Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa mara nyingine na ni SIKU NYINGINE!

>> Tuesday, June 30, 2009

MATATIZO ni yale yale,...
.....ingawa SIKU ni NYINGINE.

KWA KUWA ni siku nyingine,...
....matatizo yaleyale hudhaniwa ni mapya ,...

.....kwa kuwa ni SIKU NYINGINE.


Kwa kuwa WEWE si WATU WENGINE,....
.... baadhi ya MATATIZO YALEYALE kwa wengine,...
.... WEWE waweza kudhani ni MAPYA kwa kuwa umeyagundua SIKU NYINGINE.


Na kama unajifunza KUTOKA KWA WENGINE,...
....matatizo YALEYALE ukiyafumbia macho HUJIFUNGUA MTOTO,...
... na siku moja unaweza ukaamka na tatizo JIPYA kweli kwakuwa ni SIKU NYINGINE.


Lakini MATATIZO ndio SIRI ya UFUMBUZI wa TATIZO,...
... na kushughulikia MATATIZO ndio SUKARI YA MAISHA kama ufumbuzi wa TATIZO,...
.... na hata kama ni kweli UTAFUMBUA FUMBO la kiini cha TATIZO siku nyingine.

Na leo ni SIKU NYINGINE,....
... na kama unadhani huna TATIZO basi wewe maisha yako yaliishia jana,...
... na hukufika leo SIKU NYINGINE.Swali:
 • AU?
NI wazo tu KINGUNGE na NIMEACHA kukuzingua!:-(

Ngojea Scarface na 2PAC wakukumbushe-Smile


AU tu THE POLICE warudishe gurudumu nyuma zaidi katika ...- De Do Do Do De Da Da Da


Read more...

Katika kuongelea BILA AIBU angalau UWEZEKANO wa kuwa MIMBA ya KUKU ni YAI!

Tukiachana na swala la KUKU MJAMZITO....
....... baada ya KUKU kufanya TENDO LA NDOA kama BATA,.....

.....tuongelee binadamu kiduchu basi!

Kwa BINADAMU kuna TAMADUNI, MILA na DESTURI zifanyazo tuamini KUWA NI ukweli kuwa swala la UJAUZITO ni la wakubwa,....
..... ndio maana binadamu akiwa mtoto hudanganyika kuwa watoto wananunuliwa duka fulani au kuna ndege anawaleta hata kama anayemsimulia BINADAMU MTOTO HUYO , ana MIMBA.:-(

Na ,...
.....kwa kuwa jamii inadai kuwa MASWALA YA UJAUZITO ni maswala ya faragha kuna ambao wamepata mimba kwa kutojua MASWALA YA mpigwa chini huvimba JUU.

NDIO!
Tamaduni zetu wengi zinatufanya tuepuke kuzungumzia mambo fulani:-(

Na ujuzi wa asilimia kubwa ya vijana siku hizi ,....
......ni wakujifunza wenyewe KUPEKECHA ingawa kuna washangaao kwanini RIJALI kila siku akiingia mtandaoni akilini akiona KIBONYEZO ''search ''hakawii kuandika mbele yake neno ''SEX''.

Ndio!
Asilimia kubwa ya WABONGO niwajuao wamejifunza maswala ya KITENDO CHA KUUJAZA ULIMWENGU wenyewe kwa kuwa ndugu na hausigeli hawakuviongelea kwa kuwa MILA na DESTURI ZIMEWAFUNGA mdomo hata WAZAZI.:-(


Na tatizo kubwa katika hili ni kwamba,....
..... kama huna MUONGOZO itabidi ujishughulishe mwenyewe KUPATIA na kwa bahati mbaya kwa kujifunza bila MUONGOZO waweza kujikuta USHAZOEA KUKOSEA matumizi ya NYETI.


Kumbuka,...
... apataye MIMBA wakati anapata MIMBA kunauwezekano MKUBWA alikuwa anafikiri anapata URODA tu a.k.a MIKASI na sio alikuwa ANAMIMBISHWA.:-(

Kumbuka,...
..... mara nyingi BEBERU LIKIPANDA huwa halifikirii matokeo yake ni kumpa mimba KIMWANA mbuzi.


Na kumbuka ,....
.... mwenye mimba anapendeza kwa kuwa unajua ana mimba LASIVYO ni kweli mwenye mimba huwa ana tumbo KUBWA a.k.a BOMBA LA TUMBO na HUWA anabadilika MWENDO.

Kwa hiyo,...
..... jihadhari kumuuliza MWENYE TUMBO KUBWA asiye na MIMBA maswala ya UJAUZITO kama hutaki kufyonzwa KABLA hujashushiwa bomba la TUSI lenye uzito wa KILO KADHAA lifuatwalo na bomba la KOFI .Na kama wewe mfupi JIHADHARI kwa kuwa labda pia utapewa bomba la konzi lenye KILO TATU na NUSU hivi kwa kukosea wa KUMDADISI.

Na ni kweli,....
..... ukikutana na mwanaume akukumbushaye MWANAMKE mjamzito, basi inasemekana huyo ANAKITAMBI kitu ambacho SI AFYA kama tu toto dogo lenye tumbo kama mimba linaweza kuwa lina KWASHAKOO , UTAPIAMLO ,nk.....
........ kitu ambacho SI AFYA!:-(Na ni kweli,...
..... MIMBA ni KIBOKO ndio maana UMEZALIWA.:-(

Swali:
 • AU?

DUH!
NALIKATIZA wazo hili kabla ya KUONGELEA kuhusu MIMBA ya kuku bila KUOMBA ruhusa ya KUKU!
Swali:
 • Hivi kweli umesoma mpaka sentensi hii hapa katika SWALA HILI lenye uwezo wa kuwa ni la KIJINGA ?
 • Unafikiri lini katika ukuaji wako ulistukia MIMBA sio KITAMBI na KITAMBI sio MIMBA?
 • Unafikiri kungekuwa na uwezekano binadamu wasingehusudu KUTAGA kama kunguru ili kukwepa kuvaa MATENITE DRESI ingawa kasheshe lingekuwa ni zamu za hausigeli kuyatamia mayayi wakati bingwa YUKO kwenye KICHENI PATI?

Kumbuka ni wazo tu NA NIMELIKATIZA nikiwa nakutakia KILA la KHERI katika LAKO LIBENEKE!


Ngojea Kenny Roggers abadili hali ya hewa kwa kitu- You are so BeautifulAu tu BONGO MAFFIN watukumbushe- MAKEBA

Read more...

JINSI ya kumuibia MJANJA!

>> Monday, June 29, 2009

CHAMSINGI,...
...mfanye AAMINI unaamini kuwa yeye MJANJA!

Swali:

 • AU?
Kumbuka kutofautisha kuiba na KUPORA,....
...... na uwezekano wa kubwengwa ukidakwa kwa kukosea staili ya kumuibia MJANJA.


Nalikatizia hili WAZO hapa kwanza labda halikufundishi kitu kama wewe sio MWIZI!:-(

JUMATATU njema KIJEBA na ikiwezekana USIIBE nasikia ni DHAMBI!


Au turudi KENYA Safari SOUND BAND wakumbushe- MAMA LEA MTOTO WANGU..


Au tu GREGORY ISAACS abadili kwa -Love is OVERDUE..

Read more...

KATIKA kukumbuka TOTO zuri LIKUTISHALO ni kweli NALO bado linaenda HAJA KUBWA a.k.a KWA lugha ya kisasa -KUNYA!!:-(

>> Sunday, June 28, 2009

Labda ni KWELI,...
...hakuna BINADAMU mjanja INGAWA kuna IDAIWAO ni WAJANJA.

Na kama kuna UJANJA,...
...basi MJANJA hajazaliwa:-(

Na kama unadhani WEWE ni mjanja,..
... jaribu kuhairisha KUNYA ukibanwa TUONE.[samahani kwa matumizi ya lugha ya faragha!:-(]


Swali :

 • Unafikiri akutishaye anakutisha nini ikiwa kila BINADAMU unajua ni SPESHO?

NAACHA wazo na samahani kwa WAZO hili hapa MAWAZONI Bingwa, NA KATIKA HILO kumbuka hili ni wazo tu KIJEBA!:-(
Kwa mara nyingine JUMAPILI njema BINGWA!

Ngojea Jermaine JACKSON adai...-Do What You Do


Au tu Jermaine Jackson adai tena-Sweetest sweetest

Read more...

STORI za JUMAPILI kama tu za JUMANANE za Kalumekenge!

KalumeKENGE aliamka,...
..... na kuachia bomba la M-hayo kabla ya kujinyosha na kujamba kidogo.

Ndio ,...
....ALIAMKA halafu baadaye siku ilipoisha AKALALA kama wewe TU!:-(


Ndio,..
.... labda kuna MUDA ndani ya SIKU kwa kuwa yuko hai alifanya jambo AFIKIRIALO ni KUBWA akilini mwake kabla hajaenda MSALANI kama wewe TU!:-(


DUH!

Swali:

 • AU?
 • Hivi kwani JUMAPILI inarangi tofauti na JUMANNE ,na ukisikia njaa, njaa ya JUMAPILI ni tofauti na ya ALHAMISI?

DUH!

Ngojea NIACHE wazo hili na labda ni la kijinga!:-(

JUMAPILI njema KIJEBA!


AU ngojea MR BEAN aboreke KANISANI kiduchu katika....-Church boreAu tu tumchungulie MSENGE akishughulikiwa KANISANI na wajanja...-Church Rids Gay Demon....

Read more...

Ushawahi KUTHUBUTU?

>> Saturday, June 27, 2009

Na,....
..... hapa siongelei swala la KUTHUBUTU kwako KUNYA,(samahani kwa lugha ya faragha), namaanisha kwenda HAJA KUBWA, kwa kuwa hata KUKOJOA(samahani tena kwa lugha ya matusi), namaanisha hata HAJA NDOGO unafanikisha ukiwa PEKE yako CHOBISI shwari.:-(


Ukitaka kujihakikishia una nguvu za KUTHUBUTU,...

.... jaribu KUTHUBUTU angalau KUJAMBA mbele za WAHESHIMIWA au WAGENI ambao HUJAWAZOEA kwa MAKUSUDI!:-(

Swali:

 • AU?

Kuna uwezekano LABDA kama UNGETHUBUTU sasa hivi usingekuwa unanisoma na ungesha JIUA zaaamaniiiii HATA kwa kula sana hata MAGIMBI au tu kwa kudai kama nidaivyo MAISHA MAGUMU!:-(

DUH!

Swali:
 • Au?

Thubutu lakini kama unataka kuwa WEWE na sio kuwa WATU wakufikiriavyo wewe kama tu MUUZA SURA kwakuwa una BOMBA la PUA ingawa MWANIWANE una MIAKILI MINONO na TABIA KIJEBA!:-(

Swali:
 • Unafikiri kama wajidanganyao KUWA NI wazuri wauzavyo sura , UNAFIKIRI wewe huuzi tabia INGAWA unamaaeneo mazuri KIFICHONI yenye TABIA MBAYA YAKITEKENYWA hata kama BADO yana nywelenywele NJOLINJO?
OK Bingwa nikiacha KUKUZINGUA na UJINGA;
SWALI:
 • Unauhakika umewahi kuthubutu na bado ukabakia MASIKINI?

NAACHA wazo BINGWA!:-(

Ngojea TUKAECHINI ili TUJIFUNZE watoto WADOGO wanasemaje kuhusu KULA KONI katika-Oral Sex the New Goodnight Kiss...


Au tu tusikilize utunzi wa Michael Jackson na Lionel Richie katika-WE ARE the WORLD..


KWA MARA nyingine ASANTENI WOTE! Mkiwemo hawa kwenye picha zangu za juzi ya MTONDOGOO....

Photobucket

Photobucket


PhotobucketPhotobucket
PhotobucketPhotobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucket


Photobucket


PhotobucketPhotobucket


Photobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucketPhotobucket


PhotobucketPhotobucket
Photobucket
PhotobucketPhotobucket
Photobucket
Photobucket
Photobucket

Read more...

R.I.P Michael JACKSON!

>> Friday, June 26, 2009

Kwaheri Mkuu na Asante kwa muziki kama HUKO ULIKO unanisikia BINGWA!

Mie bado wako Mshabiki.

Ciao!


Read more...

UKIWA na uhakika wa KULA njaa haiumi HARAKA!Lakini!:-(

>> Thursday, June 25, 2009

Ukiwa na pesa za GARI,...
... mwenye gari hakuumizi KICHWA.


Ukiwa huna uhakika wa gari na unauhakika wa MKWECHE,....
....mwenye gari , ingawa ni mpaka uwe unataka gari ,ANATISHA!


Ukiwa na uhakika UTAFIKA,...
.... waliotangulia SI WAJANJA.


Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako wa KUFIKA,....
..... unaweza mpaka kuanza kufikiri UTAFIA NJIANI na waliotangulia kwako WANATISHA.

Ukiwa na mke MZURI,....
....wenye wake hawakutishi kwa kuwa unaujua MKENGE waliouvaa.

Ukiwa na mke MBAYA,...
... wake wa wenzio wanavutia MNO kwa kukosa KASORO na jicho la ubongo WAKO litabunia MPAKA umbo lao hata la kabla hawajavaa.

Swali:

 • Hivi kweli kuna mke mbaya duniani?
Ukiwa na MUME MZURI au MBAYA mie sijui nini kinatokea na SAMAHANI kwa KUKOSA UTAALAMU wa HILO!

Ndio,...
.....Ukiwa na uhakika leo hata kuhusu ya kesho,....
... walionayo leo HAWAKUTISHI.

Tatizo ni;
...Ukiwa na uhakika leo, HUO NI UHAKIKA WA LEO,....
.....na labda kesho utagundua;
 • Pesa zako zikutiazo kiburi leo hazitoshi kesho kununulia hata mkweche.
 • Uhakika uliokuwanao leo kesho haupo, na ghafla huna uhakika wa hata kufika kesho kutwa ya KESHO.
 • Kakitu ambako katafanya MKE wako mzuri leo, USTUKIE kumbe tokea ZILIPENDWA alikuwa mbaya.


NA LABDA,....
....
Kibinadamu, ALAYE SASA HIVI ndiye mwenye uhakika ANAKULA,..
... na siye wengine HATUJAPANIKI TU kwakuwa TUNA MATUMAINI TU kuwa baadaye TUTAKULA.

Uzuri ni kwamba ,...
...BINADAMU huendeshwa na TUMAINI,......

.... ndio sababu ukiwa na kibano LEO unadhani labda utafaidi mbinguni WAKATI labda KIBANO CHAKO unachodhani ni KIBANO LEO ni KILE chakutamani unywe GONGO NA WASHIKAJI halafu usinyimwe TENDO LA NDOA a.k.a URODA a.k.a MIKASI a.k.a MATUSI a.k.a UASHERATI hapo baadaye CHOBISI , ingawa LABDA mambo yote HAYO umeshafundishwa na DINI YAKO kuwa MBINGUNI hayapo, NA kule mambo yote ni JUISI kwa MAZABIBU halafu KUIMBA kwa SANA TU na MALAIKA , halafu kwa bahati mbaya hakuna KUCHOKA.:-(

DUH samahani kama nakukwaza kwa kuwa unadhani nakufuru!:-(


LAKINI,...
....UBINADAMU ni NISHAI KWELI kwa kuwa kama wewe ni BINADAMU na SIO JINI, labda KWAKO hakuna lenye uhakika!

NAACHA wazo na KUMBUKA ni WAZO TU na nakutakia kila la kheri katika kukuza lako TUMAINI.
Damn , I am depressed now.(NA samahani kwa kuingizia ung'eng'e KIDUCHU!:-()

PEACE!

Tupitie Kenya kidogo Les Wanyika wadai - Dunia KigeugeuAu tubaki tu Kenya Salim Junior adai-Ni sorry Muno..

Read more...

MAFISADI wa CHANGU changu na CHAKO changu!

Ukiwaangalia WANASIASA-mafisadi,...
... utastukia wanadhani CHAKO CHAO,....

..... KAMA HUJASTUKIA tayari KWENU wanadai ni KWAO.

Afadhali na MALAYA-mafisadi wa NGONO,.....
.....ambao CHAKO hukitakakiwe CHAO,....
....na ukiishiwa nakukistukia CHAKO ndio waweza kustukia hawakukuacha mtupu na kwa UKARIMU walikuachia angalau GONJWA LAO.


MAFISADI wa UNDUGU,....
.... ukifanikiwa wewe ndugu YAO,....
.... ila ngojea UCHACHE ndio ustukie wao si ndugu kwa KUSIKIA wadaivyo hawakujui na matatizo YAKO si YAO.Na wale MAFISADI wa URAFIKI,...
....CHAO ni CHAO na CHAKO ni CHAO,.....
.... na unaweza usistukie mpaka usiwe na CHAKO.:-(


Swali:
 • Lakini kwanini ujilimbikizie CHAKO kwa kuwa ni CHAKO KIDUDE ili iwe nini kama HUKITUMII kidude?

 • Unakumbuka ukifa hata uwe na chupi ngapi labda ni moja tu utazikwa nayo halafu makorokocho yako yote mengine utayaacha?
NAACHA wazo!

Ngojea AEROSMITH wadai..-I don't wanna miss a thing

Au tu ALAINE abadili bila kubadili hali ya hewa...-Make me WEAK

Read more...

SABABU za mlevi KUYUMBA!

>> Wednesday, June 24, 2009

NI kweli,....
.....Ujanja wa asimamaye au kutembea BILA KUYUMBA uko MASIKIONI na sio miguuni kama idhaniwavyo.


Ndio,...
...SIKIO kazi yake si KUSIKIA PEKEE kama unakumbuka HATA maswala ya balansi, bingwa ni SIKIO.

Hebu tujikumbushe BAOLOJI ya sikio kwa ndani katika NJONJOLINJO...

Semicircular canalExterior of labyrinth.


Inner ear illustration showing semicircular canal, hair cells, ampulla, cupula, vestibular nerve, & fluid


USITISHIKE,....
...... yote ni katika kukukumbusha kwa KUTEMBEA KWAKO KWA MARINGO kumbuka NI SIKIO linakusaidia kufanya hivyo NA SIO TAKO kama wewe kwa mwendo wako wa maringo huwa unatingisha tako!:-(


Halafu ni kweli,...
.... sababu kubwa ya Mlevi kuyumba ni kwamba KALEWA.

Swali:
 • AU?
 • Kwani wewe ulifikiri hadithi hii nitaisimulia kwa urefu gani?
 • Hivi sasa hivi sikio lako ukilichokonoa halina NTA ingawa sikioni mwako hakuna nyuki?

NAACHA wazo MKUU na NAKUTAKIA siku njema KINGUNGE katika libeneke!

LAKINI kama unamuda ngojea Waziri wa Utamaduni wa Brazili a.k.a Gilberto Gill atuburudishe tena kwa- Aquele Abraco

AU Ngojea tu tena Gilberto Gill adai -Waiting in Vain..

Read more...

TAFADHALI usisome STORI HII ya SIRI za MHESHIMIWA aziongeleazo CHUMBANI na kujifanya kazinunia HADHARANI!:-(

ANAYEJIHESHIMU ,...
......huaminika kuwa HUWA ndiye asiyoyaongelea MAMBO kama hivyo HADHARANI,....

.....ndio maana kuna wasahauo WAITWAO WAHESHIMIWA wengi ndio wateteao ujinga HADHARANI.


MHESHIMIWA ,....
..... inasemekana HAVAI HIVYO hadharani,....
.... ndio maana ni bingwa zaidi ya WANAMAZINGAOMBWE kwa UTETEZI wa NGUO kwa MANENO hata wakati akiwa anawazia YALIYOUCHI fikirani HADHARANI.


Na ya MHESHIMIWA yako FARAGHANI,....
.... ndio maana WASIOFIKIRI HUKOSEA wakumuheshimu HADHARANNI.


UHESHIMIWA ni kama MADAWA ya KULEVYA,...
.... aliyenaswa na KUHESHIMIWA anajikuta anaung'ang'ania hata kwa kuomba kura za vyeo asivyovistahili HADHARANI.


Na kama unataka kulogwa na MHESHIMIWA,...
....baadaye kidogo baada ya KUWINI chuki za MHESHIMIWA,.....
... toa siri zake za CHUMBANI hadharani.


NAACHA na ni wazo tu MKULU!
Kumbuka kama umenisoma mpaka sentensi hii wewe si MTIIFU kwa kuwa nilikuomba kwenye KICHWA cha habari usisome STORI HII!:-)

Swali:
 • AU?

Ngojea basi tuliwaziwe na The VERVE katika - Bittersweet Symphony


Au ngojea tu Eminem, Jay-Z, Lil Wayne waharibu wimbo huo huo katika -Bittersweet Symphony Remix

Read more...

Katika ULIMWENGU huu wa leo wa CHUNA BUZI , sijui bado BINTI Khalufani kwa KUNEMA hawezekani?

>> Tuesday, June 23, 2009

Siku hizi inasemekana,...
.... hata kama Binti Khalufani hawezekani kwa kunema, WANAUME hawawezi kustukia a.k.a KUJUA.

Lakini labda hata hapo zamani za miaka fulani iliyopita,..
... ujuzi wa Binti Khalufani au tu Binti Josef ulikuwa unapimwa kwa utiifu hata kama ni utiifu kwa mambo ya ajabu katika jamii ili mradi jamii inayaona ni DILI kama ya kukubali kutahiriwa KIDUDE na huko huko atahiriwako KUFUNZWA kuamini Mwanaume tu ndio USAHIHI WAKE ni SAHIHI.

Swali:

 • AU?
Ngojea nianze stori hii upya.......

Hadithi !Hadithi!

Nasikia enzi za ZILIPENDWA , ....
....VIMWANA walikuwa wanafunzwa kutii waume zao !:-)

Na nasikia pia ,...
....ilikuwa kama Mke wako akikushinda kwa HOJA kama tu aendeleavyo kukushinda hoja sasa hivi,.....
..... ilikuwa RUKSA kwa KIDUME kumchapa makofi halafu kabla hajamalizia kulia ilikuwa DILI kumshughulikia kunako apate MIMBA ili achunge adabu zake!
DUH !Kudadeki Walakhi!:-(


Kwa kifupi ,...
.....WANAWAKE na WANAUME enzi hizo ukitazama na kufikiria kwa jicho la kileo unaweza kugundua walikuwa hawajuani ila mmoja alikuwa anajitoa mhanga ili mwingine AFAIDI.

Swali kiduchu:
 • Hivi ni wewe ujitoaye muhanga mwenzio afaidi LEO HII au ni yeye ajinyimaye UMIMI ili wewe ufaidi halafu mahusiano YENU bado hayanogi?

Kwa bahati mbaya,...
... Bado naamini leo hii bado siye WANAUME tulio wengi hatulelewi kumuelewa au hata kumjua MWANAMKE. Halafu juu ya hilo, SI RUKSA KUMBWENGA Mwanamke wako hata pale katika klabu ya GONGO au Ulanzi kama tu pale kwa Bibi Kisebengo wauzapo DENGELUA siku hizi.

Kwa bahati mbaya,...
....naamini leo hii hata WANAWAKE walio wengi hawawaelewi WANAUME wanataka nini na kama unabisha WASIKILIZE waongeayo.:-(

Ukitaka kustukia kuwa hali si nzuri,....
 • Cheki jinsi gani Pochi lako likuzungumziavyo kuliko Roho yako katika maadili ya leo.
 • Sikiliza watu hata uhisio ni wenye busara wakizungumzia siri ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume hasa wakati unajua siri hizohizo wangapi zimewaharibia ndoa au kupoza penzi hata kama bado kidude wanapata.:-(
Swali:
 • Umestukia mpaka wafuata dini wamsukumiavyo Mwenyezi Mungu matatizo yao ya ndoa ambayo mengi yao yangetibika kwa wao kuongea tu a.k.a kuwasiliana/kusikilizana?
 • Unataka kusema hujawahi kusikia, hasa kama wewe ni MKRISTO, wakwepao kuongea moja kwa moja MPENZI na mpenzi kwa madai YA kupitia kwa Yesu na Biblia kitu ambacho huwatisha kuachana na kuendelea kuishi pamoja bila furaha kwa jina la Yesu?


Unaweza kunibishia lakini na LABDA miye siwezi kukubishia mwenzio KWA KUWA mwenzio hapa nawaza tu MKUU!:-(

Ndio ,..
....labda kati ya Mwanamme na MWANAMKE ukunaji wa kipele unaumuhimu wake ila labda ni muhimu kwanza kustukia uwepo wa KIPELE maeneo na kama ni busara kukibinya nasio kukikuna.

Na unaweza kubisha!

 • Leo hii tunavyoongea hapa bado WANAWAKE na mambo yao pamoja na KIDUDE chao yanaenda kivyao KAMA tu WANAUME na mambo yao ikiwa pamoja na UUME wao wanaenda kivyao.

Na asilimia kubwa ya wapenzi wenye tatizo la MAHUSIANO leo HII ukiwaweka vyumba tofauti na kuwauliza nini ni tatizo usishangae ukisikia hawana jibu linalofanana kama kwa mfano utakuta:
 • Mume adai tatizo hana pesa za kutosha, mwanamke akadai pesa si tatizo ila HAKUMBATIWI vya kutosha NA ndio tatizo!
 • Mwanamume akadai hapewi kidude vya kutosha , wakati MWANAMKE akadai KIDUME nyumbani haonekani na kidude hana muda nacho na katika KUGIDA anakila kwa uchovu ingawa daima NAMWANDALIA na manukato nanyunyizia.

 • Mwanamke akadai hasikilizwi wakati mwanamume akidai Mwanamke mashoga wamezidi na KIMWANA hapatikani ukitaka angalau KUMNG'ATA sikio.
 • Mwanamume akadai anatamani NA anafurahia KIMWANA akimfyonza, wakati MWANAMKE akadai alivyofunzwa kumfyonza mtu ni matusi na Kidume AMKOME BABU WEE nyooooooo!.:-(Swali:
 • Unafikiri lakini Mwanamume gani siku hizi anauhakika Binti Khalufani kwa kunema hawezekani kabla ya kukutana na Binti Khalufani ki- MKUTANO?
 • Unafikiri jamii inavyobadilika ni kwanini MAFUNDISHO ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume ambayo ndio misingi ya BOMBA LA FAMILIA hayatiliwi MAANANI yabadilike kukidhi mabadiliko ya Limwanamume na Limwanamke wa leo wajengao JAMII ya LEO?
DUH nimekumbuka miye si mtaalamu wa Mahusiano YA WATU na NAACHA TOPIKI!
NIMEACHA na kumbuka hili ni wazo tu na NAKUTAKIA siku njema JEMADARI!Ngojea niwaachie ARROW wabadili hali ya hewa kwa kitu-Hot Hot Hot

Au tu Arrow waongelee sabuni ya roho kamaitambuliwavyo na baadhi ya watu-
- money moneyASANTENI tena WADAU wote !
Asanteni hawapia ambao hamkunitenga siku za karibuni ambao baadhi ni hawa kwenye picha zangu.....

Photobucket


PhotobucketPhotobucketPhotobucket
PhotobucketPhotobucket
Photobucket
Photobucket
PhotobucketPhotobucket

Read more...

CCM OYEEE na chamoto TUNAKIONA!:-(

Hata utakekubisha,...
..... kama wewe ni Mtanzania unajua kuwa mpaka leo CCM inabomba la msuli ukilinganisha na UPINZANI.

Na kwa bahati mbaya,...
....
kwa muda wote huu chama hiki kinatawala kwa walio wengi hawajala KINGI.


Kwa bahati mbaya,...
..... hata wajanja kibao wanafikia kuamua kuwa WANACCM ili kuwa karibu na KINGI.

Swali:

 • Unabisha?

Kwa hiyo hata kama huipendi CCM,...
.... si vibaya kukiri kuwa kuna kitu wanapatia ndio maana katika STATISTIC zangu Mtakatifu Simon Kitururu ambazo sijazifanyia utafiti, ASILIMIA KUBWA YA WENYE nafuu TANZANIA ukichunguza ni WANACCM au wana uhusiano na CCM.

Swali :
 • Unabisha?


Kwa hiyo,....
.... utake usitake naweza kuwa sijakosea kwa kusema CCM OYEEE, ila zisidumu fikira za Mwenyekiti zenye mrengo wakutunyima KULA KINGI:-(


Swali:
 • Sijui Watanzania wote tujiunge na CCM kama ndio kwenye ulaji?(au unasemaje Bingwa!)
 • Kwani kuna sababu gani za kujiunga na CHAMA kingine kama ulaji uko CCM?
 • Hivi ni kweli unafikiri CCM ni CHAMA CHA MAPINDUZI?


Naacha, na kumbuka ni wazo tu KIBOSILE!
Haya basi VIVA CHADEMA!Viva CUF! Ila mnaulaji kwa wananchi wote CCM iwanyimao NANIHII?


Baadaye BASI!
Ngojea East African Melody wadai -UTAJIJU JIJI


Read more...

JICHELEWESHEE huzuni kwa angalau kujaribu KUCHEKA mwanawane!

>> Monday, June 22, 2009

Labda kuna ukweli ,..
.... WACHEKESHAO ni wale wajuao SHIDA na kwa KUKUCHEKESHA wako tu katika kukwepa HUZUNI!:-(


Labda ni kweli,...
... kwa KUCHEKA unajicheleweshea HUZUNI.

Swali:

 • AU?

CHEKA BASI KINGUNGE ,....
.....kama UMESHAFANIKIWA KUSTUKIA au unakumbuka tu kuwa MATATIZO HAYATAISHA hata UKITUNUNIA.:-(


Kumbuka,...
.... hata kwa kujichekesha BINTI Khalufani alifanikiwa KUCHEKA na hilo laweza kukutokea wewe kama ukiacha KUJINUNISHA.:-)

Ni hilo tu na JUMATATU NJEMA Kingunge!

AU tu msikilize Chameleone aongelee - Shida za dunia

Read more...

MATUSI!

Matusi ni vitendo,...
.....ingawa TUSI halihitaji VITENDO.

Matusi ni neno,....
..... ingawa bado unaweza kumtukana mtu kwa JICHO kama vile tu kwa KUMNG'ONG'A.

UMIVU la tusi hutegemea na UDHAIFU WAKO wakuoanisha UDHAIFU WAKO na tusi.

NA hakuna tusi duniani WEWE UKIAMUA,....
..... kama tu ILIVYOKUWA kuna uwezekano wa kila kitu kuwa tusi kama WEWE UKIAMUA.

Swali:

 • AU?
 • Unauhakika jina lako mtu akilitamka kwa staili fulani huwezi kuhisi ni TUSI kama tu kwa kilugha fulani Rais CHILUBA au neno GENGE ni tusi?


NAACHA halafu kumbuka ni wazo tu na wala labda halimuokoi MTU!:-(
Nakutakia LIBENEKE jema KINGUNGE!Ngojea nimuachie Gerald Campbell ahubiriye wenye matusi kichwani....


Cat Stevens a.k.a Yusuf Islam aongelee-A is for Allah


Au tu Snoop DOGG ,Dr.Dre na Dangelo waendelee kutukana huku wakilipwa :-( katika-Imagine..
..

Read more...

UNAKUMBUKA swala LA KWENDA kupima UKIMWI?

Ni hilo tu nataka kukukumbushia,...
..... kama unahisi hili swala na weye LINAKUHUSU kama tu YULE au MIMI!


Swali:

 • Kwani swala hili linahitaji maelezo zaidi?
NIMEACHA ingawa LABDA HILI swala linahitaji maelezo ZAIDI!:-(


Ngojea TENDER MAVUDLA
ambaye anaishi na MDUDU atukumbushe jambo fulani tena...

Read more...

HADITHI hii nimefundishwa na MALAYA!:-(

>> Sunday, June 21, 2009

KATIKA fundisho kumbe ni kweli,.....
.....UNAWEZA kulipia kupewa hata GONO kama tu ununuavyo viazi VITAMU.:-(

Na,...
...
mpaka konokono wanafanya ngono na kama wewe unafanya matusi/MAPENZI kwa mwingine hiyo ni NGONO tu:-(

Na ,...
.....MALAYA ni mtoto wa mtu na inawezekana ni ndugu yako au ni mtoto wa mheshimiwa kama wazazi wako kama SIO MTOTO WAKO na labda uwepo wake duniani ni matokeo ya NGONO tu.:-(

Na,...
..... si lazima ujilazimishe kupata dhambi ingawa unafanya dhambi nyingine kwa kuwa unajua ni dhambi na NONO.:-(

Na,...
..... MALAYA ni kwa wengine kama kwako unaamini ni wako na UKO NAYE na PIA ni MNONO.

Swali:

 • AU?

DUH !
Naacha wazo MHESHIMIWA na samahani kwa kukupotezea MUDA kwa kunisoma NA labda badala ya kunisoma sasa hivi HAPA ungekuwa uko chooni UKIFANIKISHA!:-(

Swali:
 • AU?
 • Unauhakika malaya ni malaya na sio ni FIKIRA ZAKO TU kwa kuwa UNASHINDWA KUTOFAUTISHA ugawaji wake MALAYA na HURUMA au unauchanganya TU na kuwa kwake na roho NZURI ya KUGAWA nanihii?


NAACHA!

Hebu tupitie tena MALAWI tukutane na Fuggie Kasipa + Njati Njedede walete za - UkaneneAu tupitie tu tena ZAMBIA Angela Nyirenda aburudishe kwa - Ngoma

Read more...

Labda kuna TITI kama CHUCHU au KIPELE kama JIPU , na hiyo LABDA sio STORI katika HADITHI hii !:-(

>> Saturday, June 20, 2009

KUMBUKA,...
...ujanja wa KANISANI sio UJANJA wa MSIKITINI ingawa zote ni IMANI:-(


Kumbuka,...
....UJANJA wa kanisani labda niwa SADAKA!:-(


Kumbuka,...
..... Ujanja wa MSIKITINI aujuavyo SIO wewe na ni SHEKHE ajuaye ndio maana akiamua UTABINUKA kwa IMANI na ukibinuka kwa kweli hiyo ni staili ya SALA na yote ni IMANI!


Kumbuka,....
...LABDA kanisani AU msikitini kama ungekuwa MJANJA ungestukia kuna WATU wanatibu hukohuko MPAKA ya UCHI kama tu CHUMBANI kama wewe ni mjanja chumbani na unajua mpaka ujanja wa MIGOMBANI na UNAKIBURI katika KUNG'ANG'ANIA nanihii hata kama hiyo haina KISHIKILIO!:-(Swali:

 • AU?

Halafu NI KWELI,....
.... labda ujanja wa TITI ni CHUCHU la sivyo hakuna KINYONYEO!:-(

Na stori hii haina uhusiano na TITI wala CHUCHU na bado hili si kielelezo cha naongea nini.:-(

Swali:
 • AU?

Ok ngojea niache KUONGEA !
Mtaalamu samahani kama NAKUKWAZA !:-(


Au ngojea tena BURNING SPEAR aongelee UZOEFU katika- This Experience:-(
Au turudi tena TU AFRIKA KUSINI Arthur MAFOKATE agune katika - OYI OYI...

Read more...

KU-mamaye/KU-dadaye Walakhi! BINGWA miye KAMA weye NIMENYIMWA kuonewa mpaka HURUMA!:-(

>> Friday, June 19, 2009

Ni tusi kuonewa huruma,...
.....
kama wewe katika SIGIDA kwa kuwa una SIGIDA ndio UNADHANI unatakiwa kuwaonea huruma wasio na SIGIDA kwa kuwa HAWASUGUI sebule ya kichwa kwa KUSALI mpaka wakaota SIGIDA!:-(Na KUONEWA HURUMA ,...
......ni siri ya UMASIKINI kama wakuoneao huruma wanakitumbua na wamefikia kukunyima KITUMBUA na huna uhakika na uwezo wako wa KUTIMBUA.:-(


Na si siri,...
.... kuna kitu nimenyimwa LEO kama MWAKA JANA kama WEWE TU ,....

.... ambacho kwa kunyimwa nakifanyia kazi na nahisi nitakibugia BAADAYE kwa juhudi.:-(


Swali:
 • Unafikiri juhudi ni nini na ni lini uliJUHUDIKA na kwa kujuhudika unaweza kuapia HUKUWEZA kufanikisha KULA?SAMAHANI kama KU-mamaye ni TU-si kwa mheshimiwa kama MHESHIMIWA huwa anafikiria KU-dadaye ni NINI!:-/


Nakatiza wazo KINGUNGE na labda wazo hili ni UJINGA ingawa kumbuka ni WAZO TU na sio USENGWILI!:-(

ASANTENI WOTE na ukiwamo WEWE, lakini kama wewe ni MHESHIMIWA kama WEWE halafu umejikuta UMESOMA mpaka sentensi hii ambayo labda ni UJINGA, samahani!:-(


NAACHA!
Swali KIDUCHU:
 • Unahisi au UNAFIKIRI ni HAKI ya MUNGU au YAKO kuonewa HURUMA na wenye HURUMA wale?
Na hivi KU-shangaziye WALAKHI kwako si tusi,....
.... KAMA utaniahidi kufikiria tena kwako TUSI ni NINI?:-(

Samahani BINGWA!
Niko MAWAZONI tu mwenzio!:-( :-( :-(
Ngojea MAXWELL aongelee MAISHA katika MNONONEKO uitwao....-LIFETIME
.....AU tu MAXWELL aendeleee kutuboa kwa kibao...-REUNION..Read more...

Kuhusu MARUDIO ya HAMU!

>> Wednesday, June 17, 2009

Kwa KURUDIA kuwa na HAMU ya KITU si lazima safari hii UTAKIDHI HAMU.

Na huwezi kujilazimisha uwe na HAMU na ni kweli kuna hamu hazijirudii kama tu ile hamu ya KUCHOMWA na MIIBA , kuumwa na SIAFU au ile ya maumivu ya LIMTU ulipendalo kukuacha SOLEMBA na Limtu jingine!:-(Binadamu ni MWEPESI kusahau na kumbuka hilo ukiisahau HAMU,...
....NA ndio maana ALIYEKUWA ANALIA JANA unaweza kukutananaye LEO anacheka ile balaa ingawa ni kweli ana meno kama NGIRI.

Na usidanganyike kwa kuwa labda umeshiba sasa hivi ukafikiri UMETIBU hamu ya KULA hapo baadaye .:-(

Kumbuka,...
.... HAMU ni MALAYA na ukiwa na WALI na MAHARAGE sasa HIVI kunauwezekano unajitengenezea mazingira ya kuwa na HAMU YA UGALI kwa CHUNGA.

Swali:

 • AU?
NI moja ya wazo tu Kingunge na NIMEACHA!


Hebu twende tena Reunion tupate Afrofusion kutoka kwa Granmoun Lele aongelee - Soleye


Au tu Jamie Foxx na Timbaland wabadili hali ya hewa katika -I don't need it

Read more...

Kama kuna FAIDA za KUISHI na KINYONGO!

Kinyongo kama tu KULAANIWA,...
.... Laana haimtesi ALIYELAANIWA na KIMPACHO laana MTU ni KUISHI NA LAANA.:-(

Ni kweli,...
.... KUISHI NA KITU ndio KASHESHE na kukifanya kitu ni rahisi hasa kama hufikirii kuwa itabidi uendelee kuishi UKIJUA ni kweli ULIFANYA KITU naKATIKA KUFANYA kumbuka WENGINE wafanyacho ni KUUA!:-(

Kama unakinyongo na mtu ,...
.... wewe unateseka na KINYONGO na wala sio huyo MTU.

Na kama unakinyongo na MTU,...
..... na unataka USITESEKE na KINYONGO, basi usiishi na KINYONGO.

Swali:

 • AU?
KUMBUKA hili NI wazo tu Kingunge!

Ngojea Barbara Kanam aongelee ya - Teti


Au tupitie tena Cape Verde Talina alete - Pour Te Revoir

Read more...

BINADAMU katika kuusingizia MOYO ya KICHWA!

>> Tuesday, June 16, 2009

Ukweli ni kwamba YA MOYONI yako KICHWANI,...
...ingawa kuna WADAIO kukupenda kwa MOYO WOTE!


Ya kichwani bila aibu HUSINGIZIWA hata ROHO,...
.... na YAAMULIWAYO na KICHWA huhukumiwa hata roho kwa roho kusingiziwa eti ni ROHO MBAYA.


Na WOGA wa MAAMUZI ya KICHWA,...
... kuna adaie kuna wasio na MOYO kwa KISA cha kushindwa kutekeleza yaliyo MUKICHWA.


NDIO!
Kustukia MAUMIVU au hata UTAMU ni kazi ya UBONGO mukichwa na hakuna kitu kiitwacho MOYO UNAUMA.


Na kwa kutumia KICHWA ,...
....YA MOYONI kama vile PENZI na IMANI yanaweza YASIELEWEKE na YASIYOELEWEKA kichwa huyasakizia au kuusingizia MOYO.


NDIO!
Ujinga wa YA MOYONI bado ni UJINGA wa ya KICHWA!


Na daima ni KICHWA kiusingiziao MOYO ya KICHWA!:-(

Na ni kichwa kiamuacho lini moyo uache KUDUNDA, na ukiacha kudunda hakuna TENA ya KICHWA!:-(


Ni wazo tu KINGUNGE na NINEACHA!

Swali:
 • Unafikiri ROHO inaishi wapi ndani yako?
Ngojea IMAGINATION wadai-JUST AN ILLUSION


Au tu nimuachie JAMES BROWN

Read more...

Ufasaha na UMAHIRI wa MTOTO MZURI mwenye SURA MBAYA na LABDA kavaa kama tu alivyoanzishiwa KUVALISHWA chupi nzuri HALAFU SAFI!

>> Monday, June 15, 2009

KATIKA dunia HII yenye WAPENDA SURA NZURI ,...
.... wenye SURA MBAYA wengi hutambuliwa kwa zao JUHUDI za vitu vyenye SURA NZURI.

Swali:

 • Unauhakika ni nani mwenye sura nzuri?
 • Ni kweli unataka mpaka kujua ukweli kuwa ni UKWELI hata kuna KINYEO chenye sura mbaya kwa mtazamaji?

Kwa juhudi unaweza usistukiwe kuwa sehemu zako za siri zina SURA MBAYA kwa kuwa kwa juhudi zako wewe ni TAJIRI na katika utajiri wako baadhi ya MATUNDA YA LA KIJINGA likufanikishalo ULE KINGI , ni lile UFANYALO lisababishalo JUHUDI ZAKO zitambulike kwa HATA WASIO WAJINGA , ...
....na labda likutambulishalo NI JINSI UJUAVYO KUHONGA hasa KWA BILA , ....
......bila kujulikana unahonga kwa wakupao KIKOJOLEO,nyuma ya kikojoleo , chuchu ,NA labda hata MAANDAZI PIA kabla hujapewa KIDUDE maeneo!:-(


Na LABDA ni kweli,....
... INASEMEKANA kuwa ni KWELI kama unatafuta waishio kwa kutegemea SURA ZAO, ...
...JAMII IITAZO NZURI na unataka USITAFUTE, ....
... tembelea shule za waliofeli au tafuta sehemu rahisi zipendelewazo na WASIOFIKIRI au TU pale uhisipo kuna WAJINGA a.k.a WAVIVU wa MHANGAIKO kwa kuwa sura inauzika hata kwa HEDIMASTA.:-(
Swali:
 • AU?

Na kumbuka,...
.... JIHAMI na MTOTO MZURI uaminiye ANAAKILI kwa kuwa kwa kumuangalia huoni kasoro ZAKE ,....
.....na hujui hata UMAHIRI wake wa kutumia NYETI na kinakufikirisha kwanini huoni kasoro ZAKE kwa kuwa labda HUONI KASORO KWA KUWA MJANJA labda HUJUI KASORO ZAKE KWA KUWA anakunya KITANDANI na wewe ni ALEJIKI na MAVI na hata SEBULENI KWAKE HUJAWAHI alikwa!:-(

NDIO!
........INASEMEKANA kirahisi JAMII iwaaminio ni wazuri bado HAO na wao husamehewa hata kama WANAKOJOA KITANDANI!:-(

Na,...
....INASEMEKANA kirahisi JAMII IWAAMINIO NI WAZURI huwapandisha hata CHEO ofisini kama tu KITANDANI , huwaSIKILIZA hata kwa yasioeleweka kama vile yao ya KUGUNA, na pia ni kweli wanaweza kusifiwa kwa USAFI WA CHOO ingawa choo chao bado KINANUKA na ungejua,...
..... labda ni kweli WANAKOSEA hata KUNYA!:-(

NDIO ,..
....ni kweli ukiamini kuna MTU MZURI ,...
....huyo anakuchezea MAZINGAOMBWE na ABRA kaDAbra YAKE labda inakufanya uweze kujikuta umeoa mpaka MTU anukaye UVUNGUNI kwa mnukio ufananao na MAITI YA SAMAKI kwa sana tu ,...
...kisa NI KWAMBATU huwa akikuchekea PUA yako HUZIBA ingawa unajua hata YEYE michezo ya BABA na MAMA yeye ni MTOTO MZURI na bado KATIKA SHUGHULI yeye ni MTOTO!:-(


Na ,...
.....LABDA inahitajika kuamini KUWA kama unaamini una SURA mbaya ni muhimu kwako kucheza mazingaombwe ya JUHUDI kwa kuwa KUWASAHAULISHA WATU yako NI sura MBAYA KWA IMANI,...
..... huhitaji JUHUDI kwa kuonyesha UBINGWA WAKO kwa kitu kingine hata ikiwa ni kwa TAALUMA yako ya KULAMBA PEREMENDE ili kusahaulisha WATU matumizi yako YASIYO MAHIRI katika ya KUSHUGHULIKA na PIPI KIJITI katika PIPI iliyo na LIJITI na yote ni ili UPENDEKE tu na ukweli ni kwamba HUPENDI PEREMENDE.:-(
Swali:
 • Unafikiri mtoto mzuri ukimzoea HUWA unakumbuka kuwa mwanzoni ulidhani uzuri wa MTOTO MZURI wake KWAKO MWANZONI ulikuwa ni SPESHO?


Nakatisha WAZO na kama nimekukwaza SAMAHANI KIBINDA NKOLE, Kadoda au weye Binti Khalufani!

Ngojea Shania Twain aongee katika-That don't IMPRESS ME MUCH


Au turudi tu TANZANIA Dr REMMY amzungumzie - Karola


Read more...

UNAKUMBUKA katika yote uliyowahi KUJIFUNZA moja wapo ni JINSI ya KUVAA CHUPI a.k.a KIFICHA NYETI?

Na ni kweli,...
...... HUTUKANI kama HUKUJIFUNZA tusi NI NINI!:-(

Na,..
...kuna MENGI unayoendelea KUJIFUNZA SASA HIVI ambayo hatuyajui na labda HUYAJUI kwa kuwa hayo si maarufu LEO kwa BINADAMU na yake bin-adamu ya KUJIFUNZA maeneo na jinsi ya kutumia ENEO!:-(


NDIO,...
...huhitaji KUJIFUNZA KUNYA ingawa ni kweli KUNYA huhitaji TAALUMA kama unataka KUNYA VIZURI .

Na....
.... ni kweli kama unahisi unapatia KITU ,...

...LABDA kuna KITU unafananisha nacho ambacho kwako ni MAFANIKIO ndio MAANA kwako hilo ni fanikio na kama hujui,...
....kumbuka hata KWA hilo ULIJIFUNZA!:-(


NA NI KWELI kwa bahati MBAYA,..
...hata UJITAHIDI VIPI,...
.... bado utakufa huku kuna KITU HUJUI!:-(


Samahani NAKATIZA wazo!:-(

Ngojea turudi ANGOLA SAVIMBI aongee nisichoelewa na nisikufiche napenda Kipochugali mpaka nishadeti Wabrazili kadhaa kwa kisa CHA kunogewa tu na WAONGEAVYO Kipochugali.:-(


Na ni kweli sijawahi deti Mpochugali wa Pochugali:-(
SAMAHANI kwa kujielezea kubwa kuliko katika swala la faragha na lisilo na UJUMBE mzuri hata kwa KIFARANGA.:-(

Huyu basi Savimbi adanganye wananchi kidogo kama afanyavyo KIKWETE kama naye hakujifunza kwa NYERERE....


Au tu LEADBELLY atusaidie kubadili hali ya hewa kwa ambacho bado sikielewi ingawa naelewa LUGHA katika...-Goodnight IreneASANTENI wadau WOTE na hasa ambao hamnitengi kama hawa waliopo kwenye picha zangu za JUUUUZZZZZI ya JAANA!:-(


Photobucket


Photobucket


PhotobucketPhotobucket

Photobucket


Photobucket


Photobucket
PhotobucketPhotobucket


Photobucket

Photobucket


Photobucket


Photobucket

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP