Tuesday, June 16, 2009

BINADAMU katika kuusingizia MOYO ya KICHWA!

Ukweli ni kwamba YA MOYONI yako KICHWANI,...
...ingawa kuna WADAIO kukupenda kwa MOYO WOTE!


Ya kichwani bila aibu HUSINGIZIWA hata ROHO,...
.... na YAAMULIWAYO na KICHWA huhukumiwa hata roho kwa roho kusingiziwa eti ni ROHO MBAYA.


Na WOGA wa MAAMUZI ya KICHWA,...
... kuna adaie kuna wasio na MOYO kwa KISA cha kushindwa kutekeleza yaliyo MUKICHWA.


NDIO!
Kustukia MAUMIVU au hata UTAMU ni kazi ya UBONGO mukichwa na hakuna kitu kiitwacho MOYO UNAUMA.


Na kwa kutumia KICHWA ,...
....YA MOYONI kama vile PENZI na IMANI yanaweza YASIELEWEKE na YASIYOELEWEKA kichwa huyasakizia au kuusingizia MOYO.


NDIO!
Ujinga wa YA MOYONI bado ni UJINGA wa ya KICHWA!


Na daima ni KICHWA kiusingiziao MOYO ya KICHWA!:-(

Na ni kichwa kiamuacho lini moyo uache KUDUNDA, na ukiacha kudunda hakuna TENA ya KICHWA!:-(


Ni wazo tu KINGUNGE na NINEACHA!

Swali:
  • Unafikiri ROHO inaishi wapi ndani yako?
Ngojea IMAGINATION wadai-JUST AN ILLUSION


Au tu nimuachie JAMES BROWN

3 kommenttia:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli usemayo. Hongera kwa kuwaza!!!!

chib said...

Mimi nafikiri roho haipo, ni imagination tu baada ya watu kushindwa kung'amua uhalisi wa utashi wa mtu unatokea wapi

SIMON KITURURU said...

@Yasinta : LABDA!:-(
@Chib: Kwa sentensi moja tu umefanikiwa kuzima hoja na imani za watu kibao!:-)