EYES




Swali:
  • Ushawahi kufurahia kaladha utamu kunoga, wakati ukisifiwa sifa za uongo mbele za watu, wakati unajua inawezekana watu wanajua kuwa hustahili sifa hizo?

Duh!

Lakini.................

  • Ukionja kuna ladha itakayokupa jibu.
  • Usipoonja kunakakitu utakakokuwa unahisi ndio jibu liwakilishalo ladha ya usichokionja.
Usipoonja , kimawazo, unawezekana umepatia , umeongezea chumvi, umepunguza kachumbari au.....katika utamu husika.

Lakini.......
............kuna mambo si lazima uonje.
Si lazima uguse moto ili kujua ladha ya kuungua.


Lakini.....

Katika kufikia jibu kabla ya kuonja.......:

  • Unaweza kuhusudu mtu mpaka ukaogopa kumuomba urafiki au ile...........kutokana na kuhisi unajua ladha ya jibu lake.

  • Unaweza kuhusudu /kupenda /kumisi mtu/watu, mpaka ukashindwa hata kuongea nao, kutokana na kuwa ndani ya moyo wako, maongezi hayafikii hata kiduchu cha jinsi ambavyo ungependa kuonyesha mapenzi yako kwao au kutokana na hisia kuwa maongezi aina ya mawasiliano, haifikii kiwango cha jinsi uuhisivyo ukali wa ladha ya mategemeo yao kwako .

Swali:
  • Ushawahi kuonja kushindwa kufikia mategemeo watu waliojenga kwako?
  • Ushawahi kuonja kushindwa kufikia mategemeo unayohisi watu wamejenga juu yako?
  • Ushawahi kuonja hisia kuwa kila mtu anafikiria hujali kwa sababu fulani fulani?
  • Ushawahi kuonja kufanikiwa kitu fulani ambacho ndio lengo lako moyoni na sio msukumo wa jamii? (hata kama kitu hicho ni kuonja kifuko cha dhambarau?)
  • Ushawahi kuonja?
Duh!

Sidhani ni lazima uonje ilikujua ladha fulani.
Tatizo hata usipoonja, kuna ladha fulani

Sasaa.........

  • Tuonje au tusionje?
Lakini...

Utamu na uchungu vyote ni ladha.
Kama hujawahi kuonja pipi, basi naweza kukusimulia kuwa ni tamu, ingawa mimi napendelea toffee na wewe labda unapendelea pipi kijiti.

Sasaaaa...

Unataka mpaka kuonja vita ili, ujue ladha yake?

Ijumaa na Wiki Mwisho Njema!

Tulia na Zap Mama wakikupa SWEET MELODIE

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 4:56 pm  

Mzee Simon natumai mambo mazuri kama picha zinavyoelezea,hongera.Mzee Simon kwa mtazamo wangu nilitegemea ukirudi humu kijijini utupe taarifa ya JUMUWATA.Kwa kweli jumuwata imekwama kwasababu kama si kukwama sasahivi tungekuwa mbali sana.

Rasta hapa.

chemshabongo 4:56 pm  

kaka umerudi? ulituacha bila kutuaga! sio fresh!
lakini umenikuna na hii
• Unaweza kuhusudu mtu mpaka ukaogopa kumuomba urafiki au ile...........kutokana na kuhisi unajua ladha ya jibu lake.

• Unaweza kuhusudu /kupenda /kumisi mtu/watu, mpaka ukashindwa hata kuongea nao, kutokana na kuwa ndani ya moyo wako, maongezi hayafikii hata kiduchu cha jinsi ambavyo ungependa kuonyesha mapenzi yako kwao au kutokana na hisia kuwa maongezi aina ya mawasiliano, haifikii kiwango cha jinsi uuhisivyo ukali wa ladha ya mategemeo yao kwako .

KARIBU TENA KIJIWENI

Simon Kitururu 10:25 am  

2Rasta: JUMUWATA ni watu, wakiwa hoi inakuwa hoi. Mimni na nguvu sasa hivi, tegemea kuwa nitapulizia pumzi ya nguvu yangu. JUMUWATA IKIFIKIA SEHEMU FULANI hutaweza kumlalamikia LOWASA:-)
@CHEMSHABONGO: Nilibanwa kaka! Unajua tena maisha! Ingawa nimebanwa bado, lakini nimerudi:-) Asante kwa kunitembelea na kunielewa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP