Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NORTH MARA GOLD MINE!

>> Wednesday, February 29, 2012

Nimesikitishwa na hii kitu!:-(
Samahani CHACHA kwa kuiweka hapa bila kukuomba!
Madhumuni yangu ni kutawanya tu hii HABARI ili izidi kujulikana!
Source: CHACHA

Greetings from North Mara in Tarime.

I wish to share with you some photos of the current situation in North Mara. Rev. Magafu and I have been assessing and identifying the victims of the last year’s and ongoing waste ponds spillage at North Mara gold mine.

New cases of the victims are coming up with symptoms that are vivid and the situation is alarming. Two cases, though, needs immediate medical attention and action. This involves Mama Otaigo from Weigita village and Paul (8 year old boy) from Nkerege village.

The situation we have found them in is far different from when we met them during the health screening done in January 7th 2010. Their health state is deteriorating from day to day. I am attaching their current photos for your review.

As the governments still remains silent on this matter attempts to get referral letters from government health facilities have proved abortive and therefore we need to act as soon as possible to save the lives of those who are critically ill.

An appeal is made to all of you to act in your different capacities.

Kind regards,

Chacha

Read more...

Yasemekana ADUI MKUBWA wa MAVI ni MAVI!

Na adui mkubwa WAKO,....
.... yasemekana ni WEWE mwenyewe!:-(

Swali:
 • Si yasemekana ni WEWE  MWENYEWE ndiye UJUAYE zaidi ya muhimu kwa  WEWE na kiutekelezaji labda bado uyapayo UMUHIMU/KIPAUMBELE  sio yako bali ya WALE wengine au angalau yale ambayo yana jicho la WASIO WEWE?

Ndio,...
.... katika YAKO,....
.....SHUGHULI ni yako hasa kwa kuwa ni WEWE mwenyewe ujuaye vizuri unasikiliziaje UTAMU,....
... au hata UCHUNGU.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA na wala USIKONDE ghafla!:-(

Hebu Ali Farka Toure na Toumani Diabate waanzishe upya kwa - Sabu YerkoyAu tu Pape Diouf azime kwa-Casse Casse

Read more...

Wakati TUPO tusubiriao MELI kwenye uwanja wa NDEGE!

>> Tuesday, February 28, 2012

Ndio,..
... kuna tuyasubiriayo KUSIKO,...

.....halafu tunashangaa TUYASUBIRIAYO yasipojitokeza  huku tukijishaua kuwa tumeyahangaikia.

Swali:
 • Na si kama umsubiriaye anakuja na basi la ARUSHA hata umsubiri vipi kwenye basi la MTWARA yawezekana ni kujipotezea tu MUDA?
 • Na kama utumiacho ni unga wa MAHINDI labda basi si usitegemee upikacho kitageuka UBWABWA?

Ndio,...
.... LABDA maishani,....
.... wengi ya NDEGE  hatuyasubirii uwanja wa ndege,...
.... na ingawa tunayahangaikia ila bado mahangaiko yetu tunakosea pakuyalenga na bila kustukia tunasubiria ya NDEGE  bandarini na ya MELI kule uwanja wa NDEGE na hapo ni kama kabisaa sio kwenye kituo cha daladala MOROGORO ambako hata BANDARI hakuna!:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!


Hebu Hugo Nyame arudie - Pardon MadameAu tu Majoie Ayi azime kwa - Aicha

Read more...

KIDONDA eti ni nyumba ya USAHA!

Na ukichokonoa KIDONDA,...
..... waweza kutumbua usaha AMBAO kwa kawaida  usingeonekana!

Swali:
 • Si NI KWELI mambo mengine  labda usiyachimbe  undani basi kama hutaki kujua ubaya wake?

Ndio,...
.... labda vipele vingine viache tu vikauke vyenyewe,...
.... ukivibinyabinya utafurumua volkano za usaha ambao usingebinya ungekaukia mumo kwa mumo!

Ni neno tu na WAZO kiaina MHESHIMIWA!
Siku NJEMA MKUU!

Hebu MBILIA BEL na TABU LEY wakukumbushe  -SHAURI ZAKO
Au tu TONTO IRIE aingilie kati na kuzima tena kwa -IT a RINGNipo,..
... ndio ni TALLIN , Estonia.

Read more...

MAZINGIRA huchagulia watu POMBE!

>> Monday, February 27, 2012

Mazingira yana laana zake,...

..... na MTU atokeaye katika mazingira ya wapika GONGO ni rahisi kujikuta kaonja GONGO.

Swali:
 • Si unajua MAZINGIRA yakiruhusu kuna WASIOJUA ambao WANGEJUA kwa kuwa tu MAZINGIRA watokayo ni SHULE tosha?
 • Na si unajua MAZINGIRA mara kibao huchagulia mpaka watu DINI?

Ndio,...
.....MAZINGIRA yangeruhusu,...
.... labda WANYWA GONGO wangekuwa wanakunywa tu BIA.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumatatu njema MKUU!


Hebu YAMI BOLO aingilie kati kwa-Cool IT DownTenor Saw arudie-FEVERHalafu tu TOM JONES abadili kabisa mchezo kwa-Sex BOMB

Read more...

Je, una kijana ambaye yuko jobless? NARCO tuna ajira yake

>> Saturday, February 25, 2012

NAFASI ZA KAZI ZA WAKALA MAUZO “SALES AGENTS”


“Kongwa Beef” ni Nyama yenye Ubora wa Kimataifa inayozalishwa na
NARCO, Kampuni ya Ranchi za Taifa Limited ambayo hivi sasa inafanya
maboresho ya namna ya kuwafikia wateja wake wa nyama ya “Kongwa Beef”.
Ili kuhakikisha tunawapatia wateja wetu huduma zinazozidi matarajio
yao, tumeamua kutoa nafasi 200 za Wakala Mauzo “Sales Agents” kwa
vijana wa kike na wa kiume wa miaka 18-30. Hii ni fursa muhimu sana
kwa vijana wote wenye uzoefu au wanaopenda kujenga uzoefu na kufanya
kazi katika upande wa Masoko na Ujasiriamali.

Kama unashauku ya kupata nafasi ya kutafuta oda za “Kongwa Beef”
kutoka kwa wateja, basi hii ni nafasi yako.


MAJUKUMU YA WAKALA MAUZO WA “KONGWA BEEF”

 Kutangaza Ubora wa Kongwa Beef na kutafuta oda kutoka kwa wateja
kwenye maofisi, mahoteli, na taasisi mbalimbali.
 Kugawa vipeperushi na kushawishi wateja kununua “Kongwa Beef”.
 Kukusanya na kutunza kumbukumbu za wateja na mauzo
 Kuelimisha wateja wajue Ubora wa Kongwa Beef


MALIPO NA FAIDA UTAKAZOPATA


 Utalipwa kwa kila kilo moja ya nyama utayoleta oda na kuhakikisha
imemfikia mteja kupitia wasambazaji wetu.
 Kadiri utakavyoleta oda nyingi zaidi na kuhudumia wateja vizuri
zaidi ndivyo utakavyopata kipato ki-kubwa zaidi.
 Utakutana na mazingira mazuri ya kufanyia kazi na kupata changamoto
za kujiendeleza kitaaluma na kimapato.
 Utapata mafunzo ya masoko, biashara na ujasiriamali ili kukuwezesha
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
 Vyeti vya heshima na vya mafunzo vitatolewa
 Utapata fursa ya kuendeleza ujuzi na taaluma yako katika fani za
biashara,ujasiriamali na masoko.


TAALUMA NA UZOEFU UNAOHITAJIKA


Mwombaji:-
 Awe na uwezo mkubwa wa kutoa huduma inayozidi matarajio ya wateja.
 Awe na uwezo wa kujieleza vizuri kwa Kiswahili.
 Uwezo wa kuongea Kiingereza kwa ufasaha itakua ni sifa ya nyongeza
 Awe mwenye shauku ya kuuza sana.
 Uwe na uwezo wa kuandaa na kutunza kumbukumbu za wateja na taarifa
za Mauzo na Masoko.
 Awe Mbunifu na Anayependa Kujiendeleza


NAMNA YA KUTUMA MAOMBI


 Andika barua kwa mkono bila kuchapisha na uambatanishe “CV” yako
pamoja na barua kutoka kwa wadhamini watatu (3) mmoja kati yao awe
mzazi au mlezi wako. Barua ziwe na namba za simu za wadhamini
 Ambatanisha namba za simu na anuani ya barua pepe kama unayo.
 Ambatanisha barua kutoka kwa Serikali za Mitaa iliyogongwa Muhuri
na yenye picha yako.

Maombi yote yatumwe kwa:

Meneja Mkuu,
Kampuni ya Ranchi za Taifa Ltd (NARCO),
Mavuno House, Azikiwe Street,
S.L.P 9113,
Dar es Salaam.

Simu : +255 22 211 0393/211 1956
Barua Pepe: info@narco.co.tz
Tovuti: http://www.narco.co.tz/

Tuma maombi yako kwa kuleta mwenyewe ofisini au kwa Posta. Kila
tutakapopokea maombi tutayafanyia kazi mara moja.

*********Wahi Wateja Wanatusubiri Tuwahudumie**********


Regards,

Immanuel Barikiel Mnzava
Marketing Manager
National Ranching Company Ltd (NARCO)
Mavuno House, Azikiwe street
P.O. Box 9113
Dar Es Salaam
United Republic of Tanzania
Tel +255 22 211 0393
+255 22 211 1956
Fax +255 22 211 1956
Mob +255 753002035
+255 715831241
+255 787831241
Web: http://www.narco.co.tz/

Read more...

Maswala ya INJINI kiuno!

Katika mwendo,...
INJINI ni KIUNO,...
Miguu ni matairi tu.


Hata katika ndoa ukiondoa kichwa,...
INJINI ni KIUNO,...
Hata sehemu za siri ni pembejeo tu.

Na katika AFYA,...
INJINI ni KIUNO,...
Ukikitumia wenye magari kiafya kwao ghali tu.


Ndio ,..
... kata kiuno ukiweza.
Kiuchumi bei nafuu,...
Kiafya  bomba kama KIUNO  chakusaidia kutembea au hata kuendesha baiskeli,...
Na kikusikilizia utamu nengua,...
  Kwenye mziki  , katika  katika hata KATIKA  uasherati katika.

INJINI KIUNO BOMBA!
Swali:
 • AU?
JUMAMOSI NJEMA MHESHIMIWA!


Hebu Lou Bega aanzishe tena kwa - Just a Gigolo (I Ain't Got Nobody)
Lou Bega aendeleze kwa -Gentleman


Lou Bega aongezee -TrumpetAu Lou Bega azime kwa-Mambo No 5

Read more...

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU DAWA BANDIA YA MALARIA

>> Friday, February 24, 2012

TAARIFA KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU UWEPO WA DAWA BANDIA YA KUTIBU UGONJWA WA MALARIA IITWAYO ELOQUINE (Quinine Sulphate 300mg USP)


Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ni wakala wa Serikali iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii yenye jukumu la kudhibiti ubora, ufanisi na usalama wa vyakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba ili kulinda afya ya jamii.

TFDA inapenda kuutaarifu umma kuwa imebaini kuwepo kwa dawa bandia ya kutibu ugonjwa wa Malaria katika soko. Dawa hiyo inaitwa Eloquine (Quinine Sulphate 300mg U.S.P) na ipo katika makopo ya vidonge 1000 (elfu moja) kila moja. Maelezo yaliyopo katika lebo yanaonesha kuwa dawa hiyo imetengenezwa na kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd cha nchini Kenya.

Hata hivyo, TFDA imebaini kuwa kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd hakitengenezi dawa yenye jina la biashara la ‘ELOQUINE’. Kiwanda hicho kimesajili Tanzania Quinine Sulphate 300mg B.P isiyo na jina la kibiashara. Aidha, kiwanda cha Elys Chemical Industries Ltd kimebainisha tofauti mbalimbali zilizopo katika lebo ya dawa bandia ikilinganishwa na dawa halisi inayotengenezwa na kiwanda hicho iliyosajiliwa na TFDA na hivyo kuthibitisha kuwa kiwanda hicho hakitengenezi dawa hiyo.

Katika kudhibiti usambazaji wa dawa hiyo hapa nchini, hadi sasa TFDA imekamata jumla ya makopo 155 ya dawa hiyo bandia ya Eloquine jijini Dar Es Salaam yaliyokuwa yakisubiri kusambazwa. Aidha, kopo moja lenye vidonge 115 limekamatwa Moshi, Kilimanjaro. Tayari mtuhumiwa mmoja amekwishafikishwa mahakamani na upelelezi wa chanzo na wasambazaji wa dawa hii unaendelea kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi.

Uchunguzi wa dawa bandia katika maabara umebaini kuwa vidonge hivyo havina kiambato hai (active ingredient) cha Quinine Sulphate kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa Malaria na hivyo matumizi yake ni hatari kwa afya ya binadamu.

Maelezo ya kina yanayotofautisha dawa halisi iliyosajiliwa na dawa bandia ni kama yalivyoainishwa katika jedwali hapa chini.

Dawa halisi iliyosajiliwaMaelezo ya dawa bandia
· Jina la dawa: Quinine Sulphate 300mg B.P

· Jina la biashara: Haina jina la biashara

· Mtengenezaji: Elys Chemical Industries Ltd, Road B, Off Enterprise Road, P.O Box 40411, 00100 Nairobi, Kenya

· Rangi ya Lebo: Nyeupe na kahawia (Brown)

· Namba ya toleo: Huanzia na namba na siyo herufi. Kwa mfano: 2167E· Muda wa matumizi (Shelf life): Miaka 4· Jina la dawa: Quinine Sulphate 300mg U.S.P

· Jina la biashara: ELOQUINE


· Mtengenezaji: Elys Chemical Industries Ltd, Road B, Off Enterpises Road, P.O Box 4011 00100 Nairobi, Kenya

· Rangi la Lebo: Njano na Nyekundu


· Namba ya toleo: GE410


· Tarehe ya kutengenezwa: 04/2009


· Tarehe ya mwisho wa matumizi: 4/2014 (Miaka 5)Wafanyabiashara wote wa dawa na wananchi wanatahadharishwa kutozitumia dawa hizi na wale wote waliouziwa dawa hizi wanaelekezwa kuzirudisha dawa hizo katika ofisi za TFDA, vituo vya afya vya Serikali au vituo vya polisi vilivyo jirani nao.

TFDA inapenda pia kuwakumbusha wafanyabiashara wa dawa, wasafirishaji wa vifurushi na wananchi kutoa taarifa haraka iwezekanavyo pale wanapohisi kuuziwa dawa duni, bandia au zilizoisha muda wa matumizi. Taarifa zitolewe ofisi za TFDA makao makuu zilizopo Barabara ya Mandela, EPI Mabibo External, Dar es Salaam na Ofisi za Kanda zilizopo mtaa wa Nkurumah, Mwanza, Mtaa wa Sakina – Arusha, Hosptali ya mkoa ya Dodoma na Jengo la Ofisi ya Mifugo Mkoa wa Mbeya.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na:-

MKURUGENZI MKUU
MAMLAKA YA CHAKULA NA DAWA
EPI MABIBO EXTERNAL,
S.L.P 77150, DAR ES SALAAM
Simu: + 255 222 450512/450751/452108
Nukushi: + 255 222 450793
Barua pepe: info@tfda.or.tz

Read more...

CHANZO cha wazo lilelile BAYA ikiwa ni RAIS NYERERE na sio MCHUNGAJI MTIKILA,....

....LABDA kuna watakao LIHESHIMU  ,...
.... kwa kuwa TU wanaheshimu na wana IMANI  na CHANZO cha WAZO!

Swali:
 • Si unajua CHANZO cha WAZO kina nguvu zake pia kwa wafuatiliao WAZO hata hasa katika kuaminisha watu kirahisi hata UJINGA?
 • Kwa wakristo si CHANZO kikiitwa ni BIBLIA kama kwa WAISLAMU wakisikia chanzo ni KORANI si kirahisi wanaweza amini jambo hata ambalo kitafsiri labda kimekosewa ila CHANZO cha fanya jambo lipewe TU shavu kiaina?

Ndio,...
.... labda hata MIMI na WEWE,...
.... kuna tuaminiyo KIRAHISI kwa kuwa tu tunaamini CHANZO cha WAZO,...
.... ingawa WAZO lenyewe ukweli wenyewe ni POTOFU.:-(

NI wazo tu hili MHESHIMIWA!
Ijumaa NJEMA MKUU!

Hebu KY-MANI  Marley na PRAS warudie- Avenues
Inner Circle wazime kwa -Discipline Child


Read more...

Katika kukumbushana ya KABUMBU la Uingereza....

.... hebu CLYDE BEST aongee....
Hebu tupunguze makali kwa msaada wa YAMI BOLO enzi hizo -Wadat 1984

Read more...

Ukifananisha labda MIHOGO, mahindi, Mchele na MAGIMBI vyote ni SAWASAWA!

>> Thursday, February 23, 2012

Kuna vilivyo SAWA,...
....ambavyo sio SAWASAWA!:-(

Ingawa ukitofautisha,....
.....labda CHIPSI DUME wala sio CHIPSI MAYAI yenye maringo ya viazi,...
.... na ndio maana kwa chai unapendelea CHAI kwa MAGIMBI ya kuchemsha!:-(

Swali:
 • SI umestukia  ukifananisha unaweza kustukia ni mengi tu kazi zake ni zilezile tu ila ni LADHA tu ifanyayo watu wapendelee MWIDU kuliko MLENDA?
 • Na ukifananisha si BINADAMU wote ni SAWA halafu ukianzakutofautisha ndio utastukia kuwa ingawa ni sawa ila sio SAWASAWA?

Ndio,...
.... labda MENGI maishani ni tofauti,...
... kwa kuwa tu sie BINADAMU tunayatafutia tofauti KIUTAMU , muonekano, UHABA au tu KIUBISHORORO wa statasi zake katika JAMII!


Ingawa labda kama una UNGA wa MUHOGO,...
..... labda wala huhitaji MCHELE au unga wa SEMBE!
Ni wazo tu hili MHESHIMIWA...
........ na kutolielewa RUKSA!
Siku njema MWANAKWETU!

Hebu New Edition waingilie kati kwa-Cool it NowHebu katika kundi la NEW EDITION tubaki na BOBBY BROWN aiyewahi kuwa mume wa Whitney Houston katika kipele-Don't be CRUEL


Halafu sijui kwanini hebu AFRIKA BAMBAATA wakija na UB 40 wazime kwa-Reckless

Read more...

Poleni wana SONGEA kwa yaliyotokea kwenye MAANDAMANO!

>> Wednesday, February 22, 2012

Nasikia sasa hivi waandamanaji TISA wametutoka!
Mungu awalaze mahali pema PEPONI!


Picha ya mmoja wapo.Source: Songea Yetu Blog
Habari zaidi :
SONGEA YETU BLOG
http://www.songeayetu.blogspot.com/

Read more...

DHAMBI wakati wa KWARESMA bado ni TAMU nasikia!

Yasemekana,...

.... kuna waogopao WATU katika kutofanya DHAMBI,....
.... kuliko waogopavyo MUNGU awaonao mpaka CHOBISI wajifungiako ili kula ngoma!:-(Swali:
 • Si yasemekana janja za WAUMINI ambao wanapenda kusifika  kwa BINADAMU wenzao janja ni kufanya dhambi makusudi kisirisiri ili wasidakwe tu hadharani?

Ndio,...
... kwa ambao wako katika KWARESMA,.......
....kumbukeni ni MUNGU wakuogopa na wala sio BINADAMU muhofiao vidole vyao HADHARANI kama nia bado nikuendeleza utamu wa DHAMBI!

MBARIKIWE SANA WOTE!
Na siku NJEMA WOTE!
AMEN!Hebu Kwaya Kuu ya Mt. Cecilia warudie pini-Bwana Unaweza
Au tubadili tu na kurudi uswahilini ili SADE arudie-Feel No Pain
Au tu tena Vanessa Paradis azime kwa-Joe le taxi

Read more...

Tatizo la KUJIFANANISHA kwa WATU,....

>> Tuesday, February 21, 2012

.... labda liko katika UKWELI,....
... hakuna WATU wawili WAFANANAO kila KITU ukiwanyambulisha.

Swali:
 • Unafikiri wadhaniwao wamefanana ni kweli wamefanana hata kama ni WALE  wafananishwao kimapacha?
Ndio,...
.... ..hata wewe ni YUNIKI a.k.a unique,...
... na UKO PEKE YAKO wa kiaina yako DUNIANI,...
.... na kwa hilo labda ni haki yako KURINGA!


NI wazo tu hili MKUU!
Nakutakia SIKU NJEMA!

Hebu Franco Luambo Makiadi aanzishe tena kwa- Mario


FRANCO akumbushie pia tena swala la UKIMWI kwa -Attention na SIDA

Read more...

Kama UNATAKA!

>> Monday, February 20, 2012


Kwa kawaida kama UNATAKA,....
.....yasemekana UTAKACHO huwa unapata KIUTAKACHO,...
.... ila UPATACHO huwa  huja na KUONDOKA kwa  makali ya ULICHONACHO!:-(


Swali:
 • Si unajua ULICHONACHO chaweza kupotea kwa wewe KUPATA kipya ambacho labda wala hata sio MUHIMU kwako kama ulichonacho sasa hivi?

Ndio,....
....UTAKACHO na UKAKIPATA,...
..... kwa hilo la kukipata tu kitu kipya LABDA huondoa BIKIRA ya ambayo ulikuwa nayo manono kwa kufanya uustukie zaidi ubaya wa uliyonayo kuliko MAZURI ambayo kwa kawaida hutunza ULIYONAYO yaliyo MUHIMU sana hata kuliko USIYONAYO sasa HIVI.:-(

Ni wazo tu hili MKUU!


Hebu Junior Reid aanzishe tena kwa- One Blood

Eric B. na Rakim wafanye tena matusi ya - Don't Sweat The Technique
Halafu Dr Dre azime kwa- Let me RIDE
Halafu sijui kwanini ila hebu tu COCOA TEA azime kabisaaa kwa-Hurry up and COME

Read more...

Kuhusu UKWELI mtandaoni kikompyuta au simu na UKWELI kikweli USO kwa USO!

Ki USO kwa USO,....
....labda UKWELI ni KWELI zaidi,...
..... ingawa yasemekana kuna ambao ukweli ki USO kwa USO hawapendi kwakuwa hata kikujamba kiuso kwa uso kuna mpaka HARUFU ambazo kisimu au katika intaneti PAFYUMU huwa hazistukiwi kirahisi,...
....kitu kifanyacho masupastaa wako wala hufikirii au hata hustukii WANAKUNYA tu mavi yanukayo aisee!:-(

Swali:
 • AU?


Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
JUMATATU NJEMA!!:-(
Hebu Super Cat na Heavy D waanzishe upya kwa - Dem Don't Worry We
SUPERCAT aendelee kwa -DON DADAHalafu SUPERCAT aongezee dozi kwa-DOLLY my BABYHebu TENOR SAW aingilie kati kwa- Ring the ALARM


Halafu tena ni SISTER NANCY ndio azime kwa -BAM BAM

Sijui kwanini ila ngojea tu tena SUPER CAT amwage tena yetu ya -OLD VETERAN

Read more...

Katika KUTONESHA kidonda!

>> Sunday, February 19, 2012

Katika KUTONESHA,...

.... labda MTONESHWAJI huweza FIKIRI  ni tamu  kama kajiandaa na MAUMIVU,...
.... na kama anajua kidonda  chake kimaumivu kinaumaje na  kuwa chake kidonda kwa ridhaa yake safari hii  na wakati huu kita kuwa ni kidude amacho  CHATONESHWA .:-(

Swali:
 • Unabisha?

Ndio,....
.... MASWALA mengine labda ni ya KUJIPANGA,....
.... kwa kuwa KABLA ya umivu MTU akijua UMIVU laja,....
......labda MAUMIVU ni UTAMU.:-(

Ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumapili NJEMA MKUU!
Hebu turudi ghafla KENYA ili MOMBASA ROOTS warudie-DISCO CHAKACHAOFFSIDE TRICK wajaribishe- KIDUDU MTU

Au tu hebu KATA MWANANGU KATAAu tu BUJU BANTON anyanyase baadhi ya watu  tena ki-Boom Bye Bye


Nipo  BADO  mpaka  DUBROVNIK Lounge .....
Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP