Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kuhusu JITIHADA za KUACHANA na MAWAZO YALIYOPINDA na YASHUKIWAYO kuwa yana KASORO KIDUUUUCHU!

>> Friday, June 05, 2009

Kama weye ni mdadisi basi kuna mengi unajiuliza na kuwaza ila kwa sababu zako kuna MENGINE unafanya yawe kwetu SIRI!


Na ,...
......huwezi kuchagua uwaze nini!:-(

Na,...
....
huwezi kujikataza kurudia kuliwaza jambo kwa kuwa ulishaliwaza juzi!

Na,....
...
haki yanani TENA ungejua kila akuangaliaye unamkuna kivipi KIMAWAZO, kuna uwachekeao UNGEWANUNIA na uwaheshimuo ungewadharau!

Na,..
...kwa bahati mbaya kila mwisho wa siku ni maelfu ya mawazo ambayo huwa unayasahau ingawa kuna uwezekano kuna wazo moja la kijinga unaweza ukalikumbuka hata mwaka kesho.

Kumbuka tu kuwa,....

.... kila MWEREVU au MWENYEBUSARA umjuaye ,....
.... HAMALIZI SIKU bila mawazo kadhaa kumpitia kichwani ambayo ni ya KIJINGA.
Swali:
  • AU?
  • Au unafikiri MANDELA,OBAMA, Liyatonga Mrema na PAPA BANEDICTO wao ni tofauti ?
Nachojaribu kusema ni,....
..... kama wewe ni muwazaji, KILA SIKU kuna WAZO LAKO ambalo labda ni SIRI na ni kweli LABDA kwa wengine LIMEPINDA na lina kasoro KIDUUUCHU!:-(

Endelea kuwaza lakini ,....
...... ingawa sio lazima utuambie kila siku au kusema ovyo kama Mtakatifu Simon Kitururu kama lile wazo lako LA labda kila ukimuona mtu kavaa kanzu moja ya wazo likupitialo MUKICHWA ni kwamba labda hajavaa chupi.

NI HILO tu KWA leo!


Asanteni kwa wote wanaoendelea KUNITEMBELEA na KUSOMA MAWAZO yangu YALIYOPINDA katika huu mtiririko naouita UjingaBUSARA.

Samahani KWA AMBAO nawakwaza kwa kuandika mawazo mawili matatu mara kadhaa ambayo kwao yana KASORO KIDUUUCHU na KUWAKWAZA!:-(

Ijumaa na WIKIenDI njEMA / AMANI KUBWA KULIKO iwe nanyi MILELE AMINA!
Naanza KIVYANGU hivyo , PEACE!


Unaweza tulia Billy Ocean aongee.....


Au tu Billy Ocean azungumzie-Suddenly

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 10:16 am  

Mmh! hapa ipo kazi, na itakuwa kazi sana kufanya jitihada kuachana na unachowaza:-(

Fadhy Mtanga 2:22 pm  

Nimependa pale pa kuwanunia uwachekeao na kuwadharau uwaheshimuo.

Fadhy Mtanga 2:23 pm  
This comment has been removed by the author.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP