Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Naitwa Simon. Duh!Ngoja nijitambulishe basi!

>> Thursday, March 15, 2007

Maswali ya pembeni yamezidi.....
Samahani najua sio wewe uliye uliza.

Lakini eeee?....

Naitwa Simon Mkodo Heri-el Kitururu. Lakini kinamna fulani badala ya Mkodo kutokea sehemu yoyote ya vyeti, haikutokea. Kuna kipindi nilivyokuwa mtoto, nilikuwanakwepa kujulikana kama Mkodo, kutokana na baadhi ya washikaji kuanza kunitania kwa kuniita Mkojo badala ya Mkodo.Lakini bado wanaonijua kutokea utotoni huniita Mkodo. Kama unavyohisi nilizaliwa Mkristo. Nilizaliwa Mlutherani.Lakini Mama yangu ni Mmenonaiti. Sijui kama unalijua kanisa hili laki-Marekani.Sasa baada ya Ulutherani wa kawaida nikaokoka ndani ya kanisa.Unajua unaweza ukawa Mlutherani wa kawaida, lakini unaweza ukawa Mlutherani mlokole. Niliimba sana kwaya vilevile katika kipindi hiki. Baadhi ya watu wanaolijua kanisa la Bungo Morogoro, kwaya ya kanisa hilo nishaimbia sana. Baada ya muda kutokana na uzinzi, na dhambi kadhalika zilizoniandama, nikahisi labda nahitaji kuokoka zaidi kinamna.Lakini kitu kikawa kinapungua bado.Kaka yangu Mkubwa ni Rasta, hivyo nikajaribu Urasta.Jah Kimbuteh na Marasta kibao watanikumbuka enzi hizo.Urasta ukanishinda. Katika mikutano ya Moses Kulola nikaokoka kabisaaaa. Nikawa mlokole. Lakini nikaona sipati majibu. Mshikaji wangu mmoja kwa jina la Abdalah akanihurumia akanitambulisha kwa Wasudani fulani waliokuwa wanafundisha pale Morogoro.Nafikiri unawakumbuka kama unaikumbuka seminari ya kwanza ya kiislamu Morogoro.Baadaye nikasikia walifukuzwa kutokana na koneksheni zao na Alkaida. Wakanifundisha Uislamu. Nikaslimu. Kwa Bahati mbaya kipindi hicho wazazi wakaamua niende bodingi.Kipindi hicho ilikuwa niende Uturuki kuendelea na dini lakini...... Unajua tena maisha!Unajua tena Maisha sisi binadamu tusivyoyatambua. Duh! Nikazamia Mazengo, Dodoma.

Duh !

Najaribu kukufanya unielewe! Acha lakini kuniuliza kisirisiri kwenye e-mail. Mimi mdini ingawa siamini kwenye dini yoyote. Lakini usifikirie kuwa sina sababu au sifuatilii dini za dunia hiii. Niulize tu waziwazi watu wote wasikie!

Usitishike kwa sababu sichani nywele. Wanaonijua watakuambia kuwa si mtu mbaya sana. Au?
Duh!

Ushastukia napenda kusema DUH!

Lakini....
Morogoro Sekondari nilisoma Sayansi.Nilikuwa Sayansi wani pale.Nilibadili Mazengo, nikaanza Uchumi.Nikaendelea na biashara. Ukiwa na maswali kuhusu hayo niulize ndio mpaka kesho naendeleanayo. Halafu namchezo wa kufaulu mambo ya shule.Lakini maisha ...........
Katika kublogu siandiki mambo kadhaa ambayo labda nayajua zaidi. Lakini.....
Lakini nahisi kuna baadhi ya maswali nimejibu.
Unabisha?
Tuendeleze basiiii!
Mzee Rasta Luhiamu nimerudi Mzee!Mpate basi Mzee Gregory Isaacs....

Au!

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Jeff Msangi 1:08 am  

Simon,
Nadhani unaweza kabisa kuandika kitabu kizuri tu cha historia ya maisha yako.Unaweza anza sasa,usingoje mpaka uwe retired top ranking govt official ndio utoke na memoir yako.Kumbukumbu uliyonayo ya maisha yako ni nzuri na inaweza kuwa kitabu chenye mvuto wa aina yake.

Simon Kitururu 4:54 am  

@Jeff:Nani atataka kusoma maisha yangu?I aint nobody.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP