Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama kuna JINSI ya KUIZOELESHA jamii kuwa UMEMUACHA MKE WAKO AMBAYE BADO unaishinaye na unamendea HAUSIGELI!

>> Wednesday, June 10, 2009

Katika jamii inasemekana HAUSIGELI ni msaidizi wa nyumbani kama vile mke hasaidii nyumbani!

Na labda kuna mke anaogopa jamii itamfikiriaje akimuacha mume na kumchumbia HAUSIBOI asaidiaye nyumbani na ya UNYUMBA kuliko LIMUME vivu!:-(

Na jamii ilivyo KIBOKO,..
... ikiuzoea UNYANYASAJI huwa ina mchezo wa KUUKALIA KIMYA!:-(

Na jamii ikikutambua kama wewe ni HAUSIBOI au HAUSIGELI inamchezo wa kukusamehe hata kama hujui kuandika na kwa jicho la jamii weye shule hustahili ukijumlisha na bado ukinyanyasika kwa unavyonyanyaswa jamii ni KIPOFU!:-(


Na unaweza kubisha,...
... lakini MKE ateswaye na MUME au Mume ateswaye na MKE hu- hurumiwa zaidi kwa teso hilo hilo ambalo ukiitwa Hausiboi au Hausigeli linafumbiwa macho.

Swali:

  • Hivi Hausigeli hawezi kuwa Mke wa Mtu au Hausiboi hawezi kuwa Mme wa mtu?
  • Hivi Hausiboi hawezi akawa ni msenge wa baba wa nyumba na Hausigeli ni msagaji wa mama wa nyumba?[samahani kwa wazo la faragha!:-(]

Ndio ,...
... inasemekana kuna WAPENZI wapendezao zaidi GIZANI au kabla WAGENI HAWAJAJA ,lakini mpenzi ni mpenzi ikiwa mpenzi wako NI MTU na si mbwa au kuku mrembo.NA kama unaficha ufanyacho ni UNAFIKI!

Jinsi jamii inavyojali statasi za watu unaweza kukuta Limwanamke lenye uwezo wa kuishi na Hausiboi limpendalo linanyanyasika kwa kung'ang'ania Limme lisilompenda wakati limme lake linashindwa hata kufikiria kazi kazini kwa kumuwaza Hausigeli mpendwa na jinsi litakavyo jaribu kumchungulia upaja jioni akipika, HAUSIGELi ambaye linahofia likionyesha pendo jamii itakuja juu halafu litadharauliwa.

Ndio!
Jamii ni kichaa na usipoangalia utaishi kama MNAFIKI kwa kuwa jamii kuna mambo HATA ya kawaida kama KUJIFIA kwa MTU a.k.a KUPENDA, huyachukulia kama ni vitendo vya aibu kama jamii ikidhani umekosea kulilenga Limtu BOMBA!:-(

Na tunasikia kuna aliyemuacha MME wake akafuata MDUNDIKO , na inashangaza kwa watu wengi waliosikia msemo huo kutoendelea kufikiria kwani huko kwenye mdundiko kuna akinanani wanogeshao MDUNDIKO!:-(

Swali:
  • Kwani unafikiri jamii itakumbuka kwa muda gani uliacha mke wako ukafuata Hausigeli?



NIMEACHA na kumbuka tu ni moja ya wazo tu MKULU!
PS :
-Mimi Simon sina Hausigeli bado na natafuta kimwana cha kuchukua chotechote na kama wewe ni hausigeli, bomba TU nistue tuangalie ule mpango VIPI!

Hebu turudi Rwanda tukasikilize wimbo wa mapenzi. Tupate Somi-Ingele


Au turudi Tanzania kwa Saida Karoli adai-Nkaba Ningya




ASANTENI wadau wote mkiwemo baadhi ambao nilikutananao juzi ya jana kama muonekanavyo katika picha zangu za juzi ya jana!


Photobucket


Photobucket

Photobucket



Photobucket







Photobucket



Photobucket



Photobucket







Photobucket



Photobucket


Photobucket




Photobucket


Photobucket



Photobucket

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:12 am  

picha nzuri.

Simon Kitururu 4:57 pm  

@Yasinta: Asante!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP