Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Busara za MWENDO wa kwendea CHOONI kabla HUJABANWA vizuri na HAJA NJONJOLINJO!

>> Wednesday, June 10, 2009

Ukijiandaa vizuri,...
.... hata kwenda chooni unaweza kutembea kwa maringo!

Tatizo la kusubiri mpaka ubanwe unaweza ukajikuta mwisho wa mwezi pesa za kodi ya nyumba ulisahau kuzitunza au tu unastukia jinsi ulivyokuwa mahiri wa kumkwepa anaye kudai!:-(

Na wakati unaenda chooni wakati hujabanwa vizuri,....
... una lakshari ya kuwaza kitu kingine wakati unausogelea mlango wa maliwato na uliwazalo likawa halina uhusiano na HAJA namba moja au ile NAMBA MBILI!

Swali:

  • Kwani nani anabisha wajiandaao vizuri mara nyingi ndio watuliao kwenye mtihani?
  • Unakumbuka kukuru -kakara usiku wa mtihani ghafla ukistukia labda hujajiandaa vizuri?
  • Unakumbuka wakati unaenda chooni huku umebanwa huwa HUPEI-ATENSHENI unavyotembea na kukanyaga mavi ya mbwa wakati uko katika safari hiyo ya chooni wakati umebanwa wala hakukufanyi upumzike ILI kusafisha kiatu?
Lakini tusisahau kuwa,...
.... ni muhimu pia kupitia mwendo wa kwenda chooni huku umebanwa ili uelewe starehe ya kutobanwa, KWA KUWA unaweza ukastukia ukibanwa tafakuri zako zinabobea kwenye haja mpaka hata HARUFU ya kinyesi cha aliyekutangulia chooni HUWA hukisikii!

Tatizo tu la kuwa choooni kwa kuwa umebanwa na unahangaikia haja bila kustukia harufu ikuzungukayo,...
..... ndio KISA utashangaa JAMAA limeingia OFISINI halifikirii UFISADI na likitoka LINANUKA UFISADI.

Swali:
  • Kwani unafikiri wapokea rushwa wengi waliingia ofisini wakiwa na nia ya kupokea rushwa?

Nachojaribu kusema,...
..... ukiingia chooni na kibano , unaweza ukatoka chooni unanuka harufu ya MAVI bila kujua!

Na kwa maana nyingine,...
...kama hujajiandaa na ukafaulu basi hiyo ni bahati tu na unaweza ukawa unaitwa Profesa wa NANIHII kwa kuwa umefaulu lakini ukweli ukawa ni Profesa waNANIHII asiyeJIAMINI!

Swali:
  • AU?

  • SI binadamu anaweza kupanga katika siku ni saa ngapi anaenda haja kubwa?
Kumbuka tu,...
.... ukijiandaa utajua kuwa hata kinyesi chako chooni hukunukia weye kwa dakika kadhaa tu wakati unaanza kukishughulikia ndio maana baada ya dakika kadhaa unaweza mpaka kuanza kusoma gazeti huko huko chooni kwa kuwa umeshazoea harufu ya kinyesi chako na atakaye ingia chooni baada yako ndio atabana pua.
Swali:
  • Unauhakika naongelea nini?

NIMEACHA!
Ngojea Ziggy Marley alete- Goodtime Accoustic



Au to Sting na Ziggy Marley walete- One World

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP