Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ETI inasemekana KUBWA ZIMA linaweza KUHARIBIKIA UKUBWANI!:-(

>> Thursday, June 04, 2009

Mambo mengi hayatokei au kuharibika GHAFLA TU kama walalamikaji wanavyofikiri!:-(

Kama unabisha iangalie Tanzania!

Swali:

  • Au?

Labda ni kweli kuna MAKUBWA kubwa zima inabidi lianze kuyaonjea UKUBWANI!

Lakini mengi kubwa zima yalinogeyalo KUYAGIDA ukubwani,.....
..... hamu za kuyaonja hata kwa staili ya NANIHII haikuanza ghafla UKUBWANI.

Ni kweli,...
... wengi huongelea MATOKEO ingawa DALILI zilikuwepo UTOTONI ndio maana wanashangaa hata ya KUBWA JINGA.

Na ni kweli,....
..... UKISHUHUDIA kitu leo mara nyingi misingi ya TOKEO ilikuwepo tu muda mrefu na washangaao TOKEO ni wachelewao KUSTUKIA DALILI ndio maana labda leo kwao LIJAMAA ni kubwa zima bado kuendelea KUCHEZA MDAKO au kupora watoto KUMBIKUMBI kama tu kuwa BOMBA LA MALAYA halafu upatikanaji wake BEI CHEE kwa kushindwa kupandisha bei!



Na kunauwezekano mpaka leo kuna TOTO huliangalii TU vizuri na ndio maana kwa kutoliangalia kwako katika mwenendo wake wakati bado KINDA a.k.a TOTO , baadaye utadhani NI KUBWA ZIMA halafu limeharibika GHAFLA ukubwani!:-(

Swali:
  • Kubwa zima unalodhani limeharibikia UKUBWANI unauhakika unalikumbuka au ulikuwa unalijua UTOTONI?

  • Unauhakika kuna KUBWA LILILOHARIBIKA na sio tu NI TAFSIRI yako ya JAMBO na ya KUHARIBIKA ni NINI inayokuponza kudhania BINADAMU anaweza kuharibika?
Ndio kuna vitu vipo TU !

Labda ndio maana huhitaji kuwafunza dume na jike staili za kutamaniana na labda wenyewe tu hata ukiwaacha pekeyao wakati bado wadogo msituni , WAKIKUA ukirudi unaweza kushangaa walizaa watoto kwa ubunifu wa MAKUBWA UKUBWANI bila MWALIMU.

Lakini kama uliwachunguza wadogo LABDA utastukia tu mwelekeo wa mtu kuweza kupewa MIMBA hapo baadaye labda kwa kustukia hawa wadogo walianza mapema kuonyesha dalili za mtu kuwezapewa ujauzito kwa kuonyesha HATA dalili za kupendana na hiyo ni kabla hawajagundua kwa kupendana kuna wavulianao nguo katika moja ya hatua za penzi.:-(



Nachojaribu kusema ni;
...unauhakika aliyeharibika kwa kuwa ni mkubwa basi maana yake kaharibikia UKUBWANI kwa kuwa umemstukia JUZI wakati MKUBWA?
NAACHA wazo!

Hebu tubadili hali ya hewa kwa kwenda Minesota tukashuhudie WAKUBWA WAKIPIGANA KANISANI!


Au ngojea tu mke wa Rais wa France a.k.a Carla Bruni alainishe ukubwa kwa-- Tout le monde

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP