Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika kuongelea BILA AIBU angalau UWEZEKANO wa kuwa MIMBA ya KUKU ni YAI!

>> Tuesday, June 30, 2009

Tukiachana na swala la KUKU MJAMZITO....
....... baada ya KUKU kufanya TENDO LA NDOA kama BATA,.....

.....tuongelee binadamu kiduchu basi!

Kwa BINADAMU kuna TAMADUNI, MILA na DESTURI zifanyazo tuamini KUWA NI ukweli kuwa swala la UJAUZITO ni la wakubwa,....
..... ndio maana binadamu akiwa mtoto hudanganyika kuwa watoto wananunuliwa duka fulani au kuna ndege anawaleta hata kama anayemsimulia BINADAMU MTOTO HUYO , ana MIMBA.:-(

Na ,...
.....kwa kuwa jamii inadai kuwa MASWALA YA UJAUZITO ni maswala ya faragha kuna ambao wamepata mimba kwa kutojua MASWALA YA mpigwa chini huvimba JUU.

NDIO!
Tamaduni zetu wengi zinatufanya tuepuke kuzungumzia mambo fulani:-(

Na ujuzi wa asilimia kubwa ya vijana siku hizi ,....
......ni wakujifunza wenyewe KUPEKECHA ingawa kuna washangaao kwanini RIJALI kila siku akiingia mtandaoni akilini akiona KIBONYEZO ''search ''hakawii kuandika mbele yake neno ''SEX''.

Ndio!
Asilimia kubwa ya WABONGO niwajuao wamejifunza maswala ya KITENDO CHA KUUJAZA ULIMWENGU wenyewe kwa kuwa ndugu na hausigeli hawakuviongelea kwa kuwa MILA na DESTURI ZIMEWAFUNGA mdomo hata WAZAZI.:-(


Na tatizo kubwa katika hili ni kwamba,....
..... kama huna MUONGOZO itabidi ujishughulishe mwenyewe KUPATIA na kwa bahati mbaya kwa kujifunza bila MUONGOZO waweza kujikuta USHAZOEA KUKOSEA matumizi ya NYETI.


Kumbuka,...
... apataye MIMBA wakati anapata MIMBA kunauwezekano MKUBWA alikuwa anafikiri anapata URODA tu a.k.a MIKASI na sio alikuwa ANAMIMBISHWA.:-(

Kumbuka,...
..... mara nyingi BEBERU LIKIPANDA huwa halifikirii matokeo yake ni kumpa mimba KIMWANA mbuzi.


Na kumbuka ,....
.... mwenye mimba anapendeza kwa kuwa unajua ana mimba LASIVYO ni kweli mwenye mimba huwa ana tumbo KUBWA a.k.a BOMBA LA TUMBO na HUWA anabadilika MWENDO.

Kwa hiyo,...
..... jihadhari kumuuliza MWENYE TUMBO KUBWA asiye na MIMBA maswala ya UJAUZITO kama hutaki kufyonzwa KABLA hujashushiwa bomba la TUSI lenye uzito wa KILO KADHAA lifuatwalo na bomba la KOFI .Na kama wewe mfupi JIHADHARI kwa kuwa labda pia utapewa bomba la konzi lenye KILO TATU na NUSU hivi kwa kukosea wa KUMDADISI.

Na ni kweli,....
..... ukikutana na mwanaume akukumbushaye MWANAMKE mjamzito, basi inasemekana huyo ANAKITAMBI kitu ambacho SI AFYA kama tu toto dogo lenye tumbo kama mimba linaweza kuwa lina KWASHAKOO , UTAPIAMLO ,nk.....
........ kitu ambacho SI AFYA!:-(



Na ni kweli,...
..... MIMBA ni KIBOKO ndio maana UMEZALIWA.:-(

Swali:
  • AU?

DUH!
NALIKATIZA wazo hili kabla ya KUONGELEA kuhusu MIMBA ya kuku bila KUOMBA ruhusa ya KUKU!
Swali:
  • Hivi kweli umesoma mpaka sentensi hii hapa katika SWALA HILI lenye uwezo wa kuwa ni la KIJINGA ?
  • Unafikiri lini katika ukuaji wako ulistukia MIMBA sio KITAMBI na KITAMBI sio MIMBA?
  • Unafikiri kungekuwa na uwezekano binadamu wasingehusudu KUTAGA kama kunguru ili kukwepa kuvaa MATENITE DRESI ingawa kasheshe lingekuwa ni zamu za hausigeli kuyatamia mayayi wakati bingwa YUKO kwenye KICHENI PATI?

Kumbuka ni wazo tu NA NIMELIKATIZA nikiwa nakutakia KILA la KHERI katika LAKO LIBENEKE!


Ngojea Kenny Roggers abadili hali ya hewa kwa kitu- You are so Beautiful



Au tu BONGO MAFFIN watukumbushe- MAKEBA

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Fadhy Mtanga 11:59 am  

Mmh swadaktan...
Raha tele moyoni....
Niwapo humu bulogini...
Wala si utani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 12:05 pm  

sijaelewa kwnini mimba sio kitambi na kitambi sio mimba hata kama kuna kofi na fyonzo

Yasinta Ngonyani 10:51 pm  

Kamala mimba ni mimba kwa vile mwisho wako anatokea binadamu. Na kitambi ni kitambi kwa vile mtu ananenepa tu amejaa mafuta yasiyo na sababu.

Simon Kitururu 8:13 am  

@Papaa Fadhy: Nashukuru sikuzingui!Asante Papaa kwa kutochoka kunitembelea!
@Papaa Kamala: DUH!

@Dada yasinta: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP