Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Duh! Sasaaaaaaaaaaa.......!

>> Saturday, March 31, 2007

Kuna mshikaji kanitumia meseji kuwa kwanini nikiweka picha watu wanarudia.Hawa ni
marafiki zangu . Lakini kama hupendi samahani.Lakini Duh!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Sasaaaaaaaa!
Ngoje nikuache na baadhi ya picha za jana. Lakini ngojea niseme.......Duh!Kiupandeupande.................:-)
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Mtimkubwa


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Dj Huyu ndio Aliko anamuamini mtaaniPhoto Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mazengo eeeh!


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mkuu wa kikao


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aliko!Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aliko eeeeeeeh!Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Chriss aka T.IPhoto Sharing and Video Hosting at Photobucket
Erick

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Erick eeh!


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Duh!
Sasa, jumamosi njema!Tukopamoja lakini hivi kwanini bongo hatuna sehemu za kutibu waaachao kinywaji?
Ngojea nikuache na Amy WinehouseAkikupa kibao kiitwacho Rehab

Read more...

Namzimia Mbu, Simba kapendelewa tu....

Mbu yuko mawazoni leo!

Unajua kuna watu kibao humsifia Simba.
Huwa pia nashangaa sana jinsi nchi za magharibi pia zitumiavyo sana Simba wa Afrika kama alama yao ya mambo mengi tu mpaka hata katika baadhi ya bendera zao. Lakini ukifikiria, mara nyingi hutumia alama ya Simba dume.
Lakini Simba dume ukimfuata porini mara nyingi yeye siye afanyaye maswala yampayo simba jina.
Au?
Ni simba jike ambaye huwinda zaidi.
Ni simba jike ambaye ni mkali zaidi.
Ndio Simba dume ananguvu. Lakini huwa anakuwa mkuu wa familia ya simba kwa muda usiozidi miaka miwili halafu anapigwa chini na simba dume mwingine. Hivyo nguvu za simba dume ambaye husifiwa sana iko kwa miaka miwili tu.Katika uwindaji pia , ukifuatilia utakuta kuwa Mbwa mwitu(wild dogs) huwa wanafanikisha kudaka wamtakaye mara nyingi kuliko afanikiwavyo simba.

Sasa turudi kwenye mbu. Huyu kijana ingawa maisha yake ni mafupi lakini mambo yake katika muda huo si utani. Kitu nimzimiacho ni jinsi tokea miaka milioni mia moja sabini asadikikavyo amekuwepo duniani mpaka kesho anabadilika kutokana na mazingira. Kila dawa utumiayo kumuua hakawi kuigeuza kuwa mzaha. Amefanikiwa kutuletea magonjwa nakutuua kwa miaka maelfu hata katika kipindi ambacho hatukuwa tumemstukia. Ukimlinganisha umbo lake na awawindao , hapo utakoma. Maana anamvaa kijeba mkubwa kwake mara milioni .

Duh!
Sawa basi nimekubali!Mbu hafikirii hilo swala la ukubwa wa amfyonzaye.

Lakini binadamu inabidi tumuige huyu kijana.

Kinachosikitisha ni kwamba watu wengi hatumjui mbu. Hatumfuatilii hata ni kwasababu gani ni mbu jike tu afyonzaye damu.

Basi ngojea tukumbushane.Mbu jike hufyonza damu kutafuta protini ambayo huitumia katika uzazi- ukuzaji wa mayai yake. Hivyo mbu akikuuma lazima ujue huyo mbu alishafanya ngono hivyo anatafuta tu protini kwa ajili ya mayayi. Na hii ndio maana ni mbu jike afyonzaye damu.

Lakini unakumbuka mzunguko mzima wa maisha ya mbu?Tukikumbuka haya tunaweza sana kuwapunguza kwa kuondoa maji yaliyo simama.Kumbuka yale makopo yaliyojaa maji pale kwenye shimo la takataka.Lile kopo pale nje utakalo kulitumia kupanda maua. Lakini usilisahau lile kopo uliloliacha pale nje baada ya kuamua kuwa hutalitumia msalani. Duh! Na haya madibwi ya maji nayo bomba la hospitali ya uzazi?

Mbu kiboko!
Eti anatemea mate kabla hajafyonza. Halafu kwa kusafirisha vidudu vya Malaria anatuua kuliko wadudu kibao.
Eti halafu twamuogopa Simba!
DUh!
Usitishike!Tunakumbushana tu!
Ngoja nikukumbushe Lambada basi.Unawakumbuka Kaoma?
Pata Lambada basi!Wikiendi njema!

Read more...

Ukiitazama Dar kama Kioo cha Tanzania

>> Thursday, March 29, 2007

Inasemekana Michael Jackson alipofika Dar kikubwa alichokuwa anakilalamikia ni kuwa pananuka.

Mvua ikinyesha Dar ni rahisi tu kustukia jinsi gani mifereji ya kusafirisha maji ilivyo na mapungufu.

DAR-ES-SALAAM(Picha kwa hisani ya MICHUZI)Leo nimekumbuka jinsi nilivyoshangaa kusikia kwa mara ya kwanza jinsi Kipindupindu kilivyokuwa kinasumbua London, Uingereza. Kutokana na ukweli kuwa mara nyingi nilipokuwa nasikia habari za ulaya na kuonyeshwa picha , hata siku moja nilikuwa siambiwi ni wapi miji hii ilikotokea.Nilikuwa naonyeshwa nakusimuliwa mazuri tu na jinsi inavyopendeza.

Swali:
Hivi kwanini wamagharibi wakiwa Afrika hupenda kupiga picha za sehemu mbovu na Waafrika wakiwa magharibi hupenda kupiga picha sehemu babu kubwa?

Basi baada ya kusikia maswala na kuanza kufuatilia miji hii nilishangaa sana.Hapo ndipo nilipoelewa msemo Roma haikujengwa kwa siku moja.

Mji wa London ukifuatilia hata jinsi ilivyokuwa vigumu kwa wanasiasa kukubali kugharamia gharama za kujenga mfumo wa kuondoa maji machafu unaweza ukamsamee diwani mtoto wa mjini Dar ambaye hata mifereji ipitayo kwake anaiziba.

Lakini tukumbuke huu mfumo wa London ulimalizika mwaka 1865.Mfumo wa Bazalgette kama ujulikanavyo kwa kufuata jina la injinia aliyesimamia shughuli, pamoja na kasheshe zote ulimalizika kwa muda wa miaka saba.Na mpaka leo hii kiini cha utokaji wa maji machafu mjini London.Inasemekana yeye ndiye aliyeshauri kuwa uchafu uelekezwe mtoni Thames hadi baharini badala ya kuupeleka ndani ya nchi.

Nacho jaribu kusema ni kuwa labda tusikate tamaa kwa hali halisi ilivyo sasa. Lakini kama Dar ndio kielelezo na ndio iko hivi basi kazi tunayo. Lakini kama London naamini mara nyingine mtu mmoja na mtazamo wake ambao akaweza kuutetea vizuri kuna wakati unaweza kuzaa matunda. Lakini kikubwa ni kwamba sisi ndio ni maskini labda ni vigumu kugharamia mifumo mbalimbali ihitajikayo nchini , lakini je tunaipa kipaumbele?Je masta plani inafuatwa?
Angalia hii picha chini....


Picha kwa hisani ya Mjengwa

Hali kama hizi kweli katika mji ambao ni kielelezo au hata mji wowote ule zinakubalika kweli?.Utaona tu hapo kirahisi jinsi gani watu wanaweza kuugua kipindupindu,malaria na bila hata ya kuwepo hapo unajua kuwa pananuka.

Nimependa kuuzungumzia mji wa London kuwa nao ulikuwa unanuka watu wakafanyia kazi. Hapo juu kwenye picha kuna mfereji hivyo inamaanisha kuna watu walifikiria kufanyia kazi hiki kitu. Tofauti ni je mfumo mzima unafanyiwa kazi? Nani anafuatilia?

Kila siku hizi tunaona jinsi majengo mapya yanavyojengwa. Lakini nasikia kunabaadhi ya sehemu imekuwa kawaida kunyea kwenye mfuko wa plastiki halafu kuutupa kinamna. Sasa tunavyojenga haya majengo mapya au tutoavyo vibali au tununuapo radar uchwara ..........
Sawa nisilalamike sana !Lakini nadhani ni muhimu kukumbushana kuangalia hii picha katika kona zote. Kwa maana sehemu yenye jengo zuri lakini linukalo laweza lisiwe na maana vilevile.


Tunaonyeshwa picha ya mambo mengi ambayo yanabadilika Dar. Natumaini mambo yatabadilika nchi nzima.Safari bado ni ndefu. Lakini kwa sasa bado Dar inanuka.
AU?

Rafiki yangu mmoja aliyoko Lagos ananiambia kuna sehemu hazikaliki kwa harufu. Hivyo hili tatizo liko Afrika nzima. Lagos inasemekana ndio mji wa wajanja kuliko yote Afrika.Sasa sijui!
Kazi ipo!Lakini tusikate tamaa.
Ngoja nikuache na BANTU akikupa Lagos Jump

Read more...

EU inasherehekea Miaka 50 .......

>> Saturday, March 24, 2007


Wakati wa Ulaya(EU) wanasherehekea miaka 50 tokea Triti ya Rome kupigwa sahihi, mimi nashindwa kujizui kuwakumbuka akina Kwame Nkurumah ambao nao tokea mbali waliwaza na kujaribu kuunganisha bara la Afrika. Waulaya imepita miaka hamsini angalibado wanajenga himaya yao. Tukikumbuka hawa ndio waliokuwa na ambao wamechangia sana kutugawa Waafrika mpaka leo hii bado wanajenga muungano wao. Hivyo naamini kabisa inawezekana kuwa Afrika pamoja nayote yatukabiliyo ni jambo zuri tu tumefanikiwa angalau kulitunza wazo la muungano wetu. Mimi naamini sisi tunahitaji sana kuungana hata kama si kwa staili ya hawa wa Ulaya. Tunahitaji kuungana ili kusaidiana kuokoa vizazi vyetu vya watu weusi vijavyo kunyanyasika hapa duniani.
Jumamosi nyema!
Duh !Lakini unamkumbuka Abeti Masikini?

Read more...

Mtu mwenye Kifafa akijamba.........

>> Friday, March 23, 2007


Kuna baadhi ya hoja hupenda kuzirudia . Hasa kutokana na baadhi ya washikaji kuniuliza maswala na pili kutokana na yanitokeayo katika maisha haya magumu ya kila siku.Moja ni hili nalo andika hapa......lakini kabla sijaanza kuandika......Watu hupenda kupata majibu au maelezo ya karibu kila kitu kiwagusacho. Lakini kama jibu halipo hupenda kubunia maelezo ambayo huchukuliwa kama ni ukweli.
Jibu ambalo watu wanashindwa kulibishia vizuri hugeuka kuwa ndio ukweli.

Inabidi tukubali tu kuwa si kila kitu kiko kama tufikiriavyo. Mara nyingine hisia za kawaida(common sense) hudanganya hasa kama malengo ni ya mbali. Na sababu kubwa ya kudanganyika na matumizi ya hisia hizi (common sense) ni ukweli kuwa ujenzi wa hii kitu unahitaji uzoefu ambao hakuna mtu anaweza kuupata katika kila kitu katika maisha haya mafupi ya binadamu.Kila mtu kunasemu tu hataweza kuijua na hisia zake zawezakuwa potofu.Hivyo kila mtu kwa kutumia hisia za kawaida huweza kujikuta kajilenga pabaya.Lakini kutokana na kwamba binadamu tofauti wananguvu za hoja tofauti , basi kuna baadhi yetu tunaweza kuwa tunaweka mapotofu yetu ya hisia za kawaida yachukuliwe na wengi kama ndio ukweli halisi.Na dunia imejaa mambo haya. Na nahisi wengi wetu tunadhurika na hisia hizi ambazo zimegeuka kuwa ndio ukweli.

Utasikia kuwa eti binadamu walikuwa wanajenga mnara kwenda mbinguni ndio Mungu akaamua kuwachanganya kwa kuwafanya wasielewane ndipo lugha nyingi zikatokea. Swala hili kwa taaluma za leo utagundua kuwa ilikuwa haiwezekani kujenga mnara wa babeli kwenda mbinguni. Lakini bado maelezo ya vyanzo vya lugha utasikia baadhi ya watu waki zungumzia hili kama moja ya sababu ya kuwa na lugha nyingi duniani.

Hivi mbinguni ni wapi?

Utasikia.....

 • Kinjekitile alidai anaweza kubadili risasi kuwa maji.
Nasikia pia hata Nigeria sasa hivi , wale wapigania haki la bonde la mafuta wanadai kuwa hawapigiki risasi.

 • Utasikia kuna watu wanadai kuwa zeruzeru hapigiki picha.
 • Kunawakati nishasikia watu wakisema wanawake wa kizungu hawadanganyi.
 • Nishasikia kuwa eti Tanzania masikini.......na kwamba Watanzania tunaamini hatuwezi kujikwamua.
 • Nakadhalika kadhaa

Nakumbuka wakati niko shule ya msingi , darasani tulikuwa na mshikaji anayeanguka kifafa. Basi ilikuwa akianguka watu tunakimbia kama vile sijui nini kimetokea. Sababu kubwa ya kukimbia huku ilikuwa kwamba tumeambiwa kuwa jamaa wakati kaanguka akijamba basi wote tutapata kifafa. Matokeo yake ilikuwa tunaumia kwakukimbia na jamaa anajing'ata ulimi kutokana na watu kukwepa kumsaidia asijing'ate wakati ameanguka.Ilichukua muda mrefu kujua kuwa hakukua na ukweli katika jambo hili.

Lakini inabidi nikubali kuwa katika mambo mengi ambayo hukutananayo na kujaribu kuyaelewa yanayoniacha hoi moja wapo ni hili la wabunifu wa maelezo ya mambo. Mambo mengi tu duniani tusiyoyaelewa kuna jamaa ambaye alifanikiwa kuelezea watu ni nini kinaendelea hata kama sababu hizo amezibuni tu.Na si watu binafsi tu .Mpaka nchi , makanisa , misikiti, masinagogi nk yameshiriki sana kutuletea tafsiri na maelezo ambayo kila siku yanazidi kugundulika kuwa mizizi ya ukweli wake inautata.Unakumbuka kuwa kanisa lilishawahi kung'ang'ania kuwa dunia iko kama meza?Na aliyebisha aliuawa. Unakumbuka Afrika Kusini kwa msaada wa kanisa walishapitisha kuwa waafrika si watu kamili?


Duh!
Ngojea turudi katika mambo ambayo hata hatuyafikirii. Mimi naamini hizi hisia za kawaida(common sense) zinatufunga mimi na wewe sasa hivi navyoongea. Kuna mambo hatuyastukii kutokana na kutumia common sense. Hizi hisia za kawaida zinatupa majibu kuwa haiwezekani. Zinatupa sababu kwanini haiwezekani- kwasababu fulani na fulani walifanya hivyo halafu haikuwezekana. Lakini kila mtu atakubaliana na mimi kuwa , kila mtu anabahati yake na kila mtu anastaili yake. Halafu wote sisi ni binadamu , hivyo hakuna mwenye ukweli asilimia mia.Kumbuka kila siku ni siku nyingine. Hiki kitu mimi nakiamini sana. Na naamini kuwa kila mtu ananafasi ya kufanikiwa.Si lazima kama jirani kaanzisha kioski anauza ndala basi wote tuanzishe kioski na kuuza ndala, lakini tukiwa wabunifu na kujiamini katika yale tuhisiyo kuwa tunauwezo nayo nadhani tunanafasi ya kufanikiwa.Sisemi kuwa ni rahisi! Hawa jamaa wa Google walipoanzisha kampuni wafanya biashara wengi wakubwa walisema kuwa haiwezekani kutengeneza pesa kwa staili yao. Sasa hivi kila mmoja kakaa kimya. Nilikuwa namsoma huyu jamaa Tyler Perry.Yeye sasahivi amefanikiwa sana kwa kuamua kuwalenga wanawake weusi Marekani.Alipoanza akiwa kama mbeba maboksi na mfagiaji na mkusanya kodi.Watu walimpuuzia. Sasa hivi wakati tayazi ana milioni mia moja mfukoni, wapo wamsemao kuwa maswala yake ni ya kijinga lakini anasoko lake. Siongelei maswala ya pesa tu. Naamini kufanikiwa kivyovyote. Hata kama unataka kujiua naamini unaweza kujiua kwa mafanikio . Labda bila maumivu sana au kusumbua watu .Fikiria tu kidogo.
Duh!Ngojea basi tujichakalishe maana itageuka kuwa stori tu. Tuulizane baadaye maswala vipi basi!

Lakini.......

Wanasayansi, mimi hupenda michezo yao, kwani huwa wanamchezo wa kuhakikisha maswala yaendavyo. Lakini pia hata wao majibu hawajapata yote. Sisemi kuwa ukijua mwenzako alishika moto akaungua ni lazima na wewe ushike moto. Lakini kumbuka si ukweli mwenye kifafa akijamba atakuambukiza kifafa.
Ngoja nimuache Vanessa ParadisRead more...

Umestukia!

>> Saturday, March 17, 2007


Kila mtu anajua. Na ukimpa nafasi atakufundisha.
Lakini tukubalikuwa hakuna ajuae yote.
Ingawa niwepesi kufundisha,tukubali kufundishwa.

Wikiendi njema!
Duh!Unasikiliza hili chakacha la KIM
Séga cé sèl médikaman nou nana

Read more...

Raisi wa Gambia agundua dawa ya UKIMWI!

Raisi wa Gambia Yahya Jammeh
Kuna habari nyingine ukizisikia huachi kupigwa butwaa.Umeipata lakini habari hii . Anasema mababu walimtonya kuhusu dawa hiii alipokuwa usingizini.Ila huwa anaponya UKIMWI jumatatu na alhamisi. Halafu kama una Athma au bronkaitisi atakutibu jumatano.
UNABISHA?

Read more...

Naitwa Simon. Duh!Ngoja nijitambulishe basi!

>> Thursday, March 15, 2007

Maswali ya pembeni yamezidi.....
Samahani najua sio wewe uliye uliza.

Lakini eeee?....

Naitwa Simon Mkodo Heri-el Kitururu. Lakini kinamna fulani badala ya Mkodo kutokea sehemu yoyote ya vyeti, haikutokea. Kuna kipindi nilivyokuwa mtoto, nilikuwanakwepa kujulikana kama Mkodo, kutokana na baadhi ya washikaji kuanza kunitania kwa kuniita Mkojo badala ya Mkodo.Lakini bado wanaonijua kutokea utotoni huniita Mkodo. Kama unavyohisi nilizaliwa Mkristo. Nilizaliwa Mlutherani.Lakini Mama yangu ni Mmenonaiti. Sijui kama unalijua kanisa hili laki-Marekani.Sasa baada ya Ulutherani wa kawaida nikaokoka ndani ya kanisa.Unajua unaweza ukawa Mlutherani wa kawaida, lakini unaweza ukawa Mlutherani mlokole. Niliimba sana kwaya vilevile katika kipindi hiki. Baadhi ya watu wanaolijua kanisa la Bungo Morogoro, kwaya ya kanisa hilo nishaimbia sana. Baada ya muda kutokana na uzinzi, na dhambi kadhalika zilizoniandama, nikahisi labda nahitaji kuokoka zaidi kinamna.Lakini kitu kikawa kinapungua bado.Kaka yangu Mkubwa ni Rasta, hivyo nikajaribu Urasta.Jah Kimbuteh na Marasta kibao watanikumbuka enzi hizo.Urasta ukanishinda. Katika mikutano ya Moses Kulola nikaokoka kabisaaaa. Nikawa mlokole. Lakini nikaona sipati majibu. Mshikaji wangu mmoja kwa jina la Abdalah akanihurumia akanitambulisha kwa Wasudani fulani waliokuwa wanafundisha pale Morogoro.Nafikiri unawakumbuka kama unaikumbuka seminari ya kwanza ya kiislamu Morogoro.Baadaye nikasikia walifukuzwa kutokana na koneksheni zao na Alkaida. Wakanifundisha Uislamu. Nikaslimu. Kwa Bahati mbaya kipindi hicho wazazi wakaamua niende bodingi.Kipindi hicho ilikuwa niende Uturuki kuendelea na dini lakini...... Unajua tena maisha!Unajua tena Maisha sisi binadamu tusivyoyatambua. Duh! Nikazamia Mazengo, Dodoma.

Duh !

Najaribu kukufanya unielewe! Acha lakini kuniuliza kisirisiri kwenye e-mail. Mimi mdini ingawa siamini kwenye dini yoyote. Lakini usifikirie kuwa sina sababu au sifuatilii dini za dunia hiii. Niulize tu waziwazi watu wote wasikie!

Usitishike kwa sababu sichani nywele. Wanaonijua watakuambia kuwa si mtu mbaya sana. Au?
Duh!

Ushastukia napenda kusema DUH!

Lakini....
Morogoro Sekondari nilisoma Sayansi.Nilikuwa Sayansi wani pale.Nilibadili Mazengo, nikaanza Uchumi.Nikaendelea na biashara. Ukiwa na maswali kuhusu hayo niulize ndio mpaka kesho naendeleanayo. Halafu namchezo wa kufaulu mambo ya shule.Lakini maisha ...........
Katika kublogu siandiki mambo kadhaa ambayo labda nayajua zaidi. Lakini.....
Lakini nahisi kuna baadhi ya maswali nimejibu.
Unabisha?
Tuendeleze basiiii!
Mzee Rasta Luhiamu nimerudi Mzee!Mpate basi Mzee Gregory Isaacs....

Au!

Read more...

Samahani kwa kupotea!

>> Wednesday, March 14, 2007

Samahani unajua tena nimebanwa kinamna .Nimekosa nafasi ya kublogu kinamna.
Lakini mimi, Mtimkubwa,Aliko na Dr Chiwalala , tunaanzisha blogu ya sanaa na wasanii wa Tanzania hivi karibuni....
Duh!Kama hutujui...
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mtimkubwa

tra

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Aliko aka Altune
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Simon. Duh!Sijui kwanini ninajina la Kizungu!Silibadili lakini:-)

Samahani! Dr Chiwalala picha yake inakosekana hapa leo.
Lakini nisikilize basi....Lakini washikaji tuliokuwa pamoja siku hizi chache ambazo sija Blogu asanteni!Hawa baadhi yao. Kama sijaweka picha yako usistuke. tukopamoja.Unajuatena!

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mkuu wa KikaoPhoto Sharing and Video Hosting at Photobucket
Deo
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Don Philly

Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Tony Asante kwa yote.Unajua namaanisha niniPhoto Sharing and Video Hosting at Photobucket
Sini
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
T.I na Wax. Lakini mlinikimbia...Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Ronaldo aka R.Kelly/50


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket
Mzee Mago aka Strategy


Aliko eeh !Unamkumbuka huyu Snoop Dogg alichotufanyia wikiendi iliyopita?.....
Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Huwa nasikiliza Hiphop lakini...
Kuna washikaji wananiambia kwanini katika blogu yangu hakuna Hiphop.Nasikiliza miziki yote. Halafu kama unanijua vizuri unajua huwa napiga miziki karibu yote saa nyingine. Au?
Ngojea nikuache na kikundi cha hiphop ambacho hakinichoshi......TribeCalledQuest..

Read more...

Duh!

>> Tuesday, March 13, 2007

George CarlinMimi sisemi...

Read more...

MAAJABU NA STAREHE YA SERIKALI ILIYOVAA CHUPI

>> Wednesday, March 07, 2007Kama unaamini biblia basi unaamini tokea Eva aonje tunda ,halafu na kumuonjesha tunda Adamu , basi hapo ndio mahitaji ya chupi yalipozaliwa.Kwa sababu inasemekana ndio michakaliko yote ya kibinadamu ikaanza.Maisha ya kula kwa kutoajasho na ....

Mambo yote yafunikayo mimi hupenda kuyaita chupi. Hivyo kunachupi za aina nyingi sana. Katika baadhi ya vitu tusivyoviona ni sheria, na ... Kusema ukweli mfumo mzima wa jinsi serikali yetu iendeshwavyo umevaa chupi.
Na kwa bahati mbaya vitu kama sheria ambazo zinatakiwa kutulinda zimevaa chupi, na naamini ni muhimu sana tuzijue.
Kabla sijaendelea kulonga hebu cheki hapa....Swali:
Hivi unapomlalamikia Rais, unamlalamikia Kikwete au Ofisi nzima?
Hivi akiwa matembezini ughaibuni nani anashikilia ofisi?


Narudi kwenye chupi...
Wengi wetu tumezaliwa tumejikuta tumesitiriwa na kanepi. Halafu baadaye chupi ikafuata.Na kama kawaida ya mazoea kubadili kisitiri hatukujua katika hatua ya mwanzo.Lakini baadaye tukajifunza kubadili kisitiri na tukajua umuhimu wa jambo hili.


Sasa ....
..mimi nafikiri kuwa ni muhimu Watanzania wakafundishwa mfumo uwazungukao.
Naamini hii itasaidia sana kuweka mambo wazi . Itasaidia kujua wapi twende. Kikubwa itaondoa moshi utufunikao macho hawa watendaji wautumiao kututuliza kwa sababu hatujui nini kinaendelea.Kumekuwa na mambo mengi ambayo ukweli wake watendaji wamejaribu tu kutufurahisha kwa kuleta vitu ambavyo vinafurahisha macho kumbe vinatunyonya, kutuumiza nk.Unasikia eti barabara imejengwa halafu ukipita mwezi , haipo mvua imeichukua. Unasikia meli imenunuliwa halafu ghafla haifanyikazi haina spea.Rada, nk.. Haya yote ni moshi tu .

Samahani narudi kwenye chupi....

Jambo kubwa alijualo mvaa chupi ni kwamba hatuvioni vilivyo ndani.Lakini anajua kuwa tunajua kuwa vipo pale kunako. Vingine visafi, vingine vinanuka. Vipo baadhi vidogo, na vingine vikubwa kuliko.Ukiachana na aina ya vilivyositiriwa ni kwamba vyote vinaaina yake yakuathiri. Na kwa sasa hivi tusivyo vijua vinatuathiri na tuvijuavyo vinatuathiri vibaya.

Matokeo ya kufunika mambo , mara nyingi ni kuyafanya yawe yanaathari kubwa zaidi.
Nafikiri serikali ingekuwa haijavaa chupi:

 • Hongo nyingi zinge kufa.
 • Mikataba mingi ya holelaholela isingewezekana kufanyika.
 • Tungejua kwa uhakika kazi ya Rais wetu ni nini
 • Tungejisikia na sisi ni sehemu ya serikali
 • nakadhalika.......kadhaa
Sisi wenyewe angalau tungejua angalau haki zetu.Tungejua jinsi yakuzipigania.

Kutokana na ukweli wengi wetu hatujui nini kinaendelea, ni kidogo sana tunaweza kuchangia mabadiliko ya muelekeo.Tunabaki kulalamika wakati tunajua kuwa wahusika wanajua dua la kuku halimpati mwewe.


Chakusikitisha ni kwamba tusipo chukua hatua yeyote, starehe ya serikali iliyovaa chupi mojawapo ni jinsi inavyoweza kuficha fangasi bila kustukiwa. Basi ndio hivyo tena kila siku tutaendelea kusikia tu jinsi mambo yanavyokwenda kiholela. Na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuta kuwa na ujanja wowote zaidi ya kulalamika tu. Lakini ukweli ni kwamba kulalamika tu hakutoshi. Tunahitaji mikakati ya kuivua chupi serikali.

Unakumbuka Black Panther walivyokuwa wanajaribu kuchukua hatua pale kwa Kichaka?Jikumbushe basi kutoka kwa huyu aliyekimbilia Tanzania....


Swali:
Ushastukia Tanzania hatuhitaji mtutu wa bunduki kutatua matatizo yetu?.....Naamini tukiivua chupi serikali tutaona mazuri yake na uozo wake. Hili litawezekana tu tuwezapo kujua serikali yetu inafanyaje kazi.Naamini hili tunaweza kulijua tukifundishana ya kweli sasa hivi.Kuna kipindi nilidhani najua mfumo wa serikali ya Tanzania. Lakini naamini nyadhifa na kazi kama zitajwavyo katika katiba na miongozo mingi tu, hazifanyiki hivyo Tanzania. Naamini hata Rais Kikwete siku nyingine hufanya kazi za waziri wa mambo ya nje. Au hata katibu wa wizara ya mambo ya nje.

Napenda kutoa changamoto kwa wanablogu wajuao mfumo kujaribu kutuelimisha. Tujaribu kujaribu kuweka wazi sehemu hasa ambazo zinatuponza hivi sasa.Tushirikiane kufunzana.
Duh!Samahani kidogo....


Ni vizuri kuanza na Raisi lakini nafikiri mfumo mzima unawalakini nyingi tu. Kama hatuwezi kufanya la zaidi basi angalau tujue sehemu gani , wahusika gani, na kujaribu kushauri ni nini kifanyike. Naamini itafikia siku wanablogu watakuwa wanasikika Tanzania.

Haya baadaye....
Lakini ngoja nikuache tena na Miriam Makeba atukumbushe mapambano.....

Read more...

Ghana -Miaka 50 Toka Ipate Uhuru

>> Tuesday, March 06, 2007

Kama ulikuwa unafuatilia shamrashamra za sikukuu ya uhuru wa Ghana, basi tulikuwa pamoja. Ila bado najiuliza!

 • Hivi Ghana iko huru eeh?
 • Tanzania Je?


Nauliza tu!
Nikinukuu Thesaurus ina tafsiri hizi hapa chini.

 • Independency -(freedom from control or influence of another or others independence)

 • Freedom -( the condition of being free; the power to act or speak or think without externally imposed restraints)


Nikijaribu kuangalia kwenye vitunza habari vingi. Bado nakuta kuna dondoo zionyeshazo nchi zote hizi mbili kuwa pamoja na kutotawaliwa moja kwa moja, bado maamuzi yake mengi huathiriwa na mataifa tajiri ya Ulaya na Marekani.Hivyo unaweza kushindwa kunibishia nikisema kuwa bado nchi zote mbili haziko huru.Halafu inasemekana China inakuja juu katika kuingia katika nchi ziathirizo mielekeo na uhuru wa nchi za Kiafrika. Kuna baadhi ya wataalamu wanadai , ukiipa muda tu, na viongozi wetu wakiendelea kuingia mikataba bila kuielewa, jasho litatutoka.

Duh ! Nisikutoe raha!
Lakini ?

Hawa wamagharibi siku hizi hutujia na sauti nzuri tu. Hawaji na ubabe kama zamani.

Tujaribu kuwa makini. Tustuane, ili tusipoteze mwelekeo na kupoteza uhuru kabisa.
Hivi wewe uko huru?
....Haya ngojea tuendelee na huyu mmagharibi mwingine(Teitur) aendeleze utamu......

Read more...

Staili ya kumfuata Mwanadada Kisimani!

>> Friday, March 02, 2007

Binadamu anaasili ya uvivu.
Karibu kila kitu anachojivunia ugunduzi wake, ni kitu kirahisishacho mambo ilikumwezesha kuishi aishivyo bila kutoka jasho sana.

Lakini pia binandamu huyo huyo si mvivu akiwa na kitu akiwaniacho, akilini mwake anaushuhuda kuwa atajitamba akikipata.

Hivyo mambo mengi binadamu akwepayo kufanya ni kwasababu tu akilini mwake hajajihakikishia kuwa apatacho kitalingana au kuzidi utoaji jasho wake.

Kutokana na hili...........

 • Wanafunzi wengine watakimbia hisabati, lakini hao hao hawatakosa mazoezini.
 • Wengine watakimbia mazoezi ya viungo lakini hawatakosa somo la ulimbwende.
 • Viongozi wengi, watakimbia kazi walizonazo ofisini, lakini hawatakwepa kutumia gari la ofisi na hata vitu vingine vya ofisi , ikiwemo kumuonja sekretari , mesenja au hata dereva.
 • Wengine watakwepa ngazi kwani wamestukia kuna lifti
 • Na kadhalika....kadhaaa
Sasa kigumu kinachojitokeza ni jinsi ya kumfanya binadamu huyu astukie mwisho wa kutoa jasho kuna utamu kunoga.

Kingine kichanganyacho ni jinsi kila mtu atafsirivyo utamu kunoga.

Hivyo kwetu sisi wenye uume, staili ya kumfuata mwanadada kisimani mara nyingi si tatizo mara tujuapo mwanadada , ambaye vichwa vyetu vyote viwili vimetuhakikishia analipa yuko kisimani. Mwenye kutambaa, atatambaa,wakukimbia ,atakimbia. Kama mashabiki wa mwanadada ni wengi, basi wengine tutamkatizia denge.

Duh!
Nimestukia sijui sana staili za akinadada za kumfuatilia mwanakaka kijiweni!

Sasa ukichukua jinsi binadamu asivyotabirika naamini wengi tumeacha kuangalia ni nini kinampamotisha.Katika semina , kuna watu wakagundua kuwa, ukitaka kumfanya mtu aende kusoma iliaelimike, basi mwambie kuna posho, na ubwabwa. Halafu mwisho wa semina kutakuwa na bomba la sherehe ambalo litakuwa na kilaji bwelele.

Duh! Lakini hivi hizi semina ni za kumfaidisha aendaye kwenye semina au aandaaye?

Duh !

usistuke!Sijui jibu.

Sijui anayeandaa kwanini anafanya hivyo, ikiwa itabidi awalipe awapao elimu.

Chakusikitisha ni kwamba , najua hizi posho hazisaidii kumpamotisha mtu atakekuelimika. Naamini zinamfanya aende kwenye semina, lakini sinauhakika kuwa zinaondoa hamu yake ya kusubiri hivi chakula saa ngapi.

Tukirudi katika kumfanya Mtanzania , Muafrika, mwanadamu apatemotisha , inabidi ajifunze kuangalia jinsi gani alipofikia hapatoshi.Ajifunze kujua alopofikia hapana tafsiri moja.

Kuna watu nimesikia kuwa wameridhika. Kitu kama hiki nikisikia huwa nashangaa sana!Kwa sababu sidhani kuwa mwanadamu katika maisha haya mafupi anaweza kuridhika. Leo ya mwanadamu ni tofauti sana na kesho ya mwanadamu, na hapo ni bila ya kuidharau jana.

Swali:
Hivi unahisi kwanini Bill Gates anaamka asubuhi kwenda kazini?Hivi unahisi ni motisha gani inamfanya Bill Gates amfuate mwanadada kisimani?


Nachosema ni kwamba, yale mambo ya kusema naona jamaa karidhika, siumeona kaota kitambi? Sikubaliani nayo. Jamaa kaota kitambi kutokana na staili yake ya maisha na mlo uendao na hicho.Au pia anawezekana akawa mgonjwa.

Kazi nzuri haiwezi ikakuridhisha kwa yote.Itakuridhisha katika takwa lako lakua na kazi nzuri. Kuna kitu tu ambacho katika maisha ya binadamu muda wowote anatakiwa akifanye. Na akiamini kuwa ndio siri ya utamu kunoga atakifanya kwa bidii.

Kuhusu Watanzania , naweza kusema kwa uhakika , kuwa sisi wote, kunakanamna ubongo wetu haujakuwa na uhakika kuwa uhangaikaji wetu ambao inabidi tuuzidishe utaleta matunda ambayo yanazidi jasho tutoalo na ambalo inabidi tulitoe.

Unaweza ukanibishia! Na utakuwa na sababu nyingi ambazo zinatoa ushahidi kuhusu.....

 • Kwanini sisi ni maskini
 • Tunamagonjwa mpaka ya kipindupindu, beriberi ,nk mpaka leo hii.
 • Umeme , hata jinsi ya kupata jenereta kwa nchi ni vigumu.
 • Ujanja ni kulia ofisini.

Meseji kwa mshikaji:
Duh!
Mshikaji usipojenga mwaka huu basi tena.Si unajua mshikaji ,naona uko jikoni!


Tukirudi katika hoja
:........Usistuke nakukubalia kuwa uko sahihi, kuhusu sababu uzihisizo zinatuweka hapa tulipo.

Lakini ukiniuliza mimi nitakuambia kuwa , bado elimu yetu, tamaduni zetu, aina ya malengo yetu ,hayatupimotisha kujitupa katika kuhangaikia ile hatua ya pili, ya tatu, nne....nk.Haitupi tafsiri nyingine ya maisha , maendeleo ,jitihada, na cha zaidi haitupi mwanga wa hatima ya yote.

Asilimia yetu kubwa kutokana nakukabiliana na umaskini , mafanikio kwetu ni pesa tu. Lakini ubinadamu ni zaidi ya pesa.

 • Muulize Warren Buffett kwanini anagawa pesa zake.
 • Muulize Bill Gates kwanini anasema anamzimia Warren Buffet.
Sasa tufanyeje?
Jibu ni moja tu. Inabidi tuende kinyume na asili yetu ya kibinadamu ya kuoanisha mafanikio na kupunguza kutoka jasho. Hili linawezekana tu pale tutakapokubali kujifunza aina mpya ya kupima utamu kunoga. Litafanikiwa pale tutakapo badili uzani ili uweze kutuhakikishia kuwa pamoja na kwamba tunatoa jasho sana sasa hivi , hii si lazima itafsiriwe kama shida. Inawezapia ikatafsiriwa kuwa ni njia mojawapo ambayo inatupa uwezo wakujijua kama binadamu na pia italipa hapo mbeleni?

Swali:
Lakini kutoka jasho kunalipa kweli?

Jibu :
Si lazima.

Lazima uwe na magoli na ujue unakokwenda, la sivyo utatoka sana jasho na mwisho wa siku utamu kunoga hupati.

Unajua usipojua kisima kiko wapi, staili zako zote za kumfuata mwanadada kisimani hazita kusaidia.

Haya basi ...
Akinadada mnajua mwanakaka yuko kijiwe gani?

Samahani akinadada kwa kumtumia mwanakaka katika ndoano. Najua wengine wenu kama mngekuwa samaki mwanakaka angekua bado hawezi kuwavuta kudakwa kwenye ndoano.

Tukiachana na hilo.......

Basi tuendeleze kuufundisha ubongo kustukia lawalawa nyama tusizoziona. Tuufundishe kukubali ladha nyingine za maisha katika haya maisha ambayo ni ya mpito tu na mafupi. Tukifanya hivyo tutapata tu peremende mwishoni, katikati na mwanzoni.

Ijumaa njema!
Lakini nawaacha Still Cool........


Read more...

Kukojoa!

>> Thursday, March 01, 2007


Katika mambo tufikiriayo ni madogo, makubwa huchanganyika mumo kwa mumo.
Ushastukia ukitaka kunya, saa nyingine unakojoa kwanza?

Kumbuka....

Mkubwa alikuwa mdogo kwanza.

Hivi haja kubwa na ndogo ipi muhimu?
Ipi isumbuayo sana?


Alhamisi njema!
Lakini !

Can U show me the way?

Basi namuachia Papa Wemba....

Read more...

Nataka , Sitaki!#1


Naamini imezoeleka.
Lakini bei ikikubalika katika maduka...na kule....
Wamachinga wakijua wanauhakika na bei sidhani kama......
Nataka sitaki itakuwa muhimu.

Au?

Nataka sitaki si -kubageini tu!

au?


Wewe ulifikiria namaanisha nini?
Acha hizoo!

Tulia na Stivu basi....

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP