Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Historia ya MAJINA ya SIKU ZA WIKI na uhusiano wake na SHENZI!

>> Sunday, June 14, 2009

Ukifuatilia majina ya siku kwa Kiingereza ,Kiroma au Kispanish hukawii kustukia uhusiano wake na majina ya MIUNGU ya wahusika!

Na ukifuatilia majina haya kwa Kiswahili hukawii kujikuta shughuli zako zinachelewa kuanzwa au zinaanzia siku ya TATU a.k.a JUMATATU halafu unashangaa kwanini umezidiwa ujanja na waliokutangulia siku MBILI.



Swali:

  • Unafikiri ni kwa nini siku ya PILI a.k.a JUMAPILI ndio iwe ya mapumziko kwa WASWAHILI waongeao Kiswahili?


Ndio!

Kama majina ya siku na shughuli zioanishwazo na majina ya siku hazikuchanganyi basi labda hujawahi kujiuliza aliyetafsi majina haya kwa kiswahili kuwa labda hajachangia WASWAHILI kuchelewa kufanikiwa.

Swali:
  • Kwani wewe kama mswahili hujawahi kujiuliza kwanini shughuli za Mtanzania zinatarajiwa kuanzwa JUMATATU na sio JUMAMOSI na siku ya pili a.k.a JUMAPILI Mtanzania hata kama ni MUISLAMU hutarajiwa kupumzika?
OK,..
... na ni kweli SHENZI ni KIJERUMANI ukifuatilia historia!


Na,...
.....LABDA siku uanzayo shughuli si MUHIMU kama ni kweli unaanza shughuli!

Swali:
  • LAKINI Unauhakika umeshaanza shughuli?
  • Ushawahi kufuatilia historia ya kwa nini JUMATATU haiitwi IJUMAA kwa kiswahili?

NAACHA wazo na JUMAPILI NJEMA Kingunge!

Ngojea Fu-Schnickens wakumbushie- WHATS UP DOC can we ROCK

Au tu Barry White alainishe kwa kukiri - Can't get enough of Ur love Babe

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 7:29 pm  

Mmmmh:-(

Simon Kitururu 1:55 am  

@Dada Yasinta: Mhh HUUH!:-(

chib 2:15 pm  

Mimi hapa ofisini nilipanga kuanza zamu za kawaida siku ya ijumaa, watu walishangaa, lakini sasa wamezoea, wa marekani wanasema thanks God it is Friday, sie tunasema Oh my God, it is Friday!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP