Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KIJIWENI NA ADUI AKUCHEKEAYE!

>> Thursday, March 27, 2008

Naweza kusema adui mzuri ni yule akuonyeshaye kuwa anakuchukia.

Kujua bomba la kitu!

Binadamu ni mjanja halafu hana uhakika, jambo ambalo hufanya wanadamu wengine wakuchekee ingawa moyoni mwao wanakujambia kinywani.

Lakini.....
...binadamu anaweza akawa anauhakika na nini anataka akufanyie cha kukudhuru lakini akakuchekea kwanza kabla haujakaa golini akulenge.

Swali:

  • Sasa akikuonyesha chuki halafu akajikuta anahitaji msaada wako hapo baadaye afanyeje?
  • Sasa akikuonyesha makucha yake ya uadui, akiwa na kiu utampa maji?
Lakini.....
.... matatizo ya adui akuchekeaye kama huna machale fulani, ndiye awezaye kukuumiza zaidi kunako. Akuchekeaye waweza ukajikuta ndiye awezaye kufikia ile sehemu yako ya siri ya maumivu.

Mapenzi yako alinacha na adui akuchekeaye utastukia machungu yake pale anapokuweka konani baada yakustukia umenasa.
Chuki itakayojitokeza baada ya wewe kunasa kutoka kwa adui akuchekeye, inaweza kusababisha ukumbuke sura ya mnuno wa adui uliyejua anakuchukia siku zote kama ilikuwa inakitabasamu fulani vile.

Swali:
  • Ushamchekea adui leo?

Maadui ndio wafanyao tuwathamini marafiki.
``Maadui ni muhimu sana´´; inaweza ikawa ni sentensi iletayo maana katika anga fulani.

DUH!

Unawakumbuka baadhi ya maadui hawa ambao inasadikika kuwa wanatudhuru Africa, Amerika, Ulaya , Asia na pote duniani?
Nina maanisha ya maadui hawa hapa:
  • Ujinga
  • Magonjwa
  • nk
Ngoja Niachie hapa kukuzingua Mkuu!

Lakini......
.... Chekewa na Mchekee!
.....Jifanye hujui au Jifanye umesahau!
Kumbuka tu kuwa katika lolote ufanyalo;
KUJUA UNAFANYA NINI NI BOMBA LA KITU, hata kama ujuacho ni busara ya kuwa hujui.

Ngoja YingYang Twins wakunong'oneze(samahani kwa lugha na wadada nusu uchi katika kideo) .

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Aliko 1:45 pm  

Ushamba una raha zake na matatizo yake... sadly mara nyingi ndani ya ushamba ni matatizo ndio yanayo surface zaidi... elimu ya mjinga Fitina na majungu.. Mansimon delete tuu anayetaka kuleta zake za ajabu MAWAZONI..tupo pamoja. jah Guide
endeleza libeneke take photos write your thoughts thinker cause thats your theme na wengi wetu humuhumu ni mashabiki those who oppose or support. msg zinafika.

Simon Kitururu 2:43 pm  

@Aliko:Tuko Pamoja !

Anonymous 2:43 pm  

sana tuuuu

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP