Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKISEMA huu ni UTAMADUNI WETU WAAFRIKA, unamaanisha NINI?

>> Wednesday, June 10, 2009

AFRIKA bado sio moja ,....
.....ingawa unaweza kunibishia!
Afrika labda haitaweza kuwa moja ,...
....ingawa unaweza kuendelea KUNIBISHIA!
AFRIKA sio moja LABDA na HILI NDILO MOJA ya sababu za WAAFRIKA kuwa wakali katika FANI YA KUBWENGANA WAO kwa WAO a.k.a VITA VYA WENYEWE KWA WENYEWE.

Na labda HAKUNA kitu kiwezacho kuitwa ''WENYEWE kwa WENYEWE'' wakati hata ''WEWE unaamini kuwa wewe sio ''MIMI''.
Swali:

  • Kwani wanaoongelea ''SISI WAAFRIKA'' kwa neno''SISI'' huwa wanamaanisha sisi ''WAHANZABE au WANGONI'', na sio sisi ''WAMISRI na WAXHOSA''?
  • Unakumbuka katika matumizi ya neno ''SISI'' hata katika kudai sisi WATANZANIA tulimpigia MKAPA kura awe Rais, ina maana unawasingizia watu lukuki na kuwaingiza katika swala la kura za Rais Mkapa wakati mpaka leo wanaamini Rais wao alikuwa ni Lyatonga MREMA?

Tukumbuke tu kuwa neno ''SISI'' ni neno KIRAHISISHI na wengi watumiao neno ''SISI '' humaanisha -''MIMI''.

Nachomaanisha ,...
... kwa wacheza MDUNDIKO Tanzania , huwa wakizungumzia Utamaduni wa Tanzania huunganishia mdundiko pia, wakati kwa Wamasai mambo yote ni KURUKA na Sindimba kwao haipandi kama tu MDUNDIKO usivyo kuwa wao Utamaduni!:-(

Swali:
  • Au?

Au nijaribu kusema tena,...
Kumbuka ndani ya TANZANIA tu na UAFRIKA WAKE,
  • Kuna wenye mila na desturi /tamaduni za kulia MSIBANI na wale wachezao disko MSIBANI.i.e Ushahudhuria msiba wa Kijaluo au ule wa Kimasai?
  • Kuna walao Mbwa na watoshekao na Panya.
  • Kuna watahirio wanaume na kuna watoshekao na mpaka kumtahiri KIDUDE mwanamke.
  • Kuna wenye utamaduni wakucheza ngoma kwa kutikisa tako huku chuchu nje na waimbao tu na kuruka bila kujali matumizi ya chupi.
Nachomaanisha ni,...
... SISI wa AFRIKA tupo wenye tabia za KIARABU na TUPO PIA tufuatao tabia za Kizungu za kuweka majaji watusaidie kuamua ni MISS gani anatembea vizuri nusu uchi au kwa chupi ya kuogelea yenye kuonyesha kidogo kiburungutu cha nywele za nyeti chini kidogo ya kitovu ili ashinde U-MISS KIBAHA!


Na ni kweli ,....
..... BISHA usibishe UKIZUNGUMZIA sisi WAAFRIKA, usisahau Wamoroko wanadai ni Waarabu na Dr Leakey wa Kenya anadai ni Muafrika!

Sasa swali:
  • Ukisema HUU NI UTAMADUNI WETU WAAFRIKA unamaanisha nini?
Ni wazo tu KINGUNGE na labda wazo lako ni sahihi kuwa ni KWELI Afrika ni moja !
NIMEACHA!

ngojea turudi South Africa ARTHUR MAFOKATE atukumbushe -Oyi, Oyi

Au tuendelee kubaki South Afrika watu fulani wapewe soseji katika-VOROSO

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP