Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa mara nyingine na ni SIKU NYINGINE!

>> Tuesday, June 30, 2009

MATATIZO ni yale yale,...
.....ingawa SIKU ni NYINGINE.

KWA KUWA ni siku nyingine,...
....matatizo yaleyale hudhaniwa ni mapya ,...

.....kwa kuwa ni SIKU NYINGINE.


Kwa kuwa WEWE si WATU WENGINE,....
.... baadhi ya MATATIZO YALEYALE kwa wengine,...
.... WEWE waweza kudhani ni MAPYA kwa kuwa umeyagundua SIKU NYINGINE.


Na kama unajifunza KUTOKA KWA WENGINE,...
....matatizo YALEYALE ukiyafumbia macho HUJIFUNGUA MTOTO,...
... na siku moja unaweza ukaamka na tatizo JIPYA kweli kwakuwa ni SIKU NYINGINE.


Lakini MATATIZO ndio SIRI ya UFUMBUZI wa TATIZO,...
... na kushughulikia MATATIZO ndio SUKARI YA MAISHA kama ufumbuzi wa TATIZO,...
.... na hata kama ni kweli UTAFUMBUA FUMBO la kiini cha TATIZO siku nyingine.

Na leo ni SIKU NYINGINE,....
... na kama unadhani huna TATIZO basi wewe maisha yako yaliishia jana,...
... na hukufika leo SIKU NYINGINE.



Swali:
  • AU?
NI wazo tu KINGUNGE na NIMEACHA kukuzingua!:-(

Ngojea Scarface na 2PAC wakukumbushe-Smile


AU tu THE POLICE warudishe gurudumu nyuma zaidi katika ...- De Do Do Do De Da Da Da


7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 11:55 am  

muulize mzee wa changamoto juu ya tatizo na tatizo lenyewe

Born 2 Suffer 1:31 pm  

Tunangoja ufafanuzi kutoka kwa mzee wa changamoto.

Anonymous 6:44 pm  

Hivi Mkuu Simon,lile la jumuwata ni tatizo? basi kama nitatizo tumelizoe ndio maana kila siku nyingine tumeona tatizo la kawaida sasa mwishowe sijui nini kitatokea.

Hahaha.... Rasta hapa.

Anonymous 4:46 pm  

SIMON,kwa mtazamo wangu ni heri kukutana na matatizo tofauti tofauti kila kukicha kuliko kukutana na tatizo lilelile kila kukicha.

Kwa mfano tatizo la JUMUWATA nakutana nalo kila kukicha,je hili tatito la jumuwata halina ufumbuzi?nakama halina ufumbuzi kwa nini tusiweke bayana?

Rasta hapa....

chib 2:50 pm  

Tatizo ni tatizo, hata kama litakuja tatizo jingine, pia nalo hilo tatizo ni tatizo. Hakuna mtu anayependa kuwa na tatizo ambalo ni tatizo, ni bora kutafuta ufumbuzi wa tatizo kuliko kukaa na tatizo likaleta tatizo jingine. Upo hapo!! Kama hujaelewa basi ni tatizo juu ya tatizo!

Yasinta Ngonyani 10:41 pm  

Simon Kaaazi kwelikweli. sikiliza hapa Matatizo, Matatizo kila kitu ninachofanya ni tatizo. Hata pumzi ninayotoa ni tatizo. Hata yule/wale ninaye/ninaowapenda ni tatizo.
Maana hata kila kukicha ni tatizo. Ni hayo tu!!!

Simon Kitururu 8:11 am  

@Wote: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP