Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu KISIMI cha NENO!

>> Saturday, February 18, 2012

NENO,....
.... labda si NENO TU kineno,....
..... na labda  ndio maana yasemekana MANENO MENGINE eti ni MATUSI,...
... halafu  eti ndio maana MANENO mengine eti ni ,....
.....NENO la MUNGU.:-(


Swali :
  • AU?


Na eti katika BUSARA za NENO,...
.....labda BUSARA si NENO ila BUSARA za NENO hutengenezwa na MSIKILIZAYE neno mwenye BUSARA,...
.... kwa kuwa eti ASIKILIZAYE neno na TAFSIRI ZAKE ndio hugeuza neno kuma kuwa tusi au uke wa NZIGE na kibusara kuamua kuwa hilo neno ni BUSARA au LA hasha.:-(

Swali:
  • AU?
  • Si eti PUMBAVU kwa mwingine  kama ni neno tu ``PUMBAVU´´ labda kimzani HILO NENO ni sawasawa tu na neno``BUSARA´´ kibusara?

Na labda,....
....KINENO kwenye sentensi yoyote ile,....
....UKINYAMBULISHA,....
... labda kila sentensi yenye MANENO ina KISIMI  chake ambacho ni NENO,...
.... na labda hata ndilo NENO  lisababishalo ustukie SALA fulani ya MTU FULANI  kimaneno kuwa ni KALI  na kuwa kuna WENYE maneno ambayo KISALA kila siku unapendelea SALA ZAO  ZAIDI kuliko za WENGINE kimsikilizo wa KIBINADAMU kwa kuwa NENO lao LIMETULIA  kama tu ujuavyo nani KINENO  kwa kutongoza kizaidi kineno ni KUBWA KULIKO kuliko WENGINE kwa kuwa ana NENO tamu kineno.


Na ni wazo tu hili MHESHIMIWA!
Jumamosi NJEMA BINGWA na si KIMANENO tu!


Hebu SOLOMON BURKE arudi tena ghafla kwa- Hold On I'm Coming

Chic warudie ya -Le Freak


Halafu BECK wazime kwa -LOSER

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 12:31 pm  

Nakusifu kwa kuwa wewe ni wewe na uandikacho ni kweli maana unaandika ukweli. Jumamosi njema kwako pia na Upendo utawale kwako:-)

SIMON KITURURU 12:48 pm  

Upendo daima@Kadala Yasinta

Yasinta Ngonyani 2:13 pm  

Kumbe unakijua kingoni Hongera KADALA ...au hukujua kama ni kingoni? aahh kumbe nimekumbuka umeishi ungonini..

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

There was an error in this gadget

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP