Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama YESU na MTUME walikuwa na MAADUI, KAWAWA je?

>> Thursday, March 13, 2008

Uhuru wa kusema /kutoa maoni/kujieleza, unamazingaombwe yake.

Ukiruhusu watu wakuambie wanakufikiriaje, watakuambia mpaka yale mambo ambayo yanakutekenya sikio.

Hukawii kusikia:

  • Mimi nalichukia tu lile jamaa.
  • Mdau kwa kupenda misifa , hata mbwa hawamfikii.
  • Mtoto mzuri huyo!Ukimbishia , atakwambia kwa sababu wewe hujamuona ziro distansi.
  • Jamaa kwa kupenda ubwabwa huyo!


Swali:
  • Kama mtembeleaji blogu nyingi, umeshastukia hata habari nzuri kuna mtu atakuja na kuitukania?


Kweli binadamu tofauti!

Mwingine matatizo ni kitu kimpacho nguvu kutatua na kwenda mbele wakati kwa mwingine ni kitu kimdhoofishacho na kumfanya asikie kufakufa.

Kweli binadamu tofauti!

Yule umpendaye , kwa mwingine ni adui kutokana na yaleyale yaliyokufanya umpende.

Mpaka dini kadhaa hazikawii kukufunza uwapende kila mtu, lakini zinakukumbusha jinsi gani wasiofuata dini yako walivyo watu nishai.
Zinakufunza umpende aliye kama wewe, na yule mwingine asiye kama wewe, unashauri ujaribu kumfanya awe kama wewe kabla hujampenda kinamna.

DUH!

Sijui kama watu kibao wamefanikiwa kuwapenda wote walioko ndani ya dini moja.

Swali:

  • Ushawahi kumchukia mtu bila sababu na kukiri unamchukia tu?
  • Ushawahi kujikuta kuwa yule uliye kuwa unahisi ni rafiki kumbe ndio adui?

DUH!

Inasemekana kuwa, hii hali ya kujaribu kueneza upendo duniani ni alinacha fulani kutokana na necha ya binadamu.

Inasemekana binadamu watachukiana ili wajue kupenda ni nini.

Swali:
  • Bila chuki , upendo ni nini?
  • Bila maadui, marafiki ni akina nani?

Lakini....

Mimi naamini katika upendo.
Na kaudhaifu kakupendapenda kirahisi.

MAADUI eeh!Si mnajua tunaweza kupendana kama kale kakitu kasababishako tuchukiane kakiwekwa pembeni!

Samahani lakini kwa niliowakosea!

AU?

Naacha basi kukuzingua!

SIKU NJEMA!
Tulia na Brian Mcknight


0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP