Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MTOTO MZURI unayehisi ananoga kama TUSI , mkileana MIGOMBANI kama huna CHUMBA!

>> Saturday, June 13, 2009

Katika kuendelea kuongelea yasiyoeleweka ,...
.. moja ya lisiloeleweka ni KULEA ndio maana kila MTU analijua TOTO tukutu mtaani na hilo ni kama hujabarikiwa kuwanalo NYUMBANI.

Na ni kweli,...
.... kingine kisichoeleweka kwa BINADAMU ni TUSI na ndio maana unaweza kumtukana mtu akafikiri UNAMSIFIA.:-(

Na chumba inawezekana hakipatikani pekee ndani ya jengo ndio maana katika neno CHUMBA ukiongezea ''M'' kuna watakaoelewa uongeleacho ni limtu lijulikanalo kwa jina '' MCHUMBA''.

Swali:

  • Hivi Migombani ni wapi, na mtoto mdogo haleleweki migombani?
  • Unafikiri ni binadamu wangapi wanajua MGOMBA ni nini?
Tukiachana na hilo.....

Kuna waongeleao na kuna WAFANYAO inayo-ONGELEWA na ni kweli IKILAZIMIKA waongelewao wanaweza KUFANYA hata matusi na ifanywayo kama mawazo yako yamepinda , KIDUDE ni MATUSI.

Na wafanyao , ...
....hata kama wanajua SALA inahitaji kupigiwa magoti wanajua kuwa hata kwa kubinuka nahuna UJANJA unaweza kutubu ndani ya SARAKASI.:-(



Tatizo ni,...
...HATA mahiri wa hata wa shughuli au UMATI udhaniao ndiye AFANYAYE,....
... afanyacho ni kweli kwa ukweli KINAWEZA kisimfaulishe hata SHULE ya vidudu kama wewe ndio MKAGUA MTIHANI kwakuwa ukweli ni kwamba anakiongelea zaidi ya KUKIFANYA!:-(

Ndio!
Kuna waongeleao na ukiwapa mtihani utajua kuwa hawajui kuisubiria BAGIA, kuigeuzageuza iive, kuipakua kwenye sinia,..... hata kabla ya kuila HAWAKUSTUKIA STAILI YA kuionja!:-(

Ndio!
Kuna waongeleao ya SEBULENI hata KIJIWENI kabla hawajawahi KUCHUNGULIA sebule, VARANDA au DIRISHA kama sio TUNDU lililo karibu ya JICHO kwa kuwa walikuwa MUDA WOTE wanawazia kilicho UVUNGUNI.


NA ndio ni kweli ,...
....MARA nyingi si kweli mtoto anaanzia kutambaa chumbani, na labda mbele ya wageni sebuleni ndio aliaanza kutambaa na kusimama.

Ndio !
Kama umechoka,...
...... MIGOMBANI kama tu CHOONI ni chumba cha kulala au kuleana!
Swali:
  • AU?
  • Nimefanikiwa kukuzingua kwa niandikacho ambacho labda HAKIELEWEKI ingawa umenisoma mpaka sentensi hii?


NIMEACHA wazo na NINAACHA kukuzingua!:-(
KUMBUKA HUHITAJI KUNIELEWA naongea nini hapa KINGUNGE!
Nawaza tu hapa kijiweni BINGWA na saa nyingine wazo hupinda!
:-(



Swali
  • AU?

Ngojea SEAL abadilishe hali ya hewa kwa wa heshimiwa..akisema - This COULD be HEAVEN




Au tu BOB MARLEY aongelee dunia inavyochanganya katika- MIX UP MIX UP..

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 1:48 pm  

Mmmmh kazi kwelikweli!!!

Simon Kitururu 11:03 am  

@Yasinta: Si utani!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP