Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika ULIMWENGU huu wa leo wa CHUNA BUZI , sijui bado BINTI Khalufani kwa KUNEMA hawezekani?

>> Tuesday, June 23, 2009

Siku hizi inasemekana,...
.... hata kama Binti Khalufani hawezekani kwa kunema, WANAUME hawawezi kustukia a.k.a KUJUA.

Lakini labda hata hapo zamani za miaka fulani iliyopita,..
... ujuzi wa Binti Khalufani au tu Binti Josef ulikuwa unapimwa kwa utiifu hata kama ni utiifu kwa mambo ya ajabu katika jamii ili mradi jamii inayaona ni DILI kama ya kukubali kutahiriwa KIDUDE na huko huko atahiriwako KUFUNZWA kuamini Mwanaume tu ndio USAHIHI WAKE ni SAHIHI.

Swali:

  • AU?
Ngojea nianze stori hii upya.......

Hadithi !Hadithi!

Nasikia enzi za ZILIPENDWA , ....
....VIMWANA walikuwa wanafunzwa kutii waume zao !:-)

Na nasikia pia ,...
....ilikuwa kama Mke wako akikushinda kwa HOJA kama tu aendeleavyo kukushinda hoja sasa hivi,.....
..... ilikuwa RUKSA kwa KIDUME kumchapa makofi halafu kabla hajamalizia kulia ilikuwa DILI kumshughulikia kunako apate MIMBA ili achunge adabu zake!
DUH !Kudadeki Walakhi!:-(


Kwa kifupi ,...
.....WANAWAKE na WANAUME enzi hizo ukitazama na kufikiria kwa jicho la kileo unaweza kugundua walikuwa hawajuani ila mmoja alikuwa anajitoa mhanga ili mwingine AFAIDI.

Swali kiduchu:
  • Hivi ni wewe ujitoaye muhanga mwenzio afaidi LEO HII au ni yeye ajinyimaye UMIMI ili wewe ufaidi halafu mahusiano YENU bado hayanogi?

Kwa bahati mbaya,...
... Bado naamini leo hii bado siye WANAUME tulio wengi hatulelewi kumuelewa au hata kumjua MWANAMKE. Halafu juu ya hilo, SI RUKSA KUMBWENGA Mwanamke wako hata pale katika klabu ya GONGO au Ulanzi kama tu pale kwa Bibi Kisebengo wauzapo DENGELUA siku hizi.

Kwa bahati mbaya,...
....naamini leo hii hata WANAWAKE walio wengi hawawaelewi WANAUME wanataka nini na kama unabisha WASIKILIZE waongeayo.:-(

Ukitaka kustukia kuwa hali si nzuri,....
  • Cheki jinsi gani Pochi lako likuzungumziavyo kuliko Roho yako katika maadili ya leo.
  • Sikiliza watu hata uhisio ni wenye busara wakizungumzia siri ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume hasa wakati unajua siri hizohizo wangapi zimewaharibia ndoa au kupoza penzi hata kama bado kidude wanapata.:-(
Swali:
  • Umestukia mpaka wafuata dini wamsukumiavyo Mwenyezi Mungu matatizo yao ya ndoa ambayo mengi yao yangetibika kwa wao kuongea tu a.k.a kuwasiliana/kusikilizana?
  • Unataka kusema hujawahi kusikia, hasa kama wewe ni MKRISTO, wakwepao kuongea moja kwa moja MPENZI na mpenzi kwa madai YA kupitia kwa Yesu na Biblia kitu ambacho huwatisha kuachana na kuendelea kuishi pamoja bila furaha kwa jina la Yesu?


Unaweza kunibishia lakini na LABDA miye siwezi kukubishia mwenzio KWA KUWA mwenzio hapa nawaza tu MKUU!:-(

Ndio ,..
....labda kati ya Mwanamme na MWANAMKE ukunaji wa kipele unaumuhimu wake ila labda ni muhimu kwanza kustukia uwepo wa KIPELE maeneo na kama ni busara kukibinya nasio kukikuna.

Na unaweza kubisha!

  • Leo hii tunavyoongea hapa bado WANAWAKE na mambo yao pamoja na KIDUDE chao yanaenda kivyao KAMA tu WANAUME na mambo yao ikiwa pamoja na UUME wao wanaenda kivyao.

Na asilimia kubwa ya wapenzi wenye tatizo la MAHUSIANO leo HII ukiwaweka vyumba tofauti na kuwauliza nini ni tatizo usishangae ukisikia hawana jibu linalofanana kama kwa mfano utakuta:
  • Mume adai tatizo hana pesa za kutosha, mwanamke akadai pesa si tatizo ila HAKUMBATIWI vya kutosha NA ndio tatizo!
  • Mwanamume akadai hapewi kidude vya kutosha , wakati MWANAMKE akadai KIDUME nyumbani haonekani na kidude hana muda nacho na katika KUGIDA anakila kwa uchovu ingawa daima NAMWANDALIA na manukato nanyunyizia.

  • Mwanamke akadai hasikilizwi wakati mwanamume akidai Mwanamke mashoga wamezidi na KIMWANA hapatikani ukitaka angalau KUMNG'ATA sikio.
  • Mwanamume akadai anatamani NA anafurahia KIMWANA akimfyonza, wakati MWANAMKE akadai alivyofunzwa kumfyonza mtu ni matusi na Kidume AMKOME BABU WEE nyooooooo!.:-(



Swali:
  • Unafikiri lakini Mwanamume gani siku hizi anauhakika Binti Khalufani kwa kunema hawezekani kabla ya kukutana na Binti Khalufani ki- MKUTANO?
  • Unafikiri jamii inavyobadilika ni kwanini MAFUNDISHO ya mahusiano kati ya Mwanamke na Mwanaume ambayo ndio misingi ya BOMBA LA FAMILIA hayatiliwi MAANANI yabadilike kukidhi mabadiliko ya Limwanamume na Limwanamke wa leo wajengao JAMII ya LEO?
DUH nimekumbuka miye si mtaalamu wa Mahusiano YA WATU na NAACHA TOPIKI!
NIMEACHA na kumbuka hili ni wazo tu na NAKUTAKIA siku njema JEMADARI!



Ngojea niwaachie ARROW wabadili hali ya hewa kwa kitu-Hot Hot Hot





Au tu Arrow waongelee sabuni ya roho kamaitambuliwavyo na baadhi ya watu-
- money money



ASANTENI tena WADAU wote !
Asanteni hawapia ambao hamkunitenga siku za karibuni ambao baadhi ni hawa kwenye picha zangu.....

Photobucket


Photobucket







Photobucket



Photobucket




Photobucket



Photobucket




Photobucket








Photobucket








Photobucket



Photobucket

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 5:51 pm  

Duh! kazi ipo

pwaniraha 2:34 pm  

Nice pics ndugu.

Simon Kitururu 2:58 pm  

@Pwaniraha:Thanx!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP