Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Ghana -Miaka 50 Toka Ipate Uhuru

>> Tuesday, March 06, 2007

Kama ulikuwa unafuatilia shamrashamra za sikukuu ya uhuru wa Ghana, basi tulikuwa pamoja. Ila bado najiuliza!

  • Hivi Ghana iko huru eeh?
  • Tanzania Je?


Nauliza tu!
Nikinukuu Thesaurus ina tafsiri hizi hapa chini.

  • Independency -(freedom from control or influence of another or others independence)

  • Freedom -( the condition of being free; the power to act or speak or think without externally imposed restraints)


Nikijaribu kuangalia kwenye vitunza habari vingi. Bado nakuta kuna dondoo zionyeshazo nchi zote hizi mbili kuwa pamoja na kutotawaliwa moja kwa moja, bado maamuzi yake mengi huathiriwa na mataifa tajiri ya Ulaya na Marekani.Hivyo unaweza kushindwa kunibishia nikisema kuwa bado nchi zote mbili haziko huru.Halafu inasemekana China inakuja juu katika kuingia katika nchi ziathirizo mielekeo na uhuru wa nchi za Kiafrika. Kuna baadhi ya wataalamu wanadai , ukiipa muda tu, na viongozi wetu wakiendelea kuingia mikataba bila kuielewa, jasho litatutoka.

Duh ! Nisikutoe raha!
Lakini ?

Hawa wamagharibi siku hizi hutujia na sauti nzuri tu. Hawaji na ubabe kama zamani.

Tujaribu kuwa makini. Tustuane, ili tusipoteze mwelekeo na kupoteza uhuru kabisa.
Hivi wewe uko huru?
....Haya ngojea tuendelee na huyu mmagharibi mwingine(Teitur) aendeleze utamu......

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 3:45 am  

Suala la uhuru wa Ghana au Tanzania nalitazama hivi:

Utumwa: walitaka nguvu kazi ya bure. Tukachukuliwa kuzalisha pamba, tumbaku, n.k.
Yakaja mapinduzi ya viwanda, umuhimu wa nguvu kazi ya mtumwa ukapungua. Viwanda vikahitaji mali ghafi. Wakajiuliza, kwanini tusiende kwenye nchi zao tukasimamie uzalishaji wa malighafi?

Ukoloni: wakaja, wakaunda mfumo wa mashamba na kilimo cha mazao tunayoyaita ya biashara. Viwanda viko kwao, mashamba yako kwetu. Basi tukazalisha kahawa, wakaichukua na kuja kutuuzia kahawa ya kwenye makopo, tukazalisha pamba, wakaichukua na kuja kutuuzia nguo, na kakao, na mazao mengine.

Baadaye ikaonekana kuwa kelele za uhuru zimezidi. Basi wakasema, tuache wasimamie shughuli nzima wenyewe ila mahusiano yatakuwa yaleyale. Sisi kuzalisha malighafi na wao kununua kwa bei wanazopanga wao kisha kuja kutuuzia bidhaa zinazotokana na malighafi hizo.

Uhuru: Wakati wa utumwa tuliwafanyia kazi kwa ajili ya kujenga uchumi wao, wakati wa ukoloni tulifanya hivyo hivyo, na hata baada ya kitu kinachoitwa "uhuru" bado tunachofanya ni kutoa jasho ili kukidhi mahitaji ya uchumi wao.

Bado hadi leo hii ukiona wakulima wa mazao hayo ya biashara wakiamka asubuhi na mapema kwenda mashambani na wachimba migodi wakikesha migodini jua kuwa tunachofanya (ingawa hakuna kuchapwa viboko) ni sawa kabisa na kilichofanyika wakati wa utumwa na ukoloni. Kanuni na sura ya mifumo hii zina tofauti za hapa na pale ila msingi wake ni ule ule.

Simon Kitururu 5:21 am  

Mzee ndesanjo! Kuna mara nyingi usemayo yanafanana na nayofikiria. Basi sisemi....

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP