Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kwa JUUJUU!

>> Thursday, June 11, 2009

Kwa JUUJUU bado sio NDANI na haijaingia.:-(


Kwa JUUJUU,...
.... amuonaye anayecheka hudhania achekaye moyoni anafuraha!

Kwa JUU JUU ,....
.....aliaye anaweza dhaniwa halii kwa furaha!


Kwa JUUJUU ni ngozi ,...
......na kuna BINADAMU weupe na weusi wasahauo kuwa wote WAFANANA kwa ndani!:-(


Kwa JUUJUU ,....
.....akaaye kimya wanadhani KASAHAU!

Kwa JUUJUU,....
..... unaweza kutomstukia atakaye hata kukupiga JUJU!

Kama unajua JUU JUU ,...
.....weye hujui undani wa KITU au MTU na ujuacho ni kwa JUUJUU na labda ni kweli udhaniaye mlevi hajalewa!


Na,...
... kwa JUUJUU labda nilichoandika ni UJINGA!:-(

----------------------------------------------------_______________----------------



NI wazo tu MKUU na NIMEACHA!

Swali:
  • Unadhani kuna umjuaye kiundani?
  • Unadhani ni mara ngapi unajaji kitu bilakukijua kiundani?
Nakutakia siku KIBONGE na mafanikio JEMADARI!

Namuacha Mr FOX adai-Yo No Tengo La Voz


Au tu YONDO SISTER alete-Mbuta Mutu

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:14 am  

Juu juu! kazi kwelikweli:-(

PASSION4FASHION.TZ 12:20 pm  

Mmmmh!Kwa juu juu kaka Simon unavijimambo wewe??

Simon Kitururu 4:57 pm  

@Yasinta na Passion4Fashion: :-)

chib 2:41 am  

Kazi kweli kweli

Mzee wa Changamoto 5:15 am  

Kwa juujuu tu unaweza kudhani ni ujinga
kwa juujuu usigundue kuwa yawezekana humuoni kwa kuwa umefumba macho
kwa juujuu unaweza kuamini kushoto yako ndio yake wakati mnaangaliana
kwa juujuu yawezekana hujaelewa kuwa uelewa wako ni juu juu
kwa juujuu niseme nasubiri kwa chinichini.
Bless I

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:49 am  

......na kuna BINADAMU weupe na weusi wasahauo kuwa wote WAFANANA kwa ndani!:-(

Simon Kitururu 2:29 am  

@Chib, Mubelwa, Kamala: ....:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP