Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UJANJA WAKUHAKIKISHIA UMATI KUWA HUTAKI UJINGA.

>> Wednesday, March 12, 2008

Kama mkubwa, ni vigumu kuruhusu umma ushuhudie kuwa mjinga au kunakaujinga unakafurahia kisiri.

Usipokuwa muangalifu, unaweza ukajistukia unakemea kwa sauti au kukiri kwa sauti kuwa hutaki ujinga.


Balaa ya ubinadamu ni jinsi tulivyo binadamu na sio malaika.

Ubinadamu unakuja na viujinga vyake ambavyo umma unaweza pia ukavishangilia kama ni vitu vya maana.

Ukichunguza unaweza kustukia kuna baadhi ya ambao umma unawasifia kuwa hawataki ujinga, ambao ndio vyanzo vya vita, ufisadi, umasikini, na taaluma nyingi muhimu duniani kama utafiti wakufundisha nyani ajuae kusoma.

Swali:

  • Hivi ujinga ni nini?
  • Ushawahi kuchekelea kaujinga wakati unajua ni ujinga?
  • Hivi katika TV zetu/Magazeti/vitabu na... vilivyotapakaa na tuangaliavyo au kusoma, asilimia ya ujinga ni ngapi?

DUH!

Lakini ukweli ni kwamba , ujinga nishai!
Tujaribu kuukwepa ikiwa, unauhakika kuwa tunauwezo wa kuukwepa.


Swali:
  • Hivi kuondokana na ujinga ni lazima uende shule?

Naacha basi!

Siku njema!

Lakini tulia na BILLY PAUL akija na kile kibao cha utamu wa penzi na mke wa mtu,kiitwacho MIMI na Mke wa Bwana JONES

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP