Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKIWA na uhakika wa KULA njaa haiumi HARAKA!Lakini!:-(

>> Thursday, June 25, 2009

Ukiwa na pesa za GARI,...
... mwenye gari hakuumizi KICHWA.


Ukiwa huna uhakika wa gari na unauhakika wa MKWECHE,....
....mwenye gari , ingawa ni mpaka uwe unataka gari ,ANATISHA!


Ukiwa na uhakika UTAFIKA,...
.... waliotangulia SI WAJANJA.


Ukiwa na wasiwasi na uwezo wako wa KUFIKA,....
..... unaweza mpaka kuanza kufikiri UTAFIA NJIANI na waliotangulia kwako WANATISHA.

Ukiwa na mke MZURI,....
....wenye wake hawakutishi kwa kuwa unaujua MKENGE waliouvaa.

Ukiwa na mke MBAYA,...
... wake wa wenzio wanavutia MNO kwa kukosa KASORO na jicho la ubongo WAKO litabunia MPAKA umbo lao hata la kabla hawajavaa.

Swali:

  • Hivi kweli kuna mke mbaya duniani?
Ukiwa na MUME MZURI au MBAYA mie sijui nini kinatokea na SAMAHANI kwa KUKOSA UTAALAMU wa HILO!

Ndio,...
.....Ukiwa na uhakika leo hata kuhusu ya kesho,....
... walionayo leo HAWAKUTISHI.

Tatizo ni;
...Ukiwa na uhakika leo, HUO NI UHAKIKA WA LEO,....
.....na labda kesho utagundua;
  • Pesa zako zikutiazo kiburi leo hazitoshi kesho kununulia hata mkweche.
  • Uhakika uliokuwanao leo kesho haupo, na ghafla huna uhakika wa hata kufika kesho kutwa ya KESHO.
  • Kakitu ambako katafanya MKE wako mzuri leo, USTUKIE kumbe tokea ZILIPENDWA alikuwa mbaya.


NA LABDA,....
....
Kibinadamu, ALAYE SASA HIVI ndiye mwenye uhakika ANAKULA,..
... na siye wengine HATUJAPANIKI TU kwakuwa TUNA MATUMAINI TU kuwa baadaye TUTAKULA.

Uzuri ni kwamba ,...
...BINADAMU huendeshwa na TUMAINI,......

.... ndio sababu ukiwa na kibano LEO unadhani labda utafaidi mbinguni WAKATI labda KIBANO CHAKO unachodhani ni KIBANO LEO ni KILE chakutamani unywe GONGO NA WASHIKAJI halafu usinyimwe TENDO LA NDOA a.k.a URODA a.k.a MIKASI a.k.a MATUSI a.k.a UASHERATI hapo baadaye CHOBISI , ingawa LABDA mambo yote HAYO umeshafundishwa na DINI YAKO kuwa MBINGUNI hayapo, NA kule mambo yote ni JUISI kwa MAZABIBU halafu KUIMBA kwa SANA TU na MALAIKA , halafu kwa bahati mbaya hakuna KUCHOKA.:-(

DUH samahani kama nakukwaza kwa kuwa unadhani nakufuru!:-(


LAKINI,...
....UBINADAMU ni NISHAI KWELI kwa kuwa kama wewe ni BINADAMU na SIO JINI, labda KWAKO hakuna lenye uhakika!

NAACHA wazo na KUMBUKA ni WAZO TU na nakutakia kila la kheri katika kukuza lako TUMAINI.
Damn , I am depressed now.(NA samahani kwa kuingizia ung'eng'e KIDUCHU!:-()

PEACE!

Tupitie Kenya kidogo Les Wanyika wadai - Dunia Kigeugeu



Au tubaki tu Kenya Salim Junior adai-Ni sorry Muno..

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

EDWIN NDAKI (EDO) 2:49 pm  

mshahiki meya kila nikipita naona umejipumzisha chelsea..aaa

siku njema jmosi nakuja

Fadhy Mtanga 3:06 pm  

Mtakatifu Simon, hata ukiwa na mke mbaya una uhakika kukipata kile kile akipatacho mwenye mke mzuri tena wewe ukiwa na presha kidogo tu.

Simon Kitururu 3:16 pm  

@Edo Ndaki: Karibu!

@Papaa Fadhy: Labda kuna ukweli unachosema!:-(

malkiory 8:10 pm  

Ndugu Kitururu,

Uzuri nadhani ni neno subjective kama wasemavyo waingereza. Aliye mzuri kwangu si lazima awe mzuri kwako au kwa mwingine, lakini pia sipingani na waswahili walionene kuwa uzuri wa mke si sura bali ni tabia.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP