Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

TAFADHALI usisome STORI HII ya SIRI za MHESHIMIWA aziongeleazo CHUMBANI na kujifanya kazinunia HADHARANI!:-(

>> Wednesday, June 24, 2009

ANAYEJIHESHIMU ,...
......huaminika kuwa HUWA ndiye asiyoyaongelea MAMBO kama hivyo HADHARANI,....

.....ndio maana kuna wasahauo WAITWAO WAHESHIMIWA wengi ndio wateteao ujinga HADHARANI.


MHESHIMIWA ,....
..... inasemekana HAVAI HIVYO hadharani,....
.... ndio maana ni bingwa zaidi ya WANAMAZINGAOMBWE kwa UTETEZI wa NGUO kwa MANENO hata wakati akiwa anawazia YALIYOUCHI fikirani HADHARANI.


Na ya MHESHIMIWA yako FARAGHANI,....
.... ndio maana WASIOFIKIRI HUKOSEA wakumuheshimu HADHARANNI.


UHESHIMIWA ni kama MADAWA ya KULEVYA,...
.... aliyenaswa na KUHESHIMIWA anajikuta anaung'ang'ania hata kwa kuomba kura za vyeo asivyovistahili HADHARANI.


Na kama unataka kulogwa na MHESHIMIWA,...
....baadaye kidogo baada ya KUWINI chuki za MHESHIMIWA,.....
... toa siri zake za CHUMBANI hadharani.


NAACHA na ni wazo tu MKULU!
Kumbuka kama umenisoma mpaka sentensi hii wewe si MTIIFU kwa kuwa nilikuomba kwenye KICHWA cha habari usisome STORI HII!:-)

Swali:
  • AU?

Ngojea basi tuliwaziwe na The VERVE katika - Bittersweet Symphony


Au ngojea tu Eminem, Jay-Z, Lil Wayne waharibu wimbo huo huo katika -Bittersweet Symphony Remix

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Born 2 Suffer 4:18 pm  

Remix bomba mkuu nipo nipo tu mkuu busy kidogo siku 2,3 hivi, Thnx kwa kuniulizia usikonde nitakuja na mpya zingine.

Simon Kitururu 5:55 pm  

@Mzee wa Taratibu:Si utani!Tuko Pamoja Mkuu!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP